Muulize Babako aliye mbinguni
Kutoka Gospel Translations Swahili
Pcain (Majadiliano | michango) (Created page with '{{info| Ask Your Father in Heaven }}<br> <blockquote> Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa maana kila aombaye hupewa, naye ataf...') |
Pcain (Majadiliano | michango) d (Aliulinda "Muulize Babako aliye mbinguni" ([edit=sysop] (indefinite) [move=sysop] (indefinite))) |
Toleo lililopo 20:51, 20 Februari 2018
By John Piper About Prayer
Translation by Desiring God
Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. 8 Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango. 9 Au ni nani miongo mwenu ambaye mwanawe akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au mwanawe akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri, wale wamwombapo! Basi chochote mnataka wengi wawafanyie, nanyi pia muwafanyie.
Unaposimama kidogo kuchunguza kuwa Mungu ana nguvu isiyokoma na anaweza kufanya kile apendacho, na ana haki isiyokoma ndipo anafanya kilicho tu haki, na ana uzuri usiokoma kuwa kila mara anajua hakika mema, na ana hekima isiyokoma na kila mara hujua hakika yaliyomema na yaliyo haki, na ana upendo usiokoma na kuwa katika nguvu zake zote na uzuri wake na hekima yake anainua furaha ya milele ya wapendwa juu kama inavyoweza kuinuliwa—unapokaa na kuchunguza hii basimwito wa ajabu wa Mungu huyu ya kumuuliza vitu vizuri kwa ahadi kuwa atavipeana, ni ya ajabu mno.
Msiba wa ukosefu wa maombi
Maanake mojawapo wa majanga wa muda mfupi kanisani sana sana ni uchache tunao katika mwelekeo katika maombi. Mwaliko mkuu zaidi ulimwenguni umepeanwa kwetu, na bila kufahamu, kila mara tunageukia vitu vingine. Ni kana kwamba Mungu alitualika katika karamu kuu kuwahi kufanyika halafu tunamrudishia jibu kwamba, “Nimenunua shamba, lazima niende kuliona,” ama, “Ndipo tu nimenunua jozi tano za ng’ombe wa kulima nami nitakwenda kuwajaribu,” ama “Nimeoa mke, kwa hivyo siwezi kuja.” (Luka 14:18-20)
Egemeo mpya wa kuomba
Hakika, hiyo ilikuwa wakati huo. Lakini ombi langu ni kuwa Mungu atatumia ujumbe huu na neno hili kutoka kwa Yesu katika Mathayo 7, na matukio mengine katika maisha yako, ili aamshe mwinuko mpya unaoshawishi kwa kuomba itimiapo mwaka wa 2007. Natumaini kwamba utauliza Mungu afanye hiyo tunapoendelea na andiko hili.
Tutaifanya kwa hatua mbili, kwanza tutaangalia himizo nane ya kuomba katika Mathayo 7:7-11. Pili, tutajaribu kujibu swali ya vile inafaa tufahamu ahadi tutakayozipokea tunapouliza, na kuzipokea wakati tutatafuta, na tunapofunguliwa mlango wakati tutakapobisha.
Himizo nane ya kuomba kutoka kwa Yesu
Sita kati ya himizo hizi zadhihirika wazi katika andiko hili na mbili ni thabiti. Inadhihirika kwangu kuwa lengo kuu ya Yesu katika mistari hii ni kutuhimiza na kutupa motisha ya kuomba. Anataka tuombe. Anatuhimizaje?
1. Anatualilka tuombe
Mara tatu anatualika tuombe—ama, unaweza sema, utakapoisikia kwa upendo, mara tatu anatuamrisha tuombe—kumwomba yale tunayohitaji. Ni idadi ya vile anatualika ambayo inavuta hisia zetu. Mstari 7-8 “Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango.” Marudio inakusudiwa kusema, “Namaanisha hii.” Nataka mfanye hii. Mmuulize baba yako yale unayoyahitaji. Mtafute Baba yako kwa usaidizi juu ya mahitaji yako. Bisha malango wa Baba yako naye atafungua na kukupa yale unayohitaji. Uliza, tafuta, bisha. Nakualika mara tatu kwa sababu kwa hakika nataka ufurahie usaidizi wa Baba yako.
2. Anatuahidi tunapoomba
Vyema zaidi na ya ajabu kuliko mialiko mitatu ni ahadi saba. Mstari 7-8, “Uliza na [#1] utapewa; tafuta, na [#2] utapata; bisha, na [#3] utafunguliwa kwa kuwa yeyote aulizaye [#4] ataupokea, na yeyote atafutaye [#5] atapata, na Yule abishaye [#6] atafunguliwa.” Hatimaye mwishoni mwa mistari 11b [#7], “Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao!”
Ahadi saba utapokea. Utapata. Utafunguliwa. Aombaye anapokea. Atafutaye anapata. Abishaye anafunguliwa mlango. Baba yenu atawapa vitu vizuri. Hakika lengo la msururu huu wa ahadi za kifahari ni kutuambia kwamba: Himizwa ili uje. Mwombe. Si bure unapoomba. Mungu hafanyi mzaha nawe. Anajibu. Anapeana vitu vizuri unapoomba. Jipe moyo. Omba kila mara, omba wakati wote, omba kwa ujasiri katika mwaka wa 2007.
3. Mungu anapatikana katika ngazi mbali mbali
Yesu anatuhimiza sio tu kwa idadi ya mwaliko na ahadi bali kwa mwaliko ya aina tofauti tofauti mara tatu. Kwa maneno mengine, Mungu anasimama wima kujibu kwa njia inayofaa unapompata katika hatua tofauti tofauti ya kumfikia.
Omba. Tafuta. Bisha. Ikiwa babake mtoto apatikana, anamwomba yale anayohitaji. Ikiwa babake mtoto yuko pahali fulani katika nyumba lakini haonekani, anatafuta babake kwa ajili ya yale anayohitaji. Ikiwa atamtafuta na kumpata ndani ya chumba chake cha kusoma, anabisha ili apate anachohitaji. Jambo linaloonekana ni kwamba haijalishi kuwa utapata Mungu mara moja kwa karibu, pahali unaweza kumguza kwa ukaribu wake, ama kuwa ngumu kuona na vilevile kuwa na vizuizi kati kati, atasikia, na atakupa vitu vizuri kwa sababu ulimwomba na sio mwingine.
4. Kila aombaye atapata
Yesu anatuhimiza tuombe kwa kuifanya wazi kuwa kila aombaye atapata, sio tu wengine. Wa 8: "Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlango.” Anapoongeza neno kila katika mstari wa 8, Anataka kuondoa woga na kusita kwetu ya kwamba kwa namna Fulani itafanyikia watu wengine lakini si kwetu sisi. Bila shaka, anakuzungumza juu ya wana wa Mungu hapa, na si binadamu wote kwa jumla. Kama hatutakuwa na Yesu kama Mwokozi na Mungu kama Baba yetu, basi ahadi hizi hautumiki kwetu.
Yohana 1:12 inasema, “kwa wale waliompokea [Yesu], walioliamini Jina Lake aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu.” Ili kuwa mtoto wa Mungu, ni lazima tumpokee Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye anatupa mamlaka ya kufanywa wana. Hao ndio ambao ahadi hizi ni kwa ajili yao.
Kwa wale wanaompokea Yesu, kila mmoja wao, anayeomba atapewa vitu vizuri kutoka kwa Baba yake. Jambo ni kwamba hakuna mtoto wake yeyote ambaye ameachwa nje. Wote wamekaribishwa na wanahimizwa waje. Martin Lurther aliona vile Yesu anapeana motisha hapa:
Anajua kwamba sisi ni waoga na wenye haya, kwamba tunajiona kama hatustahili na hivyo hatufai kuwasilisha mahitaji yetu kwa Mungu . . . Tunafikiria kuwa Mungu ni mkuu sana na sisi ni duni mno ambapo hatudhubutu kuomba . . . Ndio maana Kristo anataka kutuondoa mbali na hisia hizo za uoga, kuondoa shaka zetu, na kutufanya tupate kuendelea mbele kwa ujasiri na tukiwa imara.” (The Sermon on the Mount, iliyotafsiriwa na Jaroslav Pelikan, Vol 21. Ya Luther’s Works, [Concordia, 1956], p 234.)
5. Tunakuja kwa Baba yetu.
Tumeidokeza, wacha sasa tuiseme kwa wazi na nguvu zake: Tunapokuja kwa Mungu kupitia Yesu, tunakuja kwa Baba wetu. Mstari 11 “Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba wenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri, wale wamwombapo!” Baba hakuwa kibandiko cha kutupwa kwa Yesu. Ni mojawapo ya ukweli yote mkuu zaidi. Mungu ni Baba wetu. Maana ni kwamba hatawahi kamwe ku tupatia yaliyo mabaya kwetu. La hasha. Ni Baba wetu.
6. Baba yetu aliye mbinguni ni bora zaidi kuliko Baba yetu duniani.
Hatimaye Yesu anatuhimiza kuomba kwa kutuonyesha kwamba Baba yetu aliye mbinguni ni bora zaidi kuliko baba Yetu aliye duniani na kwa hakika atatupatia vitu vizuri zaidi ya yale waliotupatia. Hakuna uovu kwa Baba yetu aliye mbinguni vile ilivyo kwa baba yetu aliye duniani.
Mstari 11 tena: “Ikiwa ninyi basi, mlio waovu, mnajua jinsi ya kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba wenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao!”
Ninafahamu, na Yesu alifahamu zaidi, kwamba baba zetu walio duniani ni wenye dhambi. Ndiyo sababu Bibilia kila mara inaonyesha sio tu mambo yanayofanana kati ya baba waliye duniani na Baba aliye mbinguni, bali pia tofauti kati yao (Kwa mfano Waebrania 12:9-11; Matahayo5:48).
Basi Yesu anaendelea zaidi ya himizo ya kusema kwamba Mungu ni Baba yako, na tena ni mzuri zaidi kuliko baba yako aliye duniani, kwa sababu baba wote walio duniani ni waovu na Mungu si mwovu. Yesu ni wazi sana na hayumbiyumbi hapa. Hili ni tukio la wazi la kuamini kwa Yesu katika dhambi ya asili kwa binadamu. Anachukulia kuwa wanafunzi wake wote ni waovu—Hachagui neno lililo laini (kama dhambi, au dhaifu). Anasema tu kwamba wanafunzi wake ni waovu (ponēroi).
Usifikishe tu ufahamu wako wa Mungu kuwa Baba kwa yale ambayo umeyaona kupitia baba yako. Walakini, jipe moyo kuwa Mungu hana dhambi yoyote ama upungufu ama udhaifu ama yanayosushe kama ya baba yako.
Na yale Yesu anajaribu kutilia mkazo ni: hata baba ambao wamepugukiwa, na wenye dhambi huwa na neema ya kawaida ya kutosha ya kuwapatia watoto wao vitu vizuri. Kuna Baba ambao ni wadhalimu sana. Lakini, mahali pengi duniani, baba ni wenye wivu kwa wema wa watototo wao, hata wasipofahamu yaliyo nzuri kwao. Lakini Mungu ni zaidi. Kwake hakuna uovu. Basi, pingamizi ni kubwa: Ikiwa baba yako aliye duniani alikupatia vitu vizuri (ama hata kama hakukupatia!), si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri—Kila mara vitu vizuri vinakuja kwa wale waombao.
Na kuna kitu cha kututamatisha hapa kinacho onyesha himizo #4 hapa juu—Neno kila—“Kila aombaye hupewa.” Ikiwa Yesu atawaambia wanafunzi wake kuwa, “Ninyi ni waovu,” basi wale tu ambao wanaweza kuja kwa Mungu kupitia maombi ni wana wa Mungu walio waovu. Ninyi ni wana wa Mungu. Na ninyi ni waovu. Kwa maneno mengine, hata baada ya kupokelewa na Mungu katika familia yake, dhambi bado inabaki ndani yako. Lakini Yesu asema, kila atakayenipokea—kila mmoja wa wanawaovu wa Mungu! Tunaona ni kwa nini punde tu.
7. Tunaweza amini Wema wa Mungu kwa sababu tayari ametufanya wana wake.
Huu ni himizo mwingine wa kutatanisha kwa kuomba: Mungu atatupatia vitu vizuri kama wana wake kwa sababu tayari ametupatia karama ya kuwa wana wake.
Wazo hili lilitoka kwa St. Augustine: “Basi ni nini hatawapa wana wanapomwomba, ikiwa tayari amepeana kitu hicho hicho, kwamba, ndipo wafanywe wana?” Tayari tumeona kwamba kuwa mwana wa Mungu ni karama tunaoupokea tukija kwa Yesu (Yohana 1:12). Yesu aliwaambia Wafarisayo katika Yohana 8:42, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda.” Lakini Mungu si baba yao. Walimkataa Yesu. Basi, sio kila mmoja ni mwana wa Mungu. Lakini kama Mungu ametufanya wana kwa hiari, si zaidi atatupa yale tunayohitaji?
8. Msalaba ndio msingi wa maombi
Hatimaye, yanayotatanisha katika maneno haya ni msalaba wa Kristo kama msingi wa majibu yote ya ombi letu. Sababu ya kunifanya niseme hivi ni kwamba anatuita waovu na bali pia anasema sisi ni wana wa Mungu. Inawezekanaje kuwa watu waovu wanapokelewa na Mungu mtakatifu juu ya yote? Tunaweza kubaliwaje kuwa wana, wacha tu kuomba na kutaraji kupokea, na kutafuta na kutarajia kupata, na kubisha na kutarajia mlango ufunguliwe?
Yesu alipeana jibu mara kadhaa. Katika Mathayo 20:28, alisema, “Kama vile ambavyo mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.” Aliutoa uhai wake ili atufidie kutoka kwa ghadhabu ya Mungu na akatuweka katika hali ya wana wanaopokea tu vitu vizuri. Na katika Mathayo 26:28, alisema katika karamu ya mwisho,” Hii ndiyo damu yangu ya agano, ile imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondeleo la dhambi.” Kupitia damu ya Kristo, dhambi zetu zimesamehewa tunapomwamini. Ndiyo maana ingawa Yesu anatuita waovu, tunaweza kuwa wana wa Mungu na kumtegemea kutupatia vitu vizuri tunavyomwomba.
Kifo cha Yesu ndicho msingi ya ahadi zote za Mungu na majibu yote ya maombi tunayoyapokea. Ndiyo maana tunasema “Katika Jina la Yesu” mwishoni mwa maombi yetu. Kila kitu chamtegemea.
Muhtasari hadi sasa ni kuwa Yesu ananuia kutuhimiza kuomba. Kwa nini aongee hivi kuhusu maombi ikiwa lengo lake kwetu katika mwaka wa 2007 sio eti tuombe. Hivyo basi anetupa himizo baada ya himizo, kwa kiasi kidogo kisichopungua nane kwayo.
Swali mmoja la mwisho
Swali la mwisho: Je, tutazielewaje ahadi hizi sita katika mstari 7 na 8: “Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa maana kila aombaye hupewa, naye atafutaye huona, naye abishaye hufunguliwa mlang"?
Je, inamaanisha kwamba chochote mwana wa Mungu aombacho hupewa?
Nadhani huu muktadha unatosha kujibu swala huu. La, hatupati vyote tuombavyo na hatufai na hatungependa hivyo. Sababu ninasema hatustahili ni kuwa katika hali hiyo tutafanyika Mungu kama Mungu angetupa vyote tuombavyo afanye. Hatustahili kuwa Mungu. Mungu anastahili kuwa Mungu. Na sababu nasema kuwa hatuhitaji kupata kila kitu tulichokiomba ni kwamba basi itatulazimu kuubeba mzigo wa hekima isiyokoma ambayo hatuna. Hatujui kwa kukata kauli usiopungua vile kila hatua itakavyokuwa na vile tukio linalofuata katika maisha yetu, wacha hata historia, vile inapaswa iwe.
Lakini sababu ninasema kwamba hatupokei yote tunayoomba ni kwa sababu nakala inadokeza hivyo. Yesu anasema katika mistari 9-10 kwamba Mungu baba hatampa mwanawe jiwe ikiwa amemwomba mkate, na vile vile hatampa nyoka ikiwa amemwomba samaki. Maelezo haya yanatufanya tuulize, “Itakuwaje iwapo mtoto atamwomba nyoka?” Je, andiko linatupatia jibu kama Baba aliye mbinguni atampa?” Ndio, inatupatia majibu. Katika mstari 11, Yesu analeta ukweli huu katika maneno: si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao.
Yeye hupeana tu vitu vizuri
Anapeana vitu vizuri. Vitu vizuri pekee yake. Hawapi watoto nyoka. Basi andiko lenyewe linadokeza sawia katika kibwagizo ya kuwa Ombeni nanyi mtapewa kumaanisha Ombeni na mtapokea kile mlichoomba mnapouliza kwa njia inayostahili mkiombee. Haisemi hilo. Na haimanishi hilo.
Tukichukuwa aya hii kwa ujumla, inasema kuwa tunapoomba, na kutafuta na kubisha—tunapoomba kama watoto wenye hitaji bila kutazama mali tulionayo kwa Baba wetu wa mbinguni ambaye ni wa kuaminika—atatusikia na kutupatia vitu vizuri. Saa zingine yale tu ambayo tumemwomba. Wakati mwingine kwa wakati tu ambayo tumemwomba. Wakati mwingine kwa ile njia tu tunavyotamani. Na wakati mwingine anatupatia vitu bora zaidi, ama kwa wakati ambao anajua ni bora zaidi. Na kwa njia ile anajua ni nzuri.
Na hakika hii inajaribu imani yetu. Kwa sababu kama tulidhani kuwa kitu kingine ni bora zaidi, tungekiomba mara ya kwanza. Lakini sisi si Mungu. Hatujaimarika bila kikomo, ama kuwa na haki isiokoma, ama kuwa wenye hekima isiokoma, ama kuwa na upendo usiokoma. Na hivyo basi, ni neema kuu kwetu na kwa ulimwengu kutopata yote tunayoyaomba.
Tii Yesu kwa Neno Lake
Tukitii neno la Yesu, Lo! ni kiasi gani cha baraka tunakosa kwa sababu hatuombi na kutafuta na kubisha—baraka kwetu, kwa familia zetu, kanisa letu, nchi yetu, dunia yetu.
Basi jiunge nami katika juhudi mpya ya kutenga wakati wa kuomba pekee yako na katika familia na katika vikundi katika mwaka wa 2007. Wiki hii inayosalia ya maombi, na kijitabu chake maalum ambacho kimeandaliwa kwako, imekusudiwa kama kielelezo cha kuendeleza mahubiri hii.