Kufanya utume wakati kufa ni faida

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
Pcain (Majadiliano | michango)
(Created page with '{{info|Doing Missions When Dying Is Gain}}<br> ''Wheaton College'' Taarifa langu la ujumbe maishani na la kanisa langu ni, <blockquote> Tuko kwa ajili ya kueneza ari ya uku ...')
Badilisho lijalo →

Sahihisho kutoka 18:34, 14 Septemba 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Missions
Topic Index
About this resource
English: Doing Missions When Dying Is Gain

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Missions
Part of the series Wheaton College

Translation by Desiring God


Wheaton College

Taarifa langu la ujumbe maishani na la kanisa langu ni,

Tuko kwa ajili ya kueneza ari ya uku wa Mungu katika mambo yote kwa ajili ya furaha ya watu wote.

Napenda neno hilo la huduma kwa sababu nyingi. Moja ni kwa sababu haiwezi kukosa. Najua haiwezi kosa kutumika kwa sababu ni ahadi. Mathayo 24:14, “Injili ya Ufalme itahubiriwa ulimwenguni pote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo ule mwisho utakapokuja.” (Na natumai kuwa unajua kwamba “mataifa” hayamaanishi nchi ya kisiasa. Inamaanisha kitu kama makundi ya watu, mkusanyiko wa kilugha ya makabila). Tunaweza kuwa na hakika kabisa kwa kila mmoja wao atapenyezwa na Injili kwa kiwango unaweza sema kwa mashuhuda, mshuhuda anajieleza ya kueleweka, yupo.

Sasa wacha niwape badhi ya sababu ya kufanya tutegemee hayo.

Yaliyomo

Ahadi ni hakika

Ahadi ni hakika kwa sababu kadhaa.

1. Yesu si mwongo. “Mbingu na nchi yaweza pita, lakini neno langu litasimama.” Na ni Yesu ambaye alisema Mathayo 24:14 si mimi.

Basi hii huduma ambao tuko kwa pamoja itafika kikomo. Itatimia, na waweza panda na kufurahia ushindi ama kushuka na kupoteza maisha yako. Una chaguo miwili tu, kwa sababu hakuna nafasi ya katikati kama, ”Labda haitatendeka na naweza kuwa katika upande nzuri kwa kukosa kupanda.” Haitafanyika.

2. Fidia tayari imelipwa kwa wale watu wa mataifayote. Kulingana na Ufunuo 5:9-10, ”Wewe unastahili kukitwaa kitabu na kuzivunja lakiri zake, kwa sababu ulichinjwa na kwa damu Yako ukamnunulia Mungu watu utoka katika kila kabila, kila lugha, kila jamaa na kila taifa. Wewe umewafanya hawa wawe ufalme na makuhani wa kumtumikia Mungu wetu, nao watamiliki katika dunia.” Zimelipwa, na Mungu hatamrudia mwanawe kwa malipo yake.

Napenda hadithi ya Wamoravia. Kaskazini mwa Ujerumani wawili wao walikuwa wakiingia kwenye dau, wakiwa tayari kujiuza kama watumwa huko Hindi Magharibi pasipo kurudi tena. Na wakati dau lilikuwaliking’o nanga katika lindi wakainua mikono na kusema, “Na Mwana—kondoo na apokea thawabu ya kuteseka kwake. ”Kile walimaanisha ni kwamba Kristo tayari alishanunua watu hao. Na watawapata kwa kuhubiri Injili bila upendeleo, kupitia kwayo Roho mtakatifu atawaita wao kwake.

Basi hii najua haiwezi kutibuka, kwa sababu deni tayari imelipwa kwa kila mteule wa Mungu pahali pote duniani. Wale kondoo waliopotea, vile Yesu aliwaita, ambao wametawanyika duniani kote watakusanyika Baba atakapowaita kupitia kuhubiriwa kwa Injili.

3. Utukufu wa Mungu u Mashakani. Kuna msururu wa maaandiko kuhusu hii. Wacha nichukue tu moja. Warumi 15:8-9, “Kristo amekuwa mtumishi kwa wale waliotahiriwa ili kuonyesha kweli ya Mungu na kudhibitisha [ama kuhakikisha, kufanya ya kutegemewa] zile ahadi walizopewa baba zetu wa zamani, pia ili watu Mataifa wamtukuze Mungu kwa rehema zake.” Nia yote ya kumfanya awe mwili ilikuwa kuleta utukufu kwa Baba kupitia kudhihirishwa kwa rehema yake kwa mataifa.

Utukufu wa Mungu u mashakani katika mwito mkuu. Hapo nyuma mnamo mwaka wa 1983 katika Kanisa la Ubatizo wa Bethlehemu, mimi na Tom Steller—msaidizi wangu sasa kwa muda wa miaka 17—sote tulikumbana na Mungu kwa njia za ajabu. Tom, usiku wa manane, hangeweza kulala, basi akainuka, akaweka wimbo wa John Micheal Talbot, na akjilaza na akasikia mafundisho yetu ya kidini ikigeuzwa kuwa huduma (sisi ni watu waegemeao utukufu wa Bwana, lakini hatutakuwa tumemaanisha huduma ipasavyo.) John Michael Talbot alikuwa akiuimba kuhusu utukufu wa Mungu unaotapakaa duniani vile maji hutambaa baharini, na Tom akalia kwa lisasi moja. Saa hiyo hiyo Mungu alikuwa akinihimiza na Noeli kuuliza, “Nini tunaweza kufanya kugeuza mahali hapa pawe pahali pa kuzindua huduma?” Na kila kitu kikaja pamoja kuleta hali kama umeme katika maisha ya kanisa letu, na ikatiririka kutoka kwa ari kwa Utukufu wa Mungu.

4. Mungu ni huru. Mungu ni huru! Wiki chache iliyopita, ninapohubiri kupitia Waebrania, tulifikia Waebrania 6. Vile mjuavyo, hili ni andiko lililo gumu kuhusu kama watu hawa ni Wakristo ama la wanapoanguka. Na katika mistari 1-3 kuna neno la ajabu (ambalo ni sehemu ndogo zaidi ya dhihirisho ya kibibilia ya sababu mimi ni mfuasi wa mafunzo wa Calvin) ambalo linasema, “Na tusonge mbele ili tufikie utimilifu, tukiachana na mafundisho yale ya awali . . . na hayo tutayafanya ikiwa Mungu atatujalia.” Tulipotazama hii, hapo kukazuka kwa washiriki wangu kimya kikuu, kwa sababu tulijua athari. “Unamaanisha kuwa Mungu aweza kutokubali waaminiyo kusonga mbele ili kufikia utimilifu?”

Mungu ni mtawala! Anatawala kanisani, na anatawala katika mataifa! Ushuhuda mmoja kwa hii umo katika jarida la Ukristo Leo (Christianity Today) ambalo lilitokea wiki chache zilizopita ikirudia hadithi ya Jim Elliot, Nate Saint, Pete Flemming, Roger Yonderian na Ed McCully. Steve Saint anasimulia hadithi ya Babake aliyeuwawa kwa mkuki na Wahindi wa kabila la Auka nchini Ecuador. Anasimulia baadhi ya kugundua mambo mpya ya kushangaza kati ya kabila la Auka waliohusika kwa kifo hiki ijapokuwa hakikufaa kutendeka na hakikutendeka. Bali ilitendeka. Na baada ya kutambua utata huu akaandika nakala hii.

Nataka kusoma sentensi mmoja ambao ilinishika sana nilipokaa katika kiti changu kule sebuleni. Alisema,

Vile [wenyeji] walivyoeleza kumbukumbu zao, ilinijia vile haingewezekana kwenye pwani mwa mitende ndipo mauaji yalipotukia. Ni utata ambao siwezi kueleza nje ya mwongozo wa kiungu.

“Ninaweza tu kueleza mauaji ya babangu ikiwa Mungu mwenye ataingilia katikati.” Je unasikia asemayo huyu mwana? “Mungu alimuua babangu?” Anaamini hayo, nami pia naamini hivyo.

Kulingana na Ufunuo 6:11, unapokuwa na mtazamo wa haraka kwa chumba cha kiti cha enzi na waliouawa kwa sababu ya neno ambao walimwaga damu yao kwa ajili ya Injili wakisema “Ni kitambo gani Bwana? Ni muda gani hadi nitahakikisha damu yetu? Na jibu larudi, “Kisha kila mmoja wao akapewa joho jeupe, nao wakaambiwa wangoje kwa muda kidogo zaidi, mpaka idadi ya ndugu zao na watumishi wenzao watakaouwawa kama wao walivyouawa, itakapotimia.” Mungu asema, “Mpumzike hadi idadi ya wale nimewateua itakapofika.” Anayo idadi ya wale wanafaa wauawe. Itakapokamilika mwisho utafika.

Gharama ni mateso

Gharama ni mateso, na uhasama katika dunia ya leo dhidi ya kanisa haupungui. Inaongezeka, haswa kati ya makundi yanayohitaji injili. Hakuna kitu kama taifa lililofungwa. Ni fikira ya kigeni. Haina msingi ama hakikisho katika Bibilia, na ingekuwa upumbavu kwa mtume Paulo aliyehatarisha maisha yake katika kila mji aliyouenda. Basi, kuna mashahidi wafya dini katika chumba hiki.

Kihesabu ni rahisi kutabiri. Jumapili moja hivi karibuni kulikuwa na angazo kuhusu mateso ya kanisa, na wengine wenu wengi walihusika kwayo. Huduma hii ya ushirika wa Taifa inahusika kwayo, na ninyi nyote mliona video na kusikia hadithi kuhusu mahali kama Sudan pahali Utawala wa kiislamu kwa mpangilio inatesa, kuweka na kuwafanya Wakristo wawe njaa ndipo kuwe na watu kama 500 wanaouawa huko kwa siku.

Nimechoka na wale wanaokuja kutsfuts kazi Kanisani mwangu, Ilioko jijini Minneapolis. Sote tunaishi ndani ya jiji na mojawapo ya maswali wanauliza ni, “Je, watoto wangu watakuwa salama?” Na nataka kusema, “Je utauliza swali hilo kama ya kumi ama ya kwanza?” Nimechoka kulisikia hilo. Nimechoka na yale Wamarekani wanaviipa kipa umbele. Ni nani aliyesema kuwa watoto wako watakuwa salama katika mwito wa Mungu?

YWAM (Vijana Wenye Ujumbe) ni kikundi kikali kilicho na jicho pevu ninachokipenda. Nilipata barua pepe tarehe mosi Septemba,

Watu wapatao 150 waliojihami na mapanga walizingira jengo walimokuwa wakiishi kundi la vijana walio na Mwito nchini India. Kundi hilo lilikuwa limechochewa na vikundi vingine vya kidini ili wapate kuwafukuza. Vile vikundi vilivyozidi kuwasogelea mmoja katika wakati ufaao akaongea kwa niaba ya kikundi na wakaamua kuwapatia siku 30 ya kuhama. Kikundi hiki kinahisi kuwa hawafai kuhama na kuwa kazi ya huduma katika mji i matatani. Matunda mengi yameonekana katika sehemu ambapo hapo mbeleni hapakuwa pamefikiwa na kuna uwezekano ya mengi. Hapo zamani wakati ghasia ulipotukia kati ya vikundi hasimu viwili vya kanisani wengi walipoteza maisha. Waombee ili wawe na hekima.

Sasa hii ni kinyume na kile ninasikia Marekani watu wanapoamua pahali pa kuishi, kwa mfano, sisikii watu wakisema, “Sitaki kuhama, kwa sababu hapo ndipo nilipoitwa na hapa ndipo kuna hitaji.” Je, utaungana nami kugeuza nia ya mahubiri ya Marekani? Imeunganika ndani katika tamaduni yetu ya mulo tupate kusogelea starehe, ulinzi, urahisi, na mbali na shaka, mateso, hatari. Inafaa iwe kinyume! “Yule anataka kunifuata na ajitwike msalaba wake na kufa!”

Hivyo siifahamu! Ni kuelea kwa waalaji, starehe, tamaduni na makanisa pahali ambapo usalama, ulinzi na mambo mema yatendeka kwa ajili ya mmoja kwa mwingine. Na matamshi machache yenye ulinzi yatamkwa ili kuokoa watu wengi. Lakini, o hatutaishi huko, O hatutakaa hapo, si hata Marekani, bila kutaja Saudi Arabia!

Nilikuwa Amsterdam wiki nyingi iliyopita nikiongea na kikundi cha wahudumu wenye jicho pevu, wanaopita mipaka, kikiongozwa na Greg Livingstone. Ni kikundi cha ajabu mno. Watu mia tano wanaketi mbele zangu wale ambao wamehatarisha maisha yao kila siku kati ya Waislaamu. Na kuwasikiza! Wakati wa kongamano walikuwa wakipokea barua pepe, ambazo wangesimama na kusoma, wakisema, “Tafadhali muombee, fulani. Alidungwa kifuani mara tatu jana, na kilicho kibaya zaidi watoto walikuwa wakishuhudia. Yuko hospitalini katika haki mahututi.” Halafu wanasema, “Huyu ni mhuduimu katika nchi ya Uislamu, wacha tumwombee,” na tungeingia katika maombi. Siku inayofuata barua pepe zingine zikaja, na mara hii wandugu sita Wakristo huko nchini Morocco wametiwa mbaroni. “Wacha tuwaombee,” basi tukafanya hivyo. Na ikawa hivyo muda wote wa kongamano. Na mwishowe, wahudumu walikuwa tayari kurudi.

Je, mnadhani nitarudi Marekani na muwe vile mlivyo? Je, mnadhani naenda kusimama mbele na kusema, “ Tuwe na huduma njema, ya starehe na rahisi. Wacha tuwe starehe na kulindwa.” Golgotha si makaasi ya Yerusalemu. “Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukichukua aibu aliyobeba” (Waebrania 13:13).

Mateso pia ni njia

Lakini kwa kusema kuwa kutakuwa na watu wa kuuawa na lazima kuwe na mateso, sijasema kuwa kitu kikuu ni kuhusu gharama ya kufanya kazi hizo zitendeke. Hiyo ni kwa sababu mateso ndiyo njia na si tu gharama. Ni njia.

Sasa hiki hapa ni kile ninacho mawazoni. Naenda kuwasomea mstari ambao ni wa muhimu sana, na ni Wakolosai 1:24. Miaka michache iliyopita, maana yake ilinijia kwa kishindo. Nitawaonyesha vile niliipokea.

“Sasa nafurahi,” Paulo asema, “Kule kuteseka kwangu.” Paulo ni mtu wa kutoeleweka sana, “Nafurahia kule kuteseka kwangu” ni kinyume na tamaduni, si Kimerekani, ni kinyume na ubinadamu. “Nafurahi kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu na katika mwili [ni kusema kusanyiko ya wateule wa Mungu] wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake ambao ni kanisa. Sasa hapo ni karibu na kufuru. Ni nini anamaanisha kwa “kutimiliza yale yaliyopungua” katika mateso ya Mungu wetu mkuu na Mwokozi, Yesu Kristo?

Hamaanishi kuwa anaimarisha umuhimu na gharama ya uoshaji wa damu ya Yesu. Hiyo si kile anamaanisha. Basi, anamaanisha nini?

Nilichapisha katika mpangilio wangu Biblia katika tarakilishi neno “timiliza” (ama kamilisha) na neno la “kile kilichopungua” na nikapata pahali pengine tu mmoja katika andiko ambapo haya yanatukia kwa pamoja. Na ni Walipi 2:30.

Hali ni kwamba Epafrodito alitumwa kutoka kwa kanisa la Wafilipi kwake Paulo huko Roma. Anahatarisha maisha yake ili afike huko na Paulo anampongeza kwa kuhatarisha maisha yake. Anawaambia Wafilipi kuwa wanastahili kumpokea mtu kama huyo kwa heshima, kwa sababu alikuwa mgonjwa kwa kiwango cha kufa na akahatarisha maisha yake kutimiliza huduma yao kwake. Huu hapa ni mstari sambamba ya dhati.

Kwa sababu alikaribia kufa kwa ajili ya kazi ya Kristo, akahatarisha maisha yake kutimiliza kile kilichokuwa kimepungua katika huduma yao kwangu.

Huu ndio pahali pengine wa pekee ambayo hayo maneno mawili yanaunganika: “kukamilisha yale yaliyokuwa yamepungua katika huduma yako kwangu.” Niliyafungua matamshi yangu kutoka kwa Vincent yaliyo na miaka 100 juu ya Wafilipi na kusoma maelezo ya mstari huo ninavyofikiri ni tafsiri kamili ya Wakolosai 1:24, Vincent alisema,

Zawadi kwa Paulo kutoka kwa Wafilipi ilikuwa zawadi ya kanisa kama mwili. Ilikuwa zawadi ya kutoa dhabihu ya upendo. Kile kilichokosekana ni kanisa kuipeana moja kwa moja. Ilkuwa haiwezekani, na Paulo anawakilisha Epafrodito kama yule atimilizaye upungufu huu kupitia huduma yake uliojawa upendo na shauku.

Basi taswira ni ya kanisa linalotaka kuwasilisha upendo katika njia ya fedha kule Roma, na hawawezi kuufanya. Kuna wengi wao zaidi. Na ni mbali sana. Basi wanasema, “Epafrodito, anatuwawkilisha na kukamilisha kinachopungua katika kupenda kwetu. Hakuna chochote kilichopungua katika upendo wetu isipokuwa kuuwasilisha moja kwa mopja. Uuchukue na uuwasilishe kwa Paulo.”

Sasa hicho ndicho nifikiriacho Wakolosai 1:24 inamaanisha. Yesu alikufa na kuteswa kwa ajili ya watu wote ulimwenguni na mataifa yote halafu akazikwa na kulingana na maandiko, akafufuka siku ya tatu. Atapaa juu mbinguni pahali atakapotawala dunia yote. Na anaaacha kazi za kufanywa.

Kuelewa kwa Paulo juu ya huduma yake ni kuwa bado kuna kitu kimoja ambacho kimepungua katika mateso ya Yesu. Ni toleo la upendo wa Kristo ni kuuwakilishwa kibinafsi kupitia huduma kwa watu aliowafilia. Na Paulo anasema, “Nafanya haya kwa kuteseka kwangu. Kule kuteseka kwangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo.” Ni kumaanisha kuwa Kristo anakusudia ili mwito Mkuu uwe dhibitisho kwa mataifa juu ya kuteseka kwake msalabani kupitia mateso ya watu wake. Hivyo ndivyo itakamilika. Ukijisajili katika Mwito Mkuu, hichi ndicho umejisajili kwacho.

Karibu miaka mitatu iliyopita nilikuwa nikifanya kazi juu ya Wacha mataifa yawe na furaha, na nikajificha katika Trinity Seminary huko Deerfield Il. Nilijificha kwa sababu sikuwa nikitaka mtu yeyote kujua kuwa nilikuwa, ndipo wasipate kunisumbua. Bibi na watoto wangu walikuwa nyumbani, na nilikuwa nikifanya kazi kwa masaa 18 kwa siku.

Na nikapata ujumbe kuwa J. Oswald Sanders atakuwa kanisani. Mwenye miaka themanini na tisa. Shujaa. Kiongozi wa huduma kuu. Na nikajisemea, “ Je, nijitokeze kwa dharura na nihatarishe kupata kuongea na watu wengi na kupata mwaliko wa mulo wa jioni na mambo haya yote na kutofanya chochote?” lakini nilitaka kumsikiza, hivyo basi nikaenda kwa siku kupitia nyuma ya kanisa na kumsikiza. Na huyu mzee wa miaka 89 alisimama hapa juu, na nilijawa na tamaa na shauku ya kuwa hivi nikiwa na miaka 89, na akasimulia hadithi inayoguza Wakolosai 1:24.

Akisema, kulikuwa wakati mhubiri kule India aliyetembea babarani katika miji tofauti akihubiri Injili. Alikuwa mtu wa kawaida, bila elimu, alimpenda Yesu na moyo wake wote, na alikuwa tayari kuhatarisha maisha yake. Na alifika katika mji ambao haukuwa na Injili. Ilikuwa wakati wa manane na alikuwa amechoka sana. Lakini anaenda kwenye kijiji na kuinua sauti yake na kushiriki neno na waliokusanyika kwenye ua. Wanamtania, kumkejeli, na kumfukuza nje ya mji. Na alikuwa amechoka sana—bila mali ya kiroho aliyobaki nayo—anajilaza chini ya mti, akiwa amekufa moyo sana. Analala akiwa hajui kama ataamka. Wanaweza kuja kumua, kwa kile anafahamu.

Na ghafla, baada tu ya machweo, ahashtushwa na kuama. Kama mji yote wanakaa ni kama wamemzingira na kumtazama. Anafikiri yeye ni jangili. Anaanza kutetemeka, na mmoja wa watu wakuu katika kijiji anasema, ”Tulikuja kuona wewe ni mtu wa aina gani, na tulipoona vidole vyako viliyo chubuka tukajua wewe ni mtu mtakatifu. Tunataka utuambie ni kwa nini uvimbe miguuni mwako ukija kutuongelesha.” Basi akahubiri Injili na kulingana na J. Oswald Sanders, kijiji chote kikamwamini. Hicho ndicho Paulo anamaanisha na “Natimiliza yaliyopungua katika kuteseka kwangu yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo Yesu.”

Sasa nini neno moja kidogo ya maelezo juu ya J. Oswald Sanders. Katika umri wa miaka 89 alisema, “Nimeandika kitabu kila mwaka tangu nifike umri wa miaka 70! Vitabu kumi na nane tangu nifikishike umri wa miaka 70. Kuna watu katika kanisa langu na Marekani kote wanaostaafu maishani katika umri wa 65 na kufa uwani wa kucheza gofu huko Nevada, ijapokuwa wanafaa kuhatarisha maisha yao kati ya Waislamu kama Raymond Lull.

Raymond Lull, msomi wa kimsingi wa karne ya 12 na mhudumu wa uislamu, anastaafu na kurudi nchini Italia. Anafanya mabo yake ya lugha ya kimsingi kwa muda na hatimaye kujiuzulu na kuanza kuuliza, “Nimefanya nini? Naenda kufia hapa Italia. Kwa nini nisije nchini Algeria ufuoni mwa bahari ya Mediterrania. Anakaa kimya kwa kwa muda akihimiza kanisa, halafu anaamua na wakati mwema kama mwingine ule. Basi anainuka na kuhubiri, na wanamwua. Oh ni njia gani ya kuenda!

Sikiza, rafiki aliye na umri wa miaka 60, mimi nina umri wa miaka 50. Niko karibu na hapo. Napokea barua kutoka kwa Muungano wa watu waliostaafu wa Marekani (American Association of Retired Persons), na wanajaribu kuniweka katika takwimu yao ili nipate kupata hafueni nikisafiri kwa magari ya moshi na ndege. Nakaribia kufika hapo sasa najiongelesha hapa (na kanisa langu wamenisikia nikisema hili na wataenda kunishika mateka) ninaposema kuwa umekuwa umezeeka si kitu kuwa huna cha kupotesa katika mauaji, bali unapata hafueni katika nauli.

Kwa nini, tufikiri kuwa kwa kufikisha umri wa miaka 40 ama 50 kazini mwetu kunafaa kumaanisha kuwa yafaa tuendelee kwa miaka 15 za mwisho kabla ya kukutana na mfalme? Sifahamu. Ni uwongo wa Kimarekani. Tuna nguvu katika umri wa miaka 65 na hata 70. Babangu ana umri wa miaka 77. Naweza kumbuka wakati mamangu aliuawa, alikuwa karibu kuuawa, katika ajali ya gari huko Israeli. Na nikamchukua siku kumi baadaye mwili wake pamoja na ya babangu ndani ya ambulansi, na njiani yote nyumbani kutoka Atlanta hadi Greenville alilala hapo kifudifudi, kwa sasbabu majeraha yalikuwa mabaya sana hawangeweza kuyashona. Na alikuwa akisema, “Mungu lazima ana lengo kwangu, Mungu ni lazima ana kusudi kwangu!”

Na hapa tupo miaka 22 baadaye, na maisha yake imelipuka kwa huduma! Anafanya kazi kwa bidii zaidi leo katika umri wa miaka 77 kwa ajili ya mataifa kiliko huko mbeleni. Anatayarisha mafunzo kutoka Easley, Carolina kusini, ikiwa pamoja na mikanda. Na wako katika mataifa 60 wakiwa na karibu watu 10,000 wanaoamini katika Yesui kila mwaka kwa sababu Mungu alimnusuru babangu na kumfanya kutoamini kustaafu.

Thawabu yatosha

Sasa hoja la mwisho: Unapendaje kama hiyo? Utapata wapi hii? Je, unahisi kuwa tayari kwa hii? Je, unadhanai unayo ndani yako kuwa na uwezo ya kuistahimili hii?

Soma nakala ya Historia ya Utumwa wa Ukristo (A History of Christian Missions) na Stephen Neill. Katika ukurasa wa 161 anaeleza yaliyotukia nchini Japan wakati Injili ilifika mnamo miaka ya 1500. Mtawala wa Kifalme alianza kuamini kuwa kujumuishwa kwa imani ya Ukristo katika hali yao ya kidini ilikuwa inashtua na ilibidi waikomeshe. Na aliikomesha, kwa ukatili wa ajabu! Ilikuwa juu ya kanisa yote kule Japani. Na sina shaka kuwa ugumu na hali ngumu ya Japani sasa imechangia kwa kiasi kikubwa (ingawa kwa muda mfupi) na ushindi mkuu wa shetani hapo awali katika miaka ya 1600.

Wafuasi wa Yesu 27, watawa kumi na tano, na wakleri wa kidunia watano waliweza kukwepa kufurushwa. Haikuwa mpaka Aprili 1617 ambapo mauaji ya kwanza ya wazungu ulipoanza, mfuasi wa Yesu na mhudumu wa Fransiska walikatwa vichwa huko Omura wakati huo, na mhudumu wa Dominiki na wa Agostino hapo mbeleni kidogo katika mahali huo huo. Aina yote ya uhasama ulifanywa kwa waathiriwa wote wa mateso. Kusulubishwa ndicho kitendo kilichofanywa kwa Wakristo wenye asili ya Kijapani. Wakati moja watu wenye asili ya Kijapani 70 huko Yedo walisulubishwa, vichwa vyao vikiangalia chini katika maji madogo na wakazamishwa wakati maji yalikuja nyingi.

Nililia siku tatu iliyopita niliposoma hiyo, juu niko na ufahamu vizuri juu ya taswira ya kulamba maji bibi yako akiwa upande mmoja na kijana wako wa umri wa miaka 16 akiwa upande mwingine.

Je uko tayari? Je, unafikiri unayo hayo ndani mwako? La huna. Hakuna vile mtu yeyote anaweza kuwa na uwezo wa aina hiyo ndani mwake. Utampata wapi? Huyo ndiye nataka kufunga naye.

Utaupokea kupitia kuamini ahadi za Mungu. Waebrania 10:32-34 ndilo andiko linipendezalo zaidi juu ya pale utapata kuishi kwa njia hii.

Kumbukeni siku zile za kwanza, ambazo mkisha kutiwa nuru mlistahimili mashindano makali ya maumivu. Wakati mwingine mlitukanwa hadharani, wakati mwingine milkuwa radhi kuungana na wale waliofanywa hivyo.

Wacha nikome hapo na niwape hali vile ninavyoisoma. Katika nyakati za mwanzo kuteswa kwa kanisa kukazuka. Wengine wao waliteswa wazi na hadharani na wengine wakawahurumia. Utaona katika mstari unaofuata kuwa wengimne wao waliwekwa korokoroni na wengine wakaenda kuwatembelea. Basi walilazimishwa kukata kauli. Wale waliokuwa katika jela kwa wakati huo yawezekana walitegemea wengine kupata chakula na maji na aina yote ya mahitaji ya kimwili ambayo wangehitaji, lakini hiyo ilimaanisha kuwa marafiki na majirani yao ilibidi wajitokeze kwa dharura na kujitambulisha kwao. Hiyo ni jambo la hatari wakati mtu amewekwa korokoroni kwa sababu ni Mkristo. Basi wale waliokuwa huru walijificha kwa masaa machache na kuuliza, “Je, tutafanya nini?” na mtu fulani akasema “Zaburi 63:3” inasema, “Upendo wa Bwana unaodumisha ni bora kuliko uhai. Ni bora zaidi halafu uhai. Wacha tuende!

Na kama Martin Luther angekuwa hapo angesema,

Wacha mali na jamaa waende,
hii uhai unaotoweka pia.
Mwili wanaweza kuua,
ukweli wa Mungu bado utadumu.
Ufalme wake ni wa milele.
Tuende!

Na hiyo ndiyo walifanya kwa hakika. Wacha tuusome uliobaki. Mstari wa 34, “Mliwahurumia wale waliokuwa kifungoni, mkikubali kwa furaha kunyang’anywa mali zenu.”

Sasa huu hapa ni yaliyotendeka. Haichukui fikira yoyote. Sijui maelezo yote kwa dhati, lakini hapa ni yaliyotukia. Waliwahurumia wafungwa, ni kumaanisha walienda kwao. Na mali yao—nyumba, magari ya farasi, farasi, nyumbu, viti, stuli, na chochote—yalichomwa na moto na masaibu ama kuchokorwa na kutupwa barabarani na watu wenye visu vikubwa vikubwa. Na walipotazama nyuma kuona yaliyokuwa yakitendeka walifurahi.

Sasa kama huko hivi—mtu akigonga tarakilishi yako unapojaribu kuwahudumia, ama unapoendesha jijini kuwahubiria na wanavunja kioo chako cha mbele, kuiba radio yako, ama kukata tairi yako—kama huko hivi basi, hutakuwa mgombezi mzuri kuwa mtu wa kuuawa pia. Basi swali ni hili, “Utakuwaje hivi?” Nataka kuwa hivi. Ndiyo maana napenda andiko hilo! Nataka kuwas hivi.

Sisemi kuwa mimi ni mkamilifu kwa hii: lakini nataka kuwa hivi, ndipo jiwe likija na kugonga dirisha langu—vile limefanyika mara mbili katika miezi mingi iliyopita—na kuvunja kioo na mke na watoto wangu wanajigonga sakafuni bila kujua kama ni risasi au gurunedi, nataka niwe tayari kusema, “Ni pahali pema pa kuishi.” Hapa ndipo kuna mahitaji. Unaona hao vijana hao watano waliopita wakiendesha? Wanahitaji Yesu. Nikihama kutoka hapa, ni nani atawaambia kumhusu?

Kijana wako mdogo anaponyanganywa baisikeli, nataka nimshike kwa shingo anapolia na kusema “Barnabas, hii ni kama kuwa mhudumu. Ni kuwa tayari kwa kazi ya huduma! Ni ajabu!”

Nilipeana ujumbe juu ya Wakolosai 1:24 huko Pensacola, Florida miaka miwili iliyopita. Nilikuwa na kijana wangu Abraham mwenye umri wa miaka 16, na alisikia nikisema mengi ya yale nisemayo hapa, hii aina ya mateso ya hali ya juu. Na tukaingia katika gari ili tuelekee nyumbani, na bibi yangu akamwambia Abraham, “Ni nini unadhani Mungu alikuwa akifanya kule ndani? Akasema, “Naenda kununua tikiti ya kuenda pekee ya kuelekea nchi iliyo na ugumu zaidi ulimwenguni.” Hiyo ndiyo aliyoyasema. Niligonga kichwa changu kwenye ukuta. Lo! Hii ni ajabu! Asante Mungu kwa ajili ya Abraham na yale unayoyatenda maishani mwake.

Basi sijaingia katika mambo makuu katika andiko. Walikuwaje na nguvu ya kufurahi kuharibiwa mali yao na kuhatarisha maisha yao? Lisikie: “Kwa kuwa ulijua kuwa wewe mwenyewe ulikuwa na mali mazuri sana na ya kudumu.” Hii ndiyo ninaita imani kwa neema ijayo.

Ikiwa wewe ni Mkristo, Mungu anakushikilia ahadi ya ajabu yasiyoweza kuelezwa. “Sitawaacha wala kuwatupa basi, unaweza sema kwa ujasiri, “Bwana ni msaada wangu sitaogopa, mwanadamu atanitenda nini?” (Waebrania 13:5-6). Sasa, mwanadamu anaweza kukuua. Lakini hakuna kushindwa, kwa sababu unajua kile Warumi 8:36-39, inasema:

Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa . . . .kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamalaka, wala yaliyopo, wala yatakapokuja, wala wenye uwezo, wala yaloyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristyo Yesu Bwana Wetu.

Basi hakuna chochote kinachoweza kukudhuru. Kumbuka yale Yesu alisema katika Luka 21:12-19? “Baadhi wenu watauwawa na baadhi wenu watafungwa gerezani . . . . Lakini hapatakuwa na unywele mmoja wa kichwa chenu utakaoangamia.” Ni tu Warumi 8. Kila kitu, kukiwa hata kifo, chatendeka pamoja kwa wema wako. Unapokufa huangamii. Kufa ni faida.

Kufanya misheni wakati kufa ni faida ni uhai kuu zaidi ulimwenguni.

Basi naomba kuwa utanitafuata kuacha njia za ulinzi wa Kimarekani na urahisi na starehe na kujivinjari na kujiachilia na upweke. Iache nyuma na ujiunge na vuguvugu hii ya ajabu uliojawa nguvu. Kuna wanafunzi kote uklimwenguni—kama vile Korea Kusini—ambao wako tayari kusimama na kuhatarisha maisha yao kwa ajili ya Kristo. Nakualika ufanye hivyo wewe pia