Kile ubatizo huashiria
Kutoka Gospel Translations Swahili
(Created page with '{{info|What Baptism Portrays}} <blockquote> Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke. Lakini dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21Ili kwamba k...')
Badilisho lijalo →
Sahihisho kutoka 19:30, 23 Juni 2016
By John Piper
About Baptism
Part of the series What is Baptism?
Translation by Desiring God
Zaidi ya hayo, sheria ilikuja, ili uvunjaji wa sheria uongezeke. Lakini dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi. 21Ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu Tuseme nini basi? Je, tuendelee kutenda dhambi ili neema ipate kuongezeka? 2 La hasha! Sisi tuliyoifia dhambi, tutawezaje kuendelea kuishi tena katika dhambi? 3 Au hamjui ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti Yake? 4 Kwa hiyo tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti, ili kama vile Kristo alivyofufuka kutoka kwa wafu kwa utukufu wa Baba, vivyo hivyo sisi nasi pia tupate kuenenda katika upya wa uzima
Leo ni siku ya mwisho wa ujumbe huu fupi kuhusu ubatizo. Nafahamu kuwa kuna mengi ya kusema. Nasema pole kama maswali mengine yenu yameachwa bile kujibiwa. Lakini tutakuwa na fursa zaidi katika ratiba zetu kujadiliana mambo haya.
Hebu kumbuka nia yetu kuu ya kuweka funzo hii mwanzoni mwa msimu wa kiangazi, ni kuwa tunaamini agano jipya laita watu waje kwa Kristo hadharani na kwa ujasiri. Tunahitaji kuona waminio wakifikia kiwango hicho cha ushuhuda wa dharura na tunataka kuona wakiwa waaminiyo kupitia kwa ushuhuda wako na kwa huduma ya neno msimu huu wa kiangazi.
Yaliyomo |
Kwa nini Yesu aliitawaza tendo la ubatizo?
Wakati mwingine tunaweza kushangaa ni kwa nini Yesu aliitawaza tendo la ubatizo. Kwa nini kuna kitu kiitwacho ubatizo? Kama wokovu ni kwa neema kupitia imani, kuna haja gani ya kutafuta dhihirisho au ishara ya kuonyesha imani hiyo? Swali hili halijajibiwa kwa Bibilia. Lakini ujuzi, unafundisha mambo ya kusisimua.
Kwa mfano, baada ya ujumbe wangu wa kwanza wiki tatu zilizopita, mishonari mstaafu fulani wa Ufilipino alikuja kunishukuru kwa fumo, na akasema kwa nini. Bi huyo alieleza kuwa Ufilipino mahali ambapo ufuasi wa katoliki huwa kwa jina na kwa vitendo, waliojiunga upya walikubalika na kwa nadra walitambulika na jamaa zao—Hadi wabatizwe. Hapo ndipo utabiri ya udhalimu na utengano ukatimia. Kuna jambo kuhusu ishara hii ya wazi kwa imani uliopatikana upya kufanya mahali mtu asimamapo na afanyapo kuwa dhahiri na safi. Kwa maneno mengine ni kuwa tamaduni nyingi leo hali nyingi ni sawa na ya Yohana mbatizaji. Alikuja akihubiri ubatizo wa toba na kwa wale waliofikiria kuwa wanayo vyote walikasirishwa.
Wiki hiyo hiyo jarida hili la huduma (The Dawn Report, Mei 30) likaja. Katika uk. 7 kuna picha ya mtu anayebatiza kwenye hali ya huduma katika mto, na ujumbe mfupi chini ya picha: “Huduma ya nje na ubatizo katika mto kwa wakati fulani huwa njia nzuri la ukuaji.” Kwa ufupi hatujui ni kwa sababu gani Mungu alikuwa katika hekima yake kueleza ubatizo kama mfano wa kuonyesha Imani kwa Kristo aidha kujitambulisha kati yake na watu wake. Tunaweza kuzifikiria sababu kadhaa kwa nini ni mzuri, wakati fulani hatutasogea kufikiria kila kitu kizuri Mungu amekusudia. Mwisho wake ni tendo la kumtumaini Baba yetu kwamba anajua atendacho na tunafurahia kufuata sheria zake.
Kutoswa au kunyunyiziwa?
Lakini kwa leo nitajaribu kuonyesha katika Warumi 5:20-6:4 mengi kidogo maana ya kitendo chenyewe. Hii pia itashughulikia swala ambalo wengi wenu wanalo kuhusu (jinsi) ya ubatizo—kwa kutosa majini badala ya kunyunyuziwa. Kwa hakika wacha nianzie na neno ambalo lajulikana na wengi kujusu jinsi ya ubatizo ya kutoswa badala ya kunyunyiziwa. Kuna zaidi ya dhibitisho tatu kwa kuamini ya kuwa agano jipya hutoa maana na vitendo vya ubatizo ulikuwa kwa njia ya kutosa majini. (1)Maana ya neno baptizo kiugriki ni kutumbukiza au kutosa si kunyunyuzia (2) Maelezo ya ubatizo katika agano jipya ni kuwa watu waliteremka majini na kutumbukizwa bali si maji kuletwa kwao kwa vyombo ili kunyunyuziwa Mathayo 3:6 Kwenye “mto Yordani” 3:16, “Alitoka kwenye maji,” Yohana 3:23 “Palikuwa na maji mengi” Matendo ya mitume 8:38 “waliteremka majini.” (3) Kutumbukizwa ni ishara tosha ya kuzikwa na Yesu (Warumi 6:1-4, Wakolosia 2:12).
Hatutadumu juu ya hii, lakini hebu niseme kuhusu vile tunavyoweza kutazama ukweli ya kuwa kanisa na dini letu hufanya ubatizo kwa kutoswa kuwa kielelezo ya ushirika katika agano la kienyeji ya ambari (bali si katika mwili wa Kristo uliotuunganisha). Hatuamini kuwa njia ya ubatizo ni muhimu kwenye tendo la wokovu. Hatuulizi watu maswali kulingana na vile walivyobatizwa ili kuwa na msimamo wa ukristo. Basi mtu anaweza kuuliza, basi hatufai tuwasajili kuwa washirika wale waliozaliwa mara ya pili kwa uhakika lakini walinyunyuziwa maji ili kuwa waumini? kuna njia mbili za kueleza kwa nini tunakataa.
1) Je tutaita ubatizo ulioundwa na binadamu kuwa ni “ubatizo,” il hali kuna dhibitisho tunaoamini kwamba umetoka kwa Kristo ambaye ni mwanzilishi? Si hii italeta hatari ya kudunisha kuhusika kwa Kristo mwenyewe aliyewekwa katika utawazo wa ubatizo?
2) Wenyeji asasi ya wakristo, waitwao makanisa, hujengwa kwenye ushirika wa hukumu za kibibilia, nyingine ambazo ni muhimu kwa wokovu nyingine ambazo si za muhimu. Hatuelezi uzima wetu wa agano pamoja katika imani iliyo banwa zaidi ambayo lazima mtu awe nayo ili aokolewe. Tunaamini kuwa umuhimu wa ukweli na mamlaka ya maandiko hueshimiwa kama imani ya asasi ya wakristo hujitambulisha kwa vifungu vya Bibilia vinavyo hukumu na kuvitetea kuliko kuwa na ufafanuzi wa ushirika kw anjia nyingine kila wkati hukumu za mwingine kuwa na ubisi. Iwapo asasi zote za wakristo watafanya hivi wakionyesha upendo na upendo wa kindugu kwa wauminio wengine basi ukweli na upendo umetekelezwa vyema. Kwa mfano, ingawaje wanenaji wengi hukaribishwa katika Bethlehemu, kwenye kongamano ya wachungaji wanaeweza kuwa si washirika wa kanisa hili wangesema kuwa tuchukue upendo, kweli na umoja kwa mkazo.
Ambayo yasiyo na maana yatajumlishwa kutoka vizazi hadi vizazi kwa kufafanua ambari mbali mbali hutegemea pakubwa hali mbali mbali n hali mbali mbali ya kutathmini ukweli unaohitaji kutiliwa mkazo.
Kile ubatizo huashiria
Kwa chimbuko hilo hebu tutazame Warumi 5:20-6:4 ili tuone ubatizo huonyesha nini na pili una matokeo gani katika jinsi ya ubatizo. Lengo langu ni kukusaidia ili uone utukufu wa uhakika ambao ubatizo unaonyesha ili kwamba haswa ukweli huu wenyewe utakunasa na pili uzuri na onyesho la kitendo kitainuka mawazoni pia Moyoni mwako. Warumi 5:20-6:4:
Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana, 21. Ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala katika mauti, vivo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hata uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu. 6:1 Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi? 2. Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi 3. Hamkfahamu ya kuwa sisi sotre tuliobatizwa katika Yesu Kristo tulibatizwa katika mauti yake? 4. Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake kusudi Kristo alivyofufukia katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Mojawapo wa umuhimu wa nakala huu ni kwamba unaonyesha iwapo unaelewa kile ubatizo unaonyesha, basi unaelewa kwa uhakika yaliyotendeka ulipofanyika Mkristo. Wengi wetu waliamini na kubatizwa wakati hatukujua mengi. Hii ni vizuri. Inatarajiwa kuwa ubatizo ufanyika mapema katika mwenendo wa Mkristo kama bado hujafahamu mengi. Hivyo inatarajiwa pia kuwa utajifunza baadaye mengi zaidi kuhusu maana yake.
Usifikirie kuwa “Oh, Lazima nirudi nikabatizwe tena. Sikujuwa kwamba ina maana hayo yote.” Hasha. Hiyo itakuwa na maana ya kwamba utakuwa ukibatizwa kila mara kwa kuchukuwa mwelekeo mpya katika masomo ya theolojia. Wewe furahia kuwa umeonyesha imani hiyo yako rahisi katika utiifu kwa Yesu na sasa unajifunza zaidi maana yake. Hii ndiyo Paulo anafanya hapa: anatumaini kuwa wasomaji wake wanafahamu maana ya ubatizo wao. Bado anaendelea na kuwafunza hata hivyo, ikiwa hawajui au wamesahau. Jifunze kutoka kwa maandiko haya yale ulikuwa umeonyesha machoni mwa Mungu, na kilichofanyika ulipofanyika Mkristo.
Nitashughulikia mambo mawili tu ambayo ubatizo huonyesha kulingana na maandiko haya:
1. Ubatizo huonyesha kifo chetu katika kifo cha Kristo.
Mstari wa 3-4a “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Yesu Kristo tulibatizwa katika mauti yake? Hivyo tumezikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika kifo chake,” Pana ukweli mkubwa kwetu Wakristo.Tumekufa Kristo alipokufa alikufa kifo chetu. Hii inamaanisha mambo mawili; 1) Ya kwanza ni kuwa sisi si watu wale wale tuliokuwa mbeleni; utu wetu wa kale umekufa. Hatuko sawa tena. 2) Nyingine ni kwamba kifo ijacho ya mwili haitakuwa na maana sawa kwetu na vile ingelikuwa kama Kristo hangekufa kifo chetu kwa kuwa tumekufa na Kristo, na alikufa kifo chetu kwa ajili yetu, kifo chetu hakitakuwa jambo la kutisha vile ingepaswa kuwa. “Kuko wapi, Ewe mauti kushinda kwako? Uko wapi Ewe mauti uchungu wako?” (I Wakorintho 15:55). Jawabu ni kwamba uchungu na ushindi wa mauti umemezwa na Kristo. Kumbuka kuanzia wiki uliopita: alikunywa tangi. Chunguza kurudiwa kwa neno “ndani ya” katika mstari wa 3 na 4. Kubatizwa “ndani ya Kristo Yesu,” na kubatizwa “ndani ya kifo chake” (mstari wa 3) na ubatizo “Ndani ya kifo” mstari wa 4a. Hii ina maanisha ubatizo huonyesha kuungana kwetu na Kristo yaani tumeunganishwa naye kiroho ili kifo chake kiwe chetu pia uzima wake utakuwa uzima wetu. Je, tunashuhudiaje haya? Utajuaje kama haya yamekutendekea? Jibu ni kwamba inashuhudiwa kupitia kwa imani. Unaweza sikia haya kwa mistari hii ifuatayo. Wagalatia 2:20 inaunganisha na imani: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala sisi tena bali ni Kristo yu hai ndani yangu, na uhai nilio nao sasa katika mwili ninao katika imani ya mwana wa Mungu…” Kwa maneno mengine “mimi” aliyekufa alikuwa wa kale asiyeamini na muasi “mimi”, ilhali “mimi” aliyepata kuwa uhai ni “mimi” ya imani—“Uhai nilionao sasa ninao katika imani ya mwana wa Mungu “Msingi ni kuwa pamoja na Kristo— “Kristo yu hai ndani yangu.” Ninaishi ndani yake—katika umoja wa kiroho naye. Kifo chake ni changu na uzima wake unaishi ndani ya uhai wake.
Ufafanuzi mwingine ni Wakolosai 2:6-7a: “Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana endeni vivyo hivyo katika yeye, wenye shina na wenye kujengwa katika yeye, mmefanywa imara kwa imani.” “Hapa vile vile tunaona kuwa imani ndiyo njia ya kushuhudia umoja na Kristo. Unampokea kuwa Bwana na mwokozi na kwa huo imani umeunganishwa naye na kutembea “ndani yake” na kuimarika “ndani yake.”
Hivyo basi “Warumi 6:3-4a” inaposema tunabatizwa katika kifo chake. Nalichukuwa kumaanisha ubatizo huonyesha imani ambalo kwalo tunashuhudia umoja na Kristo. Huenda ikawa hii ndiyo sababu Mungu alibuni mfumo wa ubatizo kuonyesha mazishi. Ina simamia kifo ambachotunapitia tukiwekwa pamoja na Yesu. Hii ndiyo sababu tunatumbukizwa kama ishara ya kuzikwa.
Sasa muumini, jua kuwa umekufa. “Mimi” ya kale asiyeamini, aliyeasi amesulubiwa na Kristo. Hii ndiyo ubatizo wako ulimaanisha na unamaanisha hata sasa.
2. Ubatizo huonyesha upya wetu katika uzima wa Yesu.
Mstari wa 4: “basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.” Hakuna akaaye chini ya maji ya ubatizo. Tunatoka majini. Baada ya mauti huja uzima mpya. “Mimi” ya kale ya kutoamini na muasi alikufa tulipokuwa pamoja na Kristo kwa njia ya imani. Papo hapo “mimi” ya kale anapokufa “mimi” mpya alipewa uzima—mtu mpya wa kiroho, alifufuka toka kwenye wafu.
Fafanuzi muhimu zaidi ya ukweli huu ni Wakolosai 2:12 Paulo asema ; “Mkazikwa pamoja nye katika huo mkafufuliwa pamoja naye kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu.” Tazama: Tulifufuliwa na Kristo kama vile Warumi 6:4 inasema tunatembea katika upya wa uzima. Na kuna kazi ya Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu kama vile Warumi 6:4 unasema kuwa Kristo alifufuliwa kwa njia ya utukufu wa Baba. Na hi hutendeka kwa imani katika kazi ya Mungu aliyefufua Yesu kutoka kwa wafu.
Basi Wakolosai 2:12 Unaufanya wazi kile Warumi 6:4 unausitiri—kwamba ubatizo huonyesha imani yetu kwa kazi za Mungu ya kumfufua Yesu kutoka kwa wafu. Tunaamini kuwa Kristo yu hai kutoka kaburini na anatawala hata leo kwenye mkono wa kulia wa Baba kule mbinguni na atarudi tena kwa nguvu na utukufu. Na kwamba imani katika kazi ya Mungu—utukufu wa Mungu, kama aitavyo Paulo—ndivyo tunavyoshiriki katika uupya wa uzima ambao Kristo mwenyewe aliko nako.
Kwa kweli, upya wa uzima ni uzima wa imani ndani ya utukufu na kazi ya Mungu. “Nimesulubishwa pamoja na Kristo; Si mimi ninayeishi…bali uhai ninaoishi katika mwili ninaishi kwa imani ndani ya mwana wa Mungu.” Upya wa uzima ni maisha ya kuamini kazi ya Mungu siku kwa siku—utukufu wa Mungu.
Ubatizo huonyesha kinachofanyika kwetu tulipofanyika Wakristo
Basi natuweka kwa ufupi na tutamatishe. Ubatizo huonyesha kilichotutendekea tulipofanyika Wakristo. Haya ndiyo yaliyotutukia: tuliwekwa pamoja na Kristo: Kifo chake kikawa chetu. Tulikufa pamoja naye na papo hapo uzima wake ukawa wetu. Sasa twaishi maisha ya Kristo ndani yetu. Na haya yote hushuhudiwa kupitia imani.
Kuwa mkristo una maana hii—kuishi kwa uhakika wa kile ubatizo wetu unaonyesha: Kila kukicha tunatazamia kutoka kwetu kwa Mungu na kusema: “Kwa sababu ya Kristo mwanao naja kwako. Kwa yeye mimi ni mali yako. Ni ngali nyumbani na wewe. Yeye ndiye tumaini langu la pekee la kukabiliwa nawe. Napokea makubaliano haya kwa upya kila siku. Tumaini langu lina msingi kwa kifo chake kwa ajili yangu na kifo changu ndani yake. Uzima wangu ndani yake ni maisha ya imani kwako, Baba. Kwa sababu yake ninatumaini kazi yako ndani yangu na kwa ajili yangu. Nguvu na utukufu huo huo uliotumia kumfufua kutoka kwa wafu utautumia kunisaidia. Katika ahadi hiyo ya neema ujao naamini, na kwa hiyo ninatumaini. Hiyo ndiyo inafanya maisha yangu kuwa upya. Ewe Kristo, jinsi gani nakutukuza katika kile ubatizo wangu unaonyesha! Asante kwa kufa kifo changu kwa ajili yangu na kunipa uzima mpya. Amina.”