Kutafuta: Furaha! Umepatikana: Kristo!

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
Pcain (Majadiliano | michango)
(Created page with '{{info|Quest: Joy! Found: Christ!}} Blaise Pascal mtu wa asili ya Ufaransa aliyejua hesabu sana aliyekufa mnamo mwaka 1662. Baada ya kumtoroka Mungu hadi alipofikisha umri wa m...')
Badilisho lijalo →

Sahihisho kutoka 20:13, 23 Juni 2017

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Gospel
Topic Index
About this resource
English: Quest: Joy! Found: Christ!

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Gospel

Translation by Desiring God

Blaise Pascal mtu wa asili ya Ufaransa aliyejua hesabu sana aliyekufa mnamo mwaka 1662. Baada ya kumtoroka Mungu hadi alipofikisha umri wa miaka 31, mnamo tarehe 23, Novemba, 1654 saa nne wa nusu usiku, Pascal alikutana na Mungu na kwa ujasiri na bila kutetetema sawa akamgeukia Kristo. Aliandika katika kipande cha kiraka na kuishona katika koti lake pahali ilipatikana baada ya kifo chake miaka minane baadaye. Ilisema,

Mwaka wa neema 1654, Jumatatu 23 Novemba, sherehe ya St. Clement . . . kuanzia karibu saa nne nusu usiku hadi karibu saa sita unusu baada ya usiku wa manane, MOTO. Mungu wa Abrahamu, Isaki na Yakobo, si ya wasomi na wanafalsafa. Yaliyoaminiwa kuwa kweli, furaha kutoka kwa moyo, amani. Mungu wa Yesu Kristo. Mungu wa Yesu Kristo. “Mungu wako na wangu.” . . . Furaha, furaha, furaha, machozi ya furaha. . . . Yesu Kristo. Yesu Kristo. Daima nisitenganishwe naye.

Mwaka wa 1968 Pascal na C. S. Lewis na Jonathan Edwards na Dan Fuller na Biblia waliungana na kubadilisha maisha yangu milele na maneno haya, “Furaha, Furaha, Furaha, machozi ya furaha.” Kijitabu hiki, Kutafuta Furaha, ambacho unacho katika kibeti chako cha ibaada kilizaliwa wakti huo. Haki kuandikwa kwa muda wa miaka 15 ama zaidi. Lakini ilizaliwa wakati huo.

Tazama ndani ya ukurasa wa mbele. Hapa ni ubomoaji wa Pascal dhidi ya uwoga wangu wa furaha.

Watu wote wanatafuta furaha. Hapa pia hajaacha nyuma. Haijalishi ni njia gani wanatumia yote yapata nyuma. Haijalishi ni njia gani wanatumia, yote yapata kufikia hapa. Sababu ya kufanya baadhi kuenda kwa vita, na wengine kukwepa vita, ni hamu sawa katika yote mbili, iliyofanywa kwa mtizamo miwili. Hii ndio nia ya kila kitendo ya kila mwanadamu, hata wale wanaojinyonga.

Nilihisi hii ni kweli. Lakini niliogopa kila mara kuwa ni dhambi. Kuwa kutaka kuwa na furaha ilikuwa kasoro ya dhambi. Kuwa kutaka kuwa na furaha ilikuwa kasoro ya dhambi. Kuwa kutaka kuwa na furaha ilikuwa kasoro ya kimaadili. Hiyo hali ya kujinyima ilimaanisha kukataa furaha, si kukatia furaha kidogo kwa ajili ya furaha kuu zaidi. Si kukataa furaha kidogo kwa ajili ya furaha kuu zaidi. Lakini Mungu aliungana na hawa waandishi kunilazimisha kuusoma Bibilia tena. Kuipatia nafasi kuwa na msemo wake wa kweli. Na yale nilipata hapo kuhusu furaha yalinibadilisha milele. Nimejaribu kuielewa na kuliishi na kulifundisha kutokea hapo. Si jipya. Limekuwa kwa maelfu ya miaka.

Yaliyomo

Yale Bibilia inasema kuhusu furaha

Wacha niwape kionjo kwa yale Bibilia inasema kuhusu furaha.

Lengo la Yesu katika yote aliyoyafundisha ilikuwa furaha ya watu wake.

Yohana 15:11 Nimewaambia mambo haya ili furaha Yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili

Furaha ndio Mungu anatujaza nayo tunapomwamini Kristo.

Warumi 15:13 Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini.

Ufalme wa Mungu ni furaha.

Warumi 14:17 Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa bali ni haki, amani na furaha katika Roho mtakatifu.

Furaha ni tunda la Roho Mtakatify aliye ndani mwetu.

Wagalatia 5:22 Bali tunda la Roho ni upendo, furaha, amani.

Furaha ndio lengo la vitu vyote watume walitenda na kuandika.

2 Wakorintho 1:24 Si kwamba tunatuwala imani yenu, bali twatenda kazi pamoja nanyi kwa ajili ya furaha yenu.

Kuwa mkristo ni kupata furaha ambayo inakufanya kutaka kuachilie vyote.

Mathayo 13:44 “Ufalme wa Mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.”

Furaha unatunzwa na kudumishshwa na neno la Mungu lililomo katika Bibilia.

Zaburi 19:8 Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo.

Furaha itashinda huzuni yote kwa wale wamtumainiyo Kristo.

Zaburi 126:5 Wapendao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. Zaburi 30:5b Inawezekana kilio kikawepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.

Mungu mwenyewe ni furaha.

Zaburi 43:4 Ndipo nitakwenda madhjabahuni pa Mungu, kwa Mungu, furaha yangu. Zaburi 16:11 Umenijulisha njia ya uzima, utanijaza furaha katika uwepo wako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kiume.

Furaha katika Mungu Yashinda furaha yote ya dunia.

Zaburi 4:7 Wewe umejaza moyo wangu kwa furaha kubwa kuliko watu waliopata ngano na divai kwa wingi.

Ikiwa furaha yako imo ndani ya Mungu, hakuna atakaye chukuwa furaha yako.

Yohana 16:22 Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Mungu anaita mataifa yote na watu wote kuungana pamoja katika furaha apeanayo kwa wanaoamini. Hakuna utu ubaguzi wa rangi. Hakuna jumuiko la kikabila.

Zaburi 67:4 Mataifa yote wa furahi na kuimba kwa shangwe. Zaburi 66:1 Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!

Habari yote ya Ukristo kwanzia mwanzo hadi mwisho ni habari njema ya furaha kuu.

Luka 2:10 Lakini malaika akawaambia: “Msiogope. Kwa maana tazama nawaletea habari njema za furaha itakayokuwa kwa watu wote.” Isaya 51:11 wale waliolipiwa faida na BWANA watarudi. Wqataingia sayuni wakiimba, furah ya milele itakuwa taji juu ya vichwa vyao. Furaha na shangwe zitawapata, huzuni na kulia kwa uchungu utatoweka.

Tunapokutana na Kristo wakati wa kuja kwake kwa mara ya pili tunaingia kwenye furaha yake isiyo na utata.

Mathayo 25:23 Bwana wake akajibu, “Umefanya vizuri sana mtumishi mwema na mwaminifu, . . . Njoo ushiriki katika furaha ya bwana wako.”

Yawezekana yaliyonishangaza zaidi katika mwaka wa 1968 ilikuwa rahisi na ya mtazamo wa kawaida kuwa furaha hii katika Mungu inaamrishwa. Unaiona kwenye ukurasa wa pili wa kijitabu:

Zaburi 37:4 Jifurahishe katika BWANA naye takupa haja mooyo wako. Zaburi 33:1 Mwimbieni BWANA kwa furaha, enyi wenye haki. Zaburi 32:11 Shangilieni katika BWANA na mfurahi, enyi wenye haki!

Inaamrishwa kwa sababu yaliyo hatarini sit u furaha yetu lakini utukufu wa Mungu, heshima na sifa ya Mungu. Tusipofurahi ndani ya Mungu—Kama Mungu si hazina yetu na furaha yetu na kutosheka kwetu, basi anakataliwa. Utukufu wake unadunishwa. Sifa zake zinachafuliwa. Basi Mungu anaimarisha furaha yetu yote kwa wema wetu utukufu wake.

Uvumbuzi huu ulimsaidia kuelewa ujumbe wa dhati ya Kristo, ambayo ni injili—habari njema—ya Yesu Kristo. Na hiyo ndiyo kijitabu hiki ndogo, Kutafuta Furaha, imekusudiwa kufanya: kupeana muhktasari ya Injili ya Ukristo na vile inaokoa wenye dhambi na kupeana furaha ya milele.

Ni hatari kujaribu kuweka bahari katika tone la mvua—kujaribu kuweka haki na upendo wa Mungu katika kijitabu. Lakini nadhani si tu hatari, ni upendo, na inafaa. Mungu alifanya wakati mmoja. Aliuweka ukamilifu wake kwa mwanadamu mmoja, Yesu Kristo (Wakolosai 2:9). Hii ilikuwa ya ajabu sana kuliko kuweka bahari katika tone la mvua. Na ilikuwa upendo. Kwa sababu alikuwa mwanadamu na vile vile Mungu angekufa kwa ajili ya dhambi zetu. Lakini wengi haku tambua uungu ndani yake. Na natahadhari wengi wanaweza kosa kuona injili katika kijitabu hiki. Na tahadhari yangu ni kuu kwa sababu mimi si Mungu na sijakosa dosari. Lakini nawapenda na nataka muone yale Mungu amefanya kuwaokoa.

Basi, utaenenda nami kwa kijitabu hiki? Kama wewe si mwamini katika Yesu, jaribu tu kuwa wazi kwa yale Mungu anaweza kudhihirisha kumhusu na kukuhusu, na umuuliza akadhihirishe kwako yaliyo kweli na akulinde kutokana na yasiyokweli. Kam wewe na mwaminiyo, fanya upya yale uliotengeneza maisha yako kwayo, na uwe tayari kushiriki habari iliyo njema zaidi kote ulimwenguni kupitia kijitabu hiki kama Mungu amekuongoza kukitumia. Na Kristo aliyefufuka katika Jumapili hii ya Pasaka na atukuzwe!

Zingatia ukweli mbili ya kwanza kutoka kwa Bibilia kwa pamoja

Ukweli wa Kibibilia #1: Mungu alituumba kwa utukufu wake.

“Walete wana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka mwisho wa dunia . . . niliyemuumba kwa utukufu wangu.” (Isaya 43:6-7)

Ukweli wa kibibilia #2: Kila mwanadamu anafaa kuishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

“Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.” (1 Wakorintho 10:31).

Haya ani karibu sawa, ama sivyo? Tofauti ni gani? Kuna haja gani kuwa na ukurasa mbili badala ya kuyajumlisha kuwa moja? Tofauti hii ni kwmba ukweli #1 unaongea juu ya muundo wa Mungu, na ya #2 inaongea kuhusu jukumu letu. Kuziweka tofauti na katika mpangilio huu inasema kitu muhimu kuhusu ukweli. Tusipousikia, hatutauona injili kama habari yenye thamani. Kifo cha kuhuzunisha ya Kristo kutoonekana tu ni kama kujifanya. Hoja muhimu ni kuwa Mungu ndiye chanzo cha vitu vyote na kipimo cha kila kitu na lengo la kila kitu. Na mbingu na nchi yote ni ya Mungu.

Talitha, mwanangu wa miaka misaba na mimi, tulienda katika matembezi yetu ya Jumamosi jana kule Arby ilioko Lake Street kwa mlo wa mchana. Tulipopiga kona kule Hiawatha kukatokea gari yenye rangi ya buluu mbele yetu, na nikamwambia Talitha: “Sipendi hiyo bandiko.” Hakuweza kuuiona kutoka mhali alipokuwa, hivyo nikamsomea: “Yote ni kwa ajili Yangu.” “Y” ikiwa imeandikwa kwa sarufi kubwa. Hii ndio maana injili ya Yesu ni kigumu kwa watu wengi kiasi ya kutoeleweka kwao. Imepandwa katika maono tofauti ya ukweli. Yote si kwa ajili au sababu yetu. Ni kwa ajili ya Mungu.

Mungu alikusudia tuishi kwa utukufu wake. Hili lote liko katika Bibilia yote. Na hivyo basi ni mwito wetu na uhai na jukumu letu kuishi kwa utukufu wake. Jijaribu: Je upendo wa Mungu kwako unamaanisha kuwa anakufanya uwe kati, ama unamaanisha kuwa anakupa furaha ya milele—kwa gharama kuu kwake mwenyewe—ama kumfanya kiini? Hii ndio uliumbwa kwayo. Hiyo itakuwa furaha yako na utakatifu wake.

Halafu zingatia ukweli mbili za kibibilia ufuatao kwa pamoja.

Ukweli wa kibibilia #3. Wote tumekosa kumpa Mungu vile tunapaswa.

“Sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” (Warumi 3:23)

Ukweli wa kibibilia #4: Sote tuko chini ya hukumu wa haki wa Mungu.

“Mshahara wa dhambi ni mauti . . ." (Warumi 6:23).

Haya pia yaweza kujumumulishwa kwa ukurasa moja yaweza, kama tu yale ya kwanza mbili? Tungfesesma, “ Kwa sababu sisi sote ni wenye dhambi, tunastahili hukumu ya Mungu—Tunastahili kuadhibiwa.” Lakini kitu muhimu kinaweza kupotezwa tukisema hivyo. Kile kitapotezwa ni mkazo katika ukweli #3 klwa dhambi si tu vile na tumetumikia watu, bali vile tumemtumikia Mungu.

Kibandiko ya jumla kingekuwa mbaya hata kama ingemaanisha, “ Dhambi zangu ni juu YANGU.” Mungu ni mbele ya mpangilio yake katika uumbaji. Mungu ndiye chanzo ya jukumu letru kama viumbe. Na Mungu ndiye chanzo kwa kile kinamaanisha kuwa wenye dhambi: Inamaanisha, vile Warumi 3:23 inasema, kupungukiwa na utukufu wa Mungu, ni kusema, kupendelea na kufarahi baadhi ya ukuu nyingine za Ukuu wa Mungu. Dhambi kwa kabisa ni kuhusu vile tunamtumikia Mungu, si watu wengine.

Hatutapata chochote katika uwoga wa kuzimu ama msalaba wa Kristo uliojawa damu kama hatutahisi uzito wa dhambi kama kero kwa Mungu. Dhambi si tu mwanadamu kumtusi mwenzake. Sana sana ni mwanadamu kumtusi Mungu. Hii ndio maudhui makuu katika mbingu na dunia. Lazima tuhisi hii kama hukumu mbaya ya ukweli #4 hautaonekana kama haki.

Sote tumemtumikia Mungu kwa dharau, na ghadhabu yake inatujia. Hiyo ndiyo shida yetu kubwa zaidi. Kuibwa kuyliko uchumi. Kubwa kuliko uhusiano wa kitaifa na Iraki ama Korea Kaskazini kubwa kuliko oshida katika njdoa ama saratani chungu. Hii ndio injili ya Wakristo inafaa kutibu kwanza na zaidi. Tunaweza kuokolewaje kutoka kwa hukumu ya Mungu? Kuna madhara mengi pzaidi ya ajabu ya injili! Lakini hii ni muhimu na mengine ni juu yake.

Sasa injili. Hebu tutazame ukweli mawili ya mwisho za Biblia.

Ukweli wa kibibilia #5: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee Yesu kupeana uzima wa milele na furaha.

“Msemo huu ni wa kweli na unaopstahili kukubalika: Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi . . . ” (1 Timotheo 1:15).

Ukweli wa kibibilia #6: Faida iliyonunuliwa na kifo cha Kristo ni kwa wale wanaotubu na kumwamini.

“Tubuni basi mkamgeukie Mungu, ili dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwepo kwake Bwana” (Matendo ya Mitume 3:19). “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka” (Matendo ya Mitume 16:31).

Na tena tunaweza kuunamanisha hizi ukurasa hizi mbili. Tungesema: Ni nini dawa ya dhambi na hatia na hukumu? Jibu: “Mwamini Bwana Yesu Kristo, nawe utaokoka.” Lakini hilo litakuwa jibu lisilo kamili! Kama unazama, dawa si tu kupiga mayowe ili usaidiwe; ni waokoaji wa maisha na laini za waokoaji ( kama yahitajika) chombo cha kupumua. Kelele ya kuitosha usaidizi ina kuunganisha na kazi ya kuokolewa. Kama unakuwa na ugonjwa wa moyo, kupiga kwako siku kwa nambari 911 si dawa yako kuu. Ni ambualansi na matabibu wanaotumia ndege na CPR na wanguzi na wapasuaji na madawa. Simu kwa 911 ni kunganisho kwa kazi ya kuokoa.

Hivyo ndivyo iilivyo kwa kuungama dhambi zako na kumwamini Yesu (Ukweli #6). Hiyo ni kiunganishi; chako na kazi ya kuokoa katika Kristo. Kristo alitenda kitu ili atuokoe miaka 2000 iliyopita. Alikuja, akaishi maisha kamili kama Mwana wa Mungu. Na alikufa kwa ajili ya wote watakaomwamini. 1 Petero 3:18, “Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki, kwa ajili ya wasio na haki ili awalete ninyi kwa Mungu.” Imani yetu sio chanzo cha wokovu wetu. Inatuunganisha na chanzo cha wokovu wetu. Kristo ndiye chanzo cha wokovu wetu.

Kifo na kuhukumiwa kwake kwa ajili ya hukumu wetu; haki yake kamili kwa ajili ya dhambi zetu na kutokamilika kwetu. Na kufufuka kwake kudhibitisha na kuhakikisha wokovu wetu na furaha yetu milele na milele. Bibilia inasema, “Tena kama Kristo hajafufuka, imani yenu ni batili, nanyi bado mko katika dhambi zenu . . . Lakini kweli" Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala! (1 Wakorintho 15:17, 20) Kwa sababu alikufa kwa ajili yetu na kufufuka tena, wote wanaomwamini wana uzima wa milele na furaha unaozidi kuongezeka mwanuni na maisha yako.

Mwamini na ndoa yako ama ukapera wako. Mwamini na biashara yako na hali yako ya kifedha. Mwamini na afya ayako. Na chini ya yote, mwamini na dhambi zako na hatia zako na uwoga wako. Tayari ameshughulikia kuokoa. Imekwisha. Amekufa na kufufuka. Na wokovu wake waweza kuwa waovu kwa kumwamini. Na kama itakuwa, basi itakuja kutimiliza kwa nini uliumbwa: Na kama itakuwa, basi itakuja kutimiliza kwa nini uliumbwa: Utukufu pwa Mungu uliodhihirishwa katika furaha yako milele.