Mambo makuu kutoka kwa neno lako
Kutoka Gospel Translations Swahili
(Created page with '{{info|Wonderful Things from Your Word}}<br> <blockquote> '''Zaburi 119:18'''<br><br>Unifumbue macho nitazame maajabu yatokayo katika sheria yako. </blockquote> ==== Haja yetu k...')
Badilisho lijalo →
Sahihisho kutoka 16:01, 21 Julai 2011
By John Piper
About The Bible
Part of the series Praying from the Fullness of the Word
Translation by Desiring God
Zaburi 119:18
Unifumbue macho nitazame maajabu yatokayo katika sheria yako.
Yaliyomo |
Haja yetu kuu kwa angazio yaMungu
Kuna mambo muhimu ambayo tuliyaona kwenye msati huu wiki iliyopita: 1) Kuna mambo ya ajabu katika neno la Mungu 2) Hakuna mtu yeyote anayeweza kuyaona maajabu haya jinsi walivyo bila usaidizi wa Kiungu 3) kwa hivyo ni lazima tumuombe Mungu atupe angavu la Kiungu tunaposoma Biblia.
Hivyo, imizo la wiki jana ilikuwa maombi na mahitaji yetu dhati kwa Mungu kutuangazia mambo ya kiroho kwa njia ya Kiungu-ili kuona utukufu na urembo vile vile ubora wa Mungu. Waaweza kuona mengi ukija kwenye Neno bila kufungiliwa macho ya moyo wako na Mungu. Unaweza kuona neno na muundo wa kisarufi. Waweza kuona uunganifu wa kimantiki. Waweza kuona ukweli wa historia. Unaweza kuona ukakamavu wa nia ya mwandishi. Unaweza kuona hisia ya kibinadamu. Hakuna, hata moja kati haya yahitaji Mungu kufumbua macho yako Kiungu kwa njia ya kipekee.
Kile huwezi kuona ni urembo wa kiroho wa Mungu na Mwanawe pamoja na kazi zao duniani. Huwezi kuona kwamba Mungu hutamatika kwa njia kubwa juu ya kila kitu. Kipofu hawezi kuona gimba na nuru yake, ingawa anaweza kuwa na hoja tele kuhusu jua na kupita mtihani wa unajimu kwa alama ya juu kuliko mtu ambaye anaweza kuona jua. Kujua kuhusu na kwa kuona hakulandani. Kujua kwamba asali ni tamu na kuonja haifanani.
Wacha nisome tena ufafanuzi kikamilifu ya Paulo kuhusu hali zetu baadala ya umaalum, uhifadhi na angavu ya Mungu. Kwenye Waefeso 4:17b-18 Paulo anataja mambo na hulka ya binadamu na hali yanayoweza halisisha muingiliano wa Kiungu ikiwa twahitaji ukweli wa kiroho. Anasema mtaifa (kwa njia nyingine watu wa kawaida wa ulimwengu miongoni mwa mataifa mbali na neema) huishi “ikiwa akili zao zimetiwa giza na ubatili wa nia zao, wamefarikishwa na uzima wa Mungu kwa sababu ya ugumu wa nyoyo zao: tukisoma tukirudi nyuma tunaweza sema kwamba kuna hali hii kwetu sote isipokuwa tu neema kuu ya Mungu, ugumu wa moyo ambao waleta ujinga ambao waleta utengano kutoka kwa Mungu ambao waleta giza ambao waleta ubatili wa ufahamu na maisha.
Sasa hoja ya wiki iliyopita ulikuwa: kama kuna matumaini kwetu kuona maajabu na makuu katika neno la Mungu, ni sharti tuwe na uwezo wa kiroho wa kiungu ambazo twapewa na Mungu ambazo hatuna kimaumbile, “Fumbua macho yangu.” Na kama tunaweza kuwa hai kwa Mungu na kuwa hakika, bayana na shupavu kwa upendo wetu kwake, lazima tuwe na tamaa kubwa ya kuwa uwezo huu kila siku. Sasa omba, omba, omba. Soma Zaburi 119 na uone mara ngapi aliomba ili kuwa na uwezo wa kiungu kumjua Mungu na njia zake.
Kutazamia ndiyo kuwa
Lakini leo tuna hoja tofauti ya kutenda. Lakini kabla sijasema nini, wacha ni hakikishe mme elewa sababu gani hii ni muhimu. Ni muhimu kwa sababu kwa kubadilishwa kwa sura ya Kristo hutendeka kwa kuona uruzi na umuhimu na ubora wa Mungu na mwanawe na maneno yao pamoja na njia zao. Katika 2 Wakorintho 3:18 Paulo anasema, "Lakini sisi sote kwa, uso usiotiwa utaji, tuliurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho." Kutazama ni kuona.
Hii ndiyo njia ya pekee ya kikristo ya kuibadilisha hulka ili tuweze heshimu mungu. Tunabadilika kwa sababu tumeuona urembo wa hali ya juu na ustahilifu pamoja na azizi. Ukiuangalia kwenye uso wa kristo na utazame sehemu zilizoelezwa au zilizojadiliwa kwa mvuto lakini si kwa kunatwa na hali ya juu ya urembo na ustahilifu na aula na utamanifu ndani ya kristo, basi bado wewe ni ngumu na kipofu vilevile chini kwa fikira zako. Unahitajika kupiga kamsa “ Fumbua macho yangu ili ni yaone maajabu ndani ya neno lako” na bila shaka maisha yako yaonyesha. Mahali pana haina yako ni tamaa zako, furaha yako, urembo wako—hapo ndipo mtima wako upo—na magharibi na jumamosi na vile vile pesa zako. Tunabadilishwa kwa kuona utukufu wa Mungu katika neno lake. Kama Mungu si wa utukufu sana kwako na hulazimiki sana kuliko utukufu na tamaa ya dunia basi hujamuona. 3 Yohana 11 inasema, “yeyote atendaye dhambi hajamuona Mungu” (tazama pia 1 Yohana 3:6).
Sasa haya yote ni muhimu kwa sababu ukweli wote unaobadilisha maisha kumheshimu Mungu na kuna umuhimu wa kiroho huja kwa kuona utukufu wa Mungu, si kwa kutegemea orodha ya kidini ya matendo mazuri na kuyaiga hayo.
Mungu hufunua urembo wa Kristo kupitia neno lake
Leo hoja kutoka kwa somo hili ni: Mungu huonyesha urembo na azizi ya Kristo kwa wale tu wanaotafuta katika neno lake. Hii ndiyo sababu mabadiliko ya kweli ya kiroho huja kwa kusoma neno lake, kutafakari na kukariri maandiko za Bibilia. Si kwa sababu unajifunza sheria ya kutii. Ni kwa sababu hapo ndipo Mungu hufunua urembo na azizi ya Kristo.
Wacha tuweke hoja ya makali hapa: kama uliusiya ujumbe wa wiki iliyopita kwamba lazima tuone utukufu wa Mungu ili tubadilishwe, lakini hatuwezi kuiona kwa sababu ya umauti, ugumu na upofu, na ni kwamba lazima tumuombe mungu atuweke hai, na kutulainisha na kufumbua macho yetu. Na ukiwa unatamatisha kuwa: Sawa ndiyo ni sharti nijitolee kwa maombi lakini si kujifunza au kusoma na kukariri Bibilia kwa sababu ya mwanadamu tu kutoa sababu na kuona kamwe hawezi kuyaona yapasayo kuyaona. Hiyo inaweza kuwa kauli hatari kutoa kwenye kile nilichosema na kwa fumo hili.
Hoja ni kwamba. Mungu hufumbua macho ya vipofu ili kuiona utukufu wa Mungu katika neno lake walipolidurusu. Kwa mfano ukihitaji kuiona utukufu wa (Grand Canyon) walakini u kipofu, na kwa mfano Mungu akikuambia, niite na uje umuombe na nitakufumbua macho ili uone utukufu wa (Grand Canyon). Je! ungetoka Arizona hadi Florida kuomba? Au Je? ungetumia kila misuli na hisia Mungu amekupa ili ufikikie (Grand Canyon) na utayarishe macho yako kwa yale Mungu ameahidi? Changu muhimu ni kwamba hatakuonyesha utukufu wa (Grand Canyon) kama umesisitiza kuishi kwa Everglades, haumanishi uombe kiasi gani.
Wacha niseme kwa njia nyingine: Mungu ameweka wakfu kwamba kazi yake ya Roho ya kufumbua macho siku zote imeunganishwa na kazi ya kuelimisha akili ndani ya neno lake. Nia yake ni kwamba tuweze kuona utukufu wake Mwanawe(ili tubadilike). Sasa hufumbua macho yetu kama tunamtafuta Mwanawe, bali si kwa mauzo au viwandani. Kazi ya Roho na kazi ya neno huandamana pamoja katika njia ya Mungu ya ufunuo wa kibinafsi ya kiroho. Kazi ya Roho ni kuonyesha utukufu na urembo na thamani ya kile fikira huona kwa neno.
Hatuhitajiki tu kukosea kwa kufikiri kwamba tunachohitaji kutoka kwa Mungu ujumbe mpya. Tayari tumesikia ujumbe wa Mungu kwenye Biblia mara elfu kuliko vile tunavyoweza kukadiria kufurahia. Tunachokihitaji ni kuona kwa macho ya nyoyo zetu! Ujumbe wa Roho wowote tunaoweza kuongezea kwa kile tunaweza kuona kwenye Kristo ndani ya neno kufanya tuinuke 1/16 ya pauni au kupendeza Mungu.
Ikiwa Roho amekufunulia kwamba rafiki yako aliyetasa huenda akapata mimba. Na umwambie hivyo, iwapo itatendeka, nyinyi wawili mtapeperushwa kwa furaha kuhusu miujiza ya kinabii na ujauzito. Je! Umefaidika vipi Kiroho? Hakuna, mpaka tu ulirudie neno na uone-kwa macho ya moyo-utukufu na urembo wa Kristo uliodhihishwa kwenye Biblia.
Yesu mnazareti, aliyesulubishwa atafufuka ili kuwaokoa wenye dhambi na kumtukuza Mungu ambaye pia amekubariki. Furaha ya kidini kwa kuwepo kwa miujiza ni jambo la kimwili na haina umuhimu kiroho au katika hali ya Kiungu. Vipawa vya Roho ni vya thamani, lakini cha muhimu kisicho na kikomo ni ufumbuzi wa macho angavu katika Roho ili tuweze kuona utukufu wa Kristo ndani ya neno.
Si kwamba twahitaji habari mpya: ni tu macho mapya kuyaona yaliyofunuliwa kwetu katika neno la Mungu. Fumbua macho yangu ili niweze kuyaona maajabu katika neno lako!
Usiombe na upeperushwe
Wacha ni waeleze badhi ya vidokezo vilyomo hapa:
Kwanza unapoomba ili macho yako yafumbuke, ni sharti usiweke katika hisia au fikira. Usidhani ya kuwa uwezekano wa maombi humaanisha uwezekano wa kulenga mawazo kwenye neno la Mungu. Ukiomba kuona utukufu wa Kristo, usipeperuke au kusongezwa kwa urahisi kimawazo. Usingoje bila kusanya lolote. Hili ni kosa kubwa na huchipuka kutoka kwa uroho wa mashariki si kwenye Biblia. Jambo maalum kuhusu ukristo ni kwamba historia na kipekee. Yesu aliishi kwa nyakati na mahali. Mapenzi ya Mungu ni kufumbua macho yako ili yaone urembo wa kiroho na thamani ya mtu huyu kama vile alivyofunuliwa kwenye neno. Kama twaomba ili kuona lakini kifikira tunapeperushwa mbali nayo, kamwe hatuwezi kuyaona. Sasa basi usiombe na upeperushwe.
Nini basi?
1. Omba na usome
Soma neno, kibali tosha! Jukumu tosha! Uwezo tosha wa kumuona Mungu! Tazama Waefeso 3:3b-4. Paulo anaandika, “Kwa ufunuo nalijulishwa siri hiyo kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa kutazama haya muyasomapo mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo.” Ukisoma! Nia ya Mungu ni kwamba maajabu makuu ya maisha yafunuliwe katika kusoma.
Sasa lingalisha fungu la 1:18 mahali Paulo anasema, “Naomba ili macho ya mioyo yenu yatiwe nuru mjue tumaini la mwito wake jinsi ilivyo.” Sasa Waefeso 3:4 unasema kwamba maajabu hutambulika kwa kusoma. Na Waefeso 1:18 inasema kwamba, ili tuyajue yanayotupasa kuyajua. Mungu sharti afumbue macho yetu kwa kujibu maombi. Ndiyo sharti tuombe ndio tuvipofu bila usaidizi wa Mungu. Cha muhimu wiki hii ni kwamba lazima tuombe.
“Unaposoma, unaweza kufahamu siri yangu kwa maajabu ya Kristo.” Maombi hayawezi kubadilisha kusoma. Maombi yaweza kupindua kusoma kuwe kuona. Roho Mtakatifu alitumwa ili kumtukuza Kristo na utukufu wa Kristo hudhihirishwa kwa neno. Soma. Furahia kuwa una uwezo wa kusoma
2. Omba na utafakari (Taamuli)
2 Timotheo 2:15 “Jitahidi (ama: “soma” KJV) kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.” Mungu alitupa kitabu yeye mwenyewe, si kwamba tukisome kwa njia yoyote ya kutojali vile tu tunavyopenda. Paulo anasema “ Jitahidi kujionyesha . . . ukitumia kwa halali neno la kweli." Ina maana kwamba tenda kazi kwa neno kama wahitaji zaidi kwalo.
Mizani-uzi huning’inia mbele na nyuma. Wengine husema omba tena omba lakini usitegemee kisicho cha kiroho kazi ya mwanadamu wa kujifunza. Wengine pia wasema tafakari na utafakari kwani Mungu huenda hata kupa maana ya neno katika maombi. Lakini Biblia haina uhusiano wowote na mgawanyiko huu. Lazima tu durusu na tutumie neno la Mungu kihalali na lazima tuombe la sivyo hatutaona katika neno kitu kimoja cha muhimu, utukufu wa Mungu penye wajihi [uso] wa Kristo (2 Wakorintho 4:4, 6).
Benjamin Warfield, mdurusu mkuu wa Biblia aliandika mwaka wa 1911, “Wakati fulani twasikia kwamba dakika kumi magotini pako utakupa ukweli, undani, utekelezaji zaidi wa ufahamu wa Mungu kuliko saa kumi kwenye vitabu vyako. ‘Nini!’ ndio jibu mwafaka, ‘Kuliko saa kumi kwenye vitabu, magotini pako?’” ("The Religious Life of Theological Students," katika Mark Noll, ed., The Princeton Theology, [Grand Rapids: Baker Book House, 1983], p. 263). Hii inanasa kusudi la Kibibilia. Ndiyo, lazima tuombe. Hatutaona maajabu kutoka kwa na neno la Mungu kama hata yafumbua macho yetu. Lakini kuomba hakuwezi kubadili masomo, maanake Paulo anasema, “Jitahidi—soma—ili utumia neno kihalali.”
3. Omba na utafute
Mbinu yetu ya Biblia yafaa iwe kama bahili katika harakati za kung’ang’ania dhahabu au kama mposwa aliyepoteza pete ya posa, kwenye nyumba. Atatafuta nyumba vilivyo. Hivyo ndivyo twamtafuta Mungu katika Biblia.
Mithali 2:1-6 inasema,
Mwanangu, kama ukiyakabili maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu.2 hata akatega sikio lako kusikia hekima, ukauelekeza moyo wako upate kufahamu. 3 Naam ukiita busara, na kupasa sauti yako upate kufahamu 4 ukitafuta kama fedha na kuutafutiakama hazina hazina iliyositirika. 5 Ndipo utakapofahamu kumcha Bwana na kupata kumjua Mungu.6 Kwa kuwa Bwana huwapa watu hekima, kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
Pokea, hifadhi, tega sikio, elekeza moyo wako, ita kwa kupasa sauti, tafuta fedha, tafutia kama hazina iliyositirika, uikabili. Kama kuna fedha ikabili. Kwa vyovyote vile omba (kama ilivyo kwa mstari wa tatu) walakini usiyabadili maombi na kutafuta. Mungu amekusudia kuwapa wanaomtafuta kwa mioyo yao yote (Yeremia 29:13).
4. Omba na ufikiri
Yafahamu (2 Timotheo 2:7) “Yafahamu sana hayo nisemayo kwa maana Bwana atakupa akili katika mambo yote.” Kwa uhakika ni “Fikiria kuhusu (noei) ninayoyasema.” Je! Ina maana kwamba kuelewa mafundisho ya Paulo ni kwa urahi tu kibinadamu, shughuli ya kifikira tu? Hapana. Mwisho wa mstari unasema, “Mungu atakupa ufahamu.” Si wewe uwezaye kuona kibinafsi. Utambulishaji wa kiroho ni kipaji toka kwa Mungu.
Lakini Mungu amekusudia kutupa kipaji cha mwangaza wa Kiungu kupitia fikira. “Fikiria kile nisemacho kwa kuwa Bwana atakupa akili kwa mambo yote.” Sasa kwa njia zote omba na umwulize Mungu akupe nuru unayohitaji. Lakini usibadilishe kufikiri na kuomba. Fikiri na uombe. Omba na ufikiri. Hivi ndivyo Mungu ameidhamiria. Kristo wa historia. Kitabu cha uhifadhi na ufunuo. Yote hayo yasema, “soma ujifunze na utafute na ufikiri. Yote ni bure bila maombi. Zote—pamoja, si aidha—au.
5. Omba na uongee
Mungu anakusudia neno lililoandikwa ili liwe neno la kimatamshi kwa kuhubiri na kuwajenga na kuwafajiri na kuwatia moyo, kuwakanya na kuwarudia na kuwashauri watu wake. Wakolosai 3:16 inasema, “Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yetu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi na nyimbo, na tenzi za rohoni huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu . . . ” Neno la Kristo kwetu likawa neno la kila mmoja wetu.
Mimi nalihubiri. Hii ni mapenzi ya Mungu ili neno lake litangazwe upya mara kwa mara. Vile vile nanyi museme na wengine neno la Mungu. Hii ni mojawapo wa sababu za kimsingi kwa vikundi vidogo kanisani—kulifanya neno la Mungu kwetu kuwa Neno la Mungu kupitia kwetu sisi. Semeni miongoni mwenu.
Je! hii inamaanisha tunaweza kutupilia mbali maombi nyakati hizo—ya kwamba tunaweza kufumbua macho ya kiroho kuona maajabu kutoka kwa neno la Mungu kwa sababu tunalinena kwa kutuhukumu na kutushawishi kwa majibizano au ubunifu wa zamu ya fani au semi? Hii siyo kile Paulo anafundisha. Kwa kitabu hicho hicho (Wakolosai 1:9-10) anaomba—anaomba!— “Hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote . . . kuendelea kwa ufahamu wa Mungu.”
Kama kumjua Mungu na kuwa na hekima ya kiroho na ufahamu ungepatikana moja kwa moja kama neno la Kristo ladumu ndani yetu kwa wingi, basi Paulo asingependa au kuhitaji kuomba bila kukoma ili Mungu atupatie haya.
Neno na maombi pamoja
Sasa tumeona mara nyingi: maombi hayatenganishwi kama tungeona au twataka kuona utukufu wa Mungu katika neno. Vilevile tumeona kwamba kusoma na kudurusu pia kutafuta na kutafakari na kuongea neno ni muhimu pia. Mungu amekusudia kwamba kazi ya ufumbuaji wa macho na Roho wake siku zote iunganishwe na kazi ya ukuzaji wa akili wa neno lake. Nia yake ni kwamba tuone utukufu wa Mungu na pia tumulike utukufu wa Mungu. Hivyo yeye hufumbua macho yetu tunapotafuta utukufu wa Mungu katika neno lake.
Soma, durusu, tafuta, fikiria, nena, sikiza-na uombe, “Fumbua macho yangu ili niyaone mambo maajabu kutokana na neno lako.”
Kwa kumbukumbu zaidi, tazama Luka 24:45; Matendo ya Mitume 16:14; 2 Wafalme 6:17; Mathayo 16:17; 11: 2-6; 11:27.