Tianeni moyo mmoja kwa mwingine katika Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
Pcain (Majadiliano | michango)
(Created page with '{{info|Strengthen Each Other's Hands in God}}<br> <blockquote> '''1 Samweli 23:15-18'''<br><br>Daudi alipokuwa huko Horeshi katika jangwa la Zifu, akajua kuwa Sauli alikuwa amek...')
Badilisho lijalo →

Sahihisho kutoka 17:25, 8 Agosti 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Small Groups
Topic Index
About this resource
English: Strengthen Each Other's Hands in God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Small Groups

Translation by Desiring God


1 Samweli 23:15-18

Daudi alipokuwa huko Horeshi katika jangwa la Zifu, akajua kuwa Sauli alikuwa amekuja ili amwue. Naye Yonathani mwana wa Sauli akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani kwa Mungu. Akamwambia, “Usiogope Daudi, baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, nami nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.” Wote wawili wakaweka agano mbele za Bwana. Kisha Yonathani akaenda zake nyumbani, lakini Daudi akabaki Horeshi.

Ujumbe wa leo ni sitisho la msururu tuliouanzisha jumapili uliopita kutoka kwa Waefeso. Sababu ya kuisitisha ni shauku kuu tulio nayo ya haja ya kutia moyo washiriki wote wa Bethlehemu wawe katika makundi madogo madogo ya kusaidiana kupiga vita vya imani. Na mtazamo wetu leo ni kutiana mikono mmoja kwa mwingine kwa Mungu.

Ulinzi wa milele ni mradi wa kijamii

Tunaamini kwamba ulinzi wa milele ni mradi wa kijamii. Tunaamini kuwa uvumilivu wa watakatifu ni jukumu la kipamoja. Bwana huyu wa upendo ambaye alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti Yangu nami nawajua, nao hunifuata, nami nitawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka katika mikono Yangu” (Yohana 10:27-28), pia alisema, “Lakini Yule atakayevumilia hadi mwisho ndiye atakayeokoka” (Mathayo 24:13).

Kwa maneno mengine, wale waliozaliwa katika Bwana wana ulinzi wa milele mikononi mwa Yesu. Na wale wamezaliwa katika Bwana lazima wavumilie hadi mwisho katika imani ndipo wapate kuokolewa. Swali linatokea: Ni vipi Mungu amekusudia kufanya watu wake kuvumilia katika imani hadi mwisho ndipo bila kuanguka atimilize ahadi ya kuwa wamelindwa na hakuna atakayepotea?

Asubuhi hii tutaangazia pande mmoja muhimu la jibu la swali hilo: nalo ni, Mungu amekusudia kuwa tuunganike na waumini wengine kwa kiasi kuwa tunaweza kusaidiana kwa pamoja kupiga vita vya imani kwa ushindi kila siku hadi mwisho. Msingi wa Kibiblia la jibu hili ni Waebrania 3:12-14.

Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai. Lakini mtianeni moyo kila siku mtu na mwenzake, maadam iitwapo ‘leo’, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa udhabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho.

Mungu amechagua njia ya kutufanya kushikamana udhabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho. Ni hili: tutengeneze aina ya uhusiano ya Kikristo ambayo kwayo tunaweza kushikamana moja kwa mwingine kwa nguvu katika ahadi za Mungu na kukwepa udanganyifu wa dhambi. Tianeni moyo kila siku mtu na mwenzake ndipo mupate kusimama imara na mvaeni gamba lote laMungu.

Uwe mmoja katika kikundi cha Wakristo

Watoto, vijana wadogo wa shule ya upili, vijana waliokomaa wa shule ya upili, wanafunzi wa vyuo, wale hawajafunga ndoa, wale wamefunga ndoa, wajane, wanaume waliofiliwa! Je ninyi ni mojawapo katika vikundi vya marafiki wa Wakristo ambao wameapa kusaidiana kupiga vita vya imani na kujilinda kwa kuingiliwa na dhambi?

Sisemi kuwa huwezi ukaokoka bila kuwa katika vikundi hivi vidogo. Lakini yale ninasema, na ninayaamini kuwa ni neno la Mungu, ni kuwa kama huna kikundi cha marafiki kama hao katika imani, basi unapuzilia njia moja ambao imetengwa na Mungu ya kukuhifadhi na kudumisha katika imani. Na kupuzilia njia ya imani ni hatari sana kwa nafsi yako.

Basi lengo langu asubuhi hii ni rahisi sana: ni kukuhimiza uwe katika kikundi cha Wakristo pahali unaweza kutiwa moyo na pia kutia wengine moyo ili kupigana vita vya imani kila siku. Mwishoni mwa ujumbe Peter Nelson kwa ufupi atafundisha juu ya mtandao moja ya vikundi vidogo vinavyopatikana kwa ajili ya maombi yenu.

Mafunzo manne kutoka kwa mkutano Yonathani na Daudi

Neno ni 1 Samueli 23:15-18. Ni rahisi na ni picha ya yale yanayofaa yatendeke katika vita unaoendelea ya imani.

Daudi anayumba yumba kutoka eneo moja hadi lingine katika jangwa la Zif ambalo ni takriban maili 30 kusini mwa Yerusalemu, akijaribu kukwepa Sauli. Sauli, mfalme wa Israeli, anataka kumwua Daudi kwa sababu anadhani Daudi ni hasimu hatari kwa kiti chake cha ufalme. Yonathani, mwana wa Sauli, anampenda Daudi na anasikia kuwa yuko katika jangwa la Zif, na anaenda kumtia moyo kwa Mungu.

Mkutano kati ya Yonathani na Daudi unaonyesha mafunzo manne juu ya kusaidiana katika kupiga vita vya imani.

1. Hitaji ya kila mtu ya kuwa na mazungumzo ya kirafiki ya Kikristo

Watakatifu wakuu zaidi na viongozi wenye nguvu zaidi wanahitaji marafiki Wakristo ya kuwatia moyo katika Mungu. Daudi alikuwa wa ndani, Daudi alikuwa mwenye nguvu, na Daudi alihitaji Yonathani.

Mkristo wa kuongea naye kirafiki sio tu kwa wale wanaojiunga. Ni kwa kila muumini. Hatuachi kuwa na hitaji ya huduma ya Wakristo wengine. Kama unadhani kuwa huna hitaji ya kutiwa moyo kila siku katika vita vya imani, basi inawezekana kuwa moyo wako umeandamwa na uwongo za dhambi.

Daudi alikuwa mtu ambaye ailkuwa akitafuta kujua moyo wa Mungu. Alikuwa mpiga vita hodari. Bila tashwishi alikuwa ameshinda Yonathani kwa nguvu na maarifa na ufahamu wa ndani ya neno la Mungu. Lakini mstari 16 inasema kwamba Yonathani alienda na akamtia moyo kwa Mungu.

Usidhani kuwa mtu ni mwenye nguvu sana kwa kiasi kwamba haitaji kutiwa moyo katika Mungu. Na usidhani kwamba mtu fulani yuko mbele sana kwa kiasi kwamba huwezi kuwa chombo cha Mungu cha kumtia nguvu.

Charles Spurgeon aliongelesha Viongozi wengi Wakristo alipoandika,

Miaka mingi iliopita, nilipigwa na mshtuko wa kiroho. Matukio mbali mbali ya shida yalikuwa yamenitukia; tena nilikuwa mgonjwa, na moyo wangu ukavujika ndani yangu. Ndani ya matukio haya yote nililazimika kumlilia Bwana. Kabla tu niende Mentone kwa mapumziko, niliteseka sana mwilini, na zaidi moyoni, kwa sababu roho yangu ilikuwa imeshindwa. Katika misukumo hii, nilihubiri mahubiri kutoka kwa maneno, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?” Nilikuwa nimehitimu kufundisha kutoka hilo neno vile ninavyotarajia; hakika, natarajia kuwa wandugu wachache wameingia kwa undani sana katika maneno hayo yanayovunja moyo. Nilihisi kutoka kilindini hofu ya moyo ulioachwa na Mungu. Halikuwa tukio la kutamanika. Natetemeka na kubeba hisia ya kupitia katika hali ya kusitirika kwa moyo; naomba ili nisiteseke katika njia kama hiyo. (Autobiography, vol. 2, p. 415)

Nataja hili ili nisisitize kwamba watakatifu wakuu, wapiga vita wenye tajiriba kuu, hawako juu ya hitaji ya kutiwa moyo kwa Mungu, yamkini uvamizi wa shetani juu yao inaweza kufanya hitaji lao liwe kuu zaidi. Basi funzo la kwanza kutoka kwa andiko letu ni kwamba huwezi kuwa juu kwa kiasi ya kutohitaji kutiwa moyo. Mtakatifu wa ndani zaidi na kiongozi mwenye nguvu zaidi anahitaji marafiki wa kumtia moyo kwa Mungu.

2. Jitihada ya dharura

Funzo la pili ni kuwa kutiwa moyo kwa mtu katika Mungu unahitaji jitihada ya dharura.

Ni la kusudi. Hulifanyi tu kwa hewa, unainuka na kuenda Horeshi. Mstari wa 16: “Naye Yonathani mwana wa Sauli akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani kwa Mungu.”

Ni tofauti gani inaweza leta katika kanisa letu ikiwa, sisi sote tukiamka asubuhi, na TUPANGE kutia moyo mtu mwingine kusimama imara katika imani kwa Mungu! Yonathani hakukutana na Daudi kwa ajali katika Horeshi (ingawa mara nyingine hufanyika!) ALIPANGA kwenda kumtia moyo. Alama ya ukomavu wa Mkristo ni kuwa unajenga katika maisha yako nia na wakati ya kutia wengine moyo kwa Mungu. Ni kina nani utawatia moyo kwa Mungu leo? Wiki hii? Je uko na kikundi cha marafiki walio na nia (kimakusudi!) kusaidiana kupiga vita vya imani kwa njia hii?

Nimekuwa nikisoma Kitabu cha matukio cha Samuel Pearce, mojawapo ya vikundi vidogo vya wachungaji kilichoanzishwa na Jumuiya ya kwanza Ya Wamishonari wa Kanisa la Ubatizo katika mwaka wa 1792. Wengine kati yao walikuwa John Ryland na John Sutcliff na Andrew Fuller na Samuel Pearce na William Carey. Jambo moja limedhihirika zaidi ya mengine hivi karibuni: hawa watu walikuwa wamependana na walikutana pamoja na walikuwa wanahakikisha kuwa wanatiana moyo moja kwa mwingine kwa Mungu. Walifanya hili hata wakati walikuwa mbali na wenzao.

Samuel Pearce alioongoja barua yake kutoka kwa Carey kwa zaidi ya mwaka moja baada ya kutoka India. Lakini ilipofika, hivi ndivyo alivyomwandikia Carey,

Mtazamo uliotupatia ulituinua katika nguvu mpya, na ulitutitia moyo katika Bwana. Tulisoma, na kulia, na kuomba, Lo, ni nani kama si Mkristo ambaye anahisi misisimuko kama hii ambao imeunganika na urafiki wa Bwana wetu mpendwa Yesu Kristo? (p. 58)

Ni neno kuu hili: “Urafiki wa Bwana wetu mpendwa Yesu Kristo.”

Yale ninawasihi asubuhi hii ni kuwa mtengeneze nyote urafiki wa Yesu Kristo—kuwa muwe na kundi la marafiki katika imani ambao mko nao na uhusiano wa kirafiki kuwa mtaendelea kuonyeshana kwa Yesu Kristo kwa tumaini na nguvu.

3. Kutiana moyo katika Bwana

Hilo ndilo funzo la tatu. Nguvu za kupeana ni nguvu katika Mungu, sio ndani yetu. Mstari wa 16 hausemi kuwa Yonathani alisafiri hadi Horeshi kutia Daudi moyo kwa ujasiri wake. Hakufanya hivyo. Inasema akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani kwa Mungu.

Hii ndiyo tofauti ya kundi la Kirafiki la Kikristo na vikundi vya usaidizi na vikundi vya kimatibabu na vikundi vya kujisaidia. Kusudi la Kikundi cha Kirafiki cha Kikristo ni kuonyeshea kila mmoja Kristo, sio binadamu, usaidizi na nguvu.

Kuna jambo la kukanganya hapa. Kwa njia nyingine ninasema, nakuhitaji. Mungu amekuchagua kupitia neema ili unisaidie kuvumilia hadi mwisho. Kwa njia nyingine tena, lazima niseme kuwa njia ya kipekee ya kunisaidia ni kwa kusema kitu ama kufanya kitu cha kunifanya nimtegemee Mungu na sio wewe.

Hapa tupo inakaa tena tuko na maudhui yetu ya kawaida sana: Kuzingirwa kwa Mungu kwa yote tunayoyatenda, hata katika jumuiko letu la kibinadamu, kikundi chetu cha kirafiki, urafiki wetu. Lazima uwe urafiki ndani ya Yesu. Kikundi chochote cha Wakristo kinachoendelea lazima kipatikane kwa ajili ya kutiana moyo katika Bwana wala sio kwa mwanadamu. Ndilo funzo letu la tatu katika andiko letu: “Naye Yonathani mwana wa Sauli akamwendea Daudi huko Horeshi na kumtia moyo kusimama imara katika imani kwa Mungu.“

4. Kukumbushana juu ya ahadi za Mungu

La mwisho, alifanyaje hili? Tunalifanyaje? Yonathani alisema (mstari 17): “Usiogope Daudi, baba yangu Sauli hatakutia mkononi mwake. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, name nitakuwa wa pili wako. Hata baba yangu Sauli anajua hili.”

Yonathani alijuaje kuwa Daudi atakuwa mfalme juu ya Israeli? Walikuwa marafiki wa ndani na hivyo basi ni vigumu kufikiria kuwa Daudi hakuwa amemwambia Yonathani juu ya tukio hilo katika fungu la 16 wakati nabii Samueli alimpaka Daudi aliyekuwa kijana kuwa mfalme juu ya Israeli. Kwa hivyo vile Yonathani alimtia Daudi moyo katika Bwana ni kwa kumkumbusha juu ya ahadi ambayo Mungu alikuwa amefanya (1 Samueli 16:12). Sauli hangefaulu dhidi ya Daudi kwa sababu Mungu alikuwa upande wake. Basi Yonathani alimtia moyo katika Bwana kwa kumkumbusha juu ya mwelekeo wake katika kusudio la Mungu.

Na hivyo ndivyo ilivyo kwetu. Tunatiana moyo katika Bwana kwa kukumbushana ahadi za Mungu zinazoegemea hitaji ya kila mmoja.

Ni nini ungelihitaji kusikia kutoka kwa marafiki yako kama ungekuwa William Carey ambaye yuko maili 15000 kutoka nyumbani akiwa anapigana vita vya imani na rafiki moja ambaye amezingirwa na mamilioni ya watu wasioamini? Unahitaji kitu kama hiki, maneno ya Samuel Pearce, rafiki wa thamani ambaye anajua kumtia Carey moyo katika Bwana. Sikiza vile ahadi za Mungu zinajaza barua hii la Tarehe 4, Oktoba, 1794.

Ndugu, natamani kusimama karibu nawe na kushiriki katika mashambulishi hayo mengi—mashambulishi ambayo hakuna kitu chochote ila tu uoga inaweza kufanya yasifaulu. Ndio Jemedari wa wokovu wetu anatutangulia mbele. Saa zingine anaweza toa uwepo wake (lakini sio nguvu zake) kujaribu ushupavu wetu na silaha zetu za kiroho na gamba letu la kiroho. Lo, ni nini imani hai inaweza fanya kwa askari wa Kristo! Italeta ukombozi kutoka mawinguni; itamvalisha na mapambo yaliyovuviwa damu; itamweka mbele ya vita na kuweka wimbo mpya kinywani mwetu—“Walifanya vita na Mwana—Kondoo; Lakini Mwana—Kondoo atawashinda.” Kweli atawashinda—shindi ni hakika hata kabla tuingie uwanjani; taji limewekwa tayari la kupamba nyele zetu, hata taji la utukufu ambalo halifutiki, na tayari tumeshaamua la kufanya nalo—tutaliweka miguuni mwa washindi na kusema, “Sio kwa ajili yetu, ewe Bwana, sio kwa ajili yetu, lakini kwa ajili ya Jina Lako likapewe utukufu,” wakati mbingu inaungana katika wimbo, “Anastahili Mwana Kondoo.” (Memoir, p. 66)

Kwa kweli, sio kila moja wetu ana tajiriba ya kutia moyo marafiki yake na maneno kama hayo. Lakini ukiegemea akili yako katika Neno La Mungu na kuitafakari usiku na mchana vile Zaburi 1 inavyosema, basi utakuwa kizima cha maji yenye uzima na utatia wengi moyo katika Bwana. Mwito wa Mungu kwenu asubuhi hii ni: Njoo, tutiane moyo katika Bwana! Amina.