Mamlaka na umbile wa karama ya Unabii
Kutoka Gospel Translations Swahili
(Created page with '{{info|The Authority and Nature of the Gift of Prophecy}}<br> <blockquote> '''Matendo ya Mitume 2:14-21'''<br><br>Ndipo Petero akasimama pamoja na wale mitume kumi na moja, akin...')
Badilisho lijalo →
Sahihisho kutoka 17:32, 8 Agosti 2011
By John Piper
About Spiritual Gifts
Part of the series Are Signs and Wonders for Today?
Translation by Desiring God
Matendo ya Mitume 2:14-21
Ndipo Petero akasimama pamoja na wale mitume kumi na moja, akinua sauti yake na kuhutubisha ule umati wa watu, akasema: “Wayahudi wenzangu na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, jueni jambo hili mkanisikilize. Hakika watu hawa hawakulewa kama mnavyodhania, kwa kuwa sasa ni saaa tatu asubuhi! Hawa hawakulewa, ila jambo ni lile lililotabiriwa na nabii Yoeli akisema “Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangojuu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto. Hata juu ya watumishi wangu nitamwaga Roho wangu nao watatabiri. ”Nami nitaonyesha maajabu mbinguni juu na ishara duniani chini, moto na mvuke wa moshi mnene, jua litakuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu kabla ya kuja siku ile kuu ya Bwana iliyo tukufu. Lakini yeyote atakayeita jina la Bwana ataokolewa.
Wiki iliyiypoita nilijaribu kuonyesha kwamba I Wakorintho 13:18-12 inafundisha kuwa karama ya unabii utapita wakati Yesu atakayorudi—vile taswira yenye giza litapisha uso wenye uhai. Na nilieleza kwamba basi karama ya unabii bado lina maana katika kanisa ya sasa. Niliahidi kwamba leo tutafuatilia maswali: Na ni nini karama ya unabii, na unafaa utumike vipi?
Yaliyomo |
Uhisho na Ukamilifu wa Andiko
Wacha nianze na kudhibitisha uhisho na ukamilifu wa andiko, vitabu 66 vya Bibilia. Hakuna kitu chochote nisemacho kuhusu unabii wa leo ambacho kinamaanisha kuwa vina mamlaka maishani mwetu kuliko andiko. Unabii yoyote ambayo unapeanwa leo hauongezi chochote kwa andiko. Zimejaribiwa kupitia andiko. Andiko limefungwa na ni mwisho ni msingi, sio hatua ya ujenzi.
Njia nzuri ya kuona hii ni kuona vile mafundisho ya mitume yalikuwa ya mamlaka kuu katika kanisa la kwanza na vile unabii zingine haukuwa na mamlaka huu ya uhisho. Kwa mfano, Paulo anasema katika I Wakorintho 14:37-38, “Kama mtu yeyote akidhani kwamba yeye ni nabii, au ana karaha za rohoni, basi na akubali kwamba haya ninayoandika na agizo kutoka kwa Bwana. Kama mtu akipuuza jambo hili yeye mwenyewe atapuuzwa.” Athari ni wazi: fundisho la mitume lina mamlaka la mwisho. Misemo ya unabii kanisani, wakati ule na sasa, haina mamlaka hii.
Unaweza kuona kituhicho hicho katika 2 Wathesalonika 2:1-3. Paulo anasema hapa kwamba hata kama mtu anajifanya kupeana habari kuhusu kuja kwa mara ya pili kupitia “roho,” msiwaamini kama haifanani na fundisho la Paulo. “Ndugu kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi msiyumbishwe kwa rahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kwako. Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yeyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza . . . " Ni kusema, unabii lazima ujaribiwe na neno la mitume.
Sasa hoja ni hili:Leo Agano Jipya lasimama pahali pa mitume. Mamlaka zao zadhihirishwa leo kupitia maandishi yao na ya washirika wao wa karibu kama Luka na na Marko na Yakobo (ndugu wa bwana). Basi, kwa njia hiyo Paulo alifanya mafundisho ya mitume mamlaka ya mwisho yenye nguvu nyakati hizo, basi tunayafanya fundisho la kimitume la mwisho na lenye nguvu kwa wakati wetu. Hilo lamaanisha Agano Jipya ni nguvu yetu. Na kwa vile Agano Jipya ladhibitisha Agano la Kale kama neno la Mungu lililotiwa nguvu za kiungu, tunauchukua Bibilia kwa ujumla kama kipimo chetu cha mafundisho na unabii yote kuhusu yote tunayostahili kuamini na vile tunastahili kuishi.
Ninini kilichotendeka siku ya Pentekoste
Sasa tuangalie Matendo 2:16 ukiendelea mbele. Ili tuone yale tunaweza kujifunza kuhusu karama ya unabii za Agano Jipya. Hali: ni siku ya Pentekoste, siku 50 baada ya kufufuka kwa Yesu. Kuna Wakristo 120 wake kwa waume wanaoongojea Yerusalemu “kuvalishwa na nguvu kutoka juu” (Luka 24:49). Kulingana na Matendo 2:2 Roho Mtakatifu huja kwa sauti kama mvumo mkubwa wa upepo katika mstari 4. Luka asema, “Wote wakajaazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama vile Roho alivyowajalia.” Mstari 11 inaongea kwa kipekee kuhusu yale walikuwa wakinenea. Wageni wengine waliowasikia wanasema, “watu hawa wanasema katika lugha zetu wenyewe, mambo makuu ya ajabu ya Mungu.” Tafakari yaliyo katika maneno yao kwa makini sana. Hiyo itakuwa muhimu kwa kuelewa umbile wa karama za unabii.
Utimilifu wa Unabii wa Yoeli
Katika mstari wa 16 Petero anaeleza yale yanayotukia. Anasema kuwa hapa ndio yale yaliyosemwa na nabii Yoeli. Hii ndio mwanzo ya utimilifu Yoeli 2:28. Halafu ananukuu Yoeli katika mistari 17-18, “Katika siku za mwisho, asema Bwana, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto. Hata juu ya watumishi wangu nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.”
Yoeli alikwisha sema kuwa katika siku za mwisho kutakuwa na umiminaji mkuu wa Roho ulimwenguni (wote wenye mwili), na alama ya umiminaji huo utakuwa kutabiri utakaoenea; wake kwa waume, wazee kwa vijana, maskini kwa matajiri. Yoeli anasema itatendeka katika “siku za mwisho.” Ni lini hiyo? Petero asema ilikuwa ikitukia wakati ule. “Hii ndio iliyosemwa na nabii Yoeli.” Lakini kama siku za mwisho zilikuwa zikianza wakati huo, hiyo inatuweka wapi?
Siku za mwisho
Inatuweka katika siku za mwisho. Tangu Yesu aje, tunaishi katika siku za mwisho. Waebrania 1:2 inasema, “Zamani Mungu alisema na baba zetu kwa njia ya manabii mara nyingi na kwa njia mbali mbali, lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe . . . ” Tangu mwana aje, tunaishi katika. “siku hizi za mwisho.”
Basi hii inathibitisha yale tuliyoyaona wiki uliopita kuhusu unabii kuwa kitu ambacho kinafaa tutarajie wakati huu. Wake kwa waume, wazee kwa vijana, matajiri kwa maskini watatabiri katika siku za mwisho (siku zetu), na itakuwa tukio liloenea ulimwenguni kote kwa sababu, vile mstari 17 unasema, Mungu atamiminia Roho yake juu ya WOTE WENYE MWILI —Sio tu Wayahudi. Funzo la Petero laisha katika Matendo 2:39, “Kwa kuwa ahadi hii (juu ya Roho katika mstari 38) ni kwa ajili yenu na watoto wenu na kwa wale wote walio mbali na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu atamwita amjie.” Hiyo yajuumlisha hata Wayunani walioitwa na mungu. Sio wote waliotubu na kuamini watapokea Roho mtakatifu (Mstari 38). Na mojawapo ya tendo la Roho katika siku za mwisho litakuwa kuenea kwa ajabu kwa karama ya utabiri (Mistari 17-18): “Wana wenu na binti zetu watatabiri, vijana wenu wataona maono na wazee wenu wataota ndoto. Hata juu ya watumishi wangu nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.”
Usahawishi wa Roho bali si ya mamlaka ya kiungu isiyo ya dhati
Sasa jiulize swali hili: Je, Yoeli na Petero na Luka walifikiri kuwa wanaume na wanawake wote—wazee kwa vijana, watumishi wa kike na wa kiume—watakuwa manabii kwa ile kiwango ambacho Musa na Isaya na Yeremia walivyokuwa manabii, ni kusema, watu walioongea na maneno yaliotiwa nguvu za kiungu na nguvu ile ya mungu ambao wangeweza kuandika andiko lisilodanganya? Je utabiri wa Matendo 2:17 kama unabii huo? Ama kuna tofauti?
Naamini kuna tofauti. Sidhani karama za unabii leo ina nguvu kama ya manabii wa Agano la kale ama ya Yesu na mitume. Ama, kuiweka kwa njia nzuri zaidi, unabii wa aina hii unaletwa na kuimarishwa na Roho lakini bado haubebi nguvu za kiungu, isiyo ya dhati.
Sababu mojawapo ya kufanya aina hii ya unabii kuwa ngumu kukubali wakati huu ni kuwa wengi wetu hatuna vitengo katika fikira kwa ajili ya maneno yaliyo na ushawishi wa Roho ambayo hayabebi mamlaka za kiungu, isiyo ya dhati. Hiyo linakaa kinyume. Tunakumbana na aina ya gumzo ambayo imeshawishika na kuimarishwa na Roho Mtakatifu ilhali haina dosari. Lakini nitajaribu kuonyesha asubuhi na jioni hii kuwa hivi ndivyo karama za unabii ulivyo katika Agano Jipya na hata sasa. Unashawishishwa na Roho, gumzo lililoimarishwa na Roho ambalo halibebi nguvu za kiungu, zisizo dhati na yanaweza changanyika na dosari.
Basi kama hiyo inafanya karama za unabii kuonekana duni na dhaifu zingatia tamthili ya karama ya ualimu.
Tamthili ya Karama ya Ualimu
Je hutasema kwamba, wakati karama ya kiroho ya ualimu inapowekwa katika kazi, ualimu unahimizwa na kuimarishwa umekita mizizi katika ufunuo wa kiungu usio na dosari uitwayo Biblia. Karama ya ualimu ni himizo na uimarisho wa kiroho unaoeleza ukweli wa kibibilia kwa uadhilifu wa kanisa. Na sote tungesema ina thamani kuu katika maisha ya kanisa. Je kuna anayeweza kusema kuwa arifa ya mwalimu, wakati anatumia karama ya ualimu, kuwa bila dosari? La. Je, tutasema una mamlaka ya kiungu? Katika hisia ya kiwango tu ndio tunaweza kusema hivyo. Sio kibinafsi, si kiundani, lakini kutoka kwa chanzo chake, Bibilia.
Ni kwa nini karama iliyo hitimizwa na kuimarishwa na Roho iliyokita mizizi katika ufunuo usio na dosari (Bibilia) kwa hakika ina dosari, iliyochanganyika na madoa na una mamlaka duni ya kutoka kwa kitu? Jibu ni hili: Hisia za mwalimu kuhusu ukweli wa kibibilia ina dosari; na maelezo yake juu ya ukweli wa kibibilia ina dosari; Hakuna uhakika kwa uhusiano kati ya Bibilia isiyo na dosari na kanisa isiyo na dosari utakuwa usio na dosari. Karama ya ualimu hauhakikishi funzo bila dosari.
Na ingawa karama ya ualimu una dosari na umekosa nguvu za kiungu ya dhati, tunajua una thamani kuu kwa kanisa. Tumeimarishwa na kujengeka na walimu wenye kipawa. Mungu yuko ndani yake. Anautumia. Ni karama ya Roho.
Hebu linganisha hii na kipawa cha unabii. Inahimizwa na Roho na kuimarishwa kwa Roho na ni juu ya ufunuo kutoka kwa Mungu. Mungu anafunua kitu akilini mwa nabii (Kwa njia inayoshinda ufahamu wa kawaida ya kuona vitu), Mungu hakosei, tunajua ufunuo wake ni kweli. Hauna dosari kwayo. Lakini karama ya unabii haihakikishi usambasaji kwa ufunuo huo usio na dosari. Nabii anaweza kufumbua ufunuo kwa njia isiyo vyema anaweza kuuelewa kwa njia mbaya, anaweza kuuleta kwa njia mbaya. Ndiyo maana Paulo anasema tunaona taswira kama ya kwenye kioo (I Wakorintho 13:12). Karama ya unabii inaleta unabii ulio na dosari vile karama ya elimu inavyoleta ualimu ulio na dosari. “Kama ualimu inaweza kuwa mzuri kwa uimarishaji wa kanisa, basi unabii vile si pia waweza kuwa vyema kwa kuimarisha, vile Paulo anavyosema hivyo (I Wakorintho 14:3, 12, 26)—hata ingawa yote yana dosari, iliyochanganyika na upungufu wa wanadamu na inahitaji kujaribiwa?
Kuumba kitengo kipya katika fikira zetu
Hoja ambalo nimekuwa nikisema ni hili: tunahitaji kuumba kitengo kipya katika fikira zetu kwa ajili ya gumzo ambalo limewezeshwa na kuimarishwa na Roho, limekita mizizi katika ufunuo, na ilhali bado linahitaji kujaribiwa na kufanywa kuwa nyororo. Tunahitaji kitengo kipya cha nabii kando na yule nabii wa kweli, kwa njia nyingine, ambaye aliongea na maneno yaliyotiwa nguvu za kiungu ambayo hayana dosari (Manabii waliochapisha Bibilia na Yesu na mitume), Na manabii wa uongo kwa upande mwingine, waliohukumiwa katika kumbukumbu la Torati 13:3; 18:20 (Yeremia 23:16). Funzo tunalopata katika Bibilia kuhusu unabii haujakamilishwa na vitengo hivi viwili. Tunahitaji kitengo cha tatu kwa ajili ya “karama ya kiroho cha unabii”—Kilichohimizwa na kuimarishwa na Roho, kilicho kita mizizi katika ufunuo, lakini kimechanganyishwa na upungufu wa kibinadamu, nabii asiye na dosari ama nabii wa uongo anaye pita kiwango kilicho halali.
Ndio hali ya kufanya unabii zingine kuwa vyema na zingine kuwa mbaya.
Paulo anasema tukiudharau kwa sababu ya upungufu huu, tunamzima Roho. Natumai unataka kuepuka haya kwa moyo wako wote. Tunafanyaje hiyo? Kuna mengi ya kusema. Nitaanza kutoka hapa usiku huu, nipeane sababu za ziada, na athari za kuonekana. Bwana mwenyewe na atufundishe huu.