Sababu 10 maana ninashukuru kwa Biblia ya Mungu
Kutoka Gospel Translations Swahili
Sahihisho ya 01:12, 31 Januari 2010 aliyefanya JoyaTeemer (Majadiliano | michango)
By John Piper
About The Bible
Part of the series Taste & See
Translation by David Ghana
You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).
1. Biblia inazua imani, chanzo cha utiifu wote.
- Hivyo, hutoka kwa kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. (Warumi 10:17)
2. Biblia inafanya huru kutoka kwa dhambi.
- Utatambua ukweli, na ukweli utakuweka huru (Yohana 8 :32)
3. Biblia inafanya huru kutokana na shetani.
- Mtumishi wa bwana ni sharti asiwe mgomvi, ila awe mnyenyekevu kwa wote, anayeweza kufunza, mvumilivu anapokosewa, kukosoa wasiokubaliana kwa ungwana, ikiwa labda Mungu anaweza kuwasamehe iliwaweze kufahamu ukweli, na waweze kupata fahamu na kuepuka mtego wa shetani, baada ya kushikwa mateka naye ili watende matakwa yake. (2 Timotheo 2:24-26)
4. Biblia inatakasa.
- Watakase katika ukweli; Neno lako ni kweli. (Yohanna 17:17)
5. Biblia inafanya huru kutokana na ufisadi na inawezesha utakatifu.
- Uwezo wake wa Kimungu umetupa kila kitu kihusianacho na uzima na utauwa, kwa kupitia elimu ya kweli, Yeye alitetuita kwa utukufu wake mwenyewe na ubora wake. Maana kwa haya tumepewa ahadi zake za thamani na anacho, ili kwa hayo mpate kuwa washiriki wa hali ya Uungu, baada ya kuepuka ufisadi ulioko ulimwenguni kutokana na tamaa. (2. Petero 1:3-4)
6. Biblia inatumikia upendo
- Na hili naomba, ya kwamba upendo wenu uwe tele, tena kwa wingi ndani ya elimu ya kweli na ujuzi wote. (Wafilipi 1:9)
Ila madhumuni ya mafunzo yetu ni upendo kutoka kwa moyo safi na dhamiri njema na imani ya kweli. (1 Timotheo 1:5)
7. Biblia inaokoa.
- Wekeni maanani ndani yenu wenyewe na kwenye mafunzo yenu; vumilieni katika mambo haya, maana mnapofanya hivyo, mtahakikisha wokovu kwenu na pia kwa wale wanaowasikia. (1Timotheo 4:16)
- Kwa hivyo, ninawashuhudieni siku ya leo, ya kwamba sina hatia kwa damu ya binadamu wote. Kwa maana sikunyauka kwa kuwatangazieni azma yote ya Mungu.( Matendo 20:26-27) Wataangamia, kwa sababu hawakupokea upendo wa ukweli ili waokoke. (2 Wathesalonike 2:10)
8. Biblia inaleta furaha
- Haya mambo nimewazungumzia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na ili furaha yenu iwe tele. (Yohana 15:11)
9. Biblia hufunua Bwana.
- Na Bwana akaonekana tena Shilo, kwa maana Bwana alijitokeza kwa Samweli huko Shiloh kwa neon Lake. (1 Samweli 3:21)
10. Kwa hivyo, Biblia ndio msingi wa furaha nyumbani na maishani mwangu na ushiriki na tumaini la maisha ya milele na Mungu.