Ndoa: Onyesho la Mungu ya Agano itimizayo neema
Kutoka Gospel Translations Swahili
By John Piper
About Marriage
Part of the series Marriage, Christ, and Covenant: One Flesh for the Glory of God
Translation by Desiring God
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutotahiriwa kwa mwili wenu, Mungu aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote: 14 akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushtaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaliondowa lisiwepo tena, akaigongomea msalabani; 15 akisha kuzivua enzi na mamlaka na kuzifanya kuwa mkongo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo . . . 3:12 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema unyenyekevu, upole, uvumilivu 13 Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 14 Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndiyo kifungo cha ukamilifu. 15 Na amani ya Kristo iamue moyoni mwenu, ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; Huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu. 17 Na kila mfanyalo kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkishukuru Mungu baba kwa Yeye. 18 Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana. 19 Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao.
Yale tumeona kwa wiki mbili zilizopita ni kwamba, jambo la msingi sana unayo weza kusema kuhusu ndoa ni kwamba, ni tendo la Mungu na jambo la mwisho unaweza sema kuhusu ndoa ni kwamba ni ya onyesho la Mungu. Hoja haya mawili yamesemwa na Musa katika mwanzo 2. Lakini yanafanywa wazi sana na Yesu na Paulo katika agano jipya.
Yesu: Ndoa ni tendo la Mungu
Yesu aweka hoja hili sawa zaidi yakuwa ndoa ni tendo la Mungu. Mariko 10:6-9, “ lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.” [Mwanzo 1:27]Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja [Mwanzo 2:24]. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asitenganishe.” Msemo huu ni ya wazi na ya kueleweka kwa urahisi katika Bibilia yakuwa, ndoa si tendo tu la mwanadamu. Neno “alichokiunganisha” inamaanisha ni tendo la Mungu.
Paulo: Ndoa ni onyesho la Mungu
Paulo aweka hoja hii wazi na sawa zaidi yakuwa, ndoa imeundwa ili iwe onyesho la Mungu. Katika Waefeso 5:31-32, ananukuu Mwanzo 2:24 na kisha atuelezea kuhusu siri iliyositiriwa ambayo imekuwa nayo kila wakati. “Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.” Siri hili lililo sitiriwa ni kuu, na nasema yakuwa Inaashiria Kristo na Kanisa.” Kwa njia nyingine, agano ambayo imehusishwa katika kuwaacha mama na baba na kuambatana na mke na kuwa mwili mmoja ni ishara ya agano kati ya Kristo na kanisa lake. Ndoa upo kabisa, kabisa kuonyesha agano ya upendo kati ya Kristo na kanisa lake.
Kielelezo ya Kristo na Kanisa
Nilimuliza Noel kama kuna chochote angependa niseme leo aksema. “hauwezi sema mara kwa mara yakuwa ndoa ni kielelezo ya Kristo na Kanisa.” Nadhani yuko sawa na kunayo angalau sababu tatu: 1) Hii inainuwa ndoa kutoka kwa picha za Sordid Sitcom na kuipa maana kuu zaidi ambayo Mungu alimaanisha iwe nayo: 2) Hii inapea ndoa msingi dhabiti katika neema, Kwa kuwa Mungu alimpata na kumlinda mchumba wake kwa neema pekee; 3) Hii inaonyesha yakuwa uongozi wa mume na kutii kwa mke ni muhimu na yamesulubishwa. Hii ni kusema, yamesukwa ndani ya maana ya ndoa kama onyesho ya Kristo na Kanisa, lakini yote mawili yameelezwa na kazi ya Kristo msalabani ili kibuuri yao na utumwa wao utupiliwe mbali.
Tulitumia ujumbe mbili za kwanza kwa sababu hizi za kwanza: Kupeana msingi ya ndoa kama onyesho ya agano ya upendo wa Mungu. Ndoa ni agano kati ya mume na mke ambapo wana ahidiana kuwa waaminifu kama mume na mke katika upatanisho wa mwili mmoja kadri wanvyo ishi. Agano hili, limewekwa muhuri na ahadi za kweli na ya kumaanisha na kuungana ki ngono. Imeeeundwa kuonyesha neema ya mungu ya kulinda agano.
Msingi dhabiti katika neema
Hiyo ndiyo mada ya siku ya leo; “Ndoa; Onyesho la Mungu kuhusu neema ilindavyo neema.” Basi tunaenda kwa sababu ya pili, niliyoeleza kuwa Noel alieleza ukweli ya kuwa huwezi kusema kila wakati, ndoa ni kielelezo ya Kristo na kanisa: kwa sababu ya kuwa hili lina ipa ndoa msingi dhabiti katika neema kwa sababu kuanzia kitambo Kristo alimpata na kumlinda bibi harusi kwa neema pekee.
Kwa njia nyingine; hoja muhimu ya leo ni kuwa tangu a gano jipya ya Kristo na kanisa lake liiumbwa na kulindwa kwa neema iliyonunuliwa na damu, kwa hivyo, ndoa ya wanandamu yamemaanisha kuonyesha hiyo neema ya agano jipya. Na wanaionyesha kwa njia ya kupumzika kwa neema ya Mungu na kuikunja kutoka kwa kumlenga Kristo hadi uwepo unaomlenga mke na mume. Kwa mswemo mwingine ni kuwa, katika ndoa unaishi saa baada ya nyingine katika furaha ukiutumainia msamaha wa Mungu, na kufanywa haki na ahadi ya neema ya usoni, na unaelekeza kwa mke au mume wako kila saa baada ya nyingine—kama onyesho la msamaha wa Mungu na kufanywa haki na usaidizi ulio ahidiwa. Hiyo ndiyo hoja ya leo.
Kiini cha msamaha, Neema ifanyayo haki
Nina ufahamu ya kuwa wakristo wote wanafaa kufannya hili katika uhusiano wenu wote (Sio tu wakristo walio okoka): Ishi saa baada ya nyingine kwa neema ya Mungu ipeanayo yote na inayo samehe, ifanyayo haki na kisha uielekeze kwa wengine wote maishani mwako. Na Yesu asema kuwa maisha yetu yote ni onyesho ya utukufu wa Mungu (Matahyo 5:16). Lakini, njdoa imeundwa ili iwe onyesho la kipekee la agano ya neema ya Mungu, kwa sabau tofauti na uhusiano zingine zote za wanadamu, mke na mume wamefungwa na agano katika uhusiano wa karibu iwezekanavyo maishani mwao wote. Kunayo majukumu mengi ya kipekee ya uongozi na kutii, lakini hiyo si hoja langu leo. Hiyo itakuja baadaye. Leo na watazama mume na mke kama wakristo tu na siyo kama vile wanafanana kwaa kichwa na mwili. Kabla mume na mke kutenda yale yako kwenye maandiko na kwa neema ya kipekee matendo ya ukichwa na kutii, wanafaa kugundua maana ya kujenga maisha yao kwa uwepo shazari ya msamaha na kufanywa haki na usaidizi ulio ahidiwa na kisha waukunje nje kwa usambamba kwa wachumba wao. Hiyo ndio mtazamo wetu leo.
Au kuiweka kwa mtazamo wa ujumbe wa wiki uliopita: Ufunguo wa kuwa uchi na bila aibu. (Mwanzo 2:25), Wakati, kwa uhakika, mume na mke wanatenda matendo ambayo wanapaswa kuaibika kwayo, ni uwepo shazari wa msamaha wa Mungu, neema ifanyayo haki umekunjwa nje kwa usambamba kwa kila mmoja na kuonyeshwa ulimwenguni.
Ghadhabu ya Mungu inayokuja
Kwa ufupi, acha tuone msingi huu wa ukweli katika Wakolosai. Tutaanza na Wakolosai 3:6, “Kwaajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu." Ukisema yakuwa, “Kitu cha mwisho ningependa kusikia kuhusu ndao yangu ni ghadhabu ya Mungu,” Wewe ni kama mvuvi ambaye ameshushwa moyo katika magharibi ya bahari kule Indonesia wakati wa Desemba 26, 2004, ukisema “Kitu cha mwisho ningependa kusikia katika biashara yangu hii ya uvuvi yenye shida nyingi ni Tsunami.” Kuelewa kwa njia kuu na uwoga wa ghadhabu ya Mungu ndio kwa hakika yale ndoa nyingi yana hitaji, kwa sababu bila hiyo, injili itakuwa imetiwa maji hadi kiwango cha uhusiano iwe kati ya wanadamu tu na kupoteza utukufu wake wa kibiblia. Na bila hiyo, utajaribu kufikiria kuwa ghadhabu yako—hasira yako—dhidi ya mke au mume wako ni kuu zaidi kupita, kwa sababu hauja onja kwa hakika na kuona ghadhabu kuu zaidi ambayo imeshindwa na neema, mfano, ghadhabu ya Mungu dhidi yako.
Ondoleo la ghadhabu ya Mungu
Kwa hivo tunaanza na ghadhabu ya Mungu na Ondoleo lake. Sasa rejea nami kule Wakolosai 2:13-14, “ Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutotairiwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye [Kristo], akiisha kutu samehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati ilioandikwa kutushtaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu, akaiondoa isiwepo tena akaigongomea msalabani.”
Maneno hayo ya mwisho ndio ya msingi zaidi. Hati hii ya deni ambayo ilisimama dhidi yetu—Mungu aliweka kando na kuigongomea msalabani. Ulitendeka wakati gani? Miaka elfu mbili iliyopita. Haikufanyika ndani yako, na haikufanyika na usaidizi kutoka kwako. Mungu alikufanyia hayo na pasipo wewe kabla hata uzaliwe, hii ndiyo kiini kuu zaidi ya uwokovu wetu.
Hati ya deni imefutiliwa mbali msalabani
Hakikisha unaona hii ukweli nzuri zaidi na ya kushangaza zaidi kushinda zote: Mungu alichukuwa hati ya dhambi zetu zote ambayo ilikufanya mwenye deni kwa ghadhabu (Dhambi ni matendo maovu dhidi ya Mungu ambayo inaleta ghadhabu yake kwetu), na badala ya kuibeba mbele ya uso wako na kuitumia kama lesesni ya kukutupa jehanamu, anauweka katika kiganja cha mwanawke na kuweka msumari kwayo msalabani.
Dhambi za nani ziligongomewa msalabani? Dhambi za nani ziliteswa msalabani? Jibu! Dhambi zangu na Dhambi za Noeli—Dhambi za Mike wangu na dhambi zangu—Dhambi za wale wote wamekata tama ya kujiokoa wenyewe na kumtumainia Kristo pekee. Mikono ya nani ilipigwa misumari msalabani? Nani aliteswa msalabani? Yesu ndiye. kunayo jina rembo kwa hili. Linaitwa mbadala. Mungu aklihukumu dhambi zangu katika mwili wa Kristo (Warumi 8:3) Mabwana, hamuwezi kuamini haya kwa nguvu, mabibi hamuwezi kuamini haya kwa nguvu sana.
Kuhesabiwa haki ni zaidi ya msamaha
Na tukirudi nyuma na tutoe hapo kuelewa kwetu kwa kufanywa haki kutoka kwa Warumi twaweza sema mengi. Kuhesabiwa haki inaenda zaidi ya msamaha, hatujasamehewa tu kwa sababu ya Kristo bali Mungu anatuhesabu watakatifu kwa sababu ya Kristo. Mungu anahitaji mambo mawili kutoka kwetu: Kuadhibiwa kwa dhambi zetu na kuwa bila mawaa maishani mwetu. Dhambi zetu lazima ziadhibiwe na maisha yetu lazima iwe takatifu. Lakini hatuwezi beba dhawabu yetu sisi (Zaburi 49:7-8), na hatuwezi peana utakatifu wetu wenyewe. Hakuna mtakatifu hata mmoja (Warumi 3:10).
Basi, Mungu kwa upendo wake usio na kipimo alitupa mwanawe kufanya yote mawili. Kristo anabeba adhabu zetu na tena Kristo anafanya utakatifu wetu. Na tunapompokea Kristo (Yohana1:12), adhabu zetu zote na utakatifu wake wote unahesabiwa kwetu (Warumi 4:6; 5:19;5:1; 8:1; 10:14; Wafilipi 3:8-9; 2 Wakorintho 5:21).
Kufanywa haki ambao umeelekezwa nje
Hii ni ukweli shazari ambayo inafaa kuelezwa nje kwa usambaba kwa wake na waume wetu, ikiwa ndoa inapaswa kuonyesha kutengenezwa kwa agano na agaano inayolinmda neema ya Mungu. Tunaona haya katika Wakolosai 3:12-13, “basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, Watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyo wasamehe ninyi vivyo na ninyi.”
“Kama Bwana alivyo wasamehe ninyi, vivyo na ninyi”— Kwa mke au mume wako. Kama vile Mungu anavyo wastahimmili nanyi pia inafaa kumstahimili mke au mume wako. Mungu anakustahimili kila siku unapo pungua kufikia mapenzi yake. Kwa kweli, umbali ya yale Mungu ana tarajia kutoka kwako na yale unafanikiwa kutenda ni kuu zaidi kuliko umbali ya yale unatarajia kutoka kwa mke au mume wako na yale anafanikiwa kutenda. Kristo kila wakati anasamehe zaidi na anastahimili mengi kutuliko. Samehe jinsi ulivyo samehewa. Stahimili jinsi anavyo stahimili nawe. Hili linabakia hata kama umeolewea na mwamini au asiyeamini.
Acha kiwango cha neema ya Mungu kwako katika msalaba wa Kristo iwe kiwango cha neema yako kwa mke au mume wako na ikiwa umeolewa na mwamini unaweza ongeza haya: kama vile Bwana anakuhesabu mwenye haki katika Kristo, ingawa hauko katika tabia au mawazo asili, kwa hivyo, hesabu mke au mume wako mwenye haki katika Kristo ingawa yeye siyo hivyo—Kwa njia nyingine, Wakolosai 3 yasema, Chukua neema shazari ya msamaha na kufanywa haki na kuyaelekeza nje kwa usambamba kwa mke au mume wako. Hii ndiyo sababu ya ndoa, kwa hatima zaidi—Onyesho la agano ifanyayo neema ya Mungu.
Kuhitajika kwa hekima iliyo na mizizii katika injili
Basi hapa, ma mia ya hali ngumu hujitokeza na ambayo zinalilia hekima ya kindani ya kiroho ambayo ina mizizi katika ukweli wa injili na katika miaka nyingi ya uchungu na mapito ya Imani. Kwa maneno mengine, hakuna njia nyingine ningeweza kuwasilisha ujumbe huu, kwa mahitaji ya kila mtu. Kando na kuhubiri twahitaji roho mtakatifu, twahitaji maombi, twahitaji kutafakari neno, kwa ajili yetu sisi, tunahitaji kusoma hekima ya wengine, twahitaji ushauri wa marafiki walio na hekima na ambao wamepitia mateso, twahitaji kanisa itusaidie wakati kila kitu hafanyi kazi tena. Kwa hivyo sina uongo au udanganyifu yakuwa ninaweza kusema yote ambayo yanahitajika kusemwa ili ikusaidie.
Kuishi kwa ushazari kisha kuukunja nje
Inaweza kusaidia kufunga kwa kupeana sababu kadhaa, kwa nini ninasisitiza agano ya upendo kama msamaha na kumhhesabu huyo mwingine mwenye haki. Je, siamini kufurahishwa katika huyo mtu mwingine? Ndio. Uzoefu na Bibilia inatusukuma pale. Ili uwe na uhakika Yesu ameoa Bi harusi wake amabaye ni kanisa, na kwa wazi inawezekana na pia ni vyema kumfurahisha Bwana (Wakolosai 1:10). Na kwa uhakika anastahili sana kutosheka kwetu ndani yake. Hili ndilo hali nzuri katika ndoa. Watu wawili wananyenyekea na kubadilika kwa njia ya uungu ambayo inamfurahisiha wake au waume wetu na kutosheleza mahitaji ya kimwili na hisia au kuwafurahisha kwa njia yote nzuri. Ndio. Uhusiano wa Kristo na Kanisa imehuhsisha hayo yote.
Lakini sababu ya kusistiza kuishi kwa ushazari kutoka kwa neema ya Mungu na kisha kuukunja nje kwa usambamba wa msamaha na kufanywa haki kwa mke au mume wako 1) Kwa sababu kunaenda kuwa na mzozoo ambayo imesababiishwa na dhambi na kutokuwa kawaida (Na hamtaweza hata kukubaliana kati yenu kuhusu kile kisicho cha kawaida kati yenu na kilicho dhambi); na 2) Kwa sababu kazi ngumu na kisichonyooka ya kuvumilia na kusamehe ndio inauwezesha upendo kukuwa wakati unaonekana kuwa umekufa. 3) Kwa sababu Mungu anapata utukufu wakati watu wawili tofauti sana na wasio kamilifu wanatengeneza maisha ya uaminifu katika moto wa mateso kwa kumtegemea Kristo.
Katika Kristo, Mungu amekusamehe wewe na mke au mume wako
Sasa ntaendelea kutoka hapa wakati mwingine na niwaambie kuhusu uvumbuzi ambayo mimi na Noel tulifanya. Natabiri ya kuwa ujumbe utaitwa “Ujumbe wa jaa la mbolea.”
Hadi wakati huo wake kwa waume wekeni ukweli haya kwenye dhamiri yenu—Ukweli makubwa kuliko shida yoyote katika ndoa yenu—yakuwa Mungu “ameshatusamehe makosa yetu yote kwa kufutilia mbali ile hati ya deni iliyosimama dhidi yetu na mahitaji yake ya kisheria. Hii aliuweka kando akaugongomea msalabani.” Amini haya na roho yako yote na uyakunje ukiyaelekezea mke au mume wako.