Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuokoe na atulinde tuwe waaminifu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Bring Us to Faith and Keep Us Faithful

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 14 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya
wengi” (Marko 14:24).

“Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatenda
mema; nami nitawavuvia kuniacha mimi, ili kwamba kamwe
wasigeukie mbali nami” (Yeremia 32:40).

Biblia inazungumza kuhusu “Agano la Kale” na “Agano Jipya”. Neno Agano linamaanisha makubaliano kati ya watu wawili ambayo hayafai kuvunjwa. Katika Agano hili watu wote wawili wana majukumu ambayo ni lazima wayatimize. Katika Bibilia Mungu ameweka maagano na mwanadamu na katika maagano hayo Mungu anaahidi mambo fulani na mwanadamu ako na majukumu ya kutimiza.

“Agano la kale” ni lile Agano ambalo Mungu alifanya na taifa la Israeli kupitia Musa wakati alipopeana Amri Kumi. Kwa sababu moyo wa mwanadamu ni moyo wenye dhambi, Waisreali hawakuweza kuzitimiza sheria za Mungu. Kwa sababu ya hii Mungu alituma manabii ambao walizungumza kuhusu Agano Jipya. Walisema siku itakuja wakati Mungu atafanya Agano Jipya na watu wake, “Si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha” (2 Wakorintho 3:6)

Mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo ndiyo msingi wa Agano Jipya: “Kwa sababu hii Kristo ni mjumber wa agano jipya” (Waebrania 9:15). Yesu alisema kwamba damu yake ilikuwa ya, “Agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi” (Marko 14:24). Hii inamaanisha kwamba damu ya Yesu huleta baraka za Agano Jipya kwa watu wake.

Katika Agano la Kale nabii Yeremia aliongea kuhusu Agano Jipya. Mungu alisema, “‘Wakati unakuja,’ anasema Bwana, ‘nitakapofanya agano jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Halitafanana na agano nililofanya na baba zao wakati nilipowashika mkono na kuwaongoza watoke Misri, kwa sababu walivunja agano langu, ijapokuwa nilikuwa mume kwao,’ asema Bwana. Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli, baada ya wakati ule,’ asema Bwana. Nitaweka sheria yangu ndani yao na kuiandika katika mioyo yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watoto wangu. Mtu hatamfundisha tena jirani yake, au mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Umjue Bwana Mungu,’ kwa sababu wote watanijua mimi, kuanzia aliye mdogo kabisa kwao hata aliye mkuu sana.’ asema Bwana. Kwa sababu nitausamehe uovu wao na sitazikumbuka dhambi zao tena” (Yeremia 31:31-34). Kwa sababu Bwana Yesu alikufa kwa ajili ya watu wake, sisi tumeokolewa na sasa tuna baraka nyingi: Mungu hubadilisha mioyo yetu wakati anatuokoa

Agano Jipya haliwezi kukosa kufaulu kwa sababu Kristo hulihakikisha. Kristo huwapa imani watu wake na huwadumisha ili wawe waaminifu kwake. Yeye huwaokoa watu wake kutoka dhambi zao na huandika sheria zake kwenye mioyo yao, kwa sababu katika Agano Jipya “Roho huhuisha” (2 Wakorintho 3:6). “Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu; alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu” (Waefeso 2:5). Mungu anapotuokoa hutupatia maisha ya kiroho ili sisi tuje kwa Kristo kwa imani. Katika njia hii Kristo anawaita watu wake kutoka kila mahali ulimwenguni mwote.

Kwa hivyo Mungu anapotuokoa hutupatia imani. Lakini mara tunapookoka, yeye huhakikisha kwamba hatuondoki kutoka kwake na kupoteza wokovu wetu. “Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kuniacha mimi, ili kwamba kamwe wasigeukie mbali nami” (Yeremia 32:40). Wakati Yesu alikufa alihakikisha kwamba tutasamehewa na kwamba tutakuwa na uzima wa milele pamoja naye mbinguni. Yeye hataturuhusu sisi kumwacha yeye na tupoteze wokovu wetu, atatudumisha sisi katika uaminifu.