Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuokoe na dunia hii mbovu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Deliver Us from the Present Evil Age

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 20 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutukoa katika
ulimwengu huu mbaya, sawasawa na mapenzi yake Yeye aliye
Mungu na Baba yetu” (Wagalatia 1:4).

Ulimwengu ambao tuishi ndani, katika Biblia unaitwa ulimwengu ambao ni mwovu sana, na mambo itakuwa hivi hadi Bwana Yesu Kristo mwenyewe atakaporudi. Kwa hivyo wakati Biblia inasema kwamba Kristo alijitoa ili atuokoe kutokana ulimwengu huu mwovu, haimaanishi kwamba atatutoa katika ulimwengu huu. Ulimwengu huu utabaki kuwa jinsi ulivyo hadi Kristo atakaporudi. Kile Biblia inamaanisha ni kwamba Bwana Yesu Kristo atatuokoa kutokana na nguvu za mwovu ambazo ziko katika ulimwengu huu. Bwana Yesu Kristo aliomba, “Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni; bali uwalinde na yule mwovu” (Yohana 17:15).

Sababu ya Kristo Yesu kuwaombea watu wake ni, waweze kukombolewa kutoka kwa ulimwengu huu ambao ni mwovu na unatawaliwa na shetani. Shetani hana nguvu zote, lakini ako na nguvu za kudanganya na kuharibu. Biblia inasema kwamba, “Ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu” (1 Yohana 5:19). Yule mwovu anaitwa mungu wa dunia, na lengo lake kuu ni kuhakikisha kwamba watu hawaelewi neno la Mungu. “Mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu” (2 Wakorintho 4:4).

Hadi tutakapookolewa, tunaishi maisha kulingana na ulimwengu huu mwovu na tunamtumikia shetani. “Mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi ndani ya wale wasiotii” (Waefeso 2:2). Wale wote ambao hawajaokoka ni watumwa wa shetani hata kama hawaelewi jambo hili na kulikataa. Wanafikiria kwamba wao wako huru, lakini ukweli ni kwamba wao ni watumwa wa shetani. Bibilia inasema hivi kuhusu vitu vya ulimwengu huu, “Huwaahidia uhuru hao waliowanasa, wakati wao wenyewe ni watumwa wa ufisadi. Kwa maana mtu ni mtumwa wa kitu cho chote kinachomtawala” (2 Petro 2:19).

Hii ndiyo sababu Biblia inatuambia kwamba, “Wala msiufuate namna ya dunia hii; bali mgeuzwa kwa kufanywa upya nia zenu” (Warumi 12:2). Kwa ufupi kile Biblia inasema hapa ni kwamba tusifanywe watumwa wa anasa na mali za ulimwengu huu, bali tuwe huru katika Kristo Yesu.

Watu wa ulimwengu huwaza kwamba wao wako huru na ni wenye hekima, lakini Biblia inasema hivi kuwahusu, “Msijidanganye. Kama mtu ye yote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima. Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kama ilivyoandikwa: ‘Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao’” (1 Wakorintho 3:18-19). “Kwa maana ujumbe wa msalaba kwa wale wanaopotea ni upuzi, lakini kwetu sisi tunaokolewa ni nguvu za Mungu” (1 Wakorintho 1:18). Watu wa ulimwengu ambao wanaishi maisha ya dhambi hawako huru, wao ni watumwa wa dhambi. Sisi ambao tumeokoka, “Tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa...nguvu na hekima ya Mungu” (1 Wakorintho 1:23-24).

Wakati Kristo alipokufa msalabani, aliwapa uhuru mamilioni ya watu. Alimshinda shetani na akaziharibu nguvu zake. Hii ndiyo sababu Yesu alisema, “Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje” (Yohana 12:31). Ujumbe wa Yesu Kristo kwa ulimwengu ni msimfuate shetani ambaye anawafanya watu kuwa watumwa wake, bali mje kwake awape uhuru.