Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuponye kutokana na ugonjwa wa dhambi na ule wa kawaida

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Heal Us from Moral and Physical Sickness

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 18 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Adhabu iliyotuletea sis amani ilikuwa juu yake, na kwa
majeraha yake sisi tumepona” (Isaya 53:5).

“Jioni ile, wakamletea watu wengi waliopagwa na peop, naye
akawatoa wale pepo kwa neno lake, na kuponya wagonjwa
wote” (Mathayo 8:16).

Kwa sababu Bwana Yesu Kristo aliteswa na kufa, siku moja ugonjwa wote utaisha katika ulimwengu. Wakati Mungu alipoumba ulimwengu hakukuwa na kifo au magonjwa, yote yalikuja kwa sababu ya hukumu wa Mungu ambao ulikuja kwa sababu ya dhambi ya Adamu. Biblia inasema, kwa maana “Viumbe vyote viliwekwa chini ya ubatili, si kwa chaguo lao, bali kwa mapenzi Yake Yeye aliyecitiisha katika tumaini” (Warumi 8:20). Mungu alihukumu ulimwengu kuonyesha kwamba dhambi ni kitu hatari sana.

Kwa kuanguka kwa mwanadamu, kifo kiliingia ulimwenguni: “Kwa hiyo, kama vile dhambi ilivyoingia ulimwenguni kupitia dhambi hii, mauti ikawafikia watu wote” (Warumi 5:12). Pia Biblia inatuambia kwamba matokeo ya dhambi yanawadhuru hata wale ambao wameokoka: “Wala si hivyo viumbe peke yao, bali hata sisi ambao ndio matunda ya kwanza ya Roho, kwa ndani tunalia kwa uchungu tukisubiri kwa shauku kufanywa wana wa Mungu, yaano, ukombozi wa miili yetu” (Warumi 8:23).

Mambo haya yote tunaona leo ni ya muda mfupi siyo ya milele. Tunatazamia wakati ambapo uchungu wa mwili hautakuwa tena. Laana ya Mungu juu ya viumbe siyo laana ya milele. Mungu alipanga kwamba siku moja laana hii itaondolewa kwa viumbe vyote: “Viumbe vyote vipate kuwekwa huru kutoka katika utumwa wa kuharibika na kupewa uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu” (Warumi 8:21).

Kristo alikuja katika ulimwengu kukomboa ulimwengu kutoka katika laana hii. Hii ndiyo sababu wakati alikuwa hapa aliwaponya watu wengi. Kulikuwa na wakati ambapo watu walikusanyika kwake na akawaponya wote (Mathayo 8:16; Luka 6:19). Kwa kuwaponya watu alikuwa akionyesha kwamba siku moja ataondoa laana ambayo iko juu ya viumbe. “Atafuta kila chozi, kutoka katika macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (Ufunuo 21:4).

Bwana Yesu alichukua kifo juu yake, na kwa njia hii aliweza kushinda kifo. Wakati alipokuwa msalabani Mungu alimhukumu; kwa hivyo alishinda kifo na magonjwa. Hii ndiyo sababu nabii Isaya anasema, “Alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sis amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona” (Isaya 53:5). Bwana Yesu Kristo kwa kifo chake alikomboa viumbe kutokana na laana vilivyokuwamo.

Siku moja kila ugonjwa utaondolewa katika ulimwengu huu. Kutakuwapo na ulimwengu mpya, tutakuwa na miili mipya na hakutakuwa na kifo tena (1 Wakorintho 15:54; 2 Wakorintho 5:4). Biblia inasema, “Mbwa mwitu na mwanakondoo watalisha pamoja, naye simba atakula nyasi kama maksai” (Isaya 65:25). Wale wote ambao wanampenda Kristo wataimba nyimbo za kumshukuru mwana-kondoo ambaye alikufa kwa ajili ya kutukomboa kutoka kwa dhambi, kifo na magonjwa.