Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili awe fidia ya wengi

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Become a Ransom for Many

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 8 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa kuwa hata Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali
kutumika na kuutoa whai Wake kuwa ukombozi kwa ajili ya,
wengi” (Marko 10:45).

Biblia inafunza kwamba wale wote ambao hawajaokoka ni watumwa wa dhambi. Biblia inaendelea kutuambia kwamba njia moja tu ya kuokolewa ni kutolewa kutoka kwa utumwa wa dhambi. Hii haimaanisha kwamba Kristo alimlipa shetani wakati alikufa kwa ajili ya watu wake. Msalabani shetani hakulipwa chochote, bali alishindwa. Bwana Yesu Kristo alikuwa mwanadamu kamili “Ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, shetiani” (Waebrania 2:14). Msalabani shetani alishindwa.

Wakati Kristo anasema, “Kutoa maisha yangu kuwa fidia ya wengi” (Marko 10:45), anamaanisha kwamba maisha yake ambayo alitoa ndiyo fidia ambayo itawaletea faida wengi.

Labda wewe unajiuliza swali hili, Je, ni nani aliyelipwa fidia hii? Biblia inasema kwamba fidia hii ililipwa kwa Mungu. Biblia inasema, “Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhaihu kwa Mungu” (Waefeso 5:2). “Basi si zaidi sana damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo waa kutusafisha dhamira zetu” (Waebrania 9:14). Ilimbidi Kristo afe kwa ajili yetu kwa sababu tulitenda dhambi dhidi ya Mungu na kupungukiwa na utukufu wake (Warumi 3:23). Ni kwa sababu ya dhambi zetu, ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu (Warumi 3:19). Kwa hivyo wakati Kristo alipojitoa kuwa fidia yetu, Biblia inasema kwamba tumewekwa huru kutokana na hukumu ya Mungu. “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” (Warumi 8:1). Sisi sote tunahitaji kuondolewa katika hukumu ya mwisho ya Mungu (Warumi 2:2; Ufunuo 14:7).

Kwa hivyo Kristo alikufa kuwa fidia ili tuweze kuondolewa katika hukumu ya Mungu. Hii ndiyo sababu Kristo aliwaambia wanafunzi wake mara kwa mara, “Mwana wa Adamu atasalitiwa na kutiwa mikononi mwa watu nao watamwua” (Marko 9:31). Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alijiita, “Mwana wa Adamu.” Mungu hawezi kufa, lakini mwanadamu hufa. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, hii ndiyo sababu alikuwa mwanadamu.

Biblia ni wazi kwamba Yesu hakulazimishwa kufa msalabani. Kristo mwenyewe anasema kwamba, “Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika” (Marko 10:45). Alijitolea kuwa mtumishi wetu na alijitolea kufa kwa ajili yetu. Ndiyo sababu anasema, “Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe” (Yohana 10:18). Sababu ya Yeye kutoa maisha yake kwa ajili ya watu wake, ni kwa sababu ya upendo juu yao. Alichagua kufa kwa ajili yao kwa sababu aliwapenda.

Je, ni watu wangapi ambao Kristo alikufia msalabani? Alisema kwamba, “Alikuja kutoa maisha yake kuwa fidia ya wengi.” Wengi haimaanishi wote. Siyo kila mtu ataokoka; lakini watu wote wamealikwa kuja kwake ili waokolewe: “Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani, mwanadamu Kristo Yesu, aliyejitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wanadamu wote”(1 Timotheo 2:5-6).