Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili aweze kuvikwa taji la utukufu na heshima

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/So That He Would Be Crowned with Glory and Honor

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 49 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili
mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa
ajili ya kila mtu” (Waebrania 2:9)

“Bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa
katika umbo la mwanadamu. Alijinyenyekeza hata mauti, naam,
mauti ya msalaba! Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana na kumpa
jina lililo kuu kuliko kila jina” (Wafilipi 2:7-9)

“Anastahili Mwana-Kondoo, Yeye aliyechinjwa, kupokea uweza
na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa”
(Ufunuo 5:12)

Usiku kabla ya Kristo kufa msalabani Kalivari, aliomba, “Baba, unitukuze mbele Zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na Wewe kabla ulimwengu haujakuwako” (Yohana 17:5). Aliomba kwa Babaye ili aweze kupewa utukufu. Babake alijibu maombi yake: “Amevikwa taji ya utukufu na heshima kwa sababu alistahimili mauti, ili kwamba kwa neema ya Mungu apate kuonja mauti kwa ajili ya kila mtu” (Waebrania 2:9). Kwa sababu alijitolea kufa kwa ajili ya watu wake, Mungu Baba amemvika na taji la utukufu. “Alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana na kumpa jina lililo kuu kuliko kila jina” (Wafilipi 2:8-9). “Anastahili Mwana- Kondoo, Yeye aliyechinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!” (Ufunuo 5:12). Kristo Yesu alipokea utukufu kutoka kwa Mungu Baba kwa sababu alitii Baba hata kwa mauti.

Biblia inatufunza kwamba sababu ya Yesu Kristo kuvikwa na utukufu na heshima, ni aweze kuwaletea watu wake furaha na kutosheka. Fikiria juu ya mwanamume mmoja na mke wake ambao wamealikwa kwa sherehe fulani. Lakini wakati wanafika huko mwanamume anapokelewa kwa heshima kubwa sana na kutukuzwa machoni pa kila mtu. Je, mke wake atajihisi aje? Kwa kawaida atajihisi mwenye furaha sana kwa sababu mume wake anaheshimiwa na kutukuzwa na watu wote. Kwa njia hiyo hiyo, kanisa la Bwana Yesu Kristo ndiyo bibi arausi wake. Wakati Bwana Yesu Kristo anavikwa heshima na Mungu Baba, watu wa Mungu wanakuwa na furaha mingi sana; kwa sababu mtu ambaye wanampenda amevikwa na heshima na utukufu na Mungu Baba. Kwa hivyo utukufu wa Kristo Yesu unawaletea watu wake furaha kubwa.

Hii ndiyo sababu usiku kabla afe, Bwana Yesu Kristo aliomba, “Baba, shauku Yangu ni kwamba, wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu Wangu, yaani, utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu” (Yohana 17:24). Bwana Yesu Kristo anataka tuuone utukufu wake ili tupate furaha.