Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tuweze kuwa na ujasiri wa kuja kwa Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Give Us Confident Access to the Holiest Place

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 24 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa hiyo, ndugu zangu, kwa kuwa tunao ujasiri wa kupaingia
Patakatifu pa Patakatifu kwa damu ya Yesu” (Waebrania 10:19).

Katika Agano la Kale Waisraeli waliamrishwa kujenga hema ambalo liliitwa Hema la Kukutania. Wakati Waisraeli walitoka Misri na wakafika katika mlima Sinai, Mungu aliwapatia maagizo fulani kuhusu jinsi wanafaa kulijenga hema hilo. Waliambiwa, “Hakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na kile kielelezo ulichoonyeshwa kule mlimani” (Kutoka 25:40).

Baada ya miaka 1,400 Bwana Yesu Kristo alikuja hapa ulimwenguni na ilikuwa wazi kwamba hekalu hili lilikuwa mfano wa kile ambacho kilikuwa mbinguni. Katika Agano Jipya tunansoma, “Wanahudumu katika patakatifu palipo mfano na kivuli cha ile iliyoko mbinguni. Hii ndiyo sababu Mose alionywa alipokaribia kujenga hema, akiambiwa: ‘Hakikisha kuwa unafanya kila kitu sawasawa na kile kielelezo ulichoonyeshwa kule mlimani” (Waebrania 8:5).

Kwa hivyo hema katika Agano la Kale na makuhani na sadaka yote yalikuwa mfano wa yale yalikuwa mbinguni. Yalikuwa hapo kuwaonyesha watu kwamba ukweli wa mambo haya ulikuwa mkuu zaidi. Katika hema kulikuwepo na mahali ambapo makuhani waliingia kila mara na damu ya wanyama. Kwa njia hiyo hiyo mbinguni kuna mahali ambapo Kristo Yesu aliingia na damu yake. Hakuingia mara kwa mara bali aliingia mara moja.

“Kristo alipokuja akiwa Kuhani Mkuu wa mambo mema ambayo tayari yameshawasili, alipitia kwenye hema iliyokuu zaidi na bora zaidi, ambayo haikujengwa kwa mikono ya binadamu, hii ni kusema, ambayo si sehemu ya uumbaji huu. Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama, lakini aliingiia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele” (Waebrania 9:11-12). Hii inamaanisha kwamba wale wote ambao wameokoka wanaweza kuenda kwa Mungu mwenyewe kupitia kwa Kristo Yesu. Katika Agano la Kale ni kuhani mkuu pekee ambaye angeingia katika mahali patakatifu na angeingia mara moja kwa mwaka (Waebrania 9:7). Katika Agano la Kale kulikuwepo na pazia ambalo lilitenga mahali patakatifu. Biblia inatuambia kwamba wakati Kristo Yesu alikufa, “Pazia la hekalu likachanika vipande viwili, kuanzia juu hadi chini” (Mathayo 27:51).

Biblia inatuelezea kwamba hii inamaanisha, “Tunao ujasiri wa kupaingia Patakatifu pa Patakifu kwa damu ya Yesu, kwa njia mpya iliyo haituliyofunguliwa kwa ajili yetu kupitia kwenye lile pazia, yaani, mwili Wake” (Waebrania 10:19-20). Hatuwezi kuingia katika uwepo wa Mungu ikiwa hatujasamehewa dhambi zetu katika Kristo Yesu na kuoshwa kwa damu yake. Tukija katika uwepo wa Mungu ikiwa bado tuko katika dhambi zetu, tutakufa papo hapo. Hakuna chochote ambacho ni kichafu chaweza kuingia katika uwepo wa Mungu. Lakini ikiwa tumeokoka, basi tunaweza kuja katika uwepo wa Mungu bila kutatizika. Damu ya Kristo Yesu imetuosha na tumesamehewa kwa kifo chake.