Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tuweze kuwa naye baada ya kufa kwetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/So That We Would Be with Him Immediately After Death

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 40 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Yeye alikufa kwa ajili yetu ili kwamba kama tuko macho au
tukiwa tumelala tupate kuishi pamoja Naye.”
(1 Wathesalonike 5:10)

“Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida;
Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikae
pamoja na Krsito, jambo hilo ni bora zaidi.” (Wafilipi 1:21,23)

“Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili
huu na kwenda kukaa na Bwana.” (2 Wakorintho 5:8)

Biblia haisemmi kwamba miili yetu ni mibaya. Kuna dini zingine ambazo zinaamini kwamba mwili ni mbaya na nafsi yetu ndiyo tu safi. Lakini imani ya ukristo haifundishi hivyo. Kwetu wakristo, kifo ni adui kwa sababu kinaua miili yetu. Hivi ndivyo Biblia inasema kuhusu miili yetu: “Mwili wa mwanadamu haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana na Bwana kwa ajili ya mwili.” (1 Wakorintho 6:13). Bwana ni kwa mwili, kumaanisha Mungu anashughulika na miili yetu.

Lakini wakati tunakufa, mwili na nafsi hutengana. Mwili unazikwa kwa mchanga na kuoza. Na nafsi inaenda kukaa na Bwana. Hii ni faraja kubwa kwa wale wameokoka, kwa sababu nafsi zitakuwa na Bwana.

Biblia inasema mwili ni kama nguo kwa nafsi: “Kwa sababu hatutaki kuvuliwa bali kuvikwa makao yetu ya mbinguni ili kwamba kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.” (2 Wakorintho 5:4). Kile Paulo anasema hapa ni kwamba angependa kutoka kwa huu mwili wa duniani na kuingia katika mwili wa ufufuo. Hakuwa anataka wakati ambapo nafsi iwe bila mwili. Wale ambao wako hai watageuzwa na kupewa miili mipya wakati Kristo atakaporudi.

Paulo tena anaongea kuhusu wakati nafsi itakuwa na Bwana bila mwili. Anasema, “Kuishi ni Kristo, na kufa ni faida” (Wafilipi 1:21). Nafsi kuwa na Yesu Kristo ni faida kubwa hata ikiwa haina mwili. Hii ni kwa sababu mtu ameokoka akifa anaenda kuwa na Yesu. Hii ndiyo maana Paulo anasema, “Ninatamani kuondoka nikae na pamoja na Kristo, jambo hilo ni bora zaidi.” (Wafilipi 1:23).

Kuwa na Kristo, Paulo anasema ni vizuri zaidi kuliko kuwa katika mwili hapa duniani. Ni vizuri zaidi kwa sababu nafsi yake iko na Kristo na imetoka katika ulimwengu wa dhambi na maumivu. Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Naam, tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kuenda kuwa na Bwana” (2 Wakorintho 5:8). Wale wameokoka wataenda kukaa na Bwana wakikufa na wataishi naye kwa amani na furaha. Watakuwa nyumbani naye.

Hii ni mojawapo ya sababu kuu kwa nini Kristo alikufa. “Yeye alikufa kwa ajili yetu ili kwamba kama tuko macho au tukiwa tumelala tupate kuishi pamoja Naye.” (1 Wathesalonike 5:10). Mwili utaenda mchangani, bali nafsi itakuwa na Bwana mbinguni. Na wakati Bwana atakaporudi, atampatia kila mtu mwili mpya ambao utaishi milele.