Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili ukuhani wa Agano la Kale ukomeshwe na Yeye awe Kuhani wa milele

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Bring the Old Testament Priesthood to an End and Become the Eternal High Priest

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 26 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa
kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani, lakini kwa
sababu Yesu aishi milele, anao ukuhani wa kudumu. Kwa hiyo
anaweza kuwaokoa kabisa wale wanaomjia Mungu kupitia
Kwake, kwa sababu Yeye adumu daima kuomb akwa ajili yao.
Kwa kuwa ilitupasa tuwe na Kuhani Mkuu wa namna hii, yaani,
aliye mtakatifu, aiye na dosari, aliyetengwa na wenye dhambi na
kuinuliwa juu ya mbingu. Yeye alitoa dhabihu kwa ajili ya
dhambi zao mara moja tu, alipotoa Mwenyewe”
(Waebrania 7:23-27).

“Kwa maana Kristo hakuingia kwenye patakatifu palipofanywa
kwa mikono ya mwanadamu, ambao ni mfano wa kile kilicho
halisi. Yeye aliingia mbinguni penyewe, ili sasa aonekane mbele
za Mungu kwa ajili yetu. Wala hakuingia mbinguni ili apate
kujitoa Mwenyewe mara kwa mara, kama vile kuhani mkuu
aingiavyo Patakatifu pa Patakatifu kila mwaka kwa damu
ambayo si yake mwenyewe. Ingekuwa hivyo, ingelimpasa Kristo
kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini
sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe
dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu.”
(Waebrania 9:24-26).

“Katika mapenzi hayo sisi tumetakaswa na kufanywa watakatifu
kwa njia ya sadaka ya mwili wa Yesu Kristo alioutoa mara
moja tu” (Waebrania 10:11-12).

Katika Biblia tunapata maneno haya: “mara moja.” Maneno haya yanamaanisha kwamba kuna jambo kuu ambalo lilitendeka na halifai kutendeka tena. Ni kama mtu ambaye ananunua shamba, wakati ananunua shamba hilo linakuwa lake na hafai kulinunua tena.

Katika agano la kale kuhani mkuu alikuwa anaingia mahali patakatifu mara moja kila mwaka ili atoe sadaka za wanyama kwa ajili ya dhambi za watu. Sadaka ya kuhani mkuu ilikuwa itolewe mara kwa mara. Mungu alikubali sadaka hizo na aliwasamehe watu dhambi zao lakini mwaka ambao uliyofuata kuhani huyo huyo alihitajika tena atoe sadaka hiyo ndipo watu wasamehewe dhambi zao za mwaka huo.

Sadaka hizi zilikuwa zitolewe kila mwaka kwa sababu hazikuweza kuondoa dhambi kabisa. Biblia inasema kwamba, “Lakini zile dhabihu zilikuwa ukumbusho wa dhambi kila mwaka.” (Waebrania 10:3). Watu walijua kwamba walileta wanyama wakiwa sadaka lakini pia walijua kwamba mambo haya wangeyafanya kila mwaka. Hakuna mnyama ambaye angezifia dhambi za mwandamu. Hata makuhani wenyewe walikuwa kwanza watoe dhabihu ya dhambi zao. Sadaka ya wanyama haingeweze kuleta msamaha wa dhambi wa milele: “Kwa sababu haiwezekani damu ya mafahali na mbuzi kuondoa dhambi” (Waebrania 10:4).

Watu katika Agano la Kale walijua kwamba siku moja Mungu angeleta sadaka takatifu, ile ambayo ingezibeba dhambi za wanadamu wote na kuziondoa kabisa. Hili ni jambo ambalo walijua kwamba siku moja lingetendeka.

Sadaka hii ni Kristo Yesu mwenyewe. Yeye ndiye sadaka ambayo ilitolewa mara moja. Hakuwa na dhambi ndiyo maana hakutoa dhabihu ya dhambi zake kwanza. Yeye ni wa milele kwa hivyo hahitaji kubadilishwa. Yeye ni mwanadamu kamili ndipo anaweza kuzibeba dhambi za wanadamu na kuzilipia fidia. Kwa hivyo sadaka yake ndiyo sadaka ya mwisho, hatuhitaji mtu mwingine; Kristo peke yake ndiye anayeweza kutusamehe dhambi zetu na kutuosha na atulete kwa Mungu.