Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuhakikisha kufufuka kwetu kutokak wa wafu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Secure Our Resurrection from the Dead

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 41 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti Yake, bila
shaka tutaungana naye katika ufufuo Wake” (Warumi 6:5)

“Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu
anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa
wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa kwa njia ya Roho
Wake akaaye ndani yenu.” (Warumi 8:11)

“Hili ni neno la kuaminiwa: Kwa maana kama tumekufa pamoja
naye, tutaoishi pamoja naye.” (2 Timotheo 2:11)

Bwana Yesu alifanya miujiza mingi wakati alipokuwa hapa ulimwenguni. Alimfufua mtoto msichana wa miaka 12 na wanaume wawili ambao walikuwa wamekufa (Marko 5:41-42; Luka 7:14-15; Yohana 11:43-44). Lakini wale watu ambao aliwafufua hawakuishi milele katika miili hiyo kwani walikufa tena. Wakati Bwana Yesu Kristo alipofufuka kutoka kwa wafu, alishinda nguvu za kifo ili watu wote ambao wamepewa miili ya ufufuo wasije wakakufa tena.

Wakati Mungu alipomfufua Bwana Yesu Kristo kutoka kwa wafu, Mungu alikuwa anasema kwamba Bwana Yesu Kristo alifaulu katika kutulipia fidia ya dhambi zetu. Sadaka ambayo alitoa msalabani ilikubalika na Mungu. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Alijinyenyekeza hata mauti, naam, mauti ya msalaba! Kwa hiyo, Mungu alimtukuza sana na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina.” (Wafilipi 2:8-9). Wakati Kristo alipokuwa msalabani alilia kwa sauti akisema, “imekwisha” (Yohana 19:30). Wakati Mungu alipomfufua Kristo kutoka kwa wafu, Mungu alikuwa akisema, “Kweli imekwisha!” Kristo alikuwa amefidia dhambi zetu msalabani na alituondoa katika nguvu za dhambi.

Siku tatu baada ya kifo chake, Kristo alishinda kifo. Kwa sababu alifufuka, kifo hakina nguvu tena za kuwaangamiza miili ya ufufuo wa watu wote. Hii ndiyo sababu Kristo anasema, “Mimi ni Alpha na Omega”, asema Bwana Mungu, “Aliyeko, aliyekuwako na atakayekuja, Mwenyezi” (Ufunuo 1:8).

Biblia ni wazi kwamba wale wote ambao wameokoka watafufuliwa kutoka kwa wafu naye Kristo na watakaa naye milele. “Kwa maana ikiwa tumeungana naye katika mauti Yake, bila shaka tutaungana naye katika ufufuo Wake.” (Warumi 6:5). “Kwa kuwa tumeamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka, hata hivyo, Mungu kwa njia ya Yesu atawafufua pamoja naye wale waliolala mautini.” (1 Wathesalonike 4:14). “Naye Mungu aliyemfufua Bwana kutoka kwa wafu atatufufua sisi pia kwa uweza Wake.” (1 Wakorintho 6:14).

Biblia inatufundisha jinsi Bwana Yesu alivyoshinda nguvu za kifo. Biblia inasema, “Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria.” (1 Wakorintho 15:56). Hii inamaanisha kwamba sisi sote tumetenda dhambi na tutahukumiwa milele. Biblia inaendelea kusema, “Lakini ashukuriwe Mungu, Yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.” (1 Wakorintho 15:57). Kwa ufupi hitaji la torati lililipwa kwa maisha na kifo cha Bwana Yesu Kristo. Wakati dhambi zetu zinasamehewa, torati haiwezi kutuhukumu kwani haina nguvu ya kutugusa, hatuwezi kuhukumiwa milele. Badala yake, “Ghafla, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutoharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: ‘ Mauti imemezwa kwa kushinda’ ” (1 Wakorintho 15:52;54). Hii ndiyo sababu Yesu anakuita uje kwake. “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi” (Yohana 11:25).