Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kutukomboa kutoka kwa uoga wa kifo

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Free Us from Bondage to the Fear of Death

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 39 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki
katika ubinadamu wao na kuwaweka huru wale waliokuwa
utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti”
(Waebrania 2:14-15)

Yesu alimwita shetani mwuuaji: “Yeye alikuwa mwuuaji tangu mwanzo; wala hakushikana na kweli maana hamna kweli ndani yake. Asemapo uongo husema yaliyo yake mwenyewe kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo” (Yohana 8:44). Haja kuu ya shetani si kuua mtu bali ni kuhakisha mtu huyo ataishi milele jahanum. Shetani anataka wafuasi wake wafurahiye maisha ya anasa za dhambi hapa duniani na mwishowe kuhukumiwa milele jahanum. Hii ndiyo shetani anataka kwa wafuasi wake.

Tunahitaji kukumbuka kwamba si shetani anawapeleka watu jahanum bali ni dhambi zao ndiyo zinazowapeleka watu hawa jahanum. Jambo moja tu ambalo litamfanya mtu kwenda jahanum ni kwa sababu ya kukosa kutubu dhambi zake na kumwomba Bwana Yesu msamaha. Shetani hawezi kutuma mtu jahanum, anaweza tu kuwadanganya watu. Shetani huwadanganya watu kwamba maisha ya dhambi ni mazuri na hakuna haja ya kuokoka. Ikiwa watu wanakataa kudanganywa, shetani hana mamlaka kabisa.

Hii ndiyo kazi Kristo alikuja kufanya, kuondoa uwezo wa shetani wa kuwadanganya watu. Ili afanye hivi, Kristo alizichukua dhambi zetu na akazikufia msalabani. Baada ya kuchukua dhambi zetu na kuzilipia fidia msalabani, shetani hana uwezo tena wa kuwazuia watu wa Mungu kuokoka. Sasa shetani hana uwezo wowote wa kuwaangamiza wale wameokoka. Ghadhabu ya Mungu imeondolewa, na huruma ya Mungu ikawa ndiyo ngao yetu na shetani hawezi akafaulu dhidi yetu.

Kwa sababu Yesu Kristo alikuwa anakuja kutuokoa sisi, ilimbidi awe mwanadamu kamili ili apitie mauti. Ni kifo cha Mwana wa Mungu pekee kingeondoa nguvu za shetani. Hii ndiyo sababu Biblia inasema, “Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao” (Waebrania 2:14). Yesu alikuwa mwanadamu kamili kwa sababu watu wale alikuja kuwaokoa walikuwa wanadamu kamili. Wakati Kristo alikufa alizichukua dhambi zetu, kwa hivyo shetani hana uwezo wa kutuhukumu.

Kwa hivyo kusudi la Yesu lilikuwa hili: uoga wa kifo uondolewe. Kupitia kifo chake, “na kuwaweka huru wale waliokuwa utumwani maisha yao yote kwa sababu ya kuogopa mauti” (Waebrania 2:15). Uoga kwa sababu ya kifo hutufanya kuwa watumwa kwa sababu hatujui ni nini itafanyika baada ya kufa. Lakini kifo cha Yesu huondoa uoga huo wote. Wale wote wameokoka wamehakikishiwa nafasi mbinguni na hawapaswi kuogopa kamwe.

Mauti inaweza tu kuua miili yetu wala haiui nafsi. Nafsi zetu ziko kwa Kristo. Na wakati Yesu Kristo atakaporudi, miili yetu itafufuliwa tena: “Nanyi ikiwa Roho wa Mungu aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu anakaa ndani yenu, Yeye aliyemfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu ataihuisha pia miili yenu ambayo hufa kwa njia ya Roho Wake akaaye ndani yenu” (Warumi 8:11). Wale wameokoka wamewekwa huru kutoka kwa kila uoga, na Biblia inatueleza jinsi ya kutumia huru wetu: “Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.” (Wagalatia 5:13).