Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kutukomboa kutokana na mwenendo wa mababu wetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Free Us from the Futility of Our Ancestry

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 28 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutoka
mwenendo wenu usiofaa ambao mliurithi kutoka kwa baba zenu,
si kwa vitu viharibikavyo, yaani, kwa fedha na dhahabu, bali kwa
damu ya thamani ya Kristo, kama ile ya Mwana-kondoo asiye na
dosari wala doa” (1 Petro 1:18-19)

Watu wengi leo wanaamini kwamba mababa zao ambao wamekufa au wanaishi wako na ushawishi katika maisha yao. Wanaamini kwamba hali ya maisha ya mababa zao na dhambi zao zinaendelea kushawishi maisha yao. Wanawaza kwamba maisha yao yako jinsi yalivyo kwa sababu ya dhambi za mababa zao.

Lakini Biblia inasema kwamba, “Mlikombolewa kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu.” Biblia inazungumza kuhusu maisha ya wale ambao hawajaokoka, ni maisha matupu ambayo hayana maana na hayana na hayana faida. Maisha haya yanagusia maisha ya mababa zetu kwa sababu tulirithi maisha haya na tabia hizi kutoka kwao. Kifo cha Bwana Yesu Kristo kiliwakomboa watu wake kutoka kwa maisha haya. Hii inamaanisha kwamba wale wote ambao wameokoka hawafai kuwa na wasiwasi kuhusu nguvu na ushawishi wa dhambi za mababa zao.

Kristo anatukomboa kutoka kwa mwenendo ya mababa zetu si kwa vitu viharibikavyo, yaani kwa fedha au dhahabu. Fedha na dhahabu ni vile vitu ambavyo ni vya thamani sana kwa walimwengu. Biblia inasema hapa kwamba vitu hivi haviwezi vikatukomboa kutoka kwa mwenendo wa mababa zetu. Tunajua kwamba hata wale ambao ni matajiri sana ni watumwa wa tamaduni za mababa zao. Wakati wanaoa au wakati wako na matanga hawako huru kufanya jinsi wanavyotaka, bali wanafungwa kufanya kulingana na tamaduni za mababa zao.

Fedha na dhahabu hazina nguvu za kutukomboa kutoka kwa tamaduni zetu, bali ni damu ya Kristo Yesu ambayo iko na nguvu za kutukomboa kutoka kwa mambo haya yote. Biblia inasema kwamba damu yake ni damu ya thamani, kama ya Mwana-kondoo asiye na ila. Wakati Kristo alikufa kwa ajili ya watu wake, alijua kwamba walikuwa wamefungwa na tamaduni zao. Alikufa ili tuwe huru kutokana na mambo haya. Hii ni moja wapo wa sababu za Kristo Yesu kufa.

Hakuna tamaduni ambazo zinaweza kukufunga wakati umekuja kwa Kristo Yesu kwa imani. Sasa umesamehewa dhambi zako zote, umeoshwa na umevalishwa utakatifu wa Kristo Yesu na kufanywa mwana wa Mungu. “Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo, wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli” (Hesabu 23:23). Wakati Yesu Kristo alipokufa alituchukilia baraka zote za mbinguni kwa wale ambao wanamwamini. Mungu akikubariki hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukulaani.