Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kutuondoa kwa utumwa wa dhambi

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Free Us from the Slavery of Sin

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 29 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwake Yeye aliyetupenda na ambaye ametuweka huru kutoka
katika dhambi zetu kwa damu Yake, akatufanya sisi kuwa ufalme
na makuhani, tumtumikie Mungu Wake ambaye ni Baba yake.
Utukufu na uwezo vina Yeye milele na lilele!” (Ufunuo 1:5-6)

“Vuvyo hivyo Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili
awatakase watu kwa damu Yake mwenyewe” (Waebrania 13:12)

Dhambi humwangamiza mwanadamu kwa njia mbili. Kwanza, inatufanya kuwa wenye hatia mbele za Mungu ili tuwe chini ya hukumu wa Mungu. Pili, dhambi hutufanya tuwe wachafu machoni pa Mungu. Dhambi huleta hukumu na dhambi hutufanya watumwa.

Damu ya Kristo Yesu hutuondoa katika mambo haya yote. Kwanza, kwa kifo chake msalabani, Bwana Yesu Kristo alizilipia dhambi zetu na kwa hivyo hatia yetu iliondolewa. Pili, damu ambayo Bwana Yesu Kristo alimwaga inatuosha kutokana na uchafu wa dhambi na kutukomboa kutoka kwa dhambi zetu.

Biblia ni wazi kwamba hadi wakati tutakapotolewa katika utumwa wa dhambi hatuwezi kumtii Mungu. Kristo alisema, “Amri mpya nawapa: Mpendane kama Mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane” (Yohana 13:34). Hapa Kristo Yesu anatupa mfano wa kufuata, lakini hatuwezi kuufuata hadi tukombolewe kutoka kwa dhambi.

Dhambi ni kitu kibaya ambacho kinahitaji nguvu za Mungu kabla ya kukombolewa. Sisi wenyewe kwa nguvu zetu hatuwezi kujikomboa. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alikufa; kutukomboa kutoka kwa dhambi.

Jinsi anavyotukomboa ni, kwanza anaondoa hatia ya dhambi kwetu, halafu anatuondoa katika nguvu za dhambi. Mungu kwanza anatusamehe dhambi zetu halafu anatuleta katika ushirika naye, halafu anaanza kufanya kazi ndani mwetu kuondoa dhambi mioyoni mwetu.

Kwa wale ambao wameokoka, nguvu za Mungu zinafanya kazi ndani mwao kuwaondoa kwa maisha ya dhambi. Bado wako na dhambi ndani mwao, lakini Mungu ako anafanya kazi ya kuondoa dhambi hiyo kwa njia ya Roho Mtakatifu. Biblia inazungumza kuhusu tunda la Roho: “Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” (Wagalatia 5:22-23). Kwa sababu Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani mwetu, Mungu anasema, “Dhambi haitakuwa na mamlaka juu yenu, kwa sababu hampo chini ya sheria, bali chini ya neema” (Warumi 6:14). Kwa sababu tuko chini ya neema ya Mungu, tuko na nguvu za Mungu ndani mwetu. Hii inamaanishi ya kwamba, pole pole dhambi inaondolewa ndani mwetu na tunageuzwa katika mfano wa Kristo Yesu. Hii ndiyo kazi ya Mungu ambayo anafanya ndani mwetu, ni kwa neema yake. Hii ndiyo sababu Paulo anasema, “Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.” (1 Wakorintho 15:10). Mungu kwa neema yake anatukomboa kutokana na hatia na utumwa wa dhambi kwa imani ndani ya Kristo.