Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kutuwezesha kuishi kwa imani ndani Yake

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Enable Us to Live by Faith in Him

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 34 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi
bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika
mwili, ninaishi kwa imani ya Mungu, aliyenipenda na kujitoa
kwa ajili yangu..” (Wagalatia 2:20).

Katika msitari huu, Paulo anasema kwamba alisulubiwa na sasa anaishi. Paulo anamaanisha kwamba alikufa na Yesu Kristo na sasa anaishi kwa utukufu wake, yaani Yesu anaishi ndani yake.

Katika msitari huu tunaona maana ya kuokoka. Wakati mtu anaokoka, jambo fulani kubwa hufanyika kwake. Ule utu wake wa kale hufa na badala yake kiumbe kipya hufanyika. “Mtu akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya” (2 Wakorintho 5:17). “Hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Kristo Yesu, yaani, mmeokolewa kwa neema. Mungu alitufufua pamoja na Kristo na kutuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu.” (Waefeso 2:5-6).

Wakati Yesu Kristo alikufa aliwachukua watu wake pamoja naye kaburini: walikufa pamoja naye: “Utu wetu wa kale ulisulubiwa opamoja naye ili ule mwili wa dhambi upate kuangamizwa, nasi tusiendelee kuwa tena watumwa wa dhambi.” (Warumi 6:6). Wakati tunaokoka tunaunganishwa na Kristo. Utu wa kale hufa.

Katika mstari huu, Paulo anaendelea kueleza hali ya mtu ambaye amezaliwa mara ya pili, yaani mtu ambaye ni kiumbe kipya. Paulo anasema hii kuhusu mtu ambaye ameokoka, “Kristo anaishi ndani mwake.” Huu ni ukweli kwa kila mtu ambaye amekoka, kwamba Kristo anaishi ndani yake. Mtu ambaye ameokoka huwa anaishi chini ya mwongozo na utawala wa Yesu Kristo na anaishi maisha yake kwa nguvu za Yesu Kristo. “Naweza kufany amambo yote katik aYeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13); “Ninajitaabisha, nikijitahidi kwa kadiri ya nguvu zile ambazo kwa uwezo mwingi hutenda kazi ndani yangu” (Wakolosai 1:29). Hii ndiyo sababu mtu ambaye amezaliwa upya husema “Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu” (Warumi 15:18).

Hivi ndivyo msitari wa Wagalatia 2:20 unamaanisha. Kristo anaishi ndani yetu, Kristo anatuongoza na Kristo anatupatia nguvu. Hii ndiyo sababu alikufa ili watu wake waishi kwa imani ndani yake: “Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.”

Kwa hivyo kile Paulo anasema hapa ni kwamba mtu akiokoka, Kristo huja na kukaa ndani yake na kutoka wakati huo mtu huyo anaishi maisha ya imani ndani ya Kristo. Kristo anaishi ndani ya watu wake na huwapa mwongozo, uwezo na nguvu. Mtu ambaye ameokoka hupokea haya yote kwa imani.