Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuumba jamii moja ya wafuasi ambao wanajitolea kwake
Kutoka Gospel Translations Swahili
Pcain (Majadiliano | michango) |
Pcain (Majadiliano | michango) d (Aliulinda "Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuumba jamii moja ya wafuasi ambao wanajitolea kwake" ([edit=sysop] (indefinite) [move=sysop] (indefinite))) |
Toleo lililopo 17:30, 11 Agosti 2011
By John Piper
About The Death of Christ
Chapter 38 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?
Translation by Desiring God
“Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane mwenyewe,
achukue msalaba wake kila siku na anifuate” (Luka 9:23).
“Ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili
kuwa Wangu” (Mathayo 10:38).
Yesu Kristo alikufa ili awe na wafuasi ambao wataacha yote ya dunia kwa sababu yake. Biblia inatuambia kwamba Yesu Kristo alikuwa tayari kwenda Kalivari na, “Alikaza uso Wake kwenda Yerusalemu” (Luka 9:51). Hakuna mmoja angeweza kumzuia kwenda Kalivari na kutoa maisha yake kuwa sadaka kwa watu wake, Yeye mwenyewe aliamua kufanya hivyo. Wakati mtu mmoja alimwambia akiwa njiani kwenda Yerusalemu kwamba atakuwa hatarini kwa sababu ya Herode, Yesu alisema, “Nendeni mkamwambia yule mbweha, ‘Ninafukuza pepo wachafu na kuponya wagonjwa leo na kesho, nami siku ya tatu nitaikamilisha kazi Yangu” (Luka 13:32). Yesu alienda Yerusalemu akijua kwamba atashikwa na kuhukumiwa kifo. Wakati umati wa watu ulimshika, usiku huo kabla hajakufa alisema “Haya yote yametukia ili maandiko ya manabii yapate kutimia” (Mathayo 26:56).
Yesu aliteseka na anatarajia wafuasi wake wawe tayari kufuata njia hiyo hiyo. Yesu aliamua kufuata njia ya Kalivari ambayo ilikuwa na mateso mengi, na pia anataka wafuasi wake wafanye jinsi alivyofanya. Yesu anasema, “Ye yote anayetaka kunifuata ni lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku na anifuate” (Luka 9:23). Wakati Yesu Kristo alienda msalabani, nia yake kuu ilikuwa kuumba jamii moja ya wafuasi ambao wanajitolea kwake.
Yesu anatuambia tuubeba msalaba wetu kila siku. Hii inamaanisha kwamba ikiwa tutaokolewa ni lazima tufe kwa dhambi zetu, kama vile Yesu Kristo alikufa kwa sababu ya dhambi zetu. Wakati Yesu Kristo anamwambia mtu ambaye ameokoka aubeba msalaba wake kila siku, huwa anamwambia aache dhambi zake na aishi maisha matakatifu. Ikiwa hatutaishi maisha matakatifu na badala yake kuishi kama watu wa dunia, basi sisi hatutakuwa wafuasi wa Yesu Kristo. Yesu alisema, “Ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa Wangu.” (Mathayo 10:38).
Hii inamaanisha kwamba wakati mtu anadai kwamba ameokoka, anapaswa kuendelea kuziacha dhambi zake na kufuata mfano wa Kristo kila wakati. Yeye ni lazima aangamize dhambi zake zote na awe kama Kristo. “Vivyo hivyo, jihesabuni wafu katika dhambi lakini mlio hai kwa Mungu, kama watu watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu Kwake kama viombo vya haki.” (Warumi 6:11).
Kuubeba msalaba ni zaidi ya kupigana na dhambi. Inamaanisha ni lazima tuwe tayari kupata aibu kwa sababu ya Yesu Kristo. “Vivyo hivyo Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu Yake mwenyewe. Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba” (Waebrania 13:12-13). Watu watatucheka sana wakati tunaokoka na hata katika nchi zingine watu wanauawa kwa sababu ya imani yao. Biblia inasema kuhusu watu hao ambao wanauliwa: “Nao wakamshinda kwa damu ya Mwanakondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa” (Ufunuo 12:11). Kwa hivyo Mwana-kondoo alimwaga damu yake ili tumshide shetani kwa kuamini katika damu yake na tufe katika dhambi zetu. Haya ndiyo maisha Kristo anatuitia.