Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuonyesha kwamba uovu mbaya sana umekusudiwa na Mungu kwa manufaa ya watu wake
Kutoka Gospel Translations Swahili
Pcain (Majadiliano | michango) (Created page with '{{info|Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Show That the Worst Evil Is Meant by God for Good}}<br> <blockquote> ''“ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu Mataifa n...') |
Pcain (Majadiliano | michango) d (Aliulinda "Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kuonyesha kwamba uovu mbaya sana umekusudiwa na Mungu kwa manufaa ya watu wake" ([edit=sysop] (indefinite) [move=sysop] (indefinite))) |
||
(Hatuonyeshi sahihisho moja la katikati.) |
Toleo lililopo 18:20, 11 Agosti 2011
By John Piper
About The Death of Christ
Chapter 50 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?
Translation by Desiring God
“ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu Mataifa na
waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya Mwanao Yesu
uliyemtia mafuta. Wao wakafanya yale ambao uweza wako na
mapenzi yako yalikuwa yamekusudia yatokee tangu zamani”
(Matendo ya Mitume 4:27-28).
Tunaishi katika ulimwengu ambao umejaa magonjwa na matatizo. Lakini Biblia inatufunza kwamba watu wa Mungu, wale ambao wameokoka, Mungu anahakikisha kwamba majaribu na mateso yetu yanatuletea manufaa kwa nafsi zetu. Hatuwezi kabisa kuelewa jambo hili, lakini Biblia inasema, “Mambo ya siri ni ya BWANA Mungu wetu.” (Kumbukumbu la Torati 29:29).
Mara mingi katika Biblia tunasoma jinsi Mungu anavyobadilisha mambo mabaya kuwa mazuri. Katika kitabu cha Mwanzo, Yusufu aliuzwa katika nchi ya Misri na mandugu zake. Kwa miaka mingi Yusufu aliteseka katika nchi ya Misri. Lakini mwishowe, aliona kwamba huu ulikuwa mpango wa Mungu na kwamba Mungu alimtumia katika nchi hiyo kuwaokoa watu wa Israeli. Aliwaambia mandugu zake kwamba, “Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi” (Mwanzo 50:20).
Kwa njia hiyo hiyo, wakati Waisraeli walitaka mfalme, walitenda dhambi dhidi ya Mungu. Walimwambia Samweli, “Tunataka mfalme wa kututawala” (1 Samweli 8:19). Na baadaye walisema, “Tumeongezea uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme” (1 Samweli 12:19). Lakini Mungu alitumia dhambi hii kwa kufanya mazuri. Kutokana na ukoo wa Daudi, Mungu alimleta Kristo katika ulimwengu.
Katika Agano la Kale, tunasoma kuhusu dhambi kuu sana. Waisraeli pamoja na Herode na Pilato na watu wa Mataifa wote walifanya kazi pamoja kumwua Mwana wa Mungu. Mwana wa Mungu alikuwa hana dhambi lakini walimwua. Walifanya dhambi kubwa sana. Lakini kwa mpango wa Mungu, hata hii ilikuwa kwa manufaa ya watu wake. “Huyu mtu akiisha kutolewa kwa shauri la Mungu tangu zamani, ninyi, kwa mikono ya watu wabaya, mlimwua kwa kumgongomea msalabani” (Matendo ya Mitume 2:23). Njia ambayo Kristo alisalitiwa na kuteswa na kusulubiwa yote haya yalifanyika kwa dhambi, lakini pia yote yalikuwa katika mpango wa Mungu.
Hii haimaanishi kwamba Mungu ndiye aliyewaongoza watu hawa katika dhambi wakati walipomsaliti Kristo na wakamwua. Watu hawa walitenda dhambi na walikuwa watenda dhambi. Lakini Mungu ndiye amedhibiti kila jambo na alitumia matendo yao kukamilisha mipango yake. “ni kweli Herode na Pontio Pilato pamoja na watu Mataifa na waisraeli, walikusanyika katika mji huu dhidi ya Mwanao Yesu uliyemtia mafuta. Wao wakafanya yale ambao uweza wako na mapenzi yako yalikuwa yamekusudia yatokee tangu zamani” (Matendo ya Mitume 4:27-28).
Dhambi kuu mtu anaweza kufanya ni kumchukia na kumwua Mwana wa Mungu. Lakini hata wakati watu walimchukia na kumwua Mwana wa Mungu, mapenzi ya Bwana yalifanikiwa mikononi mwake (Isaya 53:10). Nia ya Mungu ilikuwa kuangamiza dhambi kupitia kifo cha Kristo Yesu: “na kwa majeraha yake sisi tumepona” (Isaya 53:5). Hii ndiyo sababu Kristo Yesu alikuja. Alikuja kuonyesha kwamba Mungu ni mwenye nguvu zote na anaweza kugeuza dhambi kuu za wanadamu kufaidisha mipango yake. Ni mtenda dhambi ambaye alimwua Kristo na ni mtenda dhambi ambaye alifaidika kutokana na kifo cha Kristo Yesu kwa sababu Kristo aliomba, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo” (Luka 23:34).