Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atimize kile sheria ya Musa ilihitaji kwetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
(Created page with '{{info|Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Cancel the Legal Demands of the Law Against Us}}<br> <blockquote> ''“Mlipokuwa wafu katika dhambi zenu na kutokutahiriwa katika<b...')
d (Aliulinda "Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atimize kile sheria ya Musa ilihitaji kwetu" ([edit=sysop] (indefinite) [move=sysop] (indefinite)))
 
(Hatuonyeshi sahihisho moja la katikati.)

Toleo lililopo 15:11, 11 Agosti 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Cancel the Legal Demands of the Law Against Us

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 7 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Mlipokuwa wafu katika dhambi zenu na kutokutahiriwa katika
asili yenu ya dhambi, Mungu aliwafanya mwe hai pamoja na
Kristo. Alitusamehe dhami zetu zote, akiisha kuifuta ile hati
yenye mashtaka yaliyokuwa yanatukabili pamoja na amri zake,
aliiondoa isiwepo tena, akiigongomea kwenya msalaba Wake”
(Wakolosai 2:13-14).

Watu wengi wanawaza kwamba wakati watakapokufa, Mungu atahesabu ni matendo mazuri mangapi wamefanya na ni matendo mabaya mangapi ambayo wamefanya. Halafu ikiwa matendo mazuri ni mengi sana kuliko matendo mabaya, basi Mungu atawakubali kuingia mbinguni. Hivi ndivyo watu wengi wanavyowaza kuhusu mbinguni. Lakini katika mawazo yao wamejidanganya. Mawazo yao ni ya upuzi kwa sababu:

1. Ni mawazo ya uongo. Watu wengi huwaza kwamba wako na matendo mazuri ambayo wanaweza kumwonyesha Mungu. Lakini ukweli ni kwamba hawana matendo mazuri kwa sababu hayo matendo ambayo wanaita mazuri hawayafanyi kwa kusudi la kumtukuza Mungu. Mungu anataka tufanye matendo mema kwa nguvu na kwa kumtukuza (1 Petro 4:11). Kwa ufupi ni kwamba matendo yetu mazuri lazima yawe na nia moja: kumtukuza Mungu.

Pia kila tendo jema lazima litoke kwa moyo ambao uko na imani. Biblia inasema kwamba, “Cho chote kinachofanywa pasipo na imani ni dhambi” (Warumi 14:23). Watu ambao wanawaza kwamba matendo yao yatawaokoa, wataona kwamba walikuwa wakijindanganya siku ile Bwana Yesu atarudi. “Cho chote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu” (Warumi 3:19). Siku ile Bwana Yesu atarudi, watajua kwamba matendo yao hayastahili chochote kizuri.

2. Hiyo siyo njia ya wokovu. Watu wengi huwaza kwamba matendo mema ni njia ya wokovu, lakini Mungu anakataa. Mtu hawezi kuingia mbinguni kwa sababu ya matendo yake mazuri. Njia moja tu mtu anaweza kuingia mbinguni ni hadi dhambi zake ziwe zimeondolewe na Bwana Yesu Kristo wakati alipokufa msalabani. Huu ndiyo wokovu ambao Biblia inafunza: wokovu kupitia kwa mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo.

Hakuna wokovu katika matendo yako mazuri. Njia moja tu ya kuokolewa, ni dhambi zako ziondolewe kabisa kupitia kwa mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo. Hesabu ya dhambi zetu lazima iondolewe kama tutaingia mbinguni. Hii ndiyo sababu Bwana Yesu Kristo alikufa msalabani.

Wakati Bwana Yesu Kristo alikufa msalabani Kalivari, dhambi zetu ziligongomewa msalabani (Wakolosai 2:13). Kristo mwenyewe alichukua dhambi zetu juu yake. Alifanyika dhambi kwa ajili yetu na akatulipia fidia ambayo sisi tulifaa kulipa. Yeye ndiye tumaini la kila mtenda dhambi na imani ndani yake ndiyo njia ya pekee ya kuokolewa na kuingia mbinguni.