Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kutuita tufuate mfano wake wa upole na upendo wenye gharama kubwa sana

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
 

Toleo lililopo 17:27, 11 Agosti 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Call Us to Follow His Example of Lowliness and Costly Love

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 37 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana ni jambo la sifa kama mtu akivumilia anapoteswa
kwa uonevu kwa ajili ya kumkumbuka Mungu. Kwa kuwa ninyi
mliitwa kwa ajili ya hayo, kwa ajili yenu, akiwaachia kielelezo,
ili mzifuaye nyayo zako.” (1 Petro 2:19:21).

“Mtafakarini sana Yeye aliyestahimili upinzani mkuu namna hii
kutoka kwa watu wenye dhambi, ili kwamba msije mkachoka na
kukata tamaa. Katika kushindana kwenu dhidi ya dhambi, bado
hamjapigana kiasi cha kumwaga damu yenu”
(Waebrania 12:3-4)

“Tuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu. Yeye ingawa
alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni
kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu, akajifanya
sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu,. Naye
akiwa na umbo la mwanadamu, alijinyenyekeza hata mauti,
naam, mauti ya msalaba!” (Wafilipi 2:5-8)

Tunapookoka, tunaanza kuufuata mfano wa Yesu Kristo. Yesu Kristo ni mwokozi wetu na pia ni mfano wetu. Akiwa mwokozi, anatuokoa kutoka kwa dhambi zetu, na akiwa mfano kwetu hutufundisha jinsi ya kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Biblia inafundisha wazi kwamba kabla hatujaanza kuufuata mfano wa Kristo ni lazima kwanza tuokolewe naye. Mtu ambaye hajaokoka hawezi akaishi kama Kristo kwa sababu yeye ni mtumwa wa dhambi.

Tunapookolewa kupitia kwa imani ndani ya Yesu Kristo tunakuwa watu wapya. Biblia inasema tunakuwa viumbe vipya. Tunakombolewa kutoka kwa dhambi zetu na tunapewa uwezo wa kutii na kufuata Kristo. Tunapaswa kwanza kumwamini Yesu Kristo kuwa mwokozi kabla hatujaanza kuufuata mfano wake.

Mtume Paulo alisema anatamani kuwa na haki ya Kristo kwa imani na kushiriki katika mateso pamoja na Kristo katika kazi yake. “Nami nionekane mbele Zake nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu kwa njia ya imani. Nataka nimjue Kristo na uweza wa kufufuka Kwake na ushirika ya mateso Yake, ili nifanane naye katika mauti Yake.” (Wafilipi 3:9- 10). Mpangilio huu uko wazi: kwamba unaokolewa kwanza halafu tunafuata mfano wa Kristo.

Biblia inatuamru “Ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele” (2 Timotheo 2:10). Hii inamaanisha tunapovumilia matatizo na shida za maisha, tunawaelekeza watu kwa Kristo. Jinsi tunavyovumilia shida kwa uvumilivi tunaonyesha ulimwengu jinsi tunaye mwokozi mkuu.