Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili aonyeshe kwamba kutahiriwa na kanuni zingine zote siyo njia ya wokovu
Kutoka Gospel Translations Swahili
(Created page with '{{info|Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Abolish Circumcision and All Rituals as the Basis of Salvation}}<br> <blockquote> ''“Ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhus...')
Badilisho lijalo →
Sahihisho kutoka 15:29, 11 Agosti 2011
By John Piper
About The Death of Christ
Chapter 13 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?
Translation by Desiring God
“Ndugu zangu, kama mimi bado ninahubiri kuhusu kutahiriwa,
kwa nini basi niteswe na Wayahudi? Ukweli kwamba bado
wananitesa, ni ushahidi kwamba bado ninahubiri wokovu kupitia
msalaba wa Kristo peke yake”
(Wagalatia 5:11).
“Wale wanaotaka kuonekana wazuri kwa mambo ya mwili
wanaotaka wawalazimishe kutahiriwa, sababu pekee ya kufanya
hivyo ni kuepuka kuteswa kwa ajili ya msalaba wa Kristo”
(Wagalatia 6:12).
Katika kanisa la Agano Jipya kulikuwa na upinzani mkubwa kuhusu kutahiriwa. Katika Mwanzo 17:10 Mungu aliamrisha kutahiriwa kwa Wayahudi. Bwana Yesu alikuwa Myahudi, na pia watume wote kumi na wawili. Na kwa hivyo kanisa lilipozaliwa katika Agano Jipya utamaduni wa kutahiriwa uliingia na kusababisha kuchanganyikiwa kwingi na mabishano.
Shida ya kwanza iliingia wakati watu wasiokuwa Wayahudi walipookoka. Halafu iliwabidi wakristo wachunguze utamaduni wa kutahiriwa. Je, mtu akitaka kuokoka, lazima atahiriwe au wokovu ulikuwa kwa imani pekee ndani ya Kristo pekee? Hili ndilo swali ambalo walijiuliza.
Wakati mitume walienda kuhubiri kwa watu ambao hawakuwa Wayahudi, ujumbe wao ulikuwa wazi. Petro alihubiri, “Kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika jina lake” (Matendo ya Mitume 10:43).
Kwa hivyo mitume walihubiri wazi: wokovu ni kwa imani pekee na sio kwa kutahiriwa au kitu chochote kama hicho. Lakini, katika kanisa la kwanza kulikuwa na wakristo wengine ambao walikuwa wamechanganyikiwa kuhusu jambo hili. “Baadhi ya watu wakashuka Antiokia kutoka Uyahudi, nao wakawa wanawafundisha ndugu walioamini kwamba, ‘Isipokuwa mmetahiriwa kufuatana na desturi aliyofundisha Mose, hamwezi kuokoka” (Matendo Ya Mitume 15:1).
Wakristo wa hiyo siku walikutana pamoja kujadili kuhusu jambo hili: “Ndipo baadhi ya walioamini wa madhehu ya Mafarisayo wakasimama na kusema, ‘Hao watu Mataifa lazima watahiriwe na waagizwe kuzitii sheria za Mose. Mitume na wazee wakakutana pamoja ili kufikiri jambo hili. Baada ya majadiliano mengi, Petro akasimama na kusema, ‘Ndugu zangu, mnajua kwamba siku za kwanza Mungu alinichagua ili kwa mdomo yangu watu Matifa wapate kusikia ujumbe wa injili na kuamini. Mungu, yeye ajuaye mioyo alionyesha kwamba anawakubali kwa kuwapa Roho Mtakatifu kama vile alivyotupa sisi. Mungu hakutofautisha kati yetu na wao, bali alitakasa mioyo yao kwa imani. Sasa basi, mbona mnataka kumjaribu Mungu kwa kuweka kongwa shingoni mwa wanafunzi ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba? Lakini sisi tunaamini ya kuwa tunaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu Kristo, kama wao wanavyookolewa. Kusanyiko lote litakaa kimya, wakawasikiliza Paulo na Barnaa wakieleza jinsi Mungu alivyowatumia kutenda ishara na maajabu kwa watu mataifa” (Matendo Ya Mitume 15:5-12)
Paulo aliona jambo hilo wazi kabisa. Aliona kwamba ikiwa watu watalazimishwa kutahiriwa ili wapate wokovu, basi kifo cha Kristo kilikuwa bila faida. Paulo alisema ikiwa tunawaza kwamba kutahiriwa kunatuokoa basi msalaba wa Kristo hauna maana kwetu Msalaba wa Kristo unatuweka huru sisi kutoka kwa matendo yote ya wanadamu kama hayo: “Kristo alitupa uhuru, akataka tubaki huru. Hivyo simameni imara wala msikubali tena kulemewa na kongwa la utumwa” (Wagalatia 5:1).