Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kukusanya kondoo wake kutoka kwa kila pembe la ulimwengu

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
Pcain (Majadiliano | michango)
(Created page with '{{info|Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Gather All His Sheep from Around the World}}<br> <blockquote> ''“Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali<br> kama Kuh...')
Badilisho lijalo →

Sahihisho kutoka 18:06, 11 Agosti 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Gather All His Sheep from Around the World

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 46 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali
kama Kuhani Mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angalikufa
kwa ajili ya Wayahudi, wala si kwa ajili ya Wayahudi peke yao,
bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili
kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe pamoja”
(Yohana 11:51-52)

“Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa
kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi
moja na mchungaji mmoja” (Yohana 10:16)

Wakati moja punda alitamka neno la Mungu (Hesabu 22:28). Wakati mwingine mhubiri au kuhani pia anaweza kutamka neno la Mungu bila kujua kile anasema. Jambo hili lilifanyika kwa mtu ambaye aliitwa Kayafa na alikuwa kuhani mkuu wakati wa Kristo. Wakati Kristo alikuwa mbele ya baraza la Wayahudi, Kayafa alisema, “Ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu” (Yohana 11:50). Kayafa alikuwa akisema kwamba ni vyema Kristo afe badala ya taifa zima liangamizwe na Warumi. Lakini Biblia inasema kwamba, “Hakusema haya kutokana na mawazo yake mwenyewe bali kama Kuhani Mkuu mwaka huo, alitabiri kuwa Yesu angalikufa kwa ajili ya Wayahudi, wala si kwa ajili ya Wayahudi peke yao, bali pia kwa ajili ya watoto wa Mungu waliotawanyika, ili kuwaleta pamoja na kuwafanya wawe pamoja” (Yohana 11:51-52).

Kristo mwenyewe alisema, “Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili, inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu, hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja” (Yohana 10:16). Mistari hii yote inafunza kitu kimoja. Inamaanisha kwamba ulimwenguni kote kuna watu ambao Mungu amechagua na wataokolewa na Kristo Yesu. Hao ni watoto wa Mungu waliotawanyika, na hao ndiyo Kristo anamaanisha wakati anasema kondoo wengine ninao ambao si wa zizi hili: yaani siyo Wayahudi. Mungu anakujikusanyia watu kutoka kila taifa la ulimwengu. Anawaita watumishi wake waende katika ulimwengu wawafanya watu kuwa wanafunzi wake na pia anaenda nao. Ako na watu ambao alichagua kabla ya kuweka misingi ya ulimwengu. Yesu alisema kwamba, “Wale wote anipao Baba watakuja Kwangu na ye yote ajaye Kwangu, sitamfukuza nje kamwe. Nimewajulisha Jina Lako wale ulionipa kutoka katika ulimwengu” (Yohana 6:37; 17:6).

Kwa hivyo Biblia inatufunza kwamba Mungu ako na watu wake kwa kila taifa la ulimwengu, na kwamba anawatuma watu wake kwa kila taifa la ulimwengu kuhubiri injili ili watu wake waokoke. Hakuna njia nyingine wanaweza kuokoka: watu wake lazima wahubiri injili. “Mlinzi humfungulia lango na kondoo huisikia sauti yake. huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi. Akiisha kuwatoa nje, hutangulia mbele yao na kondoo humfuata kwa kuwa wanaijua sauti yake” (Yohana 10:3-4).

Kristo aliteseka na akafa ili kondoo wake waweze kusikia sauti yake na waishi. Hiki ndicho kile Kayafa alisema, hata kama hakujua ni nini alikuwa akisema: Kristo alikuwa afe si kwa ajili ya Wayahudi pekee, lakini pia kuwakusanya watoto wa Mungu ambao walikuwa wametawanyika ulimwenguni kote. Alikufa ili awalete kondoo wake kwa Mungu na awaokoe milele.