Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atufanye watakatifu, bila lawama na wakamilifu
Kutoka Gospel Translations Swahili
By John Piper
About The Death of Christ
Chapter 15 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?
Translation by Desiring God
“Kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu
milele wale wote wanaotakaswa” (Waebrania 10:14).
“Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa
Kristo kwa kupatia mauti, ili awalete mbele Zake mkiwa
watakatifu, bila dosari wala lawama” (Wakolosai 1:22).
“Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya, kama vile
mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Kristo, Mwana-Kondoo
wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu”
(1 Wakorintho 5:7).
Jambo moja ambalo linawashusha mioyo wakristo ni jinsi wanavyokuwa polepole katika ukristo wao. Wanajua kwamba Mungu amewaita wampende kwa mioyo yao yote na kwa nafsi yao yote na kwa akili zao zote na kwa nguvu zao zote (Marko 12:30). Lakini wanapata kwamba katika maisha haya hawawezi kumpenda Mungu kabisa. Mara mingi wanajipata wakisema, “Ole wangu, mimi maskini! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?” (Warumi 7:24). Wanajua kwamba Mungu anawaamrisha wawe wakamilifu, na pia kwamba wawo siyo wakamilifu: “Si kwamba nimekwisha kufika, au kwamba nimekwisha kuwa mkamilifu; la hasha! Bali nakaza mwendo ili nipate kile ambacho kwa ajili yake nimeshikwa na Kristo Yesu” (Wafilipi 3:12).
Biblia inasema, “Nimeshikwa na Kristo Yesu.” Hii inatueleza ni kwa sababu gani ni lazima tuwe watakatifu. Siyo kwamba wakati tunakuwa watakatifu ndipo Kristo anatukubali kuwa watu wake. Katika mstari huu Paulo anasema kwamba, Yesu Kristo amenifanya tuwe wake. Sisi ni wake tayari, hatufanyiki wake wakati tunajitahidi kuwa watakatifu. Tunajitahidi kuwa watakatifu kwa sababu sisi ni wake tayari.
Biblia inaendelea kutueleza kwamba hata wakati tunajitahidi kuwa watakatifu, machoni pa Mungu sisi ni watakatifu tayari. Biblia inasema, “Kwa sababu kwa dhabihu moja amewafanya kuwa wakamilifu milele wale wote wanaotakaswa” (Waebrania 10:14). Kwa hivyo katika msitari huu tunaambiwa kwamba tayari tumekamilishwa.
Biblia inafunza jambo hili wakati inasema kwamba tuondoe chachu wa dhambi maishani mwetu. “Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Kristo, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu” (1 Wakorintho 5:7). Tena katika mstari huu tunaambiwa kwa sababu Kristo, Mwana-kondoo wa pasaka ametolewa kama sadaka, kifo chake kinatukamilisha. Kwa hivyo tunahitajika kupigana ili tuondoe uchafu wote miongoni mwetu. Sisi ndiyo watoto wakamilifu wa Mungu kwa hivyo inatupaswa kuishi maisha matakatifu.