Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili tukufe kwa Sheria na tuzae matunda kwa Mungu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Sahihisho ya 17:05, 11 Agosti 2011 aliyefanya Pcain (Majadiliano | michango)
(tofauti) ←Sahihisho lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Sahihisho linalofuata → (tofauti)

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/So That We Would Die to the Law and Bear Fruit for God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 31 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili wa Kristo, ili mweze
kuwa mali ya mwingine, Yeye ambaye alifufuka kutoka kwa wafu,
ili kwamba tupate kuzaa matunda kwa Mungu.” (Warumi 7:4).

Wakati Yesu alikufa msalabani, wateule wake waliunganishwa na yeye. Kifo chake kwa sababu ya dhambi zetu kilikuwa kifo chetu ndani yake. Hii inamaanisha tunapookoka tunakufa kwa dhambi na kwa sheria. Sheria ya Mungu inatueleza dhambi ni nini: “Pasipo na sheria, hapana kosa” (Warumi 5:15); “Basi tunajua ya kwamba cho chote sheria inachosema, inawaambia wale walio chini ya sheria ili kila kinywa kinyamazishwe na ulimwengu wote uwajibike kwa Mungu” (Warumi 3:19).

Sheria huwaletea laana wote wanaoanguka dhambini. Sheria ilitoka kwa Mungu na inatuonyesha makosa yetu mbele ya Mungu. Njia moja tu tunaweza kuwa huru kutoka kwa laana ya sheria ni kulipiwa fidia ya dhambi zetu. Hii ndiyo sababu Yesu Kristo alikuja: “Kristo alitukomboa kutoka katika laana ya sheria kwa kufanyika laana kwa ajili yetu” (Wagalatia 3:13).

Punde tu tunapookoka sheria ya Mungu haiwezi kutuhukumu kwa sababu Kristo ni mwokozi wetu. Wakati Yesu Kristo aliishi hapa duniani, aliishi maisha matakatifu yasiyokuwa na dhambi na akatimiza mahitaji ya sheria kwa niaba yetu. Wakati alikufa msalabani alilipa fidia kwa niaba yetu.

Hii ndiyo sababu Biblia inasema wazi kwamba wokovu siyo kwa uwezo wetu: “Hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa matendo ya sheria” (Warumi 3:20); “Mtu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria bali kwa njia ya imani katika Yesu Kristo” (Wagalatia 2:16). Hatuwezi kuokolewa kwa kujaribu kutimiza sheria ya Mungu, bali tumaini letu ni maisha na kifo cha Yesu Kristo: tunaokolewa kwa imani ndani yake. “Kwa maana twaona kwamba mwanadamu huhesabiwa haki kwa njia ya imani wala si kwa matendo ya sheria” (Warumi 3:28).

Wale ambao wameokoka, maisha yao yanatawaliwa na Kristo wala si sheria. Tunajua kwamba sheria ni nzuri na takatifu (Warumi 7:12), na kama watu wameokoka watatamani kuishi wakifuata sheria ya Mungu. Hatufanyi hivi kwa sababu tunataka tupate wokovu kwa nguvu zetu bali ni kwa sababu tumeokolewa kwa imani. Tunaishi maisha yetu tukiongozwa na Roho Mtakatifu wala si sheria: “Andiko huua, bali Roho hutia uzima” (2 Wakorintho 3:6).

Hii ndiyo sababu Biblia inasema kwamba yule ambaye ameokoka anazaa matunda ya utakatifu: “Ninyi mmeifia sheria kwa njia ya mwili ya Kristo, ili mweze kuwa mali ya mwingine, Yeye ambaye alifiufuka kutoka wafu, ili kwamba tupate kuzaa matunda kwa Mungu.” (Warumi 7:4). Mti huzaa matunda, kwa kawaida huwa haulazimishwi kuyazaa matunda hayo. Ikiwa mti umepata udongo mzuri, basi mti huo utazaa matunda mazuri. Mtu ambaye ameokoka ako na uhusiano mzuri na Yesu Kristo: yeye ni kama mti ambao uko na udongo mzuri na ataishi maisha ya kutii kwa sababu ya uhusiano wake na Yesu.