"Askari Walio Umia Tu Ndio Huhudumu"

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Loving Others
Topic Index
About this resource
English: "Only Wounded Soldiers Can Serve"

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Loving Others
Part of the series Taste & See

Translation by May Adhiambo

Review You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).


Wengine wenu mnapitia vitu wakati huu ambavyo ni vichungu ili kuwatayarisha kwa utumishi bora wa Bwana. Mtu afikapo mwisho hata kuhisi ni kama amegonga mwamba, wakati mwingine huwa ameugonga Mwamba Imara.

Nakumbuka mstari mmoja kutoka Zaburi 138:8 ambayo tulisoma Jumamosi katika ibada yetu ya asubuhi inayosema “Ee BWANA, upendo wako wadumu milele, usiziache kazi za mikono yako.” Naam, hata Musa anavyosema katika Kumbukumbu za Torati 33:27 “27Mungu wa milele ni kimbilio lako,na chini kuna mikono ya milele.”

Ndio, Yeye anakuona hata unapotetemeka na kuteleza. Ana uwezo (na mara nyingi amefanya hivo) wa kukushika kabla ya kuanguka kwako. Lakini wakati huu ana mafunzo mapya. Zaburi 119:71 yasema, “Ilikuwa vyema mimi kupata shida ili nipate kujifunza amri zako.” Hatuambiwi kuwa shida hizo zilikuwa rahisi au raha bali. “Ilikuwa vyema.”

Wiki jana nilikuwa nikisoma kitabu kilichoandikwa na James Stewart ambaye ni mhubiri kutoka Uskoti. James alisema katika utumishi wa upendo, ni askari walioumia tu ndio huhudumu. Ni kwa sababu hii na amini wengine wenu mnatayarishwa kwa huduma hii. Unapoumia usije ukafikiri kuwa maumivu yako yamekujia kinyume na mpango wa Mungu. Tena katika kumbukumbu la torati 32:29 asema. “Hakuna Mungu mwingine ila Mimi…..Mimi nimejeruhi na Mimi nitaponya.”

Nawaombea ninyi nyote mlio na maumivu. Zaidi ya hayo nangoja kwa hamu wororo upya wa Upendo mtakao funzwa katika maumivu haya.