Ari ya ukuu wa Mungu, sehemu ya 1

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Christian Hedonism
Topic Index
About this resource
English: Passion for the Supremacy of God, Part 1

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Christian Hedonism
Part of the series Passion 97

Translation by Desiring God


Sababu ya kuja kwa Ari ‘97

Sababu #1

Nataka kuanza kwa kuwaambia sababu zingine za kukuwa hapa kwangu. Mojawapo ya faida kubwa zaidi kuwa katika kanisa huku mashinani kama mchungaji kwa miaka 16-17 ni ya kuwa, kwa miezi na miaka kadhaa, maono ya kanisa na maono ya mchungaji imekuwa moja. Karibu mwaka mmoja uliopita tulichapisha ripoyi ya maono ambayo ilikuwa hivi.

Tuko kwa ajili ya kueneza ari ya uku wa Mungu katika mambo yote kwa ajili ya furaha ya watu wote.

Nadhani naweza sema bila kusita ya kuwa hiyo ndio lengo langu na la Bethlehem Baptist. Basi nilipopata mwaliko, nikasoma kuhusu kongamano hili, na nikaona neno “Ari” na kuona ukweli katika Isaya 26:8— “sisi tumekungoja; Ee Bwana shauku ya nafsi zetu inaelekea jina lako na ukumbusho wako"—nilivutiwa.

Nataka kueneza Ari ya ukuu wa Mungu katika mambo yote na kwa furaha yenu wote na watu wote wa dunia hii. Kwa hivyo hiyo ndio sababu ya kwanza ya kuwa hapa.

Sababu #2

Sababu ya pili ni yakuwa, nataka niwe kiberiti ndogo ya kuwasha furaha yenu. Nataka mtoke mahali hapa mkiwa wachangamfu na wenye furaha ndani ya Mungu.

Sababu #3

Na sababu ya tatu, nataka muone kutoka kwenye maandiko yakuwa sababu ya kwanza na ya pili yote ni moja. Yote ni moja. Hiyo ni kueneza Ari ya ukuu wa Mungu na kuwa na furaha ndani ya Mungu yote haya yanafanana kabisa. Kwasababu Mungu anatukuzwa zaidi ndani yako ukiwa umetoshelezwa zaidi ndani yake.

Kunayo sentensi ambayo nitaurejelea tena na tena: Mungu anatukuzwa zaidi ndani yako ukiwa umetoshelezwa zaidi ndani yake. Kwa hivyo nyimbo ambazo tumekuwa tukiimba na tuki ashiria ni njia ya kumpa Mungu utukufu. Kwa sababu tunavyo endelea kutoshelezwa ndani yake, ndivyo tunavyo kunywa zaidi kutoka kwake na kula katika meza lake la chakula ambayo ni yeye, ndiyo zaidi thamani yake na kututosheleza kwake unaashiria vikubwa. Kwa hivyo hakuna mashindano—na hili ni la kushangaza, hili ndilo injili kwangu, ambayo niligundua katika ‘68’, ‘69’ na ’70’ wakati Mungu alikuwa akifanya kazi maishani mwangu. Hakuna mashindano kati ya Ari ya Mungu kutukuzwa na Ari yako kutoshelezwa, kwa sababu yote ni moja.

Kuna njia nyingine ya kusema sababu hii ya tatu ya kuwa kwangu hapa: Niko hapa ili kuyayusha barafu. Niko na picha akilini mwangu, ilitokea katika Mathayo 24:12, kuangalia wakati wa mwisho, Yesu asema “Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo ya wengi utapoa.” Nimeogopeshwa hadi karibu kufa kwa sababu ya kuwa baridi. Nimechukia wazo yakuwa upendo wangu kwa Mungu au upendo wangu kwa watu siku moja utakauka na kuwa kama barafu. Na Yesu asema “inakuja!” Inakuja kama jiwe la barafu inayoteremka kutoka milimani ulimwengu kote. Kwa hivyo sehemu moja ya matarajio yangu ya siku za mwisho ni kuwa, maasi yataongezeka na upendo wa wengi uta poa. Sasa hiyo inaweza kuwa uchambuzi usiofurahisha hata kidogo kuhusu siku za mwisho. Lakini ukiendelea kusoma Mathayo 24 kuelekea chini hadi mlango wa 13, Inasema, “lakini mwenye kuvumilia hatamwisho, ndiye atakaye okoka.” . . . .Kwa hivyo kuna mtu atakaye vumilia. Na mlango ufatao unasema “Habari hii njema ya ufalme”—Badilisha ya kuwa “ Hii habari njema ya kueneza Ari ya ukuu wa ufalme wa Yesu—“ Habari njema hili la ufalme utahubiriwa kama ushuhuda kwamataifa yote, na baadaye mwisho utafika.” Sasa weka mlango wa 12 karibu na mlango wa 14 na uone kama uta hisi hali ya kutokuwa na amani.” Uaasi utaongezeka na upendo wa wengi utakuwa baridi” lakini hii habari njema ya ufalme”—wa uongozi wa kipekee wa Mungu . . . ”Utasambaa kwa mataifa na baadaye mwisho utafika.”

Sasa kuna ukosefu wa amani kati ya milango hayo mawili. Sababu ilioko najua ni kwa sababu, sio watu baridi watakao peleka habari njema katika mashule yetu hapa. Sio watu baridi ambao watafikia wale watu ambao hawajafikiwa na habari njema ulimwenguni. Sasa, najua hili namna gani? Kwa sababu ukirudi nyuma hadi mlango wa 9 (tisa), utapata kitu katika ulimwengu wa kinabii ambayo ni tofauti sana. Ina sema “Wakati huo watawasaliti ninyi mpate dhiki, nao watawaua; Mtachukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu,” Yesu asema. Sasa ikiwa hayo ni kwel—Ikiwa tutasalitiwa katika kazi ya kueneza habari njema, ikiwa tutauwawa, ikiwa tutachukiwa na mataifa tuendapo—Najua jambo moja kwa hakika: Ni watu baridi ambao wana sambaza ujumbe hili. Ni wenye kuabudu wa Mfalme Yesu walio nyeupe na moto watako ufanya. Kwa hivyo ninacho ona katika mlango wa 9-14 ya Mathayo 24 ni ya kuwa, jinsi mwisho wa nyakati unasongelea karibu, kunaenda kuwa na watu ambao wanaendelea kuwa baridi kama barafu na pia watu ambao wanakuwa moto kiwango ya kusalmisha maisha yao kwa Kristo miongoni mwa watu wote duniani.

Kwa hivyo huduma yangu hapa kanisa la Bethlehem Baptist na kufika kwangu hapa ni ku yeyusha barafu kwa moto. Nilipeana dhana hili wakati mwingine katika kanisa languna na msichana mdogo kati ya miaka sita na saba (6-7), akaja kwangu baada ya mkutano . . . Huwa nawatia moyo watoto kanisani kuchora kuhusu ujumbe wangu . . . na akasema “Niliona haya”, Alikuwa amechora jiwa la barafu nzuri likiwa limeandikwa Minnepolis; Kwa hilo mchoro palikuwa na mtu mdogo akiwa ameshika tochi ya moto na palikuwa na shimo katika jiwe hilo la barafu, Kule juu palikuwa na jua ukiwaka sana kutoka juu na kuteremka chini kupitia lile shimo

Sasa hapa kuna mafunzo yangu kuhusu nyakati za mwisho kwa ufupi. Ukiwa ume shangazwa jinsi gani chuo kikuu chenu kitafanana wakati Yesu atakapo kuja, au jinsi gani Austin au Minnepolis, au popote utokapo utafanana: Jiwe kubwa la barafu linasonga, na watu wengi wanakuwa baridi kwa mambo ya Mungu . . . kunyakua, kuwa baridi zaidi . . . Lakini hakuna kitu katika Bibilia kuhusu nyakati za mwisho ambayo inasema “Kanisa la Bethlehem Baptist” au hata “Minnepolis,” au sema, chuo kikuu cha Texas kule Austin ni lazima iwe chini ya jiwe la barafu,” Hakuna! Kama kuna watu wa kutosha na tochi ya moto yenye moto zadi, wakiuchoma jiwe hili la barafu, shimo kubwa laweza chimbuko katika chuo kikuu la eneo lenu au katika kanisa lenu, na hata katika mji wenu. Na hio ndio sababu ya kuwa kwangu hapa: Nataka kuinua tochi langu.

Spurgeon alipenda kusema akiwa Uingereza karibu miaka mia moja iliopita, wakati alikuwa akihubiri kule Metropolitan Terbanacle, Yakuwa “watu wanakuja kunitazama nikichomeka.” Wanakuja kuwasha tochi zao za moto zenye karibu kuzimika kwa tochi yangu ya moto. Kisha wanaenda na kuchomeka kwa wiki kwa ajili ya Yesu. Ningefurahishwa sana ikiwa ungeleta tochi yako iliyo karibu kuzimika hapa asubuhi hii na uiwashe na yangu. Hiyo ndio sababu niko hapa.

Yaliyomo

Sababu ya hii ujumbe: Kutengeneza msingi

Kunayo msingi ya kile nataka kufanya. Jukumu langu hapa ni kuzungumuza kuhusu kuishi kwa sababu ya utukufu wa Mungu, kuwa na ari kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Ninayo ujumbe mbili asubuhi hii na kesho asubuhi. Asubuhi ya leo ni utangulizi au msingi na kesho itakuwa ni kuitenda.

Msingi ni hili: Ari yako kuhusu ukuu wa Mungu kwa kila kitu, Umezingatiwa sana na Ari ya Mungu kwa ukuu wa Mungu kwa vitu vyote. Ubinafsi wako kwa Mungu . . . kama itadumu . . . ni lazima iwe imara ndani ya ubinafsi wa Mungu. Ukitaka Mungu awe mkuu ndani ya maisha yako, Ni lazima uone, uamini, na upende ukweli yakuwa Mungu, ni mkuu katika maisha ya Mungu. Ukitaka Mungu awe hazina yako . . . jinsi ambavyo tumeimba hapa . . . ili umthamini Mungu kuliko chochote kile, Lazima uone na uamini yakuwa hazina ya Mungu ni Mungu, na anamthamini Mungu zaidi kuliko anavyopenda kitu chochote kile. Huenda hatuwezi kuzuia Mungu furaha kuu zaidi ulimwenguni, kama, kuabudu Mungu. Hiyo ni Msingi; Hiyo ndio nataka kuzungumuzia leo.

Na kisha kesho nataka kunena kuhusu kutafuta kwako kwa furaha ndani ya Mungu, na huku kutafuta kwako ni muhimu kuashiria kwa Mungu kutafuta utukufu ndani ya maisha yako.

Mungu ana ari kwa ajili ya utukufu wake

Acha nianze na hadithi kidogo. Nilinena katika chuo kule Wheaton—kule nilikohitimia—Karibu miaka 8 au 9 uliopita. Ilikuwa nafasi yangu ya kwanza ndani ya kanisa hili kubwa, mviringo na yenye kupambwa vizuri. Na nilisimama juu, na kusema, “Sababu kuu ya Mungu ni kumtukuza Mungu na kumfurahia milele.” Na marafiki wangu wote waliokuwa nje kwenye nafasi ya nje waka sema, “Lo, ameharibu nafasi yake ya kwanza hapa alipo kuzwa kiroho kunena na wanafunzi hawa, amerejelea baada ya miaka 20 na ana nukuu vibaya Westminister katekisimu wakati tu anapoanza na kusema , ”Sababu kuuya Mungu badala ya sababu kuu ya mwanadamu.” Na nikaendelea na kusema, “Nilimaanisha yale niliyo yasema.” Na naumaanisha asubuhi wa leo: Sababu kuu ya Mungu ni kumtukuza Mungu na kujifurahisha milele.

Nililelewa katika nyumba ya Mhubiri. Babangu Bill Piper, alinifunza kutoka wakati nilikuwa mchanga zaidi, Mlango wa 1 Wakorintho 10:31: “Chochote utendacho, chochote ukulacho au chochote unywacho, fanya yote kwa utukufu wa Mungu.” Lakini sikuwahi kusikia mtu yeyote akisema kuwa, Mungu anafanya kila kitu kwa utukufu wa Mungu. Na mzizi ya kuishi kwangu kwa utukufu wa Mungu ni kwamba, Mungu anaishi kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Sijawahi ona karatasi ya mafunzo ya watoto jumapili ukiletwa nyumbani ambao unasema, “Mungu anajipenda sana kuliko anavyo kupenda, na ndani ya hiyo karatasi kunayo tumaini ya kuwa huenda aka kupenda, na ndani ya hiyo karatasi kunayo tumaini yakuwa huenda aka kupenda, Jinsi ulivyo mtu asie stahili.” Sijasoma hayo katika karatasi yoyote ya shule ya jumapili. Hiyo ndio sababu tuna tengeneza mpangilio wa mafunzo katika kanisa la Bethlehem Baptist. Wengi wetu wamelelewa kwa manyumba, na makanisa ambapo, tulifurahishwa na kuwa wakristo hadi tukafikiria kuwa Mungu alikuwa na furaha kutu husu, sio mpaka kiwango ambacho tulifurahia kuhusu Ubinafsi wa Mungu.

Ni rahisi sana kwa ulimwengu wa ubinafsi wa mwanadamu, mahali hisia za mtu kujihusu ndio thamani kuu zaidi, kwa kuwa mkristo kwa kiwango cha kuzuia yale ungalifanya tu bila Mungu. Nani angekuwa Mkristo? Basi, wewe sio Mkristo ukiupenda tu yale ungalipenda bila kukumbana na uzuri na Ubinafsi wa Mungu. Kama Mungu ni njia tu yakujiendeleza wewe binafsi na kujitukuza, badala ya wewe kuona ndani yake kitu chenye utukufu mkuu yani kama Mungu aliye jaawa na udhihirisho wa utukufuwake basi, unastahili kuchunguza kuokolewa kwako. Kwa hivyo hii ni hali kubwa ya kujichunguza hapa Austin katika Ari 97. Watu wachache wamewahi kunieleza au kunionyesha yale nimeona katika bibilia sasa, yakuwa Mungu alinichagua kwa utukufu wake.

Nakumbuka nikifunza darasa lingine kuhusu Waefeso 1 mwaka wa 1976, kwa kile tulicho ita “ya mda” huko katika chuo cha Bethel wakati huo, na kuendelea kwa makini kupitia milango 14 ya Waefeso na Ulimwengu wangu ukafunuliwa wazi tena kwa sababu mara tatu . . . .mlango wa 6,12 na 14 . . . inasema alituteuwa ndani yake kabla ya msingi ya dunia na alifu chagua tangu asili kuwa wana wake, hadi kwa sifa ya Utukufu wa neema yake.

Alikuteuwa. Kwa nini? Ili utukufu wake na neema ipate kusifika na kuinuliwa juu zaidi. Wokovu wako niwa kumtukuza Mungu. Kuchaguliwa kwako ni wa kumtukuza Mungu, kubadilishwa kwako ilikuwa ya kumtukuza Mungu, kufanywa haki kwako ilikuwa ya kumtukuza Mungu, kutakaswa kwako ni ya Utukufu wa Mungu. Na siku moja kutukuzwa kwako utakuwa kumezwa ndani ya Utukufu wa Mungu.

Umeumbwa kwa utukufu wa Mungu

Isaya 43:6 “Waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka mwisho wa dunia; kila mmoja niliyemuumba kwa ajili ya utukufu wa Mungu.”

Mungu alikomboa watu wake kutoka Misri kwa sababu ya utukufu wake

Mababu zetu, walipokuwa Misri, hawakuzingatia njia zako au matendo yako ya ajabu. Waliaasi dhidi yako pale bahari ya shamu. Lakini uliwaokoa kwa ajili ya jina lako, ili udhihirishe matendo yako makuu na utukufu wako.” Zaburi 106:7

Kwa njia nyingine alipasua bahari la shamu na kuokowa watu wake walio asi, ili nguvu zake kuu zipate kujulikana. Na ilisambaa mpaka kule Jeriko na kumuokowa kahaba, ili walipofika huko na wakawa tayari kupuliza tarumbeta, kahaba huyo aliokolewa mara ya pili kwa sababu alisema “tulisikia jina lako na ukuu wako.” Na mwanamke mmoja na familia yake waliamini ubinsfsi wa mungu na kuponea uharibifu.

Mungu alirehemu Israeli jangwani kwa ajili ya utukufu wake

Mungu aliwarehemu Israeli jangwani mara nyingi Sana. “Nyumba ya Israeli waliasi dhidi yangu kule jangwani,” Ezekieli anasema akimnukuu Mungu, “Na nilifikiri nita wa mwagia ghadhabu yangu, lakini niliwarehemu kwa sababu ya jina langu ili lisidhahakiwe na mataifa.” Basi mwishowe Mungu akawatuma Utumwani kule Babiloni, na baada ya miaka 70 aliwarehemu. Hatataliki mke wake wa agano na akawarejesha tena. Lakini kwa nini? Nini sababu ambayo imekita mizizi ndani ya moyo wa Mungu?

Isikize kutoka kwa Isaya 48:” Kwa ajili ya jina langu na zuia hasira yangu, kwa ajili ya sifa yangu nalizula kwa ajili yako ili nisiwaangamize. Tazama nimewatoa uchafu, Lakini sio kama fedha, Nimewajaribu kwenye moto wa mateso. Kwa ajili yangu mwenyewe, kwa ajili yangu nilifanya hayo, Kwa sababu gani jina langu lidhihakiwe? Utukufu wangu sitashiriki na mwingine yule.” Hiyo ni nia ya nehema uliozingirwa na utegemeo wa Mungu.

Yesu alikuja na akafa kwasababu ya utukufu wa Mungu

Je Yesu alikuja ulimwenguni kwa sababu gani? Ah ni mara ngapi lazima tunukuu Yohana 3:16 na andiko hilo ni kweli kabisa. Na kabla kumaliza asubuhi wa leo au wa kesho, utaona kuwa kusisitiza huku wakati huu na kusisitiza ambao umekuwa ukijua pengine kwa muda mrefu, sio tofauti.

Lakini ni kwa nini alikuja? Kwa nini Yesu akaja? Kulingana na Warumi 15:8 alikuja kwa sababu hii. “Kwa maana nasema, Kristo amefanyika muhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azidhibitishe ahadi walizopewa baba zetu tena ili mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema.” Kristo alikuja duniani, akiwa amevalia mwili, na akafa ili upate kumpa Baba yake tukufu kwa ajili ya rehema. Alikuja kwa niaba ya babake. Hio ndio sababu yake kuu ya kuja, kwa sababu ya utukufu wa Baba yake. Na utukufu wake unafikia kilele chake katika utele wa rehema.

Skiza neno hili kutoka kwa Warumi 3: “Mungu amekwisha kumweka Kristo awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake, ili kuonyesha haki ya Mungu. Ni kuonyesha katika nyakati hizi kuwa yeye mwenyewe ndiye haki. Hiyo ndio sababu alikufa. Alikufa ili aondolee lawama haki ya Mungu aliyepita juu ya dhambi kama uzinifu wa Daudi na mauaji. Je, ilikutia wasiwasi kuwa Mungu alipita tu juu yake na Daudi akaendelea kuwa mfalme? Basi ilimsumbua Paulo hadi kilindini mwa utu wake yakuwa Mungu sio mtakatifu kupita dhambi bila kuadhibu. Na sio Daudi tu. Palikuweko na maelfu ya watakatifu katika Agano la kale na leo pia kunao ambao dhambi zao amesahau na kutupilia mbali. Na Paulo akalia kwa sauti, “Utakuaje Mungu na ufanye hayo? Utakuaje mtakatifu na ufanye hayo? Utakuaje mwenye haki na ufanye hayo? Utakuwaje mwenye kustahili kuabudiwa na ufanye hayo?” —kama muamuzi yeyote katika Austine angefanya hivyo angeondolewa mara moja, angemsamehe anayedhulumu watoto, mbakaji, muuaji . . . ” na unaufanya kila siku, hivi wewe ni Mungu wa aina gani?”

Msalaba ndio suluhisho ya shida kubwa sana ya kithiologia, kama, Mungu atakuaje Mungu na anasamehe dhambi? Kristo alikuja ili kumtolea lawama Mungu kwa kuokoa watu kama wewe.Wokovu ni kitu kubwa na kitu tukufu kilichozingirwa na Ubinafsi wa Mungu.

Yesu yuaja kupokea Utukufu

Kwa nini yuaja tena? Yesu yuaja wenzangu, yuaja. Na acha nikuambie kwa nini anakuja na yale unaweza fanya akija, ili uwe tayari na kuyatenda.

2 Wathesolanika 1:9 “Wale ambao hawatii habari njema wataadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa bwana na utukufu wa nguvu zake. Yeye atakapokuja siku ili kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa katika wote waliosadiki katika siku ile.” Je waona vitu hivi viwili? Yuaja kutukuzwa, na kuinuliwa ndani ya watakatifu wake, na kustaajabiwa. Kama haujaanza kutenda haya sasa hautaweza kuyatenda ajapo.

Kongamano hili lipo ili iwashe moto kwenye mifupa yenu, akilini mwenu na ndani ya moyo wenu ili muwe tayari kukutana na Mfalme Yesu, ili upate kuendelea milele ukifanya yale uliumbwa kutenda, kama, kumstajabia na kumtukuza.

Ni lazima tuadhimishe ukuu wa Mungu kama vile darubini

Mmtukuze lakini sio jinsi kama tufanyavyo na darubini. Unajua tofauti kati ya kutukuza kwa jinsi zote mbili? Kuna kumtukuza jinsi ya darubini ya kutazamia nyota na ile ya labu na ni kumkufuru Mungu kwa kumtukuza Mungu kwa jinsi ya darubini ya labu. Kumtukuza Mungu kwa jinsi ya darubini ya labu ni kama kuchukua kitu kidogo na kukifanya kiwe kama ni kikubwa kuliko jinsi kilivyo. Ukijaribu kufanya hivyo kwa Mungu ni kumfukuru. Lakini darubini ya kutazamia nyota inaangazia mbingu yenye ukuu na inajaribu tu kuzisaidia zionekane kama vile zilivyo. Ndio kazi ya darubini ya kutazamia nyota.

Meremeta nyota ndogo—unatazama angani usiku na nyota zinaonekana kama ncha za pini. Wala sivyo. Wajua vile, uko katika chuo sivyo? Nyota hizo ni kubwa. Kubwa zaidi, nazo ni moto! Na huna habari isipokuwa kwamba mtu mmoja wakati fulani alibuni darubini, akattia jicho lake kwenye darubini kasha akawaza, “Ni kubwa kuliko ulimwengu, kubwa zaidi ya ulimwengu mara mamilioni.” Hivo ndivyo Mungu alivyo. Maisha yako leo yako ili kuutukuza ukuu wa Mungu katika chuo. Hiyo ni mwito mkubwa. Nitaongea kuhusu namna gani kesho.

Ikiwa Mungu ni Mungu mbinafsi, atakuwaje mwenye upendo?

Hii ndio swali muhimu zaidi ambayo nataka kufunga nayo, kwa sababu najua inaanza kuinukia hapa. Nimesema ukweli huu yakuwa Mungu ni Mungu mbinafsi na ubinafsi wake ndio mzizi wa ubinafsi wangu ndani ya Mungu. Nimeambia watu hayo kwa miaka Ishirini na swali linaibuka. “Hii haifanani na upendo kwa sababu bibilia inasema katika 1 Wakorintho 13:5 ‘Upendo hautafuti mambo yake’ na unatueleza sasa, kwa muda wa robo saa ya kuwa Mungu anatumia wakati wake wote akitafuta mambo yake. Kwa hivyo itakuwa Mungu sio mwenye upendo au wewe ni mwongo.” Na hiyo ni shida kubwa kwa hivyo wacha ni jaribu kujibu jinsi gani Mungu ni mwenye upendo kwa kutafuta kutukuzwa kwake mwenyewe.

Usaidizi kutoka kwa C.S. Lewis

Nilipata ufunguo ndani ya C.S. Lewis. Kama kuna yeyote ambaye amesoma kitabu hiki kiitwacho Kumtamani Mungu, basi utakumbuka maandishi haya. Lewis alikuwa mpagani hadi akiwa na miaka zaidi ya 20 na alichukia ubure wa Mungu. Alisema yakuwa kila wakati alisoma maandishi katika Zaburi, “Bwana asifiwe, Bwana asifiwe” . . . Na alijua mafunzo ya kidini ya kikristo ya kuwa Zaburi ilitiwa nguvu . . . alijua kuwa ni Mungu ndiye anayesema “Nisifuni Nisifuni” na ikamfanania kama mwanamke mkongwe anaye tafuta kutamaniwa. Hio ni nukuu kutoka kwa tafakari juu ya Zaburi. Na kisha Mungu kwa ghafla akamwokoa C.S. Lewis. Kisha akaandika haya:

Hakika iliyo wazi kuhusu sifa iwe ni kwa Mungu au chochote kile inanihepa. Niliiwaza kwa njia ya kupongeza, kukubali, kupatia utukufu. Sikuwa nimegundua kuwa furaha yote hububujika ndani ya sifa, ila tukikaribisha haya wakati mwingine kuzuia furaha ile. Dunia inatikiswa kwa sifa: Wapendanao wana sifu washikaji wao, wasomaji watunzi wao wazuri wa shairi, watalii wanasifu kule mashambani, wachezaji wanasifu mechi zao nzuri, sifa ya hali ya anga, mvinyo, vyakula, waigizaji, farasi, vyuo, mataifa, watu wahistoria, watoto, maua, milima, ukti ya Posta isiyo ya kawaida, wadudu tofauti tofauti, wakati mwingine wanasiaisa na wasomi. Ugumu wangu kwa ujumla hasa na sifa za Mungu ulitegemea kuwa tumenyimwa, kama mujibu wa ukuu wa thamani, yale mbayo tunafurahia kufanya—hata kama tunapenda kuyafanya—kwa mujibu wa kila kitu chenye thamani.

Basi hapa kuna sentensi muhimu:

Nadhani tunafurahia kusifu yale tunafurahia kwa sababu furaha hiyo sio kamili mpaka tu tunyeshe. Sio tu kwa sababu ya pongezi ndio wapendanao wanaelezeana kila wakati jinsi gani ni warembo. Furaha sio kamili hadi ionyeshwe kwa matendo.

Sasa hiyo ndio ilikuwa funguo kwangu ambayo ilifungua kitu kwa kuzingatia jinsi gani Mungu anaweza kuwa mwenye upendo na mwenye kujitukuza kwa yote atendayo. Ndivyo iendavyo. Acha niunganishe vipande kwa ajili yako.

Jibu la Swali

Ikiwa Mungu anafaa kukupenda, ni nini lazima akupe? Ni lazima akupe kizuri zaidi kwako. Kizuri zaidi ulimwenguni kote ni Mungu. Ikiwa angekupa afya yote nzuri, kazi nzuri, mke au mume mzuri, tarakilishi nzuri, likizo nzuri, ufanisi wa chochote utendacho, na asijipe kwako, basi angekuchukia. Na akijipa kwako na asikupe chochote tena, basi anakupenda bila kipimo.

Ni lazima niwe na Mungu kwa furaha yangu kama Mungu atanipenda. Sasa Lewis amesema ya kuwa, ikiwa Mungu amejipa kwako ili ushereheke milele, furaha hiyo hata kuwa kamilifu hadi uionyeshe kwa kumsifu. Kwa hivyo, ili Mungu akupende kabisa, hawezi kuwa wa kupuuzilia kwa wao kuleta furaha yako iwe kamilifu kupitia sifa au hapana. Kwa hivyo Mungu ni lazima atafute sifa zako ikiwa ni lazima akupende. Je hio ilieleweka? Sijui kama ni warudilie hilo sentensi. Hilo ndilo msingi wa maisha yangu. Naamini kuwa ndio msingi wa Bibilia pia.

Ili akupende ni lazima akupe yaliyo nzuri zaidi kwako. Mungu ndiye mzuri zaidi kwako. “Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako kuna furaha tele; Na katika mkono wako wa kiume mna neema ya milele” (Zaburi 16:11). Mungu anajipa kwetu kwa mema yetu sisi. Lakini Lewis ameonyesha kuwa isipokuwa tu mema hayo yaashiriwe na sifa kwa Mungu, mema hayo yana pimwa. Na basi Mungu hakutaka kupima mema yako kwa njia yoyote ile, anasema, “Nisifu mimi. Kwa yote utendayo, nisifu mimi. Kwa yote utendayo, nitukuze. Kwa yote utendayo, kuwa na Ari ya ukuu wangu,” ambayo kwa urahisi inamaanisha kuwa ari ya Mungu itukuzwe na ari yako ili ufurahie na utosheke hazihitilafiani. Yote yanaungana. Mungu anatukuzwa sana ndani yako ukiwa umetoshelezwa sana ndani yake.

Basi hiyo ndio mwisho wa mazungumuzo asubuhi hii ya leo. Acha nikueleze mahali tunaelekea na hili kesho ili upate kuiombea na ili upate kuja na uniruhusu kumaliza kwa sababu sijamaliza. Ikiwa hii ni kweli yakuwa Mungu anatukuzwa sana ndani yako ikiwa umetoshelezwa sana ndani yake . . . na basi hakuna wasiwasi au tofauti kati ya kutoshelezwa kwako ndani yake na kutukuzwa kwake ndani yako . . . kwa hivyo kazi ya maisha yako ni kutafuta mema kwako. Naiita Hedonism ya Ukristo, na nataka kunena nawe kesho kuhusu jinsi gani unatenda hayo, sababu na jinsi inavyobadilisha uhusiano wako na watu, vyuo vikuu vyenu, kuabudu kwako na hatima yako.