Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa kupata furaha yake na yetu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Gain His Joy and Ours

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 48 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza
imani yetu; ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake
aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa
kuume wa kiti cha enzi cha Mungu” (Waebrania 12:2)

Barabara ambayo inatuongoza katika furaha ya milele mbinguni ni ngumu sana. Ni barabara ngumu sana kwetu na pia ilikuwa barabara ngumu kwa Kristo kwa sababu ilimgharimu maisha yake. Kwa furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba. Kwanza kabisa kulikuwa na uchungu wa msalaba, halafu baadaye furaha ya mbinguni. Hakukuwa njia nyingine.

Kuna sababu mingi kwa nini Bwana Yesu Kristo alikuwa na furaha kubwa sana baada ya kifo chake msalabani. Kwanza, alikuwa na furaha ya kuungana na Babake: “Utanijazia furaha katika uwepo wako, pamoja na furaha za milele katika mkono wako wa kuume” (Zaburi 16:11). Pili, alikuwa na furaha kwa sababu alishinda nguvu za dhambi: “Akiisha kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi aliketi mkono wa kuume wa Ukuu huko mbinguni” (Waebrania 1:3). Tatu, alikuwa na furaha kwa sababu alikalishwa mkono wa kuume wa Mungu Baba: “Naye ameketi kwa mkono wa kuume wa Mungu” (Waebrania 12:2). Nne, alikuwa na furaha kwa sababu watu ambao alikufia wanamzingira wakimsifu: ““Kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye” (Luka 15:7).

Kwa hivyo Bwana Yesu Kristo alikuwa na furaha kubwa sana wakati alipokufa msalabani. Bibilia inasema kwamba sisi ambao tumeokoka tunashiriki naye katika furaha hii. “Nimewaambia mambo haya ili furaha Yangu iwe ndani yenu na furaha yenu iwe kamili” (Yohana 15:11). Alijua kwamba angekuwa na furaha kubwa ndiyo maana alisema, “Furaha yangu iwe ndani yenu.” Sisi ambao tumemwamini tutafurahia kwa furaha kubwa.

Barabara ya furaha ya milele ni ngumu sana. Yesu alisema, “Ulimwenguni mnayo dhiki” (Yohana 16:33). “Mwanafunzi hawezi kumzidi mwalimu wake wala mtumishi hamzidi bwana wake. Yatosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake na mtumishi kuwa kama bwana wake. Ikiwa mkuu wa nyumba ameitwa Beelzebuli, je, si zaidi sana wale wa nyumbani mwake mwenyewe!” (Mathayo 10:24-25). “Baadhi yenu watauawa. Mtachukiwa na watu wote kwa ajili ya Jina langu” (Luka 21:16- 17). Bwana Yesu Kristo hakuwaahidi wanafunzi wake maisha yenye starehe hapa ulimwenguni. Aliwaambia wazi kwamba watakumbana na mateso mengi. Hii ndiyo barabara ya kuelekea katika uzima wa milele.

Tunajua kwamba Bwana Yesu Kristo alivumilia msalaba kwa sababu alijua kwamba kulikuwa na furaha kubwa mbele yake. Kwa njia hiyo hiyo sisi pia tunaweza kuvumilia mateso katika maisha haya kwa sababu baada ya maisha haya kutakuwepo na furaha tele. Yesu alisema, “Ni heri ninyi watu watakapowashutumu na kuwatesa na kunena dhidi yenu mabaya ya aina zote kwa uongo kwa ajili yangu. Furahini na kushangilia kwa maana thawabu yenu ni kuu” (Mathayo 5:11-12). Siku moja hata sisi tutakuwa na furaha mbele ya Mungu.

Kwa sababu Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili yetu, jinsi tutavyotazama mateso yetu inafaa iwe tofauti sana. Sisi siyo kama watu wa ulimwengu ambao hawezi kuvumilia mateso na majaribu. Tunavumilia mateso kwa sababu ya kile ambacho kiko mbele yetu. “Nayahesabu mateso yetu ya wakati huu kuwa si kitu kulinganisha na utukufu utakaodhihirishwa kwetu” (Warumi 8:18). Hii ndiyo sababu mtu ambaye ameokoka anatazama mateso na majaribu kwa njia tofauti kabisa. Anajua kwamba kuna furaha ya milele ambayo inamngojea. “Inawezekana kilio kikawepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha” (Zaburi 30:5).