Hebu twenendeni na shutuma alioubeba Yesu

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Suffering
Topic Index
About this resource
English: Let Us Go with Jesus Bearing Reproach

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Suffering
Part of the series Hebrews

Translation by Desiring God

Vivyo hivyo Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji iliawwatakase watu kwa damu Yake mwenyewe. 13 Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. 14 Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunatafuta ule ujao. 15 Basi kwa njia yake, tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani, matunda ya midomo inayolikiri Jina Lake. 16 Msiache kutenda mema na kushirikiana vile mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.

Yaliyomo

Songelea hitaji, wala si kwa ustarehe

Hoja la Waebrania 13:12-16 ni dhahiri shahiri. Wakristo msogelee hitaji wala si starehe! Sogelea hitaji, wala si starehe!

Mwito wa kati kwetu upo katika mstari wa 13: “Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba. Ni kusema, enda na Yesu karibu na hitaji, wala si starehe.” Hii amri katika mstari wa 13 ni juu ya kifo cha Yesu, vile kilvyofanyika na kile kilichotimiliza. Mstari wa 12 “Vivyo hivyo Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu Yake mwenyewe [hicho ndicho kilichotumiliza], aliteswa nje ya lango la mji [hivyo ndivyo ilivyofanyika].” “Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kam . . .” Kwa mukhtadha mwingine, anasema, “Wakristo muungane na yesu katika mateso Yake!” Kwa sababu Yesu aliteswa nje ya lango la mji, tokeni nje ya kambi ya ulinzi na ufahamu na urahisi, na muwe tayari kuichukua aibu naye katika njia ya Kalvari. Na kwa sababu alikufa hapo ili awatakase, usifanye hii kwa nguvu zako ama maadili mema kama kitendo tu cha kuiga; uifanye kwa nguvu na utakatiifu ambao Yesu alikunulia kupitia kwa kifo chake. La sivyo haitakuwa kitendo cha imani bali kitendo cha ushujaa; na utapokea utukufu, wala si Kristo, na Mungu hatafurahishwa. Kwa sababu bila imani ni vigumu kumpendeza Mungu (11:6).

Basi hoja kuu ni: Mkristo, aliye na Mwokozi kama huyu, hapa ni vile inafaa muishi—sogelea karibu na hitaji wala si starehe.

Sasa najua mwito huu unaweza kutumiwa vibaya. Mama ambaye hajaolewa anaweza sema, “Sawa, nafaa kutafuta mwanaume mnyonge sana na anaye hitaji ambaye naweza kupata na niolewe naye kwa tumaini kuwa nitamtendea baadhi ya wema.” Ama msomi mdogo anaweza sema, “Sawa, ninastahili kutafuta kampuni iliyo dhaifu na isiyo sitiri sana katika biashara ya tarakilishi na nijaribu kuajiriwa pale kwa matumaini kwamba nitaifanya ipate kuimarika tena.” Ama gari lako linafaa kuundwa, unaweza kusema, “Sawa, nitatafuta fundi wa gari ambaye yuko karibu kuacha biashara kwa sababu hana mbele wala nyuma na nipeleke gari langu huko ili nikamsaidie.” Sasa ni kiasi gani ya kugutuka kwako; sogelea karibu na hitaji, wala si starehe.

Mwito mkuu wa Yesu

Shida na matumizi mabaya ya miito hii ya Yesu ni kuwa haiko muhimu ya kutosha. Ni ya kipumbavu. Kwa nini udhani kuwa unastahili kuoleka? Yawezekana kuwa mwito wa Yesu kusogeleaa karibu na hitaji wala si starehe ni mwito wa kukaa bila kuoa ama kuolewa kwa ajili ya huduma kuu. Ama yaweza kuwa mwito wa kuoleka kwa aina ya mtu ambaye ni imara ya kutosha na anayestahimili sana kuenda nje ya kambi pamoja nawe na kuteseka karibu nawe, na kuimarisha maisha yenu pamoja kwa wema wa wengine badala ya kuzama kwenye vidimbwi vidogo vya kujistarehesha vile ndoa nyingi ziko.

Na kwa nini inafaa ufikirie kuwa unafaa kuwa unatafuta kazi nchini Marekani—katika kampuni ambayo ni dhaifu ama imara—kama kazi kama hizo zapatikana katika nchi ambazo hakuna hata Mkristo yeyote na hitaji ya nuru yako ni ya yahitajika sana. Ama pengine unafaa ufanyie kampuni dhabiti kazi hapa kwa sababu kuna watu wanaoangamia hapo ama kwa sababu kutakuwa na nafasi ya ushawishi ya hali ya juu ya kueneza maadili ya ufalme na kufanya vitabu vitumikie ukuu wa Mungu katika vyote.

Kwa nini unadhani kuwa unafaa uwe na gari? Labda mwito wa Yesu maishani mwako ni kuhamia pahali na kwa watu ambao hulihitaji gari—kwa sababu hakuna barabara yoyote, wala makanisa ama wakristo. Ama labda unafaa uwe na gari ambalo ni sawa ndipo upate kuliendesha bila tatizo ukielekea karibu na hitaji, wala si starehe.

Mwito mkuu wa Yesu ili uunganike pamoja naye katika njia ya Kalvari—kuenda nje ya kambi ili tuichukue aibu aliyobeba pamoja naye—unaweza kubadilishwa na kukejeliwa na kufanywa kuonekana kipumbavu. Ni njia mojawapo rahisi ya kuponea. Ina majaribu. Inakufanya uonekane mwerevu. Inafanya Yesu kuonekana asiye ya maana. Na inakuweka huru (kwa miaka michache ya kujidanganya) kuendelea katika njia iliyotupu, iliyoshambaa, ya hali ya kutafuta starehe ambayo baadhi ya watu wanaiita maisha.

“Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba (mstari 13) . . . kwa sababu (mstari wa 12) vivyo hivyo Yesu naye aliteswa nje ya lango la mji ili awatakase watu kwa damu Yake.” Vile alivyokufa na sababu ya kifo chake kinaleta tofauti yote kwetu sisi ambao anawaita kwenda pamoja naye. Vile alikufa ilikuwa nje ya lango, kule Golgotha, kwa hiari, kidhabihu, kwa upendo. Na sababu ya kufa (mstari wa 13) ilikuwa ni kuwatakasa watu, kutufanya tuwe tofauti na watu wengine duniani, kutufanya watakatifu na wa kupendeza na wagumu na wanaojitolea na waliojawa kabisa na hatima nyingine kuliko yale ya dunia hii yatupatia.

Utakaso unamaanisha nini kwa hakika?

Zingatia mstari unaofuata (mstari wa 14) ili upate ufahamu juu ya vile watu waliotakaswa walivyo. Utakaso unamaanisha nini? Kristo alikufa ili awatakase watu; ni kusema, kuleta aina ya watu ambao wako tayari kufikiria juu ya maisha yao yote kama kuenda na Kristo nje ya kambi kuichukua aibu aliyoubeba. Kwa njia gani? Ni nini kimetenddeka kwa hawa watu? Mstari wa 14 unatuonyesha. Wako tayari kuenda pamoja na Yesu katika njia ya Kalvari ya hitaji, wala si starehe, “ Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ujao.”

Hoja hii ni gani? Hoja ni kuwa Kristo hakufa ili afanye Minneapollis wa wakati huu kuwa paradiso. Alikufa ili tupate kuwa tayari kukoma kujaribu kuufanya maisha yetu ya kibinafsi kuwa paradiso duniani—huku Minneapolis ama kwingine. Kwa nguvu gani? Kwa sabu sisi ni watu wanaofurahia katika mateso? Kwa sababu tunayapenda mateso? La. Kwa sababu “tunautafuta mji ule ujao.” Je waona hiyo? Mstari 14 Kwa kuwa hapa hatuna mji udumuo, bali tunautafuta ule ujao.” Nia yetu ya kuenda nje ya kambi—karibu na hitaji, wala si starehe, kukiichukua aibu aliyoubeba, tukijali ju ya watu—ni kwa sababu kuna mji ujao, “mji wa Mungu aishiye” (Waebrania 12:22). Ni vyema zaidi kuliko kile wakati huu unatupatia na utadumu milele, na iliyo vyema zaidi kuliko yote, Mungu atakuwepo huko, bila kupungukiwa na utukufu (12:23).

Tumeuona mtindo huo mara kadha wa kadha katika Waebrania. Tuliuona katika 10:34 pahali ambapo Wakristo walisogelea karibu na hitaji na wala si starehe kwa kutembelea wafungwa. Wakati iliwagharimu mali yao, walifurahi, Waebrania inasema, kwa maana “mlijua kwamba mnavyo mali iliyo bora zaidi idumuyo”—walikuwa wakitafuta mji ujao, si starehe na paradiso katika dunia. Basi walisogelea karibu na hitaji, wala si starehe.

Tuliuona katika sura 11:25-26 pahali ambapo Musa alisogelea karibu na hitaji, wala si starehe, “Akachagua kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa anasa za dhambi kwa kitambo kidogo tu. Aliona kushutumiwa kwa ajili ya Kristo ni utajiri mkubwa zaidi kuliko hazina za Misri.” Kwa njia gani? Kwa nguvu gani? Mstari 26 unasema, “Kwa sababu alikuwa anatazamia kupata thawabu baadaye”—ni kusema, alikuwa akiutazama mji ujao.

Tuliuona katika sura ya 12:2 pahali Yesu alisogelea karibu na hitaji, wala si starehe wakati “alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba.” Kwa nini? Kwa njia gani? Mstari wa 2 unasema ilkuwa kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake. Ni kusema, aliutazama mji ujao.

Tuliuona katika sura 13:5-6 wakristo wakisogelea karibu na hitaji, wala si starehe, kwa kulinda maisha yao kutoka kwa kupenda pesa na kuridhika na walivyo navyo. Kwa njia gani? Kwa nguvu gani? Mstari wa 5 “Kwa ajili ya [Mungu] alisema, “Kamwe sitakuacha, wala sitakupungukia, kwa hivyo tunaweza kusema kwa ujasiri; ‘Bwana ni msaada wangu, sitaogopa, mwanadamu atanitenda nini?’”—Mimi sasa na kila wakati nitakuwa salama katika kumhifadhi Mungu. Mimi ni mkaazi wa mji ujao na hakuna kitu ambacho kinaweza kunitenga nao. Basi nitasogelea karibu na hitaji, wala si starehe.

Basi hoja ya Waebrania 13:14 inathibitisha tena na tena: Kristo hakufa ili kuifanya miji ya wakati huu—ama vitongoji—paradiso. Alikufa ili tuwe tayari kukoma kufanya maisha yetu paradiso duniani—katika miji na hata kwa vitongoji, na badala yake tuende na Yesu nje ya kambi ya starehe na kujulikana na usalama hadi pahali mahitaji yako na pahali asemapo, leo (siku utakapokufa) utakuwa pamoja name paradise (Luka 23:43). Tukisogelea karibu karibu na hitaji, wala si starehe, kwa sababu tunautazama mji ujao. Ujasiri uluo tofauti katika usoni tukufu pamoja na Mungu ndiyo Kristo alifilia ili alete. Na inapokushika, utatakaswa (mstari wa 13) na kuenda pamoja na Yesu karibu na hitaji wala si starehe.

Maisha ya sifa kwa Mungu na upendo kwa watu

Wacha tuenende kimaalum. Kile kilichohusishwa katika maisha hii unaosogelea karibu na hitaji wala si starehe—hii maisha nje ya kambi katika njia ya Kalvari, tukienda pamoja na Yesu kwa mateso kwa ajili ya furaha iliyoandaliwa mbele yetu katika mji ujaop? Mstari wa 15 unapeana jibu moja na 16 lingine.

Mstari wa 15 unasema ni maisha ya kumtolea Mungu dhabihu ya sifa—hakika, inayotoka ndani ya moyo, sifa za kinywani—ile itokayo kinywani mwako kama tunda na bubujiko la roho yako. Mstari wa 15 Basi “Kwa njia Yake [Yesu], tuzidi kumtolea Mungu dhabihu ya sifa, yaani matunda ya midomo inayolikiri Jina Lake.

Mstari wa 16 unasema kuwa ni maisha ya upendo kwa watu—ya hakika, ya kuonekana, kushiriki maisha yako kwa wema wa wengine: “Msiache kutenda mema na kushirikiana vile mlivyo navyo, kwa kuwa dhabihu kama hizo ndizo zinazompendeza Mungu.”

Kwa maneno mengine, tunapoenda pamoja na Yesu katika mahali pake pa dhabihu nje ya kambi, tunaona kwa wazi sana kuwa dhabihu yake kwetu—kujitolea, mara moja kwa ajili ya wenye dhambi (Waebrania 9:26-28)—yakamilisha dhabihu zote isipokuwa za aina mbili: dhabihu ya sifa kwa Mungu (mstari 15) na dhabihu ya upendo kwa watu (mstari 16).

Sasa hapa tupo nje ya kambi katika njia ya Kalvari pamoja na Yesu, tukibeba aibu tukisogelea karibu na hitaji, wala si starehe—na hii ni njia gani? Inaelekea wapi? Sana sana, mchana huu? Kwako? Wiki hii? Mwaka huu? Labda ni njia ielekeayo kwa kufunga na kuwaombea watu wasiofikiwa kumi kati ya mianya arobaini, · ama kwa Ukumbi wa Huduma kushiriki na mayatima wenye asilia ya Ukraine, ama katika makazi mapya ya Kliniki ilyoko karibu nasi ya kuavya mimba, hospitali ya wanawake ya Midwest, ama katika barabara ya South 5th Street ili kuwasaidia Sara na Naomi na wengine kusimamia uhai, · ama nyumbani mwa Glen na Patti Larson, na wengine wanaosimama katika ufuo wa milele, · ama katika ukurasa wa 18 wa Jarida la maombi kwa kanisa linaloteswa ili tupate mashirika yanayoweza kukupatia njia ya kivitendo ya kuwatunza Wakristo wanaoteseka kote ulimwenguni, · ama kwa simu ili kufanya mawasiliano magumu kumsihi rafiki mpotovu ili arudi kwa Yesu, · Ama kwa jirani ambaye unajua anaangamia katika kutoamini.

Njia ya Kalvari ya kuelekea karibu na hitaji, wala si starehe inaelekea kwa elfu za sehemu zinazowezekana za upendo na sifa.

Mungu na aitumie Waebrania 13:13 ili akutikishe uwe huru

Ombi langu asubuhi hi ni kwamba kati yenu vijana wadogo ambao hatima yao bado haijaimarika, na nyinyi wazee waliostaafu ambao bado wako na nguvu na uhuru zaidi, na nyinyi wengine wa hapo kati ambao wangetaka kuyatumia yote na kufanya kitu fulani tofauti sana na maisha yenu vile thenashara wengi wa watu ambao hawajaoleka au kuoa wamefanya katika kanisa hili katika miaka hii—ombi langu ni kwamba kati ya nyinyi wote, Mungu apate kutumia neno hli kutoka Waebrania 13:13 ili awatikishe kwa misingi na kuwafungua kutoka mahali penu na kuwatuma kwa watu ambao hawajafikiwa wa ulimwengu na Injili ya utukufu ya neema ya Mungu katika Yesu Kristo. Najua hii si wiki ya huduma, lakini hili ndilo ninalolisikia kutoka kwa andiko hili kwa baadhi yenu asubuhi hii.

Mamia ya maelfu wa Wakristo ulimwenguni wanahatarisha maisha yao ili wawe tu Wakristo asubuhi hii. Tunajua kutoka kwa Ufunuo 5:11 kuwa sababu Kristo alienda nje ya kambi na kuteseka ilikuwa ni kukomboa watu kutoka kwa kila kabila na ndimi na watu na taifa. Na kama hiyo ndiyo sababu alienda, basi je inafaa imaanishe nini wakati Waebrania 13:13 inaposema, “Kwa hiyo basi na tumwendee nje ya kambi, tukiichukua aibu aliyobeba?” Inafaa imaanishe kwa wengi wetu: Kutoka kwa kambi! Kutoka kwa kambi! Kutoka kwa kambi ya Bethlehemu yenye starehe. Kutoka kwa kambi ya Minneapolis yenye starehe. Kuacha kazi salama, iliyo na starehe. Na kuungana na Yesu katika njia ya Kalvari inayoelekea kwa hitajii wala si starehe.

La, hakuna haja ubadilishe tamaduni ndipo ulitii andiko hili. Nimepeana taswira sita ya hiyo. Lakini sikiza: Yesu aliteseka nje ya kambi kwa ajili ya mataifa, mamia kati yao ambao hawana kanisa, vitabu, huduma ambayo yaweza kuwajulisha kwa habari ya kuwa Kristo alikuja duniani kuwaokoa wenye dhambi. Natilia mkazo hii: Waebrania 13:13 ni mwito wa kusogelea karibu na hitaji na wala si starehe. Na hitaji linalolilia masikioni mwangu Jumapili hii ni hataji la watu pahali Wakristo wanaangamia kwa sababu ya mateso, na mahali wenye dhambi wanaamgamia kwa sababu hakuna Wakristo waliotayari kuteswa.

Nawasihi, mnapoota kuhusu siku zenu za usoni, hata kama uko na umri wa miaka 8 ama 18 am 38 ama 80, muiote Waebrania 13:13, kwa hiyo basin a tumwendee nje ya kambi, tukichukua aibu aliyobeba.

Hatuendi pekee yetu

Tunaenda kujitakasa kwa hii kwa kuimba wimbo wa mwisho uliochapishwa katika kibeti chenu cha ibada, Tunajilaza Kwako, wengi wenu wanajua kuna hadithi kuhusu hii ambayo inapatia nguvu spesheli kwa wakati huu. Jim Elliot, Pete Fleming, Ed Mc Cully, Nate Saint na Roger Youderian waliuawa mwezi wa Januari, 1956, nchini Ecuador, wakielekea karibu na hitaji la Wahindi wa Auca na wala si starehe. Dibaji ya sura ya 16 ya nakala ya Elisabeth Elliot ya mauaji kwa ajili ya neno ni mstari kutoka kwa wimbo huu. “ Hatuendi pekee yetu.”

Muda mfupi kabla ya vifo vyao huko Palm Beach walimba wimbo huu. Elliot anaandika,

Katika tamati ya maombi yao, wanaume watano waliuimba mojawapo ya nyimbo zao walizozipenda sana. “Tunajilaza Kwako” wakiongozwa na sauti ya “Finlandia.” Jim na Ed walikuwa wameshauimba wimbo huu tangia nyakati zao za chuo na walijua mistari yote. Katika mstari wa mwisho sauti zao zilijawa na imani ya kiundani. Kwako tunajilaza, mlinzi na ngao yetu, vita ni Vyako, sifa ni Kwako, Tunapopitia katika malango yaliyopambwa ya washindi, tutakaa pamoja Nawe hadi siku ambazo hazitakoma.

Katika ujasiri huo, walimwendea Yesu nje ya kambi. Walisogelea karibu na hitaji, wala si starehe, na wakafa. Na maombi ya Jim Elliot yakadhihirika kuwa kweli: “Yeye si mpumbavu kupeana kile ambacho hawezi kukihifadhi ili kupokea kile hawezi kukipoteza.” “ Hapa hatuna mji udumuo, lakini tunautafuta ule mji ujao” (Mstari wa 14).

Nakualika uuimbe. Na unapoyafikia maneno, “Na katika Jina Lako tunaenda,” uumaanishe, na.