Huduma kwa mchungaji wako

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Church Issues
Topic Index
About this resource
English: Ministering to Your Pastor

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Church Issues

Translation by Trufosa Ogonda

Review You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).


The Bible Friend (Sehemu ya 75, Nambari 8), Minneapolis, MN

Hebu tuanze na kifungu cha Maandiko kutoka Warumi 1:8-12. Paulo anaiambia kanisa:

Kwanza, ninamshukuru Mungu kwa kupitia Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa kuwa imani yenu imetangazwa duniani kote. Mungu ninayemtumikia kwa roho yangu katika injili ya Mwanawe, ni shahidi yangu kuwa siku zote ninawataja katika maombi yangu bila kukoma, nikiomba ya kuwa kwa njia moja au nyingine, kwa mapenzi yake Mungu, nitaweza kufaulu kuja kwenu. Kwa kuwa nina hamu ya kuwaona, ili niweze kuwagawia kipaji cha kiroho kitakachowapa nguvu- ili tuweze kutiana moyo kwa kupitia imani ya kila mmoja wetu, imani yenu na yangu.

Ningependa tujadiliane kuhusu jukumu letu la kumhudumia mchungaji wetu. Tumesikia mara nyingi ya kuwa Wakristo ni wahudumu, kulingana na kitabu cha Waefeso 4:12. Katika mafunzo ya Jumapili kwa watoto wadogo, tunasisitiza umuhimu wa kuombeana na kutiana moyo katika imani, lakini mara nyingi tuna mazoea ya kusahau ya kuwa mchungaji ni mmoja wetu. Kwa hivyo, ningependa kutukumbusha sababu zinazofanya tupaswe kumhudumia mchungaji wetu, namna tunavyoweza kuifanya kwa njia bora zaidi, na matokeo tunayoweza kuyatarajia.

Kwanza kabisa, kuna umuhimu gani wa kumhudumia mchungaji wetu? Sababu ni kuwa yeye ni binadamu na ni muumini kama sisi. Kwa kuwa yeye ni binadamu, anapata majaribu kama sisi sote. Imani haimjii bila pingamizi eti kwa kuwa yeye ni mchungaji. Pia si rahisi zaidi kwake kuwa mwenye upendo na mwenye matumaini kuliko ilivyo kwetu. Raslimali zake katika vita vya imani sio nyingi zaidi kuliko zetu. Yeye ni mmoja wetu.

Zaidi ya hayo, mizigo ya kipekee inayohusiana na wito wake inahitaji msaada wetu wa kiroho kwake, kwa mfano, mzigo wa kiutawala wa kuhakikisha ya kuwa mambo yote yameshughulikiwa ipasavyo. Mara nyingi huwa hata hatujui mengi kati ya mambo haya. Kisha kuna mzigo wa kusikiliza na kuwasilisha ujumbe kutoka kwa Mungu wiki baada ya wiki. Usidanganyike ya kuwa ujumbe huu humjia mchungaji kwa urahisi. Ili kuhakikisha ya kuwa ujumbe unaambatana na mafunzo ya Bibilia, mchungaji anapaswa kutia bidii. Machozi mengi hutiririka wakati mchungaji anaposhindwa kupata ujumbe. Wakati tunapokaukiwa kiroho, tunaweza kukosa kuja kanisani au tunaweza kuhuduria maombi ya kututia moyo, lakini je mchungaji anaweza kuenda wapi?

Kisha kuna ule mzigo wa kuwataka wafuasi wake kuiga mfano wa Yesu na kuwa mwanga wa dunia. Paulo aliwaambia Wagalatia (4:19), “Niko tena katika uchungu wa kuzaa hadi pale ambapo Kristo ataumbwa ndani yenu!” Hakuna kinachomtatiza roho mchungaji kuliko pale ambapo watu hawakui katika imani, upendo, na uadilifu.

Unaweza kuunda orodha ndefu zaidi ya matatizo yanayowakumba wachungaji, lakini kwa sasa, tutaangalia namna ambavyo tunaweza kumhudumia mchungaji wetu.

Njia mwafaka ya kubeba mzigo wa mchungaji wako ni kuwa Mkristo. Paulo alisema katika Wafilipo 2:2-3, “Timiza furaha yangu kwa kuwa watu wenye moyo sawa, kwa kuwa na upendo sawa, kwa kuishi kwa amani kamili na kwa kuwa na mtazamo mmoja. Usifanye lolote kutokana na ubinafsi au majivuno bali katika unyenyekevu, waone wengine kuwa ni wa maana kukuliko wewe.” Kwa maneno mengine, hakuna kitakachomtia moyo mchungaji wetu kama waumini walionyenyekea, wenye upendo na wanaoiga mfano wa Kristo. Paulo aliliambia kanisa la Warumi, “Ninatamani kuwaona...ili tuweze kutiana moyo kwa kupitia imani ya kila mmoja wetu” (1:11-12). Imani yetu ni chanzo cha faraja kuu kwa mchungaji wetu. Kwa hivyo tunapaswa tuwe watu wenye imani.

Bali na haya, nina pendekezo tatu dhahiri ya mambo tunayoweza kuyafanya ili kumjenga mchungaji wetu na kuhakikisha ya kuwa huduma yake inazaa matunda zaidi.

  1. Mwombee kila siku. Iandike chini ili usisahau. Na usiseme tu “Mungu mbariki mchungaji.” Ombea mambo maalumu. Ombea afya yake, mahubiri yake, familia yake, matembezi yake, kasoro na udhaifu wake. Jiweke pahala pake na ujaribu kuhisi anvyohisi wakati unapomwombea.
  2. Pili, jitolee kumwambia maneno yanayotia moyo. Mwandikie waraka katika kadi ya kujiandikisha, mtumie barua mara kwa mara nyumbani kwake; mpigie simu. Mtafute akiwa peke yake wakati mwingine, mtazame usoni na useme, “Ninathamini kazi yako, mchungaji, na ninakuombea kila siku.” Usitosheke na salamu za juu juu zinazotolewa mlangoni baada ya ibada ya Jumapili.
  3. Tatu, mkosoe kwa roho wa msamaha. Sijawahi kuzungumza na yeyote maishani mwangu aliyefurahishwa kitimilifu na mchungaji wake. Na sababu ni rahisi sana: Binadamu wote wana kasoro. Inaonekana ya kuwa kuna watu ambao hawajajifunza jambo hili, na wanaruka kutoka kanisa moja hadi lingine wakimtafuta mchungaji asiye na kasoro. Hiyo ni kazi bure. Ni bora zaidi kutafuta kanisa unakojihisi kuwa nyumbani na uchukue jukumu la kumsaidia mchungaji kukua. Kila mtu angependa kubadili jambo moja au lingine kuhusu mchungaji wake, lakini ni wangapi kati yetu waliojitolea kumuombea? Na ni wangapi wamekaa chini naye na kwa moyo mkunjufu na wenye msamaha wamemwambia abadilike? Kama tunampenda, tutafanya hivi... kwani atutishi kiasi cha sisi kutoweza kuzungumza naye.

Hizo ni baadhi ya njia za kumhudumia mchungaji wako. Unaweza kufikiria njia zingine.

Swali la mwisho nililoliuliza lilikuwa, ni nini ambayo tunaweza kutarajia kutokana na huduma yetu? Kwa ufupi, tunaweza kutarajia kuwa na mchungaji aliyetiwa moyo, mwenye matumaini na aliye imara. Kwa hivyo, huduma yetu kwake itaturudia kama rada na itawafanya waumini kuwa wenye nguvu, matumaini na walio imara. Kisha dunia itatambua ya kuwa Kristo yuko kwa kweli na anafanya kazi kati yetu.