Kristo Aliteseka Akafa ili Kutukomboa kutokana na Uovu Uliopo

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Christ Suffered and Died to Deliver Us from the Present Evil

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Part of the series Taste & See

Translation by Jescah Abuti Muyia

Review You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).



Wagalatia 1:4

[Yeye] ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu, ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama anavyopenda Mungu, Baba yetu.

Hadi tutakapoaga dunia, au hadi Kristo atakaporudi kuweka ufalme wake, tunaishi katika "dunia hii mbovu iliyopo sasa" Kwa hivyo, Biblia inaposema kuwa Kristo alijitoa nafsi yake "ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa," haimaanishi kuwa atatuondoa ulimwenguni, bali kuwa atatukomboa kutokana na nguvu za mwovu ndani duniani. Yesu alituombea ifuatavyo: "Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu" (Yohana 17:15).

Sababu inayompelekea Yesu kuomba kwa ajili ya ukombozi dhidi ya "yule mwovu" ni kwa kuwa "dunia hii mbovu iliyopo sasa" ni kipindi ambacho shetani amepewa uhuru wa kudanganya na kuharibu. Biblia inanena, "Dunia yote pia hukaa katika yule mwovu" (1 Yohana 5:19). Huyu "mwovu" huitwa "mungu wa dunia hii" na nia yake kuu ni kupofusha watu wasione ukweli. "mungu wa dunia hii amepofusha fikra zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu" (2 Wakorintho 4:4).

Hadi pale tutakapojikwamua kutokana na hali yetu ya kihoro iliyogubikwa na giza, tutaishi kwa makubaliano na"dunia hii mbovu iliyopo sasa" na mfalme wake. "ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi" (Waefeso 2:2). Bila kujua, tulikuwa wafuasi wa ibilisi. Kile kilichoonekana kama uhuru ilikuwa utumwa. Biblia inanena moja kwa moja na mashabiki, wapenzi, wanaopenda mno mtindo wa karne ya 21 inaposema, "wakiwahaidia uhuru, nao wenyewe ni watumwa wa uharibifu, maana mtu akishindwa na mtu huwa mtumwa wa mtu yule" (2 Petro 2:19).

Kile kinachoenda sambamba na uhuru kwenye Biblia ni: "Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu"(Warumi 12:2). Kwa maneno mengine, kuwa huru! Usidandanywe na maguru wa kipindi hiki. Wapo leo na wala kesho hawatakuwepo. Kila mpenda utumwa humuiga mwenzake. Miaka thelathini kutoka sasa alama za chale hazitakuwa alama za uhuru, bali ukumbusho usioweza kufutika wa kuegemea mrengo fulani.

Hekima ya dunia hii ni upuuzi kwa Mungu. "Mtu asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona mwenye hekima miongoni mwenu katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima ya dunia hii ni upuuzi mbele za Mungu. . . . Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuuzi" (1 Wakorintho 3:18-19; 1:18). Ni nini haswa hekima ya Mungu ya dunia hii? Ni kifo kikuu cha Yesu Kristo kinachokomboa. Wafuasi wa kwanza wa Yesu walisema, "bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulubiwa . . . nguvu ya Mungu (1 Wakorintho 1:23-24).

Yesu aliposulubiwa msalabani, aliwaweka huru mamilioni ya watumwa. Aliweka wazi hila ya ibilisi na kuvunja nguvu zake. Hii ndiyo maana ya maneno yake msalabani aliposema "sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje" (Yohana 12:31). Usimfuate adui aliyeshindwa. Mfuate Kristo. Inagharimu. Utakuwa mtumwa katika dunia hii ya sasa. Lakini utakuwa huru.