Kumtukuza Mungu na fedha

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Money
Topic Index
About this resource
English: Magnifying God with Money

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Money
Part of the series Worship God

Translation by Desiring God

Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme. (33) Uzeni mali zenu mkawape masikini. Jifanyeni mfuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwizi hakaribii wala uondo haharibu. (34) Kwa maana hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwa pia.

Kusudi la ndani la kuabudu ni kuthamini Mungu kama aliye na thamani juu ya yote. Aina ya nje ya ibada ni matendo ya kuonyeshavile tunavyomthamini Mungu. Hivyo maisha yote inafaa iwe ya kuabudu kwa sababu Mungu alisema lolote mfanyalo kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu (1 Wakorintho 10:31). Fedha na vitu ni sehemu kubwa ya maisha, na hivyo Mungu ananuia ziwe sehemu kubwa ya kuabudu—Kwa kuwa maisha yote inafaa iwe ya kuabudu. Basi vile unaabudu kwa fedha na mali yako ni kuzichukuwa na kuzitumia na kuzipoteza kwa njia ya kuonyesha vile unavyothamini Mungu—si fedha. Hili ndilo jambo katika andiko hili. Na hivyo basi ni andiko kuhusu kuabudu.

Sasa kuna nafasi ya kuabudu kama kikundi—Yale tunayasikia kwa pamoja Jumapili asubuhi. Na maelezo yaya haya yana maana sawa hapa vile yalivyo kwingine: Maana ya ibada hapa ni kumthamini Mungu kwa undani kama aliye na thamani isiyokoma. Na njia za ibada ndiyo matendo yanayodhihirisha thamana hii ya ndani ya Mungu (Kuhubiri na kulisikia neno la Mungu, kuomba kuimba, matoleo, kushiriki meza ya Bwana, vingine vingi.) Aina mojawapo ya matendo ya ushirika hapa Bethlehemu ni lile tunaita “toleo”—Jambo lilo karibu na katikati ya ibada yetu ya ushirika ambapo tunaabudu na fedha, kwa kuzitoa mikononi mwetu na katika benki zetu, na katika huduma ya Kristo.

Basi aina hili la kipekee la tendo la kuabudu katika ibada ya ushirika ni mojawapo ya sehemu ndogo kutoka kwa sehemu kubwa ya kuabudu na fedha zetu ambalo tunalifanya kila siku kupitia kwa njia tupatayo mshahara na kuutumia na kuweka akiba na kupeana fedha zetu. Neno la leo, Luka 12:32-34 ni kuhusu njia kubwa ya vile tunavyoabudu kwa fedha zetu, na hivyo basi kimadili inalingana na yale tunafanya na fedha zetu katika ibada ya ushirika pia. Basi wacha tutazame mambo makuu katika arifa hii, na wacha ifanyike katika maisha yetu ya kawaida na kupeana kwetu kwa ushirika.

Yaliyomo

Usiogope

Jambo la kwanza katika andiko (katika mstari wa 32) ni kuwa Mungu anatuamuru kuogopa ikifika katika fedha na vitu. Usiwe na shaka, usiogope. “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme.” Lakini kuna njia nyingine kusema jambo linalopenyeza ndani. Sababu ya Mungu kututaka kutoogopa kuhusu fedha na vitu ni kuwa hiyo itatukuza vitu vitano vikuu kumhusu. Kutoogopa kutaonyesha vile tunathamini vitu hivi vitano kumhusu Mungu. Kwa maneno mengine, kutoogopa kutakuwa tendo la ndani la kuabudu.

Kwanza, kutoogopa kunaonyesha kwamba twathamini Mungu kama mchungaji wetu. “Msiogope enyi kundi dogo.” Sisi ni kundi lake na Yeye ni mchungaji wetu. Na kama yeye ni mchungaji wetu, basi zaburi 23 lafaa, “BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu.”—Ni kusema, sitapungukiwa na chochote ninachohitaji kwa hakika. Kutoogopa kunatukuza thamani ya mchungaji wetu.

Pili kutoogopa kunaonyesha kuwa tunamthamini Mungu kama Baba yetu. “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme. “Sisi si tu kundi lake; bali watoto wake, na yeye ni Baba yetu. Umuhimu wa hiyo ni wazi katika mstari wa 30, “Watu wasiomjua Mungu husumbuka sana kuhusu vitu hivi vyote. Naye baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mwavihitaji na atafanya kazi kwenu kuhakikisha kuwa mnavyo vile mnavyohitaji (Jihadhari kumsurutisha Mungu kwa yale unafikiria ni “hitaji” baada ya kufahamu yale anayafikiria kama ni ”hitaji”

Tatu, kutoogopa kunaonyesha kuwa tumthamini Mungu kama mfalme. “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme.” Anaweza kutupatia “ufalme” kwa sababu Yeye ni mfalme. Hili linaongeza sehemu kuu ya nguvu kwa Yule atupaye. “Mchungaji” laonyesha ulinzi na usaidizi. “Baba “linaonyesha upendo na uororo na mamlaka na usaidizi na ulinzi. “Mfalme” linaonyesha nguvu wa aliye mkuu juu ya yote na utajiri. Basi tunapomwamini Mungu kama Mchungaji wa baba na mfalme, na kutoogopa kuhusu fedha na vitu, hivyo basi tunaonyesha vile Mungu ni hakika na wa thamani kwetu sisi katika njia hizi zote. Mungu ataabudiwa.

Cha nne, kutoogopa kunaonyesha vile Mungu ni huru na mkarimu “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme.” Tazama anapeana ufalme. Hauzi wala kukodisha ufalme. Anaupeana. Ana utajir i usiokoma na haitaji malipo yetu. Kila ambacho tungetaka kumpa tayari ni yake. “Ni nini ulicho nacho ambacho haukupokea?” (1 Wakorintho 4:7). Basi Mungu ni mkarimu na huru na mali yake. Na hii ndiyo tunaitukuza kwake bila kuwa na uoga bali tunamwamini na mahitaji yetu.

Mwisho, kutoogopa kunamaanisha kuwa tunamthamini Mungu kama mwenye furaha. “Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi ufalme kwa furaha.” Ni “furaha njema.” “Inamfurahisha” kuwapa ninyi ufalme. Anataka kufanya hiki. Inamfurahisha kukifanya. Si sisi wote walio na baba kama huyu—ambaye alipenda kutupa vitu, ambao walifurahi kupeana kuliko kupokea. Lakini hiyo haijalishi, kwa sababu sasa unaweza kuwa na Baba, na Mchungaji na Mfalme kama huyo. Mwamini Baba yako kupitia kazi ya Yesu ya upatanisho, na mtampata kama Baba yako.

Basi Neno la kwanza kutoka kwa andiko hili ni kwamba inafaa tumthamini Mungu kama mchungaji na Baba na mfalme wetu mkarimu na anayefurahi kutupatia Ufalme wake—kutupa ufalme wa mbingu, uzima wa milele na furaha, na kila kitu ambacho tunahitaji kufika huko mbinguni. Tunapothamini Mungu kwa njia hii—tunapomwamini—hatutaogopa na Mungu ataabudiwa. Hii ndio msingi wa neno lililosalia na funzo hili. Lile linakuja lawezekana kwa sababu ya ahadi hii.

Mchocheo wa urahisi badala ya kusanyiko

Jambo la pili ni hili: Kumwamini Mungukwa njia hii kunabeba mchocheo mkuu kwa urahiisi badala la kusanyiko. Mstari 33: “Uzeni mali zenu mkawapa masikini. Jifanyieni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha mahali mwivi hakaribii wala nondo haharibu."

Tafakari kidogo juu ya maneno, “Uzeni mali zenu.” Alikuwa akinena na nani? Mstari wa 22 unapeana jibu. “Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake. “Sasa hawa watu kwa hatua kuu hawakua matajiri. Hawakuwa na mali nyingi. Lakini bado anawaambia, “Uzeni mali zenu.” Hasemi mali kiasi gani ya kuuzwa. Kwa mtawala tajiri katika Luka 18:22 Yesu alimwambia, “Nenda ukauze kila kitu ulicho nacho, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate. Uza kila kitu ulicho nacho. Wakati Zakayo alipokutana na Yesu, alimwambia (Luka 19:8), “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu nawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.” Basi Zakayo alipeana nusu ya mali yake. Katika Matendo ya Mitume 4:37 inasema, “Barnabas aliuza shamba alilokuwa nalo, akaleta hizo fedha alizopata na kuziweka miguuni pa mitume.” Basi aliuza zaidi ya shamba moja.

Basi bibilia haituambi kiasi ya mali ya kuuza. Lakini kwa nini inasema tuuze mali? Kwa nini? Kupeana zaka kuzitumia pesa zako kuonyesha upendo kwa wale hawana mahitaji muhimu ya maisha na bila Injili (hitaji la uzima wa milele)—ni muhimu sana kwa kiasi kwamba kama humiliki kitu cha kuonekana, inafaa uuze kitu fulani ndipo upate kupeana. Lakini sasa tafakari kile hiki kinamaanisha kwa mukhtadha. Hawa wanafunzi si matajiri walioishiwa na pesa ambao pesa zao zimefungwa kwa hisa ama biashara ya ujenzi wa nyumba. Watu wengi kama hao, kwa hakika, huwa na akiba za ndani. Lakini Yesu hakusema, “chukueni kiasi ya akiba yenu na mpeane kama zaka.” Alisema, “muuze kitu, na mkapeana kama zaka.” kwa nini? Jambo la kudhaniwa ni kana kwamba hawakuwa na pesa za kupeanana ikawabidi wakiuze kitu ndipo wapeane. Na Yesu aliwataka watu wake wasogelee urahisi, wala sio kusanyiko.

Kuna haja gani? Jambo ni kwamba kuna mchocheo wenye nguvu katika maisha ya Mkristo kuelekea urahisi wala sio mkusanyiko. Mchocheo unaotokana na kumthamini Mungu kama mchungaji na Baba na Mfalme kuliko vile tunazithamini mali zetu zote. Na mchocheo huu una nguvu kwa sababu mbili. Kwanza ni kwa sababu Yesu alisema, “Tazama ni jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri (Kusema wale wanavimiliki vitu.) Kuingia katika ufalme wa Mungu!” (Luka 18:24). Katika Luka 8:14. Yesu alisema kuwa utariji “hunyonga” neno la Mungu. Lakini tunataka kuingia katika ufalme kwa hali ya juu kuliko vile tunahitaji vitu. Na hatutaki neno la Mungu linyongwe maishani mwetu. Basi kuna mchocheo wa nguvu wa kurahisisha badala ya kukusanya. Sababu nyingine ni kuwa tunataka thamani ya Mungu idhihirike kwa ulimwengu. Na Yesu atuambia hapa kuwa kuuza vitu na kutoa zaka ni njia mojawapo ya kuonyesha kwamba Mungu ni hakika na wa thamani kama Mchungaji, Baba na Mfalme.

Jambo la pili ni kwamba kumwaminji Mungu kama Mchungaji, Baba na Mfalme kunabeba mchocheo kwa urahisi badala ya kusanyiko. Na hii inaleta kuabudu kutoka kilindini mwa moyo kilichofichika na kwa matendo yanayoonekana kwa utukufu wa Mungu.

Kulihifadhi hazina zetu mbinguni, wala si duniani

Jambo la tatu kutoka kwa andiko ni kuwa lengo la fedha ni kuhifadhi hazinazetu mbinguni, wala si duniani. Mstari 33 tena: “Uzeni mali zenu mkawapa masikini. Jifanyeni mifuko isiyochakaa, mkajiwekee hazina mbinguni isiyokwisha, mahali ambapo mwivi hakaribi wala nondo huharibu.” Kuna uhusiano gani kati ya kuuza mali hapa ndipo ukatimize mahitaji ya wengine (sehemu ya kwanza ya mstari), na kujiweka hazina mbinguni (mwishoni mwa mstari)?

Kiunganisho kinaonekana kuwa: njia upatavyo pesa ni vifungo visivyochakaa na vile unahifadhi hazina mbinguni ambazo mwivi hakaribii ni kwa kuuza mali yako kukimu mahitaji ya wengine. Kwa maneno mengine, kurahisisha kwa ajili ya upendo duniani huhifadhi furaha yako mbinguni.

Usipitwe na jambo hili la muhimu sana. Ndio jinsi Yesu anafikiri na kuongea wakati wote. Kuwa na hisia za mbingu kunaleta tofauti wenye upendo humu duniani. Watu ambao wameshawishika kwa nguvu kwa kile kinafaa na hazina ya mbingu, sio hifadhi kubwa ya pesa hapa duniani, ndio wale kila mara ataota juu ya njia za kurahisisha na kutumika, kurahisisha na kutumika. Watapeana na kupeana na kupeana. Na hakika watafanya kazi na kufanya na kufanya, vile Paulo anasema katika Waefeso 4:28, “ili [wawe] na kitu cha kuwagawia wahitaji.”

Uhusiano na kuabudu ni hii. Yesu antuamuru kuhifadhi hazina mbinguni, hivyo ni kusema, kuimarisha furaha yetu katika Mungu. Anasema kuwa njia ya kufanya hii ni kuuza na kurahisisha kwa ajili ya wengine. Basi anahimiza urahisi na huduma kwa tamaa yetu ya kuimarisha furaha yetu katika Mungu. Ambayo unamaanisha matumizi yetu yote ya fedha inakuwa dhihirisho ya vile tunafurahia ndani ya Mungu kuliko fedha na vitu. Na hii ni kuabudu.

Moyo wako husogelea kile ukipendacho

Sasa jambo la mwisho asubuhi hii kutoka kwa andiko hii: moyo wako usogelea kile ukipendacho, na Mungu anataka tumsogelee. Mstari 34: “Kwa maana hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwa pia.” Hili ndio sababu ya kutufanya kutafuta hazina ya mbingu iliyo na dosari. “Kwa maana hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakuwa pia.” Kama kitu ukipendacho ni Mungu aliye mbinguni, moyo wako utakuwa pamoja na Mungu huko mbinguni. Utakuwa pamoja na Mungu. Lakini kama kitu ukipendacho ni pesa na vitu viliyomo duniani, basi moyo wako utakuwa duniani. Utakuwa duniani, utatengwa na Mungu.

Hili ndilo Yesu alimaanisha katika Luka 16:13 aliposema, “Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.” Kuutumikia pesa ni kupenda pesa na kufuata faida zote pesa zinaweza kuleta. Moyo wafuata pesa. Lakini kumtumikia Mungu kunamaanisha kumpenda Mungu na kufuata faida zote anaweza kupeana. Moyo watafuta Mungu. Na hiyo ni kuabudu: moyo unatamani Mungu na unamtafuta kama hazina zaidi ya hazina zote.

Sadaka—njia ya kuabudu

Nafunga kwa kulinganisha mambo haya manne na njia ya ibada ya ushirika ambao tunaita “sadaka”. Wakati huu na tendo hili katika ibada yetu itakuwa kuabudu kwako bila kujali kiwango—kutoka kwa kidogo cha mjane hadi maelfu ya bwenyenye mwenye mamilioni kama kwa kutoa unasema kutoka kwa Moyo: 1) Huu hapa nakuamini, Mungu, kama Mchungaji, Baba wa Mfalme wangu mkarimu na mwenye furaha, hivyo basi sitaogopa nikiwa na pesa kidogo kwangu ya kukimu mahitaji ya wengine; 2) Huu hapa nakataa ushawishi katika utamaduni wetu ya kuhifadhi nyingi na nyingi na napeana kwa mchocheo wa urahisi kwa ajili ya wengine; 3) Huu hapa nahifadhi azina mbinguni na sio duniani ndipo furaha yangu katika Mungu utaimarika milele; na 4) Kwa sadaka/toleo hili natangaza kwamba kwa kuwa hazina yangu i mbinguni, moyo wangu utatafuta Mungu.