Mungu yu kwetu ama yu kwa ajili yake mwenyewe?

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Glory of God
Topic Index
About this resource
English: Is God for Us or for Himself?

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Glory of God

Translation by Desiring God


Mwaka iliyopita nilihudhuria mkutano wa Injili wa Billy Graham kule Anaheim, California. Kulikuwa na watu wapatao 50,000 hapo usiku huo, nadhani, na nikakaa katika viti vya kushoto uwanjani na ningeweza kuona umati mkubwa ukizingira uwanja. Tulipoimba “Jinsi wewe ulivyo mkuu,” niliweza kuimba maneno machche na baadaye sikuwa naweza kuimba tena. Sikuwa nimesikia kitu chochote kama hicho. Sauti 50,000 zikiimba sifa kwa Mungu; ilishtua moyo wangu kwa kiasi ya kwamba sijawahi kuusahau wakati huo. Hakuna kitu chochote ambacho kiliwahi kuonekana kuonekana haki, ama kizuri zaidi ama chenye furaha kuu kuliko viumbe 50000 wakiimba pamoja.

Naamini usiku huo nilipata picha kidogo cha mbingu, kwa sababu Ufunuo 5:11-13 unaonyesha mbingu hivi:

Nami nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wane na wale wazee ishirini na wane, idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu. Nao wakiimba kwa sauti kuu wakisema, “Anastahili Mwana Kondoo, Yeye alichinjwa, kupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na sifa!”

Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake wakiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake Yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana—Kondoo, milele na milele."

Ufunuo wa mbingu ni ufunuo wa viumbe wengi waliohesabika wanaomsifu Baba na Mwana kwa nguvu zao zote. Na wale ambao wameonja utukufu wa Mwana—Kondoo hawawezi kuikosa kwa ajili ya ulimwengu.

Mungu Anafuatilia Sifa Yake Mwenyewe

Mwana—Kondoo anastahili. Mungu Baba anastahili. Hivyo basi tunatupasa kuwasifu. Na hakika tutawasifu. Waumini wengi hawatatizwi na ukweli huo. Lakini kwa wiki mbili sasa tumeona kutoka kwa maandiko kuwa Mungu hajachukua hatua ili tu kustahili sifa, lakini zaidi, ameifanya jukumu lake kujishindia sifa. Mungu haongojei tu kuinuliwa kwa sababu ya nguvu zake na haki na neema, amechukua hatua kutoka milele kuliinua Jina Lake ulimwenguni na kuonyesha utukufu Wake. Yote afanyayo ni kupitia shauku yake ya kupewa utukufu. Isaya 48:11 ndicho kibango kilicho juu ya matendo yote ya kiungu:

Kwa ajili Yangu mwenyewe, kwa ajili Yangu mwenyewe, nafanya hili. Kwa jinsi gani niliache Jina Langu lichafuliwe? Sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.

Yeremia 13:11 linaliweka hivi:

Kwa maana kama vile mkanda ufungwavyo kiunoni mwa mtu, ndivyo nilivyojifunga nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda; asema Bwana, ili wawe watu wangu, kwa ajili ya utukufu wangu, sifa na heshima yangu.

Lengo la Mungu katika yote afanyayo ni kupokea sifa na utukufu wa Jina Lake.

Na tusije tukafikiri kuwa hili liko tu katika Agano la Kale, tutazame kwa makini andiko la asubuhi: Waefeso 1. Ni kitabu cha ajabu mno! Sio tu kwa maneno yanayofika hadi mistari kumi na moja kwa urefu bali pia hadi mbingu kwa urefu. Kuna fungu la maneno uliorudiwa mara tatu katika mistari 6, 12 na 14 ambao unaonyesha wazi fikira ya Paulo kuhusu lengo la Mungu katika kutuokoa kutoka dhambini na kwa ajili Yake mwenyewe. Tazama mstari 5 na 6:

Kwa upendo alitangulia kutuchagua tuwe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo kwa furaha yake na mapenzi yake mwenyewe.

Mstari 12:

Sisi tuliokuwa wa kwanza kuweka tumaini katika Kristo, tupate kuishi kwa sifa ya utukufu Wake.

Ya mwisho, mstari 14:

Roho Mtakatifu ni hakikisho ya urithi hadi tuupokee hati yake katika sifa ya utukufu wake.

Kutoka kwa amri za kale za milele za Mungu ya furaha ya milele ya siku za usoni za urithi wetu za miaka ijayo, lengo la Mungu na kusudi imekuwa kwamba utukufu wake usifiwe, hasa utukufu wa neema wake.

Kwa kuwa Mungu anastahili sifa, kwa kuwa tunapaswa kumsifu, kwa kuwa tutamsifu – huu ndio ukweli kawaida kati ya Wakristo, na tunayathibitisha kwa furaha. Lakini ni nadra sana kusikia ukweli kwamba sifa za utukufu wa Mungu si tu matokeo ya hatua yake bali pia lengo na madhumuni ya hatua hiyo. Anatawala dunia kwa makini hadi mwisho ili apate kutamaniwa, kusujudiwa, kuinuliwa na kusifiwa. Kristo yuaja, Paulo asema katika 2 Wathesalonike 1:10 katika tamati ya nyakati zake, “kutukuzwa katika watakatifu wake na kustaajabiwa miongoni mwa wote walioamini.” Nimepata kutambua kwamba watu wanaupokea ukweli huu shingo upande. Ni vyema Mungu atukuzwe, lakini halionekani vyema kwake kutafuta kutukuzwa. Yesu mwenyewe anasema, “Yule anajiinua atashushwa na yule anayejinyenyekeza atainuliwa?” Bali, kusudio la Mungu kutoka kwa andiko ni kujitukuza machoni pa wanadamu.

Lengo langu kuu katika ujumbe huu ni kuonyesha, vile niwezavyo, kuwa lengo la Mungu na jitihada zake za kujitukuza ni vyema vyote na halina dosari ya aina yoyote na ni tofauti sana na kujitukuza kwa wanadamu kwa sababu ni dhihirisho la upendo. Hivyo basi tutakubali ukweli huu kwa furaha na kuungana na Mungu katika lengo lake kuu.

Njia mbili za kukumbana na undani wa Mungu ya Mungu

Kuna sababu mbili, nafikiri, inayotusababisha kukumbana na upendo wa Mungu kupitia utukufu wake na shauku yake ya kufanya watu kumsifu kwayo. Kwanza ni kuwa hatupendi wanadamu wanaojifanya kwa njia hiyo, na nyingine ni kuwa Biblia inaonekana kutufundisha kwamba mtu hafai kutafuta utukufu wake. Hivyo basi watu wanakashifu Mungu kujitukuza kwa sababu ya yale wanakumbana nayo kila siku na pia kwa sababu ya maandiko fulani.

Hatupendi watu wanaoonekana kama wamezingirwa na akili zao ama mitazamo yao. Hatupendi wasomi ambao wanajaribu kuonyesha maarifa yao maalum ama wanatunukulia maandishi yao na mafundisho yao. Hatupendi wafanyi biashara wanaondelea mbele kuzungumzia vile, kwa bidii wamewekeza pesa nyingi na jinsi walivyobaki juu katika soko ndivyo wapate kurudi chini na kuanguka kila mara. Na kama sisi hatuko pamoja na wao, tunawakemea wanawake na wanaume wanaovaa sio tu kulingana na sherehe na kirahisi na bila kuudhi, lakini wanajitahidi kuwa katika mtindo wa kisasa ndivyo waonekane ya kupendeza, wakarimu ama yale dunia wiki hii inasema kuwa inafaa ufanane nayo.

Kwa nini hatupendi hayo? Nafikiri ni kwa sababu watu wote hao si hakika. Wao ni wale Ayu Rand anawaita, “Watu mitumba.” Hawaishi kutokana na furaha inayotoka kwa kupokea waliyoyathamini kwa ajili yake. Bali, wanaishi kimitumba kwanzia sifa na maambatanisho kwa wengine. Na hatutamani watu gushi. Tunatamani watu wanaojiamini kwa kiasi kwamba hawana haja ya kuficha udhaifu wao na kufunika upungufu wao wa kweli kwa kujaribu kutafuta sifa nyingi iwezekanavyo.

Inabaki, kusema kuwa mafundisho yoyote yanayoonekana kuonyesha Mungu kama gushi ni ya kushukiwa kwa Mkristo. Kwa wengi, mafundisho kuwa Mungu anatafuta sifa na anataka kutamanika na anafanya vitu kwa ajili ya Jina Lake linaonekana kana kwamba linamweka katika kitendo hiki. Lakini linafaa liwe hivyo? Kitu kimoja ambacho tunaweza sema kwa hakika: Mungu si mdhaifu na Mungu hana upungufu: “Vitu vyote vyatoka ni kwake, na viko kwake na ajili yake.”(Warumi 11:36). Alikuweko, na vyote vilivyo, na kuweko kwa vyote ni kwaye na kwa hivyo hawawezi kuongeza chochote kwake kwa yale yasiyotiririka kutoka kwake. Hilo ndilo maana ya kuwa Mungu wa milele na si kiumbe. Basi, shauku ya Mungu ya kutafuta utukufu wake na kusifiwa na binadamu si kwa sababu anaficha udhaifu ama kulipisha kwa udhaifu mwingine. Anaweza kuonekana, kwa mtazamo wa kilimwengu, kuwa katika kitendo hiki cha watu mitumba, lakini Yeye si kama wao na usawa ya kilimwengu lazima uelezwe kwa njia nyingine. Lazima kuwe na nia zingine za kufamfanya kutafuta sifa kwa utukufu wake.

Kuna sababu tena katika matukio ya kutofanya tusipende wale wanaotafuta utukufu wao. Sababu sio tu eti wao ni watu bila uhakika, wanaojaribu kuficha udhaifu na upungufu, lakini pia kuwa hawana upendo. Wanajali sana mfano wao na sifa kwa kiasi cha kutojali yale yanayotukia kwa watu wengine. Mitazamo hii inatuelekeza kwa sababu ya Kibiblia, kwani ni maudhi kwa Mungu kutafuta utukufu wake. 1 Wakorintho 13:5 inasema, “Upendo hautafuti mambo yake.” Sasa hili, kwa hakika, linakaa kuleta hali ya mtafaruku, kwa kuwa, vile ninafikiri mafundisho yanafundisha kwa dhati. Mungu analifanya lengo lake la kipekee kutukuzwa na kusifiwa, hivyo basi anawezaje kuwa wa upendo?” Kwa kuwa “Upendo hautafuti mambo yake.” Kwa muda wa wiki tatu tumeona maandiko yanayotufundisha kuwa Mungu yu kwa ajili yake mwenyewe. “Kwa ajili Yangu mwenyewe, kwa ajili Yangu mwenyewe, nafanya hili, sitautoa utukufu wangu kwa mwingine.”(Isaya 48:11). Lakini kama Mungu ni Mungu wa upendo, lazima awe kwa ajili yetu. Hivyo basi, Mungu yu kwa ajili Yake mwenyewe ama Yu kwa ajili yetu?

Upendo wa Mungu usiokoma katika kutafuta sifa zake

Jibu ambalo nataka niwasihi kuwa ni ya kweli ni hili: Mungu ni wa ajabu kama mwenye utukufu nyingi juu ya viumbe vyote na amejitoshelesha, lazima awe kwa ajili Yake mwenyewe ndipo awe kwa ajili yetu. Kama angetoroka lengo la kujitukuza kwake, tungekuwa wapotevu. Lengo lake ni kuleta sifa kwake mwenyewe na lengo lake la kuleta utamu kwa watu wake ni lengo moja na linasimama na kuanguka pamoja. Nafikiri tutaona haya tunapojiuliza swali lifuatalo.

Kwa kutazama urembo ya kutamanika usiokoma na nguvu na hekima ya Mungu, je upendo wake kwa viumbe ungeugharimu nini? Ama uiweke hivi. Ni nini Mungu angetupatia tukifurahia kumwonyesha kama mwenye upendo kuliko vyote? Kuna jibu mmoja tu linalowezekana, haliko? YEYE MWENYEWE! Kama Mungu atatupa yaliyo vyema zaidi, ya kutoshelesha zaidi, ni kusema, kama angetupenda kwa upendo kamili,lazima atupe yasiyopungua Yeye mwenyewe kwa mipango yetu na kwa ushirika wetu.

Hakika hili ndilo lililokuwa lengo la Mungu kumtuma Mwanawe. Waefeso 2:18 inasema kwamba Kristo alikuja ili kupitia kwake “tunaweza kukaribia Baba katika Roho mmoja.” Na 1 Petro 3:18 inasema “Kwa kuwa Kristo naye aliteswa mara moja tu, mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili awalete ninyi kwa Mungu.” Mungu alipanga mipango yote ya ukombozi kwa upendo ya kuleta watu tena kwake, jinsi mzaburi anavyosema “Katika uwepo wako kuna furaha kamili, mkononi mwako wa kuume kuna furaha za milele.” (16:11) Mungu atufuata kutupa yalo vyema zaidi—sio majivuno, mali, ama hata uzima katika maisha hii, lakini ufunuo ya kutosha na kushiriki pamoja naye.

Lakini sasa tuko katika ufuo wa yale kwangu, yalikuwa uvumbuzi kubwa, na ninafikiria pia, ni suluhisho ya shida zetu. Ni kuwa, ili tuwe wa kupenda zaidi, lazima Mungu atupe yaliyo bora sana kwetu sisi na ya kutufurahisha zaidi; lazima atupe Yeye mwenyewe. Lakini, ni nini tunalofanya tunapopewa ama kuonyeshwa kitu kizuri sana, kitu ambacho tunakifurahia? Tunakisifu. Tunasifu watoto waliozaliwa,ambao hawajajikunja wakati wa kuzaliwa. “Lo,tazama,kichwa hicho mduara na cha kupendeza; nyele hizo zote; mikono yake,si, ni mikubwa!”

Tunausifu uso wa mpendwa tunapokosa kumwona kwa muda: “Macho yako ni kama wingu; nyele zako ni kama Hariri; Lo, wapendeza kwangu.” Tunasifu mianguko mikuu tukiwa chini kwa mikimbio mitatu. Tunasifu miti iliyoko kando ya njia ya St Croix wakati wa safari za dau wa msimu wa baridi.

Lakini uvumbuzi kuu nilioufanya, kwa usaidizi wa C.S. Lewis, sio tu kuwa tunalisifu kile tunakifurahia bali pia sifa ni kilele cha furaha yenyewe. Halipigwi msumari baadaye; ni mojawapo ya furaha. Sikiza njia ile Lewis anavyoueleza undani huu katika kitabu cha Zaburi:

Lakini neno la hakika sana kuhusu sifa—kwa Mungu ama kwa kitu chochote—kwa kushangaza ilinipita. Nilifikiria kulihusu kwa njia ya ziada, kubali; ama kupeana heshima. Sikuwahi kugundua kwamba furaha yote kwa pamoja yanatiririka zaidi kwa sifa ijapokuwa (Saa zingine hata kama) kuaibika ama hofu ya kutosisimua wengine yanaangaziwa kwa hila. Dunia imejawa na sifa —Wapendanao wakisifu wapendwa wao, wasomi wakisifu wahariri, watembezi wakisifu mashambani, wachezaji wakisifu michezo wanaoipenda—sifa kwa hali ya hewa, mvinyo, vyakula, waigizaji, farasi, vyuo, mataifa, watu wakuu wa historia, watoto, maua, milima, muhuri adimu, hata wakati mwingine wanasiasa na wasomi. Yangu yote, yaliyo vigumu, kuhusu sifa kwa Mungu, yaliegemea kwangu kujikana kwetu, kulingana na yaliyo ya thamana ya kiungu, yale tunafurahia kufanya, na yale ambayo lazima tuyafanye, kuhusu yale yote tunayoyathamini.

Nadhani tunafurahia kusifu yale yanayotusisimua kwa sababu sifa haielezi tu bali inakamilisha msisimuko; ni njia yake ya kuchomoza. Sio kwa utani, wapendwa wanaendelea kuambiana jinsi walivyo warembo, na furaha haikamiliki mpaka ionyeshwe (Mausia kuhusu Zaburi, pp 93-95)

Hapo ndipo kuna ufunguo: si kamili mpaka ionyeshwe kupitia sifa. Kama hatungeruhusiwa kuzungumzia yale tunayathamini na kusheherekea yale tunayapenda na kusifu yale tunayatamani, furaha yetu haingekamilika. Hivyo basi, kama kwa kweli Mungu yu kwa ajili yetu, kama angetupa yaliyo bora zaidi na kufanya furaha yetu yawe kamili, lazima alifanye lengo lake kupokea sifa zake kwaye. Sio kwa sababu kuwa anataka kuficha udhaifu wake fulani ama kuficha ukosefu wake, lakini kwa sababu anatupenda na anatafuta ukamilifu wa furaha yetu ambayo inapatikana tu kwa kumjua na kumsifu, lililo zuri zaidi juu ya viumbe vyote.

Mungu ndiye kiumbe kimoja ulimwenguni kote, ambaye kupitia kwa kutafuta sifa zake mwenyewe ni tendo la kupendeza. Kwake, kujitukuza ndilo jambo zuri zaidi. Anapotenda kila kitu “Kwa ajili ya sifa za utukufu wake” vile Waefeso 1 inasema, anatuhifadhi na anatupa kitu cha kipekee ulimwenguni kote ambacho kinaweza kutoshelesha tamaa zetu. Mungu yu upande wetu, na hivyo basi amekuwa, hivi sasa, na wakati wote atakuwa, kwa Yeye mwenyewe. Bwana asifiwe! Wsacha chochote kilicho na pumzi kimsifu Bwana.