Neno alifanyika mwili

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Incarnation
Topic Index
About this resource
English: The Word Was Made Flesh

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Incarnation

Translation by Desiring God


Yohana 1:1-18

Hapo mwanzo alikuwako Neno. Huyo neno alikuwa pamoja na Mungu, nay neno alikuwa na mungu. 2 Tangu mwanzo huyo neno alikuwa pamoja na Mungu. 3Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa. 4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu. 5 Nuru hung,aa gizani nalo giza halikulishinda. 6 Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu jina lake Yohana. 7 Alikuja kama shahidi apate kushuhudia hiyo nuru ili kupitia Yeye watu wote wapate kuamini. 8 Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru. 9 Kwamba nuru halisi imulikayo kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni. 10 Huyu Neno alikuwepo ulimwenguni na ingawa ulimwengu uliumbwa kwa Yeye haukumtambua. 11 Alikuja kwa walio wake, lamina woo hawakumpokea. 12 Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale walioamini jina lake . 13 Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu. 14 Neno alifanyika mwili akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15 Yohana alishuhudia habari Zake akapiga kelele akisema “Huyu ndiye niliyewaambia kwamba,’Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi,kwa kuwa alikuwako kabla yangu." 16 Kutokana na ukamilifu Wake,sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Mose,lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote,ila ni Mungu Mwana pekee,aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Katika mwisho wa msimu wa baridi wa 1974 nilikuwa katika hali ya kutamatisha masomo yangu kule Ujerumani. Mhadiri wangu mkuu alikuwa amefariki na wa kuchukuwa pahali pake, msomi mkuu wa Agano jipya aitwaye Oscar Cullmann alisafiri kutoka Basel hadi Munich kufundisha injili ya Yohana. Katika wiki kumi na tatu zilizotangulia hiyo muhula wa wiki kumi na nane, ninavyo kumbuka, tulipitia tu mistari kumi na minne katika kitabu cha Yohana. Hivyo ndivyo mistari hii vina rutuba.

Ujumbe wa Krismasi wa ukweli maalum kuhusu Kristo

Basi nimelichagua andiko hili kwa hofu na tetemeko ili kwamba sitalitendea haki kwa kulihubiri kwa fundisho mmoja. Nalichagua kwa sababu mbili. Kwanza ni kuwa ni neno kuu la Krismasi. Mstari mkuu unaoegemea Krismasi ni mstari wa 14. “Neno alifanyika mwili akakaa miongoni mwetu.” Hilo ndilo maana ya Krismasi. Mungu amekuja ulimwenguni, amezaliwa na bikira, kwa jina la Yesu Kristo ambao inatupasa tujue na kukumbatia.

Hili lina umuhimu leo kwa sababu, vile nilivyosema wiki uliopita katika makaribisho yangu, hata dini yasio ya Kristo ulimwenguni wanaongea siku hizi ni kana kwamba wanamcha na kutii na kwa kadri fulani, wanaamini Yesu. Unalisikia hili, siku hizi, kutoka kwa viongozi wa dini ya Kiislamu ambao wanataka tuone kwamba wanamthamini Yesu kutuliko kwa sababu hawafikirii kuwa Mungu angekubali ateseka na kuuawa kama mhalifu msalabani. Ni muhimu basi Wakristo wamjue Yesu vizuri, na kutofautisha Kristo wa Biblia na Kristo ambaye dini nyingine wanajifanya kumtii.

Basi yale ningependa kufanya na andiko hili kuu ya Yesu Kristo, lililoandikwa na Yule ambaye alimjua kwa undani kuliko mtu mwingine yeyote, kuhani yohana, ni kuonyesha na kuzungumzia na kufurahia juu ya ukweli tano kuhusu Neno kufanyika mwili, na baadaye kutofautisha mitazamo tofauti ambayo unaweza kumpatia asubuhi huu. Lengo langu ni kwamba upate kumtambua jinsi alivyo na kufanywa kumpokea kama Bwana wako na Mungu wako na mali yako uliyeithamini. Na kama umeshampokea, naomba upate kumkumbatia, na kumthamini na kufurahi ndani yake na kumfuata na kumwonyesha jinsi hujawahi fanya.

Wacha tuanze na ukweli tano kuhusu,”Neno-AlifanyikaMwili” katika mstari huu.

Mstari 17: ”Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa, lakini neema na kweli imekuja kupitia ”

“Yesu” ndilo jina Yusufu aliambiwa amwite mtoto na malaika wa Bwana kwa sababu maana yake ni “Mwokozi”. “Malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana yeye ndiye nitakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

“Kristo” ndilo jina alilopewa Mfalme wa Wayahudi ambaye atapeana ushindi kwa watu na uweza wa kifalme u begani mwake. Wakati Andrea, nduguye Petro, alipomwambia kuwa alikuwa amekutana na Yesu alisema (katika Yohana 1:41),”Tumemwona Masiya”[na Yohana anaendelea akisema (Yaani Kristo).

Sasa Yule tunaongea juu yake katika mistari hii anajulikana katika Biblia na ulimwenguni kote kama,”Yesu Kristo” na kila jina linabeba maana ya ajabu. Ni Mwokozi na Mfalme.

Katika mstari 1: “Hapo mwanzo, alikuwako Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.”

Kumekuwa na watu wa madhehebu ambao wamekana ajabu lililoko katika maneno haya mawili,”Neno alikuwa pamoja na Mungu,” na “Neno alikuwa Mungu,” wanasema, kwa kuunganika kimwili kibinadamu, huwezi ukawa nayo kwa njia yote. Labda alikuwa Mungu ama alikuwa pamoja na Mungu. Kama alikuwa pamoja na Mungu, basi hakuwa Mungu. Na kama alikuwa Mungu, basi hakuwa pamoja na Mungu. Kwa kuhepa ukweli ulioko katika maneno haya mawili, mara nyingine wanabadilisha tafsiri yake(vile Mashahidi wa Yehova wanavyofanya) ili isome kwamba, “Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa mungu.” Lakini kuna sababu ya kilugha mzuri na pia sababu ya kimaandishi katika sehemu zingine za Injili ya Yohana na vitabu vingine katika Biblia ya kufanya kanisa la Kristo kutokubali mafundisho haya kama kweli na ya kushikilia Wakristo.

Kile mstari wa kwanza kinatufundisha ni kuwa Yule tunamjua kama Yesu Kristo, kabla ya kufanywa mwili, alikuwa Mungu, na Baba pia alikuwa Mungu. Kuna watu wawili na Mungu mmoja. Hii ndio sehemu ya ukweli tunaoujua kama utatu. Ndiyo maana tunaabudu Yesu Kristo na kusema pamoja na Tomasi katika Yohana 20:28, “Bwana wangu na Mungu wangu.”

Yohana 1:1: “Hapo mwanzo alikuwako Neno, na Neno alikuwako pamoja na Mungu na Neno alikuwa Mungu.”

Kwa nini aliitwa “Neno?” njia mojawapo ya kulijibu ni kutafakari kuwa angeitwaje na vile jina hili halingeambatana na “Neno” kwa mfano angeitwa “Tendo.” , “Hapo mwanzo alikuwako Tendo, na Tendo alikuwako pamoja na Mungu na Tendo alikuwa Mungu.” Tofauti moja kati ya tendo na Neno ni kuwa tendo linaweza kutafsiriwa kwa njia nyingi tofauti. Tukidhani kuwa maneno yetu saa zingine hayaeleweki na yanaweza kunukuliwa kwa njia tofauti tofauti basi matendo hayaeleweki zaidi na yanaweza kunukuliwa kwa njia mbali mbali. Ndio maana kila mara tunajieleza kupitia maneno. Maneno yanatoa maana ya yale tunayoyatenda kwa uwazi kuliko matendo yenyewe.
Mungu alitenda mambo mengi makuu katika historia, lakini aliyatilia manani kwa Neno. Sababu mmoja, nafikiri, ni kuwa anathamini sana maelewano na mawasiliano.

Mfano mwingine ni kuwa Yohana angeliita “Fikira.” “Hapo mwanzo alikuwako Fikira, na Fikira alikuwako pamoja na Mungu na Fikira alikuwa Mungu.” Lakini tofauti mojawapo kati ya fikira na Neno ni kuwa Neno kwa kawaida huonekana kama ya kusogelea kwa nje kutoka kwa Yule ana fikira kwa ajili ya kuwasiliana. Nafikiri Yohana alitaka tujue kwamba Mwana wa Mungu alikuwa kwa ajili ya mawasiliano kati Yake na Baba, na kwa ajili ya kuonekana katika historia kama njia ya mawasiliano ya Mungu kwetu sisi.

Mfano wa tatu ni kuwa Yohana angemwita,”Hisia.” “Hapo mwanzo alikuwako Hisia, na Hisia alikuwako pamoja na Mungu na Hisia alikuwa Mungu.” Tena, ninasema, hisia haibebi maana ya kina , ama kusudio, ama lengo. Hisia, kama tendo, si wazi na inahitaji maelezo zaidi—na maneno. Basi inaonekana kwangu kwamba kumwita Yesu “Neno” ni njia ya Yohana kusisitiza kuwa kuweko kwa Mwana wa Mungu ni kwa ajili ya mawasiliano. Kwanza kabisa, anaishi,na alikuwa akiishi, kutoka milele yote kwa ajili ya mawasiliano na Baba. Tena, lakini cha muhimu zaidi kwetu sisi. Mtu aweza kusema, kwa kutamatisha, kumwita Yesu “Neno” inamaanisha Yeye ni “ Mungu anayejieleza.”

Yohana 1:3: “Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.”

Kuna sababu zaidi ya mbili Yohana anasema hili kulihusu Neno hapa. Kwanza inadhihisha kuwa Yeye ni Mungu. Tunapotafakari juu ya Mungu, tunafikiria kwanza juu ya Muumba. Mungu ndiye mwanzo na sababu ya yalivyo isipokuwa Yeye, Mungu.
Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.” Linamaanisha Yeye ni Mungu na hakuumbwa.

Sababu nyingine inapatikana katika mstari 10 “Huyu Neno alikuwepo ulimwenguni na ingawa ulimwengu ulimwengu uliumbwa kwa Yeye, haukumtambua.” Neno hapa linaonyesha kiwango cha upofu wa ulimwengu na kiwango kikuu cha maovu ya dunia ya kukataa Yesu. Anakuja kwetu kama muumba wetu, nab ado dunia haukumkubali.

Hadi sasa tumetambua nini kuhusu Neno alifanyika mwili?
1) Yeye ni Yesu Kristo, mwokozi na mfalme mteule 2) Yeye ni Mungu, mtu wa pili katika utatu 3) Yeye ndiye Neno—Mungu katika mawasiliano, Mungu anajieleza 4) Ni muumba wa vitu vyote.

Yohana 1:4: ”Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.”

Uzima yote yatoka katika Neno. Ni hakika kwa sababu vile tumeona Yeye ndiye muumba wa vyote. Lakini hapa tunaangazia maisha ya kiroho. Kwa muktadha mwingine kuna shida mbili kuu tunayokumbana nayo kama wanadamu; tumekufa kiroho na hivyo basi tumepofuka kiroho. Yohana asema hapa: Yesu ndiye suluhisho ya shida hizi zote: Anayo uzima tunayouhitaji.

Yohana 5:21 linasema, “ Mwana huwapa uzima wale anaopenda.” Kwa neno linguine, anatutendea kiroho yale alitendea Lazaro aliposimama mbele ya kaburi ya Lazaro na akamwambia Lazaro mfu, “Lazaro, njoo huku!”(Yohana 11:43).

Na ni jinsi gani uzima huo, uliopewa na Yesu, ina uhusiano na nuru? Kwa njia mbili. Kwanza, inatuwezesha kuona. Wafu wakipewa uzima, wao huona. Ama kubadilisha picha, unapozaliwa, wewe huona. Vile ilivyo kiroho. Yesu akamwambia Nikodemo, “Amin,amin nakuambia, mtu hawezi kuuona ufalme wa Mungu, asipozaliwa mara ya pili” Yohana 3:3. Basi, kwanza Yesu anapeana uzima halafu uzima unakuwa nuru—uwezo wa kuona ukweli wa kiroho.

Njia nyingine ya vile uzima Yesu anaupeana unahusiana na nuru sio tukuwa inakuwezesha tu , kuona ,bali Yesu mwenyewe ndiye nuru anayeonekana. Ni nini,tumepofuka kwayo, tukiwa wasioamini? Tumepofuka kwa ukweli na uzuri na thamana—utukufu—wa Yesu. Yohana anaposema, “ Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu,” Hakika anamaanisha Yesu Kristo, Neno alifanyika mwili, ni nguvu ya kuona angavu ya kiroho na angavu kuonekana.

Ndiyo sababu mstari 14 unasema, “ Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukaona utukufu wake.” Hilo ndilo Yesu aliloliombea katika Yohana 17:24, “ Baba shauku yangu ni kwmba, wale ulionipa wawe pamoja name pale nilipo,ili waweze kuuona utukufu wangu.” Na hayo ndiyo aliyoyadai wakati wakati alisema kwa mara mbili, “Mimi ndimi nuru ya dunia” (Yohana 8:12, 9:5). Basi Neno alifanyika mwili ana uzima kwaye, na huo uzima ukafanyika nuru ya watu. Yeye ndiye nguvu ya kuona na angavu ya kuonekana.

Kujumulisha pamoja, ukweli tano kuhusu Neno alifanyika mwili ambayo tumeuona?

  1. Yeye ni Yesu Kristo baada yakufanyika mwili: mwokozi na mfalme aliyeteuliwa na Mungu kwa wote.
  2. Yeye ni Mungu: alikuwako pamoja na Mungu, naye ni Mungu.
  3. Aliitwa Neno: Mungu katika mawasiliano, Mungu akijieleza.
  4. Yeye ni Muumba: “Vitu vyoteviliumbwakwa Yeye, na Yeye hakuumbwa.
  5. Yeye ni uzima na nuru: nguvu ya kuona na angavu ya kutosha ya kuonekana.

Mwishoni, ni jibu gani basi unaweza kupeana kuhusu ufunuo huu wa Yesu Kristo, Neno-Alifanyika-Mwili?

Jibu la kwanza: simjui na sitampokea

Mojawapo limeelezwa katika mstari wa 10-11, “Huyu Neno alikuwepo ulimwenguni na ingawa uliumbwa kwa Yeye, haukumtambua. 11 Alikuja kwa wale walio wake, lakini hawakumpokea. Unaweza kusikia hayanakusema, “Simjui na sijampokea.” Hilo ni jambo la kutisha la kusema kuhusu muumba wako na uzima wako na nuru yako. Nawasihi, msiseme hayo kwa urahisi krismasi huu.

Jibu linguine: Namjua na ninampokea

Jibu linguine linapatikana katika mstari 12-13, “Bali wotewaliompokea, aliwapa uwezo wa kuwa wana wa Mungu, ndio wale waliaminio jina Lake. 13Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu.” Hili ndilo jibu ambalo ninaliombea asubuhi huu. Pokea neno hili kuu Neno likafanyika mwili. Mpokee kama Mwokozi na mfalme na Mungu na Neno na Muumba na Uzima na Nuru. Na yale Mungu alivyo kwako kupitia kwake!

Krismasi ni kama vile Mungu kutuma Mwana wake ulimwenguni kupata kina Bin Ladens wa dunia, wanaojificha katika mapango ya giza na mauti. Badala ya kurusha miale ya moto pangoni, kwanza anasimama malangoni mwa pango na kusema,”Njoo kwa nuru kwa sababu nimefilia wenye dhambi; ukinipokea kama Mungu wako na wako wa akiba na thamana yako, kifo change kinahesabika kama kifochako, na haki yangu kinahesabika kama yako, na utakuwa na uzima milele.