Ni nini kinachotendeka katika kuzaliwa upya? sehemu ya 2

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Conversion
Topic Index
About this resource
English: What Happens in the New Birth? Part 2

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Conversion
Part of the series You Must Be Born Again

Translation by Desiring God


Basi palipokuwa na mtu mmoja wa mafarisayo jina lake Nikodemo mkuu wa wayahudi. Huyo alimjia usiku akamwambia,”Rabi,twajua kuwa u mwalimu umetoka kwa Mungu ,kwa maana hakuna awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyayo wewe usipokuwa Mungu yu pamoja naye.” Yesu akajibu akamwambia, “Amin amin nakuambia,mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuona ufalme wa Mungu.” Nikodemo akamwambia, "Awezaje mtu kuzaliwa akiwa mzee? Awezo kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?” Yesu akajibu, “Amin Amin nakuambia,mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho. Usistaajabu kwa kuwa nilikwambia, “Hamna budi kuzaliwa mara ya pili.” “Upepo huvuma upendako na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka walaunakokwenda: kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho” Nikodemo akajibu, akamwambia , ”Yawezaje kuwa mambo haya?” Yesu akajibu akamwambia, “Je wewe u mwalimu wa Israeli na mambo haya huyafahamu?”

Leo tunamaliza ujumbe wa wiki iliyopita kuhusu kinachofanyika katika kuzaliwa upya.Yesu alimwambia Nikodemo katika Yohana3:7, “Usistaajabu kuwa nilikuambia, “hauna budi kuzaliwa mara ya pili,” Vilevile kwenye mstari wa 3,Alimwambia—nasi pia—kwamba uzima wetu wa milele hutegemea kuzaliwa mara ya pili: Amin amin nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili hawezi kuuona ufalme wa Mungu.Basi hatuhusiki kwa jambo ambalo ni la kufikiria wala si ya lazima wala si la kurembesha katika maisha ya Ukristo. Kuzaliwa upya si kama mapambo ambayo wahifadhi maiti hutumia kwa maiti ili aonekane kana kwamba yu hai. Kuzaliwa mara ya pili ni uumbaji wa uzima wa kiroho si uigizaji wa maisha.

Tulianza kwa kujibu swali: Nini hufanyika katika kuzaliwa upya ?Wakati uliopita kwa maelezo mawili 1) Kuzaliwa upya si kupata dini mpya bali uzima mpya 2) Kuzaliwa upya si kuthibitisha tu uungu ndani ya Yesu bali ni kushuhudia uungu ndani yako.

Yaliyomo

Uzima mpya kupitia Roho mtakatifu

Nikodemo alikuwa mfarisayo na alikuwa mengi kuhusu dini. Lakini hakuwa na uzima wa kiroho. Aliona kazi ya kiuungu ya Mungu ndani ya Yesu lakini hakushuhudia haya ndani yake.Tukiweka maelezo yetu pamoja tangia muda uliopita,kile Nikodemo alikihitaji, Yesu akamwambia ; ni uzima mpya wa kiroho ambao hupatiwa kwa njia ya kiungu kupitia Roho mtakatifu. Kinachofanya uzima mpya kuwa wa kiroho na wa kiungu ni kuwa ni kazi ya Mungu Roho. Ni kitu ambacho ni zaidi ya maisha ya Asili ya mwili wa moyo wetu na ubongo.

Mstari wa 6, Yesu anasema : Kilichozaliwa kwa mwilini mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho.”Mwili una uzima wa aina yake. Kila mwanadamu ni mwili wenye uzima. Lakini si kila binadamu ana Roho yenye uhai. Kuwa na Roho yenye uzima au kuwa na uzima wa kiroho, Yesu anasema, lazima “Tuzaliwe katika Roho.” Mwili huzalisha uzima wa aina moja. Roho naye huzalisha aiina nyingine ya uzima. Bila kuwa na uzima wa pili (wa Roho) hatuwezi kuuona ufalme wa Mungu.

Kwa Roho ndani ya Yesu

Basi tulivyotamatisha wakati uliopita,tuligundua mambo mawili muhimu:Uhusiano kati ya kuzaliwa upya kwa Yesu na kuzaliwa upya kwa imani. Yesu alisema, “Mimi ndimi njia ukweli na uzima.” (Yohana 14:6). Mitume Yohana alisema, “Mungu hutupa uzima wa milele na uzima huu umo katika mwanawe. Yeye alliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima (1 Yohana 5:11-12) Sasa kwa upande mwingine, uzima mpya tunaohitaji. “umo ndani ya Mwana”—Yesu ndiye uzima huo. ukiwa naye una uzima mpya wa kiroho na wa milele. Kwa upande mwingine katika Yohana 6:63 Yesu anasema “Roho ndiye aitiaye uzima.” na mtu asipozaliwa kwa Roho hawezi kuingia kwenye ufalme wa Mungu” Yohana 3:5

Basi tuna uzima kwa kuunganishwa na Mwana wa Mungu ambaye ni uzima wetu na tuna uzima huo kwa kazi ya Roho. Tulimalizia basi kwamba kazi ya Roho kwa huisho ni kutia uzima mpya kwetu kwa kutuunganisha na kristo. John Calvin anaifafanua hivi, “Roho mtakatifu ndiye kiunganishi ambacho kristo hutuunganisha nayo kwake kikamilifu? (Chuo cha III, 1, 1)

Kuunganishwa na Yesu kupitia Imani

Tulifanya unganisho na Imani hivi: Yohana 20: 31 inasema “Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo Mwana wa Mungu na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.” Na 1 Yohana 5:4 inasema “Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu, hiyo Imani yetu.” Kilichozaliwa na Mungu. Ufunguo wa ushindi.Imani ufunguo wa ushindi. Kwa kuwa Imani ndiyo njia tunayoshuhudia kuzaliwa na Mungu. Basi tuliweka kwa ufupi kwa pamoja ujumbe wa wiki uliopita hivi: Katika kuzaliwa upya Roho mtakatifu kwa njia ya kiungu hutupa uzima mpya wa kiroho kwa kutuunganisha sisi na Yesu Kristo kwa njia ya Imani.

Kuzaliwa upya: Kiumbe kipya si kuimarisha ya kale

Hii inatuleta kwenye njia ya tatu ya kueleza kinachofanyika katika kuzaliwa upya.kinachotendeka katika kuzaliwa upya si kuimarishwa umbile wako wa kale bali uumbaji wa asili mpya—asili ambayo hakika ni wewe aliyesamehewa na kutakaswa na asili ambayo ni hakika mpya, na inafanywa kukaa ndani yenu kupitia Roho ya Mungu.

Nitakuelekeza kwa andiko fupi ambalo lilinifanya niufikie mtazamo huu. Katika Yohana 3:5, Yesu anamwambia Nikodemo, “Amin Amin nakwambia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia ufalme wa Mungu.Kwa kutaja maneno haya Yesu anamaanisha nini? “Kwa maji na kwa Roho” Madhehebu mengine yanaamini kuwa hii ni asilia ya ubatizo wa maji kama vile Roho hutuunganisha na Kristo. Kwa mfano matandao mmoja unaueleza hivi.

Ubatizo takatifu ni msingi wa uzima kikamilifu wa Mkristo, lango la kuingia uzimani katika Roho na mlango unaotupa uwezekano wa kufikia sakramenti zingine.Kupitia ubatizo tuko huru kutoka kwa dhambi zetu na kuzaliwa upya kama wana wa Mungu; tunakuwa washirika na Kristo, tumejumuishwa kwenye kanisa na kufanywa washirika katika huduma yake: “Ubatizo ni sakramenti ya huisho kupitia maji katika neno.”

Milioni ya watu wamefunzwo kuwa kubatizwa kwao kuliwafanya kuzaliwa mara ya pili.Kama hii si kweli, basi ni balaa kubwa ulimwenguni. Na mimi siyaamini kuwa ni kweli. Sasa basi Kristo anamaanisha nini?

Kwa nini “Maji” si asilia ya ubatizo katika Yohana 3

Hapa pana sababu kadhaa kwa kufikiria kuwa maji kama ni asilia ya ubatizo ya Wakristo si kweli. Hatimaye tutaona yaliyomo yanatuelekeza wapi.

1) Hakuna mtajo wa ubatizo katika Sehemu iliyobaki ya Sura hii

Kwanza kama hii ingekuwa asilia kuwa ubatizo wa ukristo na kuwa muhimu kwa kuzaliwa upya,(kama wengine wanavyosema),inaonekana geni kuwa imeachwa nje ya kile Yesu anasema katika sura hii,anapotuambia njia ya kupata uzima wa milele. Mistari wa 15: ”Kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika yeye.” Mstari wa 16: kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele. Mstari wa 18: “Amwaminiye yeye haukumiwi? Itaonekana ya kushangaza, kama ubatizo ungekuwa muhimu, haingetajwa pamoja na imani.

2) Ubatizo haitoshi kufananishwa na upepo

Pili, ufananisho na upepo kwenye mstari wa 8 ungeshangaza kama kuzaliwa mara ya pili kungeunganishwa imara na ubatizo wa maji. Yesu anasema, “upepo huvuma upendako, na na sauti yake waisikia,lakini hujui unakotako wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa Roho.Kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa kwa Roho. Hii ni kuonekana kusema kuwa Mungu yuko huru kama upepo kufanya huisho. Lakini kama itafanyika kila wakati mtoto akuapo haitaonekana kuwa kweli. Kwa sababu hii upepo ungezuiliwa katika sakramenti.

3) Ubatizo haitoshi kwenye maneno ya kukaripia ya Yesu kwa Nikodemo

Tatu, kama Yesu anamaanisha ubatizo wa ukristo, ingeonekana ajabu kwamba angemwambia Nikodemo Mfarisayo, kwenye mstari wa 10, “Je, wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?” Hiyo ina maana Yesu anapotaja kitu kilichofundishwa katika agano la kale,lakini kama ana maanisha ubatizo hiyo ingekuwa baadaye na kupata maana kutoka kwa uzima na mauti ya Yesu,haionekani kana kwamba angekaripia Nikodemo kuwa ni mwalimu wa Israeli na hajui asemacho.

4) Maji na Roho zimeunganishwa katika ahadi za agano jipya

Hatimaye maelezo hayo kwenye mstari wa 10 yaturejesha kwenye agano la kale kwa chimbuko, tunapata kuwa maji na Roho zina uhusiano wa karibu katika ahadi za agano jipya,hasa Ezekiel 36. Basi wacha tutazame hapo pamoja.Yaliomo hapa ndiyo msingi wa sehemu ya ujumbe uliosalia.

Maji na Roho katika Ezekiel 36

Ezekieli anasisitiza kile Mungu atafanyia watu wake anapowarejesha kutoka kwa nchi geni ya Babiloni.Matokeo hapa ni makubwa zaidi siyo tu kwa wana wa Israeli; kwa kuwa Yesu anadai kulinda agano jipya katika damu yake kwa wote wamtumainio (Luka 22:30) na hili ni andiko ambalo ni la ahadi za agano jipya kama katika Yeremia 31:31. Tusome pamoja Ezekieli 36:24-28:

Maana nitawatwaa kati ya mataifa nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.nami nitawanyunyuzia maji safi,nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenyu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya,nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.

Ninafikiria kuwa ufahamu huu ndiyo uliofanya Yesu kuongea maneno haya: “Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Anamwambia nani.” Nitawanyunyuzia maji safi nami nitakuwa Mungu wenu.” (Mist 28)? Mstari wa 25: Kwa wale ambao anawaambia,“ Nami nitawanyunyuzia maji safi, nanyi mtakuwa safi nitawatakaseni na uchafu wenu wote.” Na mstari wa 26. Kwa wale ambao nawaambia,” Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia Roho mpya, ndani yenu.” Kwa maneno mengine anasema, wale watakao ingia katika ufalme ni walio na upya wenye utakaso na usafi wa ya kale ni uumbaji wa upya.

Ninamaliza nikisema ”Maji na Roho” zinamaanisha hali aina mbili katika upya wetu tukizaliwa mara ya pili.Na sababu zote mbili ni muhimu ni hii: Tunaposema Roho mpya,moyo mpya tumepewa hatumaanishi kwamba tukome kuwa wanadamu—wanaoajibika kimaadili—ambayo tumekuwa siku zote. Mimi John Piper nilikuwa binadamu kibinafsi kabla nizaliwe mara ya pili na mimi bado ni binadamu kibinafsi baada ya kuzaliwa mara ya pili.Kuna kuendelea. Hii ndiyo sababu lazima kuwe na utakaso. Kama mtu wa kale John Piper, angeangamizwa, mawazo ya msamaha kwa jumla na utakaso hayangekuwa na maana. Hakungebakia chochote kwa ya kale kumsamehe na kumtakasa.

Tunajua bibilia inavyosema kwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja na Kristo (Warumi 6:6) na kwamba tumekufa pamoja na Kristo (Wakolosai 3:3) “tuchukulie kuwa tumekufa” (Warumi 6:11) na “tuvue utu wa kale” (Waefeso 4:22). Lakini haya yote haimaanishi kuwa Binadamu huyo hayuko tena kwenye uzima tunaouona.Ina maana kwamba kulikuwa na utu wa kale na tabia zake, utawala wake na uharibifu ambao wahitaji kuondolewa.

Sasa njia ya kufikiria kuhusu mioyo yenu mpya,roho mpya,asili mpya ni kwamba bado ni nyinyi tu na mwahitaji msamaha na utakaso—hii ndiyo sababu ya kutaja maji. Maovu yangu ni lazima yaoshwe mbali. Utakaso kwa njia ya maji ni taswira hii.Yeremia 33:8 inaeleza hivi: Nami nitawasafisha na uovu wao wote ,ambao kwa hou waminitenda dhambi:nami nitawasamehe maovu yao yote ambayo kwa hayo wamenitendea dhambi na kukosa juu yangu.” Sasa utu wetuambao unaendelea kuishi—ni sharti usamehewe na uovu wake usafishwe mbali.

Hitaji ya kuwa upya

Lakini msamaha na kusafishwa hayatoshi. Ninahitajika kuwa mpya. Kubadilishwa. Na kuwa na uzima. Nahitaji mtazamo mpya ya kuona,kufikiria na kuthamini.Ndiposa Ezekieli anena kuhusu moyo mpya na Roho mpya katika mstari wa 26 na 27: “Nami nitawapa ninyi moyo mpya,nami nitatia roho mpya,ndani yenu nami nitatia roho mpya,ndani yenu name nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili yenu name nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.”

Hivi ndivyo ninavyoelewa mistari hii: Kuwa na uhakika moyo wa jiwe una maana ya moyo uliokufa usioweza kuhisi na kuitikia ukweli wa roho—moyo mliokuwa nao kabla ya kuzaliwa upya ungehisi: ungeitika kwa mapenzi na tamaa ya vitu vingi. Lakini ni jiwe kuhusu ukweli wa kiroho na uzuri wa Kristo, Utukufu wa Mungu na njia ya utakatifu. Hii ndiyo sharti ibadilike iwapo tutaona ufalme wa Mungu. Basi katika kuzaliwa upya Mungu huondoa moyo wa jiwe na kutia moyo wa nyama. Hapa neno nyama halimaanishi “tu binadamu” kama katika Yohana 3:6. Inamaanisha mwororo, unaoishi, kuitikia, na kuhisi, badala ya jiwe bila uhai.Katika kuzaliwa upya kufa kwetu na kuchoka na Kristo hubadilishwa na moyo unaoohisi (hisia za kiroho) umuhimu wa Yesu.

Ezekieli anasema katika mstari 26 na 27, “Roho mpya nitatia ndani yenu . . . na kuwaendesha katika sheria zangu,” nafikiria kuwa anamaanisha ya kwamba katika kuzaliwa upya, Mungu hutia kwenye mioyo yetu uzima wa kiungu na wa kiroho—na huyo Roho mpya ni kazi ya Roho mtakatifu mwenye atiaye umbo na sura katika mioyo yetu mipya.

Taswira ninayo kwenye mawazo ni kuwa moyo mpya huu changamfu, wa kuguzwa,na wa kuitika ni kama tuta laini la udongo na Roho mtakatifu anapenya ndani yake na kumpa sura na maadili ya kiroho kulingana na umbo lake mwenyewe. Kwa kuwa yeye binafsi ndani yetu,mioyo na akili zetu zachukua tabia zake—Roho yake. (Waefeso 4:23).

Mpokee kama hazina yako

Hebu sasa tuweze kuhitimisha wiki hizi mbili. Ni nini kinachotendeka katika kuzaliwa upya? Roho mtakatifu kwa njia ya kiungu hutupa uzima mpya wa kiroho, kwa kutuunganisha na Yesu Kristo kwa njia ya imani. Kwa njia nyingine, Roho hutujumulisha na Kristo mahali pana utakaso wa dhambi zetu na kubadilisha ugumu na kutoitika kwa moyo mwororo ambao unamthamini Yesu kuliko vitu vyote na kubadilishwa kwa uwepo wa Roho kuwa aina ya moyo wa unaopenda kutenda mapenzi ya Mungu. (Ezekieli 36:27).

Kwa kuwa unaweza kuyashuhudia yote haya kwa imani,nakualika sasa katika Jina la Yesu na nguvu za Roho yake, umpokee kama anayesamehe na anayebadilisha hazina ya uzima wako.