Tafuta Furaha

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Evangelism
Topic Index
About this resource
English: Quest for Joy

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Evangelism

Translation by Go Fishnet Ministries

Review You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).


Ukweli sita za Kibibilia

Je unajua Mungu anatuamurisha kufurahi?

“Nawe utajifurahisha kwa Bwana naye atakupa haja za moyo wako” {Zaburi 37:4}

1) Mungu Alituumba Kwa Utukufu Wake

“Waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka mwisho wa dunia,…… niliyemuumba kwa ajili utukufu wangu” { Isaya 43: 6-7 }.

Mungu alituumba ili tuadhimishe ukuu wake – vile darubini huadhimisha ukuu wa nyota. Atuumba kuweka uzuri wake, ukweli, urembo, hekima na haki kwa tamasha. Tamasha kuu la utukufu wa Mungu huja kwa kupendezwa kindani kwa vyote vile alivyo. Hii ina maana ya kuwa Mungu hupata sifa nasi twapata furaha. Mungu alituumba ili atukuzwe kwa ukuu ndani yetu wakati tunapotoshelezwa ndani yake.

2) Kila Mwanadamu Na Aishi Kwa Utukufu Wa Mungu

“basi mlapo au mnywapo, au mtendapo neno lolote , fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu," {1 Wakorintho 10:31}

Ikiwa Mungu alituumba kwa utukufu wake, basi ni dhahiri kwamba ni sharti tuishi kwa utukufu wake. Wajibu wetu unatoka kwa uvumbuzi wake. Hivyo sharti la kwanza ni kuonyesha thamana ya Mungu kwa kutosheka na yote aliyonayo kwetu. Hii ndiyo kiini cha kumpenda Mungu (Mathayo 22:37) na kumwamini (1 Yohana 5:3-4) na kumshukuru (Zaburi 100:2-4) huu ndio mwanzo wa utiifu wa kweli, hasa kuwapenda wengine (Wakolosai 1:4-5)

3) Sote Tumepungukiwa Kumtukuza Mungu Inavyotupasa

“Kwa sababu wote wamefanyya dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (Warumi 3:23)

Ni nini maana ya kupungukiwa na utukufu wa Mungu?
Ina maanisha kuwa sote hatujamwamini na kumthamini Mungu vile itupasavyo. Hatujatosheka na ukuu wake na kutembea kwa njia zake. Tumetafuta kutoshelezwa kwa vitu vingine na kuvifanya vya thamani kumliko Mungu. Na hiki ndiko kiini cha kuabudu miungu (Warumi 1:21-23). Tangu dhambi zije ulimwenguni sote tumekuwa tukipinga kwa dhati Mungu kuwa mtoshelezaji wa thamanaa zetu zote (Waefeso 2:3). Hili ni chukizo la kutisha kwa ukuu wa mungu (Yeremia 2:12-13)

4) Sote Tuko Chini Ya Lawama Za Haki Za Mungu

“Mshahara wa dhambi ni mauti …." (Warumi 6:23)

Sote tumerahihisha utukufu wa Mungu. Namna gani? Kwa kutanguliza vitu vingine juu yake. Kwa kukosa shukrani, uaminifu na kutotii. Hivyo Mungu yuko katika hali ya kutufungia nje ili tusifurahie utukufu wa milele “Watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake” (2 Wathesalonike 1:9)

Neno “Kuzimu” limetumika mara kumi na mbili kwa agano jipya – Mara kumi na moja na Yesu mwenyewe. Siyo hadithi zilizoundwa na wahubiri waliokufa moyo na wenye hasira. Ni onyo nzito kutoka kwa mwana wa Mungu aliyekufa ili akomboe wenye dhambi kutokana na laana zake. Ni hatari kwetu kukosa kujali.

Kama biblia ingalikomea hapa kwa utafiti wa hali ya binadamu, hatungekuwa na matumaini na maisha ya mbeleni, hata hivyo, biblia halikomi hapa.

5) Mungu Alimtuma Mwanawe Wa Pekee Yesu Ili Atupe Uzima Wa Milele Na Furaha.

"Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi” (1 Timotheo 1:15)

Habari njema ni kuwa Kristo alikufia wenye dhambi kama sisi. Na akafufuka kimwili kutoka kwa wafu ili adhibitishe nguvu za ukom bozi kwa kifo chake na kufungua milango ya uzima wa milele na furaha (1 Wakorintho 15:20). Hii ina maana ya kuwa Mungu anaweza kuachilia huru wenye dhambi na bado awe mwenye haki (Warumi 3:25-26) “Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu “ (1 Petro 3:18). Kutoshelezwa kwa kamili na wa milele kunapatikana kwa kumrudia Mungu.

6) Manufaa Yaliyopatikana Kwa Kufa Kwa Kristo Ni Ya Wale Waliotubu Na Kumwamini.

“Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifuatwe." (Matendo 3:19) “Bwana Yesu na utaokoka” (Matendo 16:31)

“Toba” yamaanisha kuacha ahadi zote za uongo za dhambi. “Imani” yamaanisha kutosheka na yeyote ambayo Mungu anaahidi kuwa ndani ya Yesu, “yeye aniaminiye” Yesu asema “hataona kiu kamwe” (Yohana 6:35). Hatufanyi kazi ili tupate wokovu wetu wala haki juu yake. (Warumi 4:4-5).

Ni kwa neema kupitia Imani (Waefeso 2:8-9). Ni karama ya bure (Warumi 3:24) tutakuwa nayo iwapo tutathamini juu ya mabo yote (Mathayo 13:44). Tunapofanya hivyo, lengo la mungu la kuumba limekamilika. Anatukuzwa ndani yetu nasi tunatosheka ndani yake milele.

Je, Hili Lina Maana Yoyote Kwako?

Je, unalo tamani la furaha ambalo huja na kutosheka na yote Mungu aliyonayo kwa ajili yako ndani ya Yesu? Kama ndiyo, basi Mungu anafanya kazi ndani ya maisha yako.

Unapaswa Kufanya Nini?

Toka kwa ahadi za uongo za dhambi. Mwite Yesu akukomboe kwa adhabu na minyororo ya dhambi. “Wote watakaoliita jina la Bwana wataokoka” (Warumi 10:13) tumainia yote ambayo Mungu aliyonayo kwa ajili yako ndani ya Yesu. Vunja nguvu za ahadi za dhambi kwa imani na kutoshelezwa na ahadi za Mungu. Anza kusoma biblia ili utambue ahadi kuu za Mungu za kipekee, ambazo zinaweza kukuweka huru (2 Petro 1: 3-4). Tafuta Kanisa linaloamini biblia na uanze kuabudu na kukuwa pamoja na wale wanaothamini Mungu juu ya mambo yote (Wafilipo 3:7).

Habari iliyo njema ni kwamba hakuna mvutano kati ya furaha zetu (binadamu) na utakatifu wa Mungu. Kutosheka na yote Mungu aliyonayo kwetu ndani ya Yesu inamdhihirisha kama hazina kuu.

“Utanijulisha njia ya uzima, mbele za uso wako ziko furaha tele, na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele" (Zaburi 16:11)