Tumeona utukufu wake, amejaa neema na kweli

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Jesus Christ
Topic Index
About this resource
English: We Beheld His Glory, Full of Grace and Truth

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Jesus Christ
Part of the series The Gospel of John

Translation by Desiring God

Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. 15 (Yohana alishuhudia habari Zake, akapiga kelele akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwako kabla yangu.’ ") 16 Kutokana na ukamilifu Wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema. 17 Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo. 18 Hakuna mtu ye yote aliyemwona Mungu wakati wo wote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba ndiye ambaye amemdhihirisha.

Na tuanzie mstari 14: ili tuone mambo makuu  katika aya hii. “Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.” Rejelea mstari wa 1 ili ukumbuke huyu neno ni nani. “Hapo, mwanzo alikuwako, naye neno alikuweko kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu.” Yohana 1:1. Hivyo Neno lina maana ya Mungu  Mwana.

Ninatumia neno Mwana kwa sababu limedokezwa katika mstari wa 14 Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba.” Hivyo Neno ni Mwana wa Mungu.

Yaliyomo

Mungu mmoja, watu watatu

Waislamu hujikwaza juu ya hili neno Mwana, kama vile wengine wafanyao. Baadhi yao hufikiria kuwa Mungu alifanya mapenzi na Mariamu na kumzaa Mwana. Hii si kile Biblia inachomaanisha Yohana 1:1: “Hapo mwanzo alikuwako Neno.” Huyo ni Mwana wa Mungu. Na hakuwa na mwanzo wake. Alikuweko tangu mwanzo. Alikuweko umbali wa mwanzo uwezavyo kwenda—milele. Mstari wa 3 unasema, “Vitu vyote viliumbwa kwa Yeye, wala pasipo Yeye hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa.” Hii ina maana kuwa yeye hakuumbwa. Yeye si sehemu ya kiumbe kwa vyovyote vile. Na haya ndiyo tunayojua kuhusu Mwana wa Mungu. 1) Yeye ni Mungu, 2) Baba yake pia ni Mungu 3) Mwana si Baba, alikuweko na Baba 4) Yeye hakuumbwa na ni wa Milele.

Kuna mengi ya kusema kuhusu fundisho la utatu—Mafundisho ya kwamba Mungu yuko kama Mungu mmoja katika watu watatu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Lakini kwa sasa, hifadhi mengi haya kwenye mawazo na moyo wako. Mwana na Baba ni Mungu mmoja, lakini ni watu wawili. Wana maumbile ya kiungu mmoja. Wao ni Mungu mmoja wenye hisia mbili.

Mungu alifanyika binadamu—bila kukoma kuwa Mungu

Sasa kile mstari wa 14 inasema—na hii ndio tukio ambao ni muhimu zaidi katika historia —kwamba Neno, Mwana, alifanyika binadamu bila kukoma kuwa Mungu. Ujumbe huu ndio tutaangalia zaidi kwa muda wa wiki mbili: Tunajuaje kuwa huu ndio uhakika, na je hii ina maana gani kwetu binafsi?

“Neno alifanyika mwili” yaani, Neno la Kiungu, Mwana wa Kiungu wa Mungu, alifanyika binadamu bila kukoma kuwa Mungu. Je, twafahamu vipi mambo haya? Na je ina maana gani kwetu sisi? Tutauchukua muda wetu wote leo kwa kujibu haya kutoka mstari wa 14.

Neno Alikaa miongoni mwetu

Sababu ya kwanza tunasema kuwa neno la kiungu halikukoma kuwa na uungu wakati alipofanyika binadamu ni tamko ilioko katika mstari wa 14. ya kwamba Neno “alikaa miongoni mwetu.” Mada la kitenzi alikaa ni Neno. Na neno ni Mungu. Hivyo njia ya kawaida ya kuchukua hii ni kwamba Mungu, ambaye ni Neno, alikaa miongoni mwetu. Hii ndiyo sababu malaika alisema katika Mathayo 1:23. “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina lake Imanueli’’ (maana yake, Mungu pamoja nasi). Neno ambaye ni Mwana, hakuacha kuwa Mungu alipofanyika binadamu.

Utukufu kama mwana wa pekee wa Mungu

Sababu yetu ya pili, ya kuamini hii ni tamko ifuatayo katika mstari 14, “Nasi tukaona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba. Utukufu wa nani? Utukufu wa Neno—Neno ambaye ni Mungu. Na je, hii ni utukufu wa aina gani? Ni “Utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba.”

Yohana anaposema utukufu wa neo kuwa mwili ni “utukufu kama tu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba,” je, neno kama lina maana kuwa ni utukufu wa kuigizwa? Si utukufu hakika wa Mwana bali kama utukufu wa Mwana? Sidhani ni hivyo. Nikisema, kwa mfano, “Nina kitabu cha kupeana na ningependa nikupe wewe kama chaguo langu la kwanza,” na ukose kuitika, “mimi si chaguo lako la kwanza; Mimi ni kama tu chaguo lako la kwanza.” La sivyo neno kama halimaanishi hivyo nikisema, “Ninakupa wewe kama chaguo langu la kwanza.” Ina maanisha kuwa: ninakupa kwa kuwa hakika wewe ni chaguo langu la kwanza. Yohana anaposema, “Tumeona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana wa pekee atokaye kwa Baba,” anamaanisha, “Tumeona utukufu wake, utukufu vile ilivyo kwa hakika—utukufu wa Mwana wa Mungu.”

Tunajua haya kwa sababu, katika sehe—mu ya kwanza wa mstari 14, Yohana alisema kwa utaratibu kwamba , “tumeona utukufu wake”—hakuna hitimu! Utukufu wa nani? Utukufu wa Neno wa milele, ambaye ni Mwana. “Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake.” Hivyo hamna kupunguka kwa ajabu ya kutwa utu. Neno ikawa mwili, na alifanya hivyo bila kuwacha kuwa Mungu. Yeye hudhihirisha utukufu wa Mungu.

Hii ina maana gani kwetu?

Mistari ya 15-18 inaeleza sababu zaidi ili kuamini kuwa Neno alifanyika mwili bila kuacha kuwa Mungu. Tutafafanua haya wiki ijayo, Mungu akitujalia. Lakini kwa sasa, wacha tujiulize kwenye mstari wa 14 kinachomaanisha kwetu sisi ya kuwa Neno alifanyika mwili—kwamba Mwana wa Mungu alifanyika binadamu bila kukoma kuwa Mungu. Haja gani niulize swali hili? Kwanza, ni kwa sababu fungu hili inatupa jawabu. Lakini pia kuna sababu nyingine.

Kukuza tamaduni wa kihusiano

Je, wakumbuka miezi michache iliyopita. Niliyahubiri ujumbe kadhaa nikimsihi Mungu kwamba azitumie ili kukuza kinachoitwa tamaduni wa kihusiano wa kanisa yetu? Nilifafanua nilichomaanisha katika asilia ya Wafilipi 2:3-4, “Msitende jambo lolote kwa nia ya kujitukuza, bali kwa unyenyekevu, kila mtu akimhesabu mwingine bora kuliko nafsi yake. Kila mmoja wenu asiangalie mambo yake mwenyewe tu, bali pia ajishughulishe kwa faida ya wengine.” Kwa maneno mengine, wacha na tukue kama kanisa kwa mienendo yetu nje ya ubinafsi, tuhudumie wengine na kufikiria mambo yao.

Na je, mnakumbuka ni nini msingi wa huo utumishi na mawazo wa uhusiano? Mistari inaofuata inaeleza: “Tuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Kristo Yesu. Yeye ingawa alikuwa sawa na Mungu, hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho, bali alijifanya si kitu, akajifanya sawa na mtumwa, akazaliwa katika umbo la mwanadamu” (Wafilipi 2:5-7). Kwa vingine, msingi wa kujidhili, utumwa, upendo na kufanywa upya utamaduni wa kihusiano pale Bethlehemu ulikuwa: Neno alifanyika mwili naye alikaa miongoni mwetu—na akatufia.

Kufanyika mwili na utekelezaji

Sababu yangu kuu ya kuelezea haya ni kwamba tusije tukasema, “Nam, tulifanya haba kwa kutilia mkazo uhusiano majira ya kiangazi iliyopita, na sasa tuko katika theolojia.” Hapana. Theolojia ambayo inahesabika kwa vyovyote ni ile aina ya Wafilipi 2, ambayo iko sawa na Injili ya Yohana. Inatusaidia kujua Kristo na utukufu wake. Pamoja na kubadilishwa na Kristo kwa ajili ya upendo. (13:34; 15:12)— ina maana kuwa inabadilisha kanisa letu kihusiano. Inatufanya kupenda zaidi, kusaidiana zaidi, kuhudumiana na kujaliana bila majivuno, bil ubinafsi na kutohusika.

Ndio mana nisemapo, “tusiache mstari wa 14 hadi tujiulize ni maana gani kwetu kwamba “Neno alifanyika mwili,” waweza kusikia baadhi ya fikira ilioko nyuma ya swali hilo. Huwa ninajiuliza tofauti gani hii theolojia kuu inafanya katika maisha zetu za kibinafsi na za kihusiano.

Ndani ya Yesu tunaona utukufu wa Mungu

“Tumeona utukufu wake, utukufu kama Mwana wa pekee atokaye kwa Baba amejaa neema na ukweli.” Ina maana ya kuwa ndani ya Yesu tunaweza kuona utukufu wa Mungu. Na ina maana kuwa utukufu wa Mungu ambao unafunuliwa katika Yesu haututeketezi katika dhambi zetu. Walakini, “Umejawa neema na ukweli.” Yaani, utukufu wa Mungu ndani ya Kristo ni dhihirisho ya neema kwetu bila kusaza ukweli na uaminifu wake mwenyewe. Na hii dhihirisho wa neema ni kuu sana. Ndiposa ametumia neno jaa—neno jaa inaeleza zaidi kuhusu utukufu. Utukufu wa Mwana wa Mungu umejazwa na neema kwetu sisi wenye dhambi bila kusaza ukweli wa Mungu.

Amejaa neema . . .

Hili kwa hakika ni habari njema. Mungu angechagua kufanyika mwili na kuwa hakimu na mhukumu. Na  sote tungepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya milele. Lakini hakufanyika mwili kwa njia hiyo. Neno, Mwana, ambaye ni Mungu alifanyika mwili ili kufunua utukufu wa kiungu iliyo “jaa neema na ukweli.” Neno la Mungu likafanyika mwili ili awe mwema kwetu. Neno alifanyika mwili ili hii wema wake kwetu iwe sawia na ukweli wa Mungu. Hii haiwezi kuwa neema wa dufu, usiyo na msimamo au hisia.

Hii itakuwa neema wa haki wa kumuinua Mungu na wa gharama. Itaelekea moja kwa moja hadi Kifo cha Yesu msalabani. Kwa hakika hii ndiyo sababu alifanyika mwili. Ilimpasa kuwa na mwili ili afe. Ilimbidi kuwa mwanadamu ili afe kama Mungu-Mtu badala yetu (Waebrania 2:14-15). Neno alifanyika mwili ili kifo cha Yesu kingewezekana. Msalabani ndipo ukamilifu wa neema uling’aa zaidi. Ilifanyika pale na kununuliwa pale.

. . . Na ukweli

Na sababu ilifanyika kupitia kifo ni kwamba Mwana wa Mungu amejawa neema na ukweli. Mungu ni wa mwema kwetu na mwaminifu kwake. Hivyo basi, Mwanawe akija, alijawa na neema na ukweli. Yesu alipokufa, Mungu alikuwa mwaminifu kwake mwenyewe, maanake dhambi iliadhibiwa. Na Kristo alipokufa, Mungu alikuwa mwema kwetu, kwa sababu Kristo aliubeba adhabu bali sio sisi.

“Neno alifanyika mwili” lina maana kwetu kuwa utukufu wa Mungu umedhihirishwa katika historia, jinsi haujawahi fanyika, yaani, kwa ukamilifu wa neema na ukamilifu wa ukweli unaong’aa zaidi katika kifo cha Yesu kwa wenye dhambi.

Kuona urembo wa kiroho

Jihadhari sana ili usiseme, “Nam, sikuwepo ili nimwone kwa hivyo utukufu huo haupo kwangu  ili niuone. Nyinyi wenye dini  mnaweza sema vyovyote kuhusu utukufu wa Mwana wa Mungu, lakini hayupo hapa ili tumwone.” Jihadhari. Usidhani utukufu huu katika mstari wa 14: Kama tu kung’aa au urembo wa nje. Yesu hakung’aa au kuwa na urembo wa kimwili. “Hakuwa na hadhi au umbo la kuweza kufanya tumtazame, hata urembo wa kutamanika” (Isaya 53:2).

Na usifikirie utukufu huu katika mstari wa 14 kama tu maonyesho ya miujiza. Kuna wale walioona miujiza, kuna waliyefahamu yaliyotendeka, na hawakuona chochote kizuri au cha utukufu. Walitaka kumuua (Yohana 11:45-48).

Hapana, “utukufu” uliofunuliwa wa Mwana wa Mungu, utukufu wa Neno, utukufu wa Yesu Kristo, alipokuja mara ya kwanza, ni utukufu kuu wa kiroho, uzuri wa kiroho. Hili si jambo la kuona kwa macho ya kimwili lakini kwa macho ya kiroho (Waefeso 1:18). Tunatazama jinsi anavyoongea, matendo yake, upendo na kufa, na kwa neema twaona utukufu au urembo wa kiungu unaojidhihirisha kwa wazi.

Uchanganyiko usio na kifani wa neema na ukweli

Paulo asema hivi katika 2 Wakorintho 4:4 “Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu.” “Utukufu wa Kristo aliye sura ya Mungu” ndiyo Yohana 1:14 inaita “utukufu wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.”

Na ukumbuke, Paulo anasema na watu ambao hawakumwona Yesu akiwa humu duniani, naye Yohana anaandika injili kwa watu ambao hawakumwona Yesu humu duniani—watu kama sisi. Utukufu wa Yohana 1:14 na utukufu wa 2 Wakorintho 4:4 ni utukufu ambao unaonekana tu kwa kiroho unaposikia hadithi za Yesu.

Hauhitajiki kumwona kimwili. Yesu alisema katika Yohana 20:29. “Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.” Unakutana naye katika Injili ya Yohana na maandiko mengine katika Biblia. Unapo kutana naye, kupitia hizi hadithi za maneno na matendo yake yaliyovutiwa pumzi, utukufu wake una ng’aa—urembo unaojithibitisha binafsi wa huo uchanganyiko usio na kifani wa neema na ukweli.

Kuzaliwa upya kupitia injili

Si ajali kwamba mstari wa 12-13 unaeleza kuzaliwa mara ya pili, na mstari 14 unaeleza juu ya kuona utukufu wa Mwana wa Mungu. Mistari ya 12-14:

Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake. Hawa watoto wamezaliwa si kwa damu wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali kwa mapenzi ya Mungu. Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi takauona utukufu Wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli

Kumbuka mstari wa 4: “Ndani Yake ndimo ulimokuwa uzima na huo uzima ulikuwa nuru ya watu.” Wakati uzima mpya wa kiroho umepewa, nuru mpya hufanyika. Nuru hii si ya kimwili. Ni nuru ya kiroho ya utukufu wa Mwana wa Mungu ambao umeelezwa katika mstari wa 14: Hivi ndivyo tunavyopata kuona!

Na je, hiyo maisha mpya ya kiroho inafanyika kwetu kwa jinsi gani? Mstari 13 inasema inafanyika tunapozaliwa si kwa mapenzi ya mwili bali kwa Mungu. Inafanyika tu katika kuzaliwa mara ya pili. Hivyo ndivyo twafikia imani na kumpokea Kristo na kuwa watoto wa Mungu. (Yohana 1:12).

Kwa Injili—kwa kusikiza hadithi za matendo na maneno za Yesu ambayo yanaokoa— Mungu anaumba ndani mwetu uzima wa kiroho. Tunazaliwa kwa Mungu kupitia Injili (1 Petro 1:23-25). Na huo uzima wa kiroho huona nuru ya utukufu wa  Kristo (Yohana 1:4). Inafanya hivyo mara moja. Ndiposa Yohana 8:12 unautaja “Nuru ya Uzima.” Unapopewa uzima wa kiroho, utauona utukufu wa kiroho.

Tazama utukufu

Kusema kwa njia nyingine, kulingana na mstari 12, ni kwamba huu uzima upya na mtazamo huu unaamini nuru na unaupokea nuru kama ukweli na utukufu wa Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Na katika huo uzima na nuru na kuamini na kupokea, mstari 12 unasema tunapata haki ya kuitwa watoto wa Mungu. Yaani, sisi ni wana wa Mungu kwa sababu huu uzima na nuru na kuamini na kupokea ni haki yetu kuwa watoto wa Mungu.

Sasa ninainua mbele yenu Mwana wa Mungu aliyefanyika mwili: Neno alifanyika mwili na akakaa miongoni mwetu bali kuwacha kuwa Mungu. Tazama utukufu wake, utukufu kama Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli. Mtazame, kwa utukufu vile alivyo, na uishi. Amina.