Tutapendaje jirani wetu ambaye ni Muisilamu?

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About World Religions
Topic Index
About this resource
English: How Shall We Love Our Muslim Neighbor?

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About World Religions
Part of the series Taste & See

Translation by Desiring God

Kuna majibu mengi kwa swali hili vile ilivyo njia nyingi ya kutenda wema badala ya maovu. “Upendo hautendi maovu kwa jirani” (Warumi 13:10.) “Upendo huvumilia kila kitu, huamini kila kitu, hutumaini kila kitu, huvumilia kila kitu” (Wakorintho 13:4). Haya ni vitu, ambavyo kwangu vyaonekana, vinastahili kutiliwa mkazo katika nyakati zetu.

[Jambo jipya: Kusema tupende maadui yetu haijakusudiwa kumaanisha kuwa Waisilamu wote wanahisi ama wanatenda mambo kwa njia ya kiadui kwa Wakristo. La! Hasha. Mara nyingi ni wakarimu na wanajali. Jambo ni kwamba hata kama mtu anatuchukua kwa njia ya kiadui (haijalishi ni wa dini ama si wa dini), inatupasa tuendele kupenda.

Maelezo mengine yahitajika katika hali yetu ya sasa. Ninaposema kuwa upendo unatihimiza kutenda wema katika njia zinazoonekana ya kukimu mahitaji yetu ya kimwili si maanishi kuwa usaidizi huu upeanwe tu wakati Muislamu amekuwa Mkristo. Upendo wa kudhihirika ni ushuhuda wa upendo wa Kristo. Mshuhuda hafichwi pahali anahitajika zaidi. Gumzo ambazo zimeshurutishwa kwa nguvu ama kwa fedha zinaenda kinyume na umbile wa imani iokoayo. Imani iokoayo ni kuukumbatia Yesu kama mwokozi wetu, Bwana wetu, na hazina kuu kwa hiari. Sio njia ya hazina. Yeye ni hazina.]

1. Waombe Baraka zote kutoka kwa Kristo hata kama wanakupenda ama hawakupendi.

2. Watende wema kwa njia zinazoonekana ambazo zinatimiza mahitaji yao ya kimwili.

3. Usilipize uovu kwa uovu ukiwa umetendewa mabaya.

4. Kaeni nao kwa amani ikiwezekana kwa kuwa inakutegemea wewe

5. Watafutie furaha ya uhuru kutoka kwa dhambi na hukumu kwa kuwaambia ukweli wa Kristo.

6. Kwa hakika tamani kuwa wajiunge nawe mbinguni kwa Baba kuwaonyesha njia, yaani Kristo Yesu.

7. Tafuta kufahamu yale wanayoyasema, ndipo unayokubali ama kukaripia yanatokana na kuelewa kwa kweli, sio mkanganyiko ama picha tatanishi.

8. Wakanye kwa machozi kuwa wale ambao hawatapokea Kristo Yesu kama mwokozi aliyekufa na kufufuka ambaye anaondoa dhambi za ulimwengu, wataangamia kwa ghadhabu za Mungu.

9. Usiwaelekeze kwa njia mbaya ama kuwapa tumaini lisilo la kweli kwa kusema “Waisilamu wanamwabudu Mungu wa kweli.”

Neno hili linaonyesha karibu kila mtu taswira sahihi ya moyo wa Muisilamu ujuao, upendao na kumcha Mungu wa kweli. Lakini Yesu anafanya jibu la kibinafsi ya mtu mwenyewe kama jaribio la uhakika wa mtu katika kumcha Mungu. Na yeye ni wazi kuwa mtu akimkataa kama mtauwa apeanaya maisha yake kama fidia kwa ajili ya dhambi na amefufuka tena—Huyo mtu hajui, wala kupenda ama kumcha Mungu wa kweli.

Upendo hautaelekeza Waisilamu, ama wale wanaowajali kwa njia mbaya, kwa kusema kuwa ‘wanamjua’ ama ‘kumcha’ na ‘kumpenda’ Mungu wa kweli kama hawatampokea Yesu vile alivyo. Hatuwezi kuiona mioyo ya watu. Tunajuaje kama wanamjua na kumcha Mungu wa kweli? Tunaweka chini uhai wetu ili kuwapa Yesu. Wakimpokea, wanajua na kupenda na kumcha Mungu. Wasipompokea Yesu, naye Mungu pia hawajampokea. Yesu ndiye jawabu.

Hilo ndilo hoja katika neno la Yesu katika Luka 10:16’ “Yeye amkataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.” Na katika Mathayo 10:40, “Yeyote atakaye nipokea mimi atakuwa amepokea Yeye aliyenituma.” Na katika Yohana 5:46, “kama mngelimwamini Musa, mngeliniamini Mimi.”

Kitu cha kupendeza ambacho tunaweza kuwafanyia Waisilamu ama mtu yeyote Yule, ni kuwaambia ukweli kamili kuhusu Yesu, kwa njia ya tunzo la kidhabihu kwao na kuwa tayari kuteseka kwa ajili yao badala ya kuwaacha, na halafu kuwasihi kuacha “kuabudu isiyo faida” (Mariko 7:7) na kuupokea Kristo kama mwokozi aliyesulubishwa na kufufuka kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao na tumaini ya uzima wa milele. Hii ingekuwa furaha yetu kuu—Kuwa na ndugu na dada kutoka kwa Waisilamu ulimwenguni.