Usalama wa Milele ni Mradi wa Jamii

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Perseverance of the Saints
Topic Index
About this resource
English: Eternal Security Is a Community Project

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Perseverance of the Saints
Part of the series Hebrews

Translation by Desiring God


Waebrania 3:12-19

Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai. 13 Lakini mtiane moyo kila siku mtu na mwenzake, maadam iitwapo ‘leo’, ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho. 15 Kama ilivyonenwa: “Leo, kama mtaisikia sauti Yake, msifanye mioyo yenu migumu kama mlivyofanya wakati wa kuasi.” 16 Basi ni nani wale waliosikia lakini bado wakaasi? Je, si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Mose? 17 Lakini ni nani aliowakasirikia miaka arobaini? Je, si wale waliofanya dhambi ambao miili yao ilianguka jangwani? 18 Nao ni nani ambao Mungu aliapa kuwa kamwe hawataingia rahani Mwake isipokuwa ni wale waliokataa kutii? 19 Hivyo tunaona kwamba hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutokuamini kwao.

Yaliyomo

Ikiwa Miwili Mikubwa

Wiki iliyopita tulilenga shabaha kwenye ikiwa mikubwa miwili katika mstari wa 6 na mstari wa 14. Hebu tuziweke mbele yetu tena ndio tutazame jinsi maisha yetu pamoja hapa Bethlehemu inaweza kutusaidia kutimiza ikiwa miwili mikubwa.

Mstari 6b: "Kama Mwana katika nyumba ya Mungu, sisi ndio nyumba Yake, kama tutashikamana na ujasiri wetu na katika tumaini tunalojivunia." Tazama kwa makini. Haisemi: tutakuwa nyumba ya Kristo ikiwa tutashikamana na ujasiri wetu na katika tumaini tunalojivunia. Inasema: Sisi ni nyumba yake ikiwa tutashikamana na ujasiri wetu na katika tumaini tunalojivunia. Kwa maneno mengine, kushikamana katika tumaini yetu Kwa maneno mengine, kushikamana kwa matumaini yetu ni thibitisho na ushahidi kuwa sisi sasa ni nyumba yake.

Kisha tazama ikiwa wa mstari wa 14: "Kwa kuwa tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu la kwanza hadi mwisho." Tena, tazama maneno vizuri. Haisemi: "Tutakuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu." Inasema, "tumekuwa washiriki [kipindi iliopita], kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu." Kwa maneno mengine, kushikamana kwa tumaini yetu inathibitisha kuwa kitu cha kweli na la kudumu ilitutokezea, yaani, tulikuwa washiriki wa Kristo. Kwa kweli tulizaliwa mara ya pili. Kwa hakika tulibadilishwa. Kwa kweli tulifanyishwa kuwa sehemu ya nyumba ya Kristo.

Nini basi itakuwa hitimisho kama hatutashikamana na tumaini wetu? Jibu ni kuwa si kwamba utawacha kuwa mshiriki wa Kristo, lakini kwamba haujawahi kamwe kuwa mshiriki wa Kristo. Soma kwa makini: "tumekuwa washiriki wa Kristo, kama tukishikamana tu kwa uthabiti na tumaini letu." Hivyo basi, "tusiposhikamana kwa maungamo yetu, basi hatujakuwa washirika wa Kristo."

Waebrania Inafundisha Usalama wa milele

Kwa msingi wa nakala hii, nilisema wiki iliopita kuwa kitabu hiki inafundisha usalama wa milele. Maanake, inafundisha kuwa kama kweli umekuwa mshirikiw wa Kristo, daima utakuwa mmoja. Atafanya kazi katika ninyi kuhifadhi imani na matumaini. Njia nyingina la kuisema ni kuwa kama wewe ni mwana wa Mungu, huwezi kusitisha kuwa mtoto wa Mungu. Lakini sote tunajua kwamba kuna watu wengi amabao huanza maisha ya Kikristo na kisha wanaanguka mbali na kuacha Bwana.

Mtu wa aina hiyo yupo kabisa katika fikira za huyu mwandishi. Anajua kinachotokea na anaishughulikia katika nakala hii na jinsi ya kuizuia kufanyika. Lakini inapotokea, maelezo yake ni si kuwa huyo mtu alikuwa mshiriki wa Kristo, lakini kwamba kamwe hakuwahi kuwa mshiriki wa kweli wa Kristo. Tukishikamana na tumaini letu, tumekuwa washiriki wa Kristo; tusipo, basi hatujakuwa washiriki wa Kristo.

Kwa maneno mengine kudumu katika imani na matumaini, kushikamana na ujasiri wetu katika Mungu, si njia ya kujizuiya kwa kupoteza msimamo wako katika Kristo; ni njia ya kudhihirisha kuwa una msimamo katika Kristo. Msimamo huo hauwezi kupotezwa kamwe, maanake umepewa kwa neema ya bure ya Mungu, na kwa sababu Kristo ameahidi na ahadi na kiapo (Waebrania 6:17-19) kuweka wale walio wake. (Waebrania 13:5; 20-21).

Kwa maneno mengine, usalama wangu na uthibitisho si uamuzi au maombi ambao ninakumbuka kufanya hapo awali katika kipindi kilichopita; usalama na uthibitisho wangu ni uaminifu na uwezo wa Mungu kwa kuniwezesha kumtumaini katika siku zijazo. Usalama wangu ni kwamba " Yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Kristo Yesu" (Wafilipi 1:6).

Je Unawezaje "Kuanguka Kutoka kwa Mungu" kama Kamwe Haukuwahi Kuwa Muumini?

Jambo hili linafufua maswali mengi. Ya kwanza ni: Naam, Kama kushindwa kwetu kushikilia imara tumaini letu na ujasiri ina maana ya kuwa hutukuwahi kamwe kuwa washiriki wa Kristo, basi ni nini ambayo tunaanguka mbali kutoka katika mstari wa 12?

Ndugu zangu, angalieni, asiwepo miongoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, unaojitenga na Mungu aliye hai.

Ni jnsi gani kunaweza kuwa kuanguka mbali na au kujitenga na Mungu ikiwa kweli hatukuwahi kuwa wake?

Jibu moja rahisi ni kwamba kunaweza kuwa utengano kweli tena chungu na mchumba ambao si kutengana na mkewe. Nadhani jinsi mwandishi anataka tuwaze kuhusu mambo haya imetolewa kwa mfano wa watu wa Israeli katika mistari 7-11 (= Zaburi 95). Anasema katika mstari wa 9 kwamba watu "walikuwa wameona matendo Yangu kwa miaka arobaini" na bado walifanya mioyo yao kuwa mgumu dhidi ya Mungu (v. 8) na kupotoshwa mioyoni mwao (v. 10). Maanake walikuwa wamemwona Mungu akigawanya Bahari ya Shamu na kuwarehemu kwa kuwaokoa kutoka Misri. Walikuwa wamemwona akitoa maji kutoka kwenye mwamba, mana kutoka angani, uwongofu na nguzo wa wingu na moto, ukombozi kutoka kwa maadui, sheria nzuri za kuishi, na msamaha kwa ajili ya uasi wao. Lakini licha ya hayo yote walifanyika mgumu katika mioyo yao na kuwacha kumtumaini Mungu. Walitaka kurudi Misri, waliunda sanamu na kunun'gunika. Hayo ndiyo mwandishi ana maanisha na "kujitenga na Mungu aliye hai."

Walikuwa wamevutwa katika utendaji mkuu wa Mungu. Walikuwa wameonja nguvu zake na kufaidika kutoka kwa Roho na wema wake. Walikuwa wamepata nuru ya ufunuo wa Mungu zaidi ya mtu yeyote ulimwenguni. Na walikwa wameanguka mbali. Hivyo ndivyo ilivyokuwa na baadhi ya watu wengi katika nyakati za Agano Jipya. Na hivyo ndivyo ilivyo leo. Watu hawa walikuwa wamevutwa katika ishara na maajabu yaliyotajwa katika Waebrania 2:4. Walikuwa wameonja nguvu za wakati ujao. Walikuwa wamekunjwa katika watu wa upendo na kujua mpimo wa kazi wa Roho miongoni mwao na katika maisha yao. Walikuwa wameuona mwanga wa injili. Walikuwa wamebatizwa na kushiri katika meza ya Bwana na kusikiza mahubiri na labda pia wenyewe walikuwa wamefanya kazi fulani za ajabu.

Lakini, ilivyo kuwa na Israeli, mioyo yao yakawa mgumu, na moyo mbovu wa kutoamini ukaimarika miongoni mwao, na wakanza kuweka tumaini yao katika mambo mengine badala ya Kristo, na hatimaye walitengana na wema wote ambao walikuwa wamezungushwa nazo. Na maelezo ya Waebrania ni kuwa "hawakuwahi kuwa washiriki wa Kristo." Walikuwa wameshiriki katika hatua kadha za kutaalamika na nguvu na furaha; lakini (kwa kutumia maneno ya Yesu) hakukuwa na mizizi kwa mmea na hivyo ukakauka, wakati wengine wakasongwa na wasiwasi na anasa za maisha haya (Luka 8:13-14).

Kwa maneno mengine, unaweza kuanguka mbali na Mungu kwa kiasi ambao umekuja karibu na kazi ya Mungu—upendo wa watu wake, nuru ya Neno lake, na fursa ya maombi, na nguvu ya kimaadili ya mfano wake, kipaji na miujiza ya Roho wake, baraka za riziki yake na ufunuo wa kila siku wa jua na mvua. Inawezekana kuonja mambo hayo, na kuguzwa zaidi na hayo, na kupotea katika kutoamini, kwa sababu Yesu Kristo mwenyewe si furaha wa moyo wako na matumaini na ujasiri na tuzo.

Yesu alifunza mambo hayo tena na tena ili kuonya dhidi ya uthibitisho wa uwongo. Kwa mfano, alisema katika Mathayo 7:21-23,

“Si kila mtu aniambiaye, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa Mbinguni bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kufanya miujiza mingi? Ndipo nitakapowaambia wazi, “Sikuwajua kamwe. Ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!”

Kutangaza ujumbe, kukemea mapepo, na kufanya miujiza kwa jina la Yesu sio thibitisho kwamba Yesu ame "tujua," au kwamba sisi ni washiriki wa Kristo. Kuna wezekano wa kufanya mambo hayo kwa moyo mgumu usiobailika. Ushahidi wa "kujulikana" na Kristo ni kwamba Yesu ni tumaini wetu, ujasiri wetu, thamini wetu, tuzo letu (Waebrania 10:24; 11:25-26). Huo ndio ukweli wa ndani ambao unabadilisha maisha yetu.

Hilo ni swali moja: Wawezaje kutengana mbali aukmgeuka Mungu, kamakwanza hukuwahi kuwa mshirika wa Kristo? Jawabu: kunanjia nyingi ya kushiriki hali ile ya kuwa karibu naMungu bila ya kumuamini na kumtumainia na kumpenda. Kunazo njia nyingi sana za kumtenga mbali sana Kriso bila hata kuwa mshirika wake.

Twawezaje kuwa na hakika ya usalama wa milele

Basi swali la pili ni: Tufanyeje? Tutajuaje na kufurahia na kuwa na hakika ya usalama wa milele? Katika mlango 12 na 13 tunapata jawabu mbili: moja ya majibu ikiwa jumla sana na lingine likiwa moja kwa moja.

Kwanza jibu la ujumla ni mlangowa 12: “Ndugu zangu angalieni asiwepo mioyoni mwenu mtu mwenye moyo mwovu usioamini, uliojitenga na Mungu aliye hai. Jibu la ujumla ni kwamba “chunga!” au “angalia!” au “tahadhari!” Ni kusema usiwe mtu asiyejali hali ya moyo wake au asyezingatia usalama wake moyoni au mtu shelabela. Iangalie. Jinsi Paulo asemavyo katika 2Wakorintho 13:5, Jichunguzeni wenyewe mwone kama mnaishi kwa imani, au Petro asemavyo katika 2Petro 1:10, “Kwa hiyo ndugu zangu, fanyeni bidii zaidi kuudhibitisha wito wenu na uteule wenu.” Msikubali kutoswa na mawimbi huku nakule kisha kuupuuza uvumilivu wenu kwa imani. Kila aina ya hisia inamenyana katika maisha yetu kila siku ilikuiba imani yenu na kubadilisha Kristo na kuweka hazina tofauti. Kuwa makini, uwe mwangalifu! Kesha! Tahadhari juu ya moyo wako. Kama jinsi Mithali 4:23 inavyosema, “Linda sana moyo wako kuliko vyote kwa maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Hilo ndilo jibu la mlango 12. Linda!

Mtu huenda akauliza, “Sawa, nikiwamshirika wa kweli jinsi ninavyo amini, kwanini nahitajika kuchunga na kuwa mwangalifu vile baada yaw ewe kusema kwamba ni salama milele wala siwezi kosa sehemu yangu na Kristo?” N’nafikiri linadhania jambo ambalo agano jipya linasema si kweli. Linadhania kwamba njia ya Mungu alilotengea wateulewakekufika Mbinguni halihitaji uangalifu wala kumakinika au hata kujichunguza mtu binafsi na kutenda mahitaji kwa bidii. Lakini Yesu kweli katika Luka 13:24 alisema “Jitahidini kuingia kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana, nawaambia, watajaribu kuingia lakini hawataweza. Naye Petro anasema, Mwe na kiasi nakukesha maana adui wenu iblisi, kama samba angurumaye huzunguka zunguka zkitafuta mtu ili apate kummeza (1 Petro 5:8) Kweli si kwamba waKristo wa kwelim hawastahili kukesha na kuwa waangalifu juu ya mioyoyao; lakini umfahamu kwamba wewe ni mKristo wa kweli kama ukiwamwangalifu juu ya moyo wako.

Ni waKristo wenye nidhamu na wa kutamanika wanaostahili kuwa waangalifu na kuwa na tahadhari kuhusu nafasi yao katika Kristo. Waliobatizwa na kutembea au kuomba na kuisongea meza la Bwana wakija kanisani, lakini hawampendi Kristo au kumhesabu kuwa hazina yao kuu au kumtumaini na kutazamia kumwona, ambao wanasema kuwa “Kuishini Kristo na kufa ni mara nyingine.” Hawa ndio wnaojitia udhabiti wenyewe na ndi wanaostahili kuhisi kutokuwa na salama (ona Kumbukumbu la Torati 29:19) Hawa watu huja kila mara kanisani, wanaochukua wokovu wao kama chanjo. Wanasema kuwa walipata chanjo hili zamani na kudhani mambo yote sawa bila ya kuangalia hatari karibu nao. Wanasema, “Nilipata kuwa na kinga dhidi ya jehanamu nikiwa na miaka minane—au miaka sita.” Basikufika mbinguni hainihusu kuwa mwangalifu juu ya moyo wao ili usiwe mgumu na kutoamini. Ni kuhakikisha tu kwamba kutiwa kinga kulitendeka. Hawa watu wamo katika hatari kuu sana.

Hilo ni jibu la kwanza la jinsi ya kukaa katika udhabiti wa usalama wa milele: Chunga moyo wako, linda sana moyo wako dhidi ya kutoamini. Hivi ni kusema, kesha ili kutunza ujasiri na tumaini lako kwa Kristo dhidi ya hazina zote pingamizi.

Jawabu la pili li dhahiri sana katika mlango 13: “Lakini mtiane moyo kila siku mtu na mwenzake, maadamu iitwapo ‘Leo’ ili asiwepo hata mmoja wenu mwenye kufanywa mgumu kwa udanganyifu wadhambi.” Jibu la pili ni kuwa usalama wa milele ni mradi unaoshughulikiwa na jamii. Tutafanya nini Yerusalemu ilikuepuka “moyo huu muovu wa kutoamini” bila kufanyika kuwa wagumu kwa udanganyifu wa dhambi zinazotujaribu kila siku ili tuzifanye hazina zaidi ya Kristo?

“Kanisa Linatusaidiaje kuepuka moyo mbovu wa kutoamini?”

Jibu ni kuwa baina ya sisi tunastahili kuwa kanisaist. Na ni nini haswa ambalo kanisa linafanya baina yao? Tuna zungumziana kwa njia inayotuepusha kuwa na moyo mgumu na kutufanya kuwa na moyo wa imani kwa nidhamu ya kiKristo juu ya vyote. Tunang’ang’ana kutunza imani baina yetu wenyewe na kuonyana ili tufuate ukweli na nidhamu ya Yesu. Hii ndiojinsi ya kukinga moyo mbovu wa kutoamini. Kutoamini maanake ni kukosa pumziko ndani ya Yesu kama hazina yako ilio kuu zaidi.

Kwa hivyo kusaidiana kuamini maanake ni kuonyesha watu sababu za kwa nini Yesu awe wa kutamanika zaidi, kupendwa na kuaminiwa zaidi ya chochote kile. Hapa hapa kuna ufafanuzi za sbabu ya Mungu kuteua kwamba maish ya KiKristo yawe yakibinafsi na ya kulindwa na jamii. Kuwa njia hiiya kuishi maisha ya ki Kristo inasababisha utukufu wa Kristo kuwa kivutio cha kila eneo la maisha yetu ya kila siku. Kama usalama wa milele ungalikuwa chanjo basi Kristo ngaliheshimiwa siku yakutoa chanjo na kisha baadaye kusahaulika, jinsi tunavyosahau chanjo zetu. Lakini sio hivi kama usalama huu wa milele utajumlisha vitata vyakilasiku dhidi ya kutoamini ambapo vifaa vyetu vya vita na ushahidi ni kujengana imani tukizileta sababu za kuaminika kwa Kristo, ukuu wake, na dhamani yake kuu juu ya vitu vyote. Tukilazimika kunena hivi baina yetu sisi ili kuhakikisha kwamba sote tunaendelea kuamini, basi anafanyika kuwa kivutio kila siku. Kwa hivyo Mungu anateua kwamba usalama wa milele uwe mradi wa kijamii kwa sababu hataki Mwanawe awe kama chanjo ambalo linasahauliwa, lakini kusherehekewa kila siku kama haina kuu zaidi ulimwenguni.

Sasa ni dhahiri katika mlango 12 na 13 kwamba jambo zaidi ya mahubiri linahitajika hapa. N’najaribu kulifanya katika mahubiri yangu—kuonya kila juma ili msiwe na moyo muovu wa kutoamini lakini maandiko yanasema mambo mawili zaidi ya hayo. Moja (katika mlango 13) ni kwamba kuonya kunastahili kufanyika kila siku wala sio tu mara moja kwa juma. Na lingine litendeke kati yetu baina ya mmoja na mwingine (mlango 13)—kwamba mnastahilikufanyiana mmoja na mwingine, wala sio kupata kutoka kwa mhubiri.

Ushawishi huu—kwamba huduma hii ya mmoja na mwingine ni wa maana sana kwa uvumilivuwako kwa imani, na wokovu wako—ushawishi huu ni sababu ulileta wazee kuamua kuunda vikundi vidogo vidogo muhula huu kule Bethlehemu. Twaamini kwamba hakuna njia katika kanisa kiasi hii ya kuweza kuruhusu vita vya umati mkubwa vya imani kuliko kutengeneza eneo kubwa kwa sababu ya vikundi vidogo ambavyo vitalenga kufanya kazi kubwa. Ndio maana mwanzo wa Septembakila Juma Pili usiku utatengwa kwa ajili ya kuunganika mmoja na mwingine katika kula pamoja katikati ya juma, tukiabudu pamoja kama kanisa, kutoa hadithi za kujenga imani kuhusu matendo ya Mungu katika imani, kufundisha watoto wetu, vijana na hata atu wazima neno la Mungu ili usipatikane kati yetumoyo wa kutoamini ukituongoza kutengana na Mungu aishiye.

Nimesisimka kuhusu uwezo wa huduma kwa hatua hizi—1) Ubunifu wa vikundividogo kwa kusababishakila usiku wa Juma Pili kuwa wazi kwa matumaini ya kuwa vikundi vingi vitakuwa zaidi na zaidi kamavikundi vya huduma za kuonyana kila siku; na pia 2) Mfumo wa ushirika wa kila jioni ya Juma Tano, kuabudu, mafunzo, na hadithikuhusu nguvu na uwezo mkuu wa Mungu nyakati hizi.

N’nawahimizeni kwa moyo wangu wote kwamba mchukue maandiko haya kwa makini mkiwaza kama kweli maisha yenu yanaambatana na mtindo huuwa maisha ya uKristo. Si pengine mkutano huu wa kila mara wa vikundi vidogo vya waumini, ambao wamejitolea kupigania imani yao baina ya wenyewe, utaleta furaha ya udhabiti na usalama zaidi ya vyote ulivyowahi kufahamu na kukuweka hurukwa ajili ya ushuhuda na huduma ulimwenguni? N’nafikiri ndio mwito wa Mungu kwetu.