Utukufu wa Mungu na Furaha Isiyokuwa na Kifani Mioyoni mwa Binadamu ni Kitu Kimoja

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Glory of God
Topic Index
About this resource
English: God's Glory and the Deepest Joy of Human Souls Are One Thing

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Glory of God

Translation by Jescah Abuti Muyia

Review You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).



Vidokezi Kumi na Tano

Jonathan Edwards anaandika:

Mungu, kwa kutafuta utukufu wake, anatafuta wema kwa viumbe vyake, kwa sababu ya kitovu cha utukufu wake . . . inaashiria . . . furaha ya viumbe vyake. Na kwa kuwajulisha kuwa amejitolea kikamilifu kwa ajili yao, anafanya hivyo kwa ajili yake, kwa sababu wema wao, anaoutafuta, unaenda sambamba na kuwa na ushirika naye binafsi. Mungu ndiye wema wao. Ukuu wao na furaha yao si chochote ila ni chanzo na uendelezaji wa utukufu wa Mungu. Mungu, kwa kutafuta utukufu na furaha yao, anajitafuta mwenyewe, na kwa kujitafuta, ina maanisha, yeye anasambazwa. . . anatafuta ukuu wao na furaha yao.

Kwa hivyo, ni rahisi kutambua ni kwa namna gani Mungu anapaswa kutafuta wema wa viumbe vyake . . . hata furaha yake, kwa kujitazama kwa ukuu; kwa sababu furaha yake inatokana na . . . viumbe wanaoheshimu ukuu wa Mungu . . kwa kushuhudia ukuu wa Mungu, kwa kuutukuza na kuupenda, na kwa kuufurahia.

Heshima ya Mungu kwa wema wa viumbe, na heshima yake kwake binafsi, sio heshima iliyogawanyika; bali imeunganika na kuwa kitu kimoja, kwa sabadu furaha ya viumbe inayokusudiwa ni furaha ya kuwa na ushirika na yeye binafsi.

Katika kitabu chake, God's Passion for His Glory: Living the Vision of Jonathan Edwards (with the complete text of The End for Which God Created the World (Wheaton, Ill.: Crossway Books, 1998), John Piper anatoa vidokezi kumi na tano kwa ukweli uliotolewa hapo juu.

1. Mapenzi ya Mungu kwa ukuu wake binafsi na mapenzi yake kwa furaha yangu ndani yake hayakinzani.

2. Kwa hivyo, Mungu amejitolea kwa kiwango sawa kuhakikisha nina furaha isiyokoma inayoongezeka kila uchao ndani yake jinsi afanyavyo kwa ajili ya utukufu wake.

3. Mapenzi ya Mungu kwa watenda dhambi hayahusiani sana na hali yao, bali hali yake ya kuwaweka huru kupitia neema na kuwawezesha kumfurahia mno.

4. Tabia zote nzuri miongoni mwa wanadamu ni sharti ziwe na nia ya kuwafanya watu kufurahia ukuu wa Mungu.

5. Matokeo ni kuwa dhambi ni ubadilishanaji mbaya wa utukufu wa Mungu na mabirika ya viumbe yaliyovunjika.

6. Mbingu haitakwisha kamwe, na kila uchao kutakuwa na ongezeko la ugunduzi wa utukufu zaidi na zaidi wa Mungu na furaha isiyokuwa na kifani ndanimwe.

7. Bila shaka, jahanamu ipo, inatambulika, inatisha na kudumu milele – tukio ambalo Mungu hutumia kuthibitisha umuhimu wa ukuu wake kupitia hasira takatifu dhidi ya wale wasiofurahishwa na ukuu wake.

8. Winjilisti unamaanisha kufafanua urembo wa Kristo na kazi yake ya ukombozi kupitia mapenzi ya dhati kwa nia ya kuwasaidia watu kuridhika ndanimwe.

9. Vivyo hivyo, mahubiri ya kikristo, kama sehemu ya ibada ya kanisa la Kristo la pamoja, inafichua kwa furaha utukufu wa Mungu ndani ya neno lake, na kusudi la kuwashawishi watu wa Mungu kuepukana na raha zitokanazo na dhambi ili kujinyima kwa kutii na kuridhika ndani yake.

10. Umuhimu wa kushiriki ibada ya pamoja ni kuonyesha kuridhika kabisa na utukufu wa Mungu, kama ishara kuwa hatuna na tuna shauku kubwa ya kuupata.

11. Misheni ulimwenguni huonyesha utukufu wa Mungu miongoni mwa watu wote ambao hawajafikiwa, kwa lengo la kuwaleta pamoja waobuduo ambao humtukuza Mungu kupitia furaha ya maisha yenye utiifu mkubwa.

12. Maombi ni kuomba Mungu msaada. Hii ni wazi kuwa ni wa utukufu mkubwa na tunanyenyekea kwa furaha tukihitaji neema.

13. Jukumu la usomi wa kikristo ni kusoma ukweli kama sehemu ya utukufu wa Mungu, kunena juu yake kwa uwazi, na kuonyesha urembo wa Mungu ndani yake.

14. Jinsi ya kumtukuza Mungu kupitia kifo ni kuona kifo kuwa na faida.

15. "Ni jukumu la Mkristo, jinsi mnavyofahamu, kwa kila mmoja kuwa na furana kadiri anavyoweza" (C. S. Lewis)