Wakati Ambapo Miaka Yako Ya Ishirini Imegubikwa na Giza Kushinda Vile Ulitarajia
Kutoka Gospel Translations Swahili
By Paul Maxwell About
Translation by Jescah Abuti Muyia
You can help us improve by reviewing this translation for accuracy. Learn more (English).
Mwili wa binadamu huanza kufa afikishapo umri wa miaka 25. Umri wetu wa miaka ishirini hutupika makofi kwa kutukumbusha tarehe ya mwisho za laana ya dhambi (Mwanzo 6:3): polepole, katika kano zetu; kukaza, kwenye fumwele zetu; kwa ustadi, tukitafuta uvimbe; kidesimali, na ongezeko la uhusiano uliopo kati ya urefu wako na uzani wako (BMI). Huwa tunahisi kifo kwa miaka ya ishirini; kimhemko na kimahusiano, kwa njia mbaya na za kuchukiza. Kifo hutufunga na minyororo yake, na polepole kutuzamisha zaidi katika kutafuta jibu la swali "Kifo u wapi mwiba wako?" (1 Wakorintho 15:55). Miaka yetu ya ishirini hutoa majibu mengi kwa swali hili-mabadiliko, kushindwa, kutamauka, utegemezi, shutuma, uajibikaji, kushindwa kwa maadili, kutosonga mbele, kutoridhika. "Mwiba" si neno mwafaka. Miaka yetu ya ishirini inaweza kuwa nyakati za giza.
Yaliyomo |
Vipengee vya Mvutano wa Robo-Maisha
Kuna (angalau) hisia tano zinazoangamiza na kuwakatisha tamaa vijana watakatifu waliochanganyikiwa, siku baada ya siku.
1. Kutoridhika
"Nilidhani mambo yangeenda vizuri kushinda yalivyo."
"Nilidhani ningekuwa vizuri zaidi kushinda nilivyo."
"Nilidhani urafiki ungedumu."
Tunawasili kwenye mlango wa miaka ya ishirini na katikati ya miaka ya ishirini tukiwa na matumaini ya kutimiza ndoto zetu za utotoni. Inajiri kuwa tulijiwekea matumaini makubwa ya siku zetu za usoni. Hakuna kazi maalum ya mwana anga. Hakuna maendeleo. Hakuna mwenzi wa ndoa wala watoto. Hakuna nyumba. "Subiri, maisha ni mabaya na yanachukiza mno?" Matarajio hayaonyeshwi kuwa ya uongo-huonyeshwa tu kuwa kiwango kidogo cha kupimia kile tunachotumainia hasa; kukumbwa na ukosefu mkubwa wa fedha, kutoridhika kimhemuko, kutopendezwa kitaaluma, na kutosonga mbele kiroho. "Nilidhani kufikia sasa ningekuwa nimeacha kutenda hii dhambi". Kuishi watu wengi katika vyumba vya kupangisha vilivyopakwa rangi nyeupe hutughadhabisha mno. "Haiwezekani kamwe." Haiwezekani kuwa haya ndiyo yote yaliopo. Milango ya utotoni imefungwa nyuma yetu. Maisha, yanaonekana, kuashiria kuwa mambo yatazidi tu kuwa mabaya zaidi.
2. Kutokowa na furaha
"Sina furaha jinsi nilivyokuwa nayo hapo awali."
"Ninahisi kushindwa kabisa kuona upande mzuri wa maisha."
"Uwezo wangu wa kuhisi furaha umevunjika."
Kila siku-siku baada ya siku-huchafua moyo. Kila siku, ina makusudi yaliyopungua kiasi, imekosa udhahiri kiasi, nyakati chache za urembo halisi uliopungua , na mambo machache ya kuvutia yanayoweza kustahimilika. Kuchanganyikiwa kusikokoma. Msongo wa mawazo. Uzembe wa kiroho. Polepole-chini, kudidimia-chini, kupindapinda-chini. Kwa kukosa nguvu, kutoona mbali. "Giza" si neno mwafaka. Uzito. Uchovu. Uchapwa. Kosa hamu. Kokosa furaha.
3. Kutamauka
"Haijalishi ninafanya nini."
"Ninaenda kukwama hapa milele."
"Wazazi wangu hawajaridhika kamwe."
"Marafiki wangu wote wanaendelea vizuri kunishinda."
"Maisha yanaonekana tu kuwa kama mbio za panya."
Kutamauka ni msuli wa kimawazo wa "Oh Mungu, hali hii haitafikia kikomo kamwe". Lipa. Umelazimishwa. Utamaushi ni akaunti ya benki iliyo na deni-uchechefu wa matumaini. Tafadhali tia imani zaidi ili kutoa kitu" Na hatuna chochote. Barua za kukataliwa, kuvunjika kwa mahusiano ya kimapenzi, vifo vya wazazi na ndugu, na taarifa mbaya zinazoingiliana vizuri na wasiwasi zetu kuu. Yametuaibisha kwa kuwa tuna mikono mitupu. Ni wezi wa matumaini. Watekaji nyara wakubwa wa ndoto. Hali, mawazo na mahusiano yetu-tunajitanganya iwapo hatufikiri kuwa vitu hivi vimeshonwa katika vazi la imani zetu. Na vinapokufa, hali ya kutamauka hujiuisha.
4. Hofu
"Kanisa halielewi au halishughulikii matatizo yanoyonisumbua."
"Ninahisi kuhukumiwa na Mungu kila wakati."
"Sidhani kama Mungu yupo. Na iwapo yupo, sijali."
Hofu imetakazwa na kutawazwa na kizazi cha milenia cha umri wa miaka ya ishirini na kitu-wingi wa matusi, kuhani na mfalme wetu mpya: hali ya kushangaza. "Mungu, iwapo watu wamejawa na mapenzi, basi kwa nini." . .” "Mungu, iwapo wewe ni mkuu sana, basi kwa nini. . .” "Mungu, iwapo wewe si mpenda ukatili, usiyejali, basi kwa nini. . .” Tunapozidi kudidimia zaidi katika hali ya kutamauka, tunakumbatiana na hofu. Imani yetu inageuka kutoka "Atarudi tena" hadi "Wakati ule mmoja ambapo. . .” -kutoka "Ninaamini" hadi "Kuna wakati niliamini"
5. Ukiwa
"Sijamhisi Mungu kwa mda mrefu mno."
"Marafiki ni wa bandia."
"Sina mahali ninapohisi kuwa ni nyumbani"
Ukiwa-"Maumivu makubwa au upweke; hali ya utupu mkubwa au uharibifu"-kutokana na neno la Kilatini desolare, "kutelekeza." Upweke unaweza kuwa nguvu kuu duniani inayoangamiza. Uchungu wa kutoka nyumbani unahitaji zaidi ya hekima na zaidi ya meza ya kahawa- inaweza kuchukua, kuumbua na kurarua roho. Kupoteza kwa mara ya kwanza kushikana mikono, hali ya kujali kimapenzi, jicho linalojali, msaada usiokoma-linaweza kuwa jambo la kusikitisha. Mpweke; kwa hivyo, mpweke daima, kwa hivyo, kutojimdu. Kuwa mkiwa ni kuvunjwavunjwa na utupu. Na tunavunjwavunjwa.
Mungu na Giza katika Miaka Yetu ya Ishirini
Wakati mmoja, Mungu alikuwa na umri wa miaka ishirini na kitu-Kristo katika mwili. Lakini kuna zaidi. Aliumba hali ya miaka ya ishirini na kitu. Alikufa kwa ajili ya miaka ishirini na kitu na akafufuliwa kwa ajili ya miaka ishirini na kitu. Ninafahamu, Ninafahamu. Haijalishi. Haibadilishi chochote. Yesu Kristo habadilishi chochote, unachoweza kufikiria.
Leslie Newbigin alisema, "Mimi si rajua wala msorajua; Yesu Kristo amefufuka kutoka kwenye wafu." Je,Yesu hafai? Kugaagaa kwenye upembuzi wa kujilaumu na kujihurumia kunaendeleaje? Je, hali hii inakufanyia vitu? Je, hali hii inafanya zaidi ya yale yamefanywa na Yesu? Kama ni hivyo, achana na makala haya. Achana na mtandao wa intaneti. Enda ukalewe na kusherehekea angalau, kwa sababu kesho utafariki (1Wakorinzo 15:32). Lakini iwapo unajitahidi kukamata -kitu fulani, kitu chochote-endelea kusoma. Kwa hakika, Yesu hubadilisha kwa kiwango fulani. Hapa kuna vitu vitano anavyotoa.
1. Bidii
Majukumu hututoa jasho. Labda si zaidi ya vile tunavyohisi joto lake kwa mara ya kwanza, tunafikiri hayatakwisha. Ili kuhisi hamu ya kusonga mbele kwa hatua mpya maishani, tunapaswa kufanya kazi ngumu ya kuachilia maisha yetu ya zamani- maisha mazuri, kama watoto, wasiojali, warajua, wenye mchezo, wasiokuwa na hofu na walio na uhuru wa kuota zaidi ya uwezo wetu. Hali hii imekwisha. Sio chuku kusema kuwa tunawezahitaji kuomboleza rasmi utoto wetu, ili tuweze kuusahau. "Sisi ni kama samakigamba ambao huendelea kufunga na kufungua magamba yao katika nyumba zao zenye kujaa maji na kupwa baada ya kuhamishwa hadi kwenye tangi la maabara au jikoni mkahawani"(William Bridges, “Transition”). Tunahitaji kuzoea mazingira yetu mapya.
Katika mabadiliko mabaya yanayosababisha msongo wa mawazo, Ezra "na kuungama, akilia na kujiangusha kifudifudi" (Ezra 10:1). Watu walimpa kazi-kutoa nafasi kwa Mungu: "Inuka, maana shughuli hii yakuhusu wewe, na sisi tu pamoja nawe; uwe na moyo mkuu, ukaitende" Kabla ya chochote kile, tunahitaji kitu kimoja katika miaka yetu ya ishirini:shughuli inayonufaisha. Ni sehemu ya katiba yetu kama wanadamu- kutafuta na kutazamia na hata kuomboleza ukosefu wa shughuli yenye manufaa: "mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza" (1Wathesalonike 4:11). Bidii hutoa fursa inayohitajika kwa injili kupenya ndani ya mawazo yanayolemaza yanayoweza kusababishwa na umri wa miaka ya ishirini. Bidii wakati wa kuomboleza, wakati wa kusonga mbele,wakati wa kuzoea, na wakati wa kuendelea mbele- bidii wakati wa kumaanisha ni chombo muhimu cha kukabiliana na mgogoro wa maisha robo.
2. Ndoto
Mwanzo, iwapo unachukulia giza kuwa pigo linaloua matumaini, wewe ni mfu tayari. Hakuna uwezekano wa kushinda giza cha utamaushi iwapo hakitakutana na moyo wa kujitolea. Lakini si pigo la kifo. Utamaushi ni hatari inajitokeza-hapa, katika miaka yetu ya ishirini, ni sharti tujifunze ukatili wa vita vya kuvizia vya maisha ya Mkristo "Usiingie na upole katika huo usiku mwema. Ghadhabika, ghadhabika dhidi ya kufifia kwa mwangaza." Hakuna haja ya utaratibu. Utamaushi sio nabii wala rafiki-utamaushi kila mara huzungumza kigaidi, na unahitaji umwagikaji damu kikatili. Hiili si swala la kawaida. Ni swala la maisha-ndani-ya- Roho. Nabii wa Yeremia Baruchi alilia, "Ole wangu! Kwa maana BWANA ameongeza huzuni pamoja na maumivu yangu. Nimechoka kwa ajili ya kuugua kwangu, wala sioni raha"(Yeremia 45:3). Mungu anajibu, "lakini roho yako nitakupa iwe nyara, katika mahali kote utakapokwenda"(Yeremia 45:5). Mungu hutusaidia kupigana, iwapo tutapigana. Mtume Yohana anawaandikia vijana kwa sababu "mmemshinda yule mwovu" na kwa sababu "mna nguvu" (1 Yohana 2 :13-14).
Pili , hizo hisia za giza haziwezi kuwa nyeusi sana. Zinaweza kumaanisha kitu fulani. Zinaweza kuwa ishara ya onyo: "Fanya kile kitu kingine." Au "Usisalie hapa daima." Paulo anasisitiza: "Lakini kama Bwana alivyomgawia kila mtu, kama Mungu alivyomwita kila mtu, na aenende vivyo hivyo" (1 Wakorintho 7:17). Je unafuata ndoto za wazazi wako? Jamii yako? Je ndoto zako ni mtumwa wa hofu zako? Urafiki na ushirika wetu binafsi na Kristo unatupa uhuru wa kukoma kuishi ndoto za watu wengine. Mungu ametoa wito kwako binafsi. Ni vyema kudhubutu, na kuwa na ndoto kubwa kwa ajili ya utukufu kwa Mungu.
3. Kutoridhika
Haujaridhika? Vyema. Dunia imejawa na karamu zinazoshibisha mwili, lakini kwa wakati uo huo zikikosesha roho chakula. Kuwa na imani zaidi kujihusu kuliko "dunia hii mbovu iliopo sasa"(Wagalatia 1:4). Iwapo tutaamini ujumbe wa ulimwengu kuwa hatujakamilika, tuko duni, hatutoshelezi kwa kiwango ambacho tunaweza kufanya marekebisho-na fesibuku(Facebook) ya kutosha- na fedha za kutosha, na ngono ya kutosha, na vitu tunavyopenda kufanya-basi sisi ni watumwa wa hivyo vitu. Sote tunazidi kukosa matumaini, na tuna sababu nyingi za kutumaini, kushinda vile tunaweza kufikiria. Mungu anaidhinisha kutoridhika kwako kwa kifurushi cha dhana-binafsi cha dunia: "Kubwa, na sehemu ya kujishuku na chembechembe za hatia-shika Yesu" Ni jinsi gani inatabirika kutofurahisha.
Hali ya kujichukia hujirudiarudia- si fikra ya pekee; huzama ndani mwetu na kujitokeza kwa mzunguko wa mchapuko. Tunatoa hukumu kwa matamanio yetu: yana mapungufu, hayajakamilika, ya thamani ndogo, ya kipumbavu, yasiyowezekana. Usijaribu kubadilisha hali yako ya kutoridhika na kukataliwa kwa kujihukumu na kujiachilia. Ni mzunguko unaosababisha maisha yasiweze kusonga mbele na kuonekana yaliokufa ganzi. Tafuta moto. Miaka yetu ya ishirini inaweza kuwa unusu kaputi-inaweza kugandisha kwa machungu na kuua motisha. Iwapo tunaweza kuachana na fikra za kukatisha tamaa na kukosesha furaha kabisa, tutatambua kuwa hali yetu ya maisha isiyoweza kustahimilika kutokana na hofu kubwa si nabii wa mambo mabaya- ni machungu kutokana na mafadhaiko, kutoka ndani mwetu. "Nalikuwa kama mjinga, sijui neno; Nalikuwa kama mnyama tu mbele zako. Walakini mimi ni pamoja nawe daima, Umenishika mkono wa kuume" (Zaburi 73:22–23). Hali ya kutoridhika ndiyo hutumiwa na Mungu kututofautisha na wanyama.
4. Utegemezi
Mungu ni baba mwenye upendo. Nukta. Sehemu ya kifurushi hicho. Mungu anajali mahitaji yako ya wazazi. Kama ulikuwa ma mahusiano ya kunyanyasa, yanayovunja roho, yanayotia kiwewe, au uhusuhiano mbaya na wazazi wako, hilo ni janga na mzigo. Hata hivyo, Mungu-Baba yako mkamilifu- anajali kuhusu hadithi yako. David Powlison anaeleza, "Saikolojia yenye mabadiliko [hugeuza] uhusiano wa kale na wazazi kuwa fimbo ya miujiza ya kueleza maisha yote. Biblia hutoa . . .maelezo dhabiti ya kubadilisha maisha" ("Nini Iwapo Baba Yako Hakukupenda?")
Mungu hatarajii uwe mkurugenzi wa kampuni kubwa. Mungu hatamani kuwa ungekuwa unapata mshahara mkubwa. Mungu hatamini kuwa ungekuwa na hulka ya furaha-bahati. Mungu hatamini kuwa "tayari ungejikusanya pamoja!" Hatuko kivyetu. Hatujavunjika zaidi ya kushindwa kurekebishwa. Hatujalaaniwa kuwa wazazi wetu(2 Wafalme 21:21; 2 Wafalme 22:2). Hatujahukumiwa na Baba wetu wa mbinguni kwa kuwa kwenye mchakato (2 Petro 3:15). Anatufahamu na anatupenda na anafanya kazi kwa uvumilivu ndani yetu na pamoja nasi: "Nawaandikia ninyi, watoto, kwa sababu mmemjua Baba"(1 Yohana 2:13). Unaweza kumtegemea kupata mapenzi, uthibitisho, upendo, marekebisho, mkono unoelekeza, na huduma yake isiyokuwa na kikomo. Pumua.
5. Kujitolea
Mungu amejitolea kwetu. Hali hii inaonekana kuwa ya kushangaza-Je hatujajitolea kwa Mungu? Je kujitolea siyo kitendo duni? La. Mungu amejitolea kwa Kristo na sisi ni wamoja na Kristo: "Msiogope wala msiwahofu. . . Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja na wewe. Hatakupungukia wala kukuacha" (Kumbukumbu la Torati 31:6). Kiwango kile Mungu amejitolea na kuwa pamoja na Kristo, amejitolea kwetu na kuwa pamoja nasi (Waefeso 1:20) Mungu hawezi kujitolea zaidi kwetu kushinda alivyo sasa, hata atakaporudi tena: Tunao "wokovu ule ulio katika Kristo Yesu" (2 Timotheo 2:10).
Hii inaweza kuonekana kuwa jambo la kawaida mno. Hiyo ni sawa. Mungu hatoi ahadi kuwa ukweli huu kila mara utakuwa na werevu na wa kushangaza kama yule mtu katika maandishi yako bunifu. Ile shahada ya uzamili (MFA) inayokuweka kwenye madeni ya $25,000. Mungu husema mambo ya kawaida mno. Mungu hurudiarudia mara kwa mara ukweli mmoja, usiokuwa na uasili, uliotiwa chumvi kiasi, na kuwa kama mziki uliochezwa kupindukia kwa sababu sisi huusahau kila mara. "mfanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi"(Hagai 2:4). "mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari"(Mathayo 28:20). "BWANA yu karibu nao waliovunjika moyo"(Zaburi 34:18).
Mungu yu pamoja na walio na upweke na waliovunjika moyo "Wapi?" Yu wapi? Yupo . . . Yupo. Wakati mwingine kuna mengi ya kunena, na wakati mwingine hakuna. Unapinga: "Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia,wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumuona mtu"(Zaburi 34:18). Hataacha kurudiarudia: "maana yeye awagusaye ninyi aigusa mboni ya jicho lake"(Zekaria 2:8).