Wake kwa waume Mungu aliwaumba kwa mfano wake

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About Manhood & Womanhood
Topic Index
About this resource
English: Male and Female He Created Them in the Image of God

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About Manhood & Womanhood
Part of the series Biblical Manhood and Womanhood

Translation by Desiring God

Ndipo Mungu akasema, “Tufanye mtu kwwa mfano wetu, kwa sawa yetu, wakatawale juu ya samaki wa baharini na ndege wa angani, juu ya mifugo, juu ya dunia yote, na juu ya viumbe wote wataambao juu ya nchi.” Kwa hiyo Mungu alimwuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe, kwa mfano wa Mungu alimwuumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na mkaongezeke, mkaijaze tena dunia na kuitiisha. Mkatawale samaki wa baharini, ndege wa angani na kila kiumbe hai kiendacho juu ya ardhi.”

Mimi nataka kuwaza nanyi asubuhi ya leo kuhusu mambo matatu yanayofundishwa katika Nakala hii. Kwanza ni kwamba Mungu aliumba binadamu. Pili ni kwamba Mungu alituumba kwa mfano wake. Tatu ni kwamba Mungu alituumba kiume na wa kike.

Yawezekana kukuballi ukweli huu na kukosa kuwa Mkristo. Ama kwa kweli yote yanafundishwa papa hapa katika maandiko ya Kiyahudi. Yamkini Myahudi aaminiye maandiko mema atakubali ukweli huu. Hata ingawa unaweza kuuamini ukweli huu tatu na kukosa kuwa Mkristo, yote yaegemea Ukristo. Yote yahitaji ukamilifu ambo watoka kwa kazi na Kristo. Hicho ndicho kile ningependa kuongea kukihusu, hasa kuhusu ukweli wa tatu—tuliumbwa mke na mume kwa mfano wa Mungu.

Yaliyomo

1. Mungu aliwaumba wanadamu

Wacha tutazame ukweli wa kwanza: kwamba wanadamu wameumbwa na Mungu. Nadhani hii inahitaji maelezo. KWA NINI alituumba? Unapotengeneza kitu, unayo sababu ya kukitengeneza. Na je, ulimwengu vile tujuavyo, unapeana jibu la swali hilo? Agano la kale laongea juu ya mtu kuleta ulimwengu chini ya utawala wake. Inaongea kuhusu kuumbwa kuonyesha utukufu wa Mungu (Isaya 43:7). Inaongea juu ya dunia kujawa na ufahamu na utukufu wa Bwana.

Lakini tunaona nini? Tunaona dunia iliyo na uasi dhidi ya Muumba. Tunaona maandiko ya Kiyahudi zikifika kikomo na hadithi ya uumbaji ambao imekamilika kabisa na tumaini la utukufu ikiwa bado haujajaa. Hivyo basi kuamini tu kuwa Mungu aliwaumba wanadamu vile maandiko ya Kiyahudi yalivyoeleza yahitaji hadithi iliyozalia kusimuliwa, hivyo ni kusema, Ukristo. Kupitia tu kwa Kristo ndipo lengo la uumbaji kita hitimizwa.

2. Mungu alituumba kwa mfano wake

Ama uuchukue ukweli wa pili kwa mfano: Mungu alituumba kwa mfano wake. Kwa hakika hii inahusiana na sababu ya kuwa kwetu hapa. Lengo lake la kutuumba lazima kungekuwa na jambo la ajabu ukichukua kuwa sisi si vyura ama mburukenge ama ndege ama tumbili. Sisi ni wanadamu katika mfano wa Mungu, sisi tu, wala si mnyama mwingine.

Lakini ni fujo mingi tumefanya na huu hadhi ya ajabu. Tungali kama Mungu? Hakika, ndio na la. Ndio, tuko kwa mfano wa Mungu hata tukitenda dhambi na kutoamini bado kuna ufananisho. Tunajua haya kwa sababu katika Mwanzo 9:6 Mungu alimwambia Noah, “Yeyote amwagaye damu ya mwanadamu, damu yake itamwagwa na mwanadamu, kuwa katika mfano wa Mungu, Mungu alimuumba mwanadamu.” Kwa maneno mengine, hata katika ulimwengu ambao dhambi hupatikana (vikiwemo mauwaji) bado wanadamu wako katika mfano wa Mungu. Hawawezi kuuliwa kama fuko na mbu. Unapoteza maisha yako ukiua binadamu (Tazama Yakobo 3:9)

Lakini, je tuko katika ule mfano Mungu alituumba kwayo? Si mfano huu huaribiwi wakati mwingine kwa kiasi cha kutotambulika? Je unahisi kwamba unafanana na Mungu kwa kiwango inafaa ufanane naye? Basi hapa pia imani ya kuwa tuliumbwa katika mfano wa Mungu yahitaji kukamilika—katika hali hii ukombozi, kufanywa upya, uumbaji upya. Na hali hii hakika ndicho Ukristo huleta. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu—si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema . . . mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawa sawa na mfano wa Mungu katika haki yote na utakatifu.” (Waefeso 2:8-10; 4:24). Mungu alituumba kwa mfano wake, lakini tumeuharibu kwa kiasi cha kutotambulika na Yesu ndiye jawabu. Anakuja kwa Imani, husamehe, husafisha, na kuanza mradi ya kutengeneza upya uitwayo utakaso ambao utafika katika utukufu ambao Mungu alikusudia wanadamu hapo mwanzo. Basi kwa kuwa tunajua kuwa tuliumbwa kwa mfano wa Mungu, dhambi zetu na ufisadi wetu unahitaji jibu. Na Yesu ndiye jawabu.

3.Mungu alituumba mwanamume na mwanamke

Ukweli wa tatu katika mstari huu ni kuwa Mungu alituumba mwanamume na mwanamke. Na hili pia inaonyesha Ukristo na yahitaji ukamilifu wa Kristo. Kwa njia gani? Kwa njia zaidi ya mbili. Mmoja yatoka kwa fumbo la ndoa. Nyingine inatoka kwa taswira mbaya ya kihistoria ya uhusiano katika dhambi kati ya mke na mume.

Fumbo la ndoa

Chukua fumbo la ndoa. Katika Mwanzo 2:24, baada tu ya hadithi ya vile mwanamke alivyoumbwa, Musa (Mwandishi wa kitabu cha Mwanzo) anasema, “Kwa sababu hii, mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe na hawa wawili watakuwa mwili mmoja.” Sasa wakati mtume Paulo anaponukuu kutoka kwa mstari huu katika Waefeso 5:31, anasema “Siri hii ni kubwa, bali mimi nanena kuhusu Kristo na Kanisa.” Na kwa hiyo kama kielelezo chake, anafafanua maana ya ndoa: Ni maana ya upendo wa Kristo kwa Kanisa iliyowakilishwa kwa mwanamume kama kichwa kumpenda bibiye; na ni alama ya kanisa kumtii Kristo kwa furaha iliyowakilishwa katika uhusiano ya mwanamke kwa bwanake.

Anaita Mwanzo 2:24a “fumbo” kwa sababu Mungu hakufumbua lengo lake la ndoa katika ya mwanamke na mwanamume katika kitabu cha Mwanzo. Kulikuwa na vielelezo na mambo ya kuashiria katika Agano la Kale kuwa ndoa ilikuwa kama uhusiano kati ya Mungu na watu wake. Lakini ni wakati tu Kristo alipokuja ndipo fumbo la ndoa lilifumbuliwa kwa kina. Inakusudiwa kuwa taswira ya agano kati ya Kristo na watu wake, jitihada zake kwa kanisa.

Je hivyo basi mwaona, vile Mungu kwa kuumba mwanamume na mwanamke na kudhibitisha ndoa kama uhusiano ambao mwanamume anaacha mamake na babake na kuambatana na bibiye katika juhudi la Agano—Vile tendo hili la uumbaji na thibitisho la ndoa lahitaji ufunuo wa Kristo na Kanisa lake. Yanahitaji Ukristo kama ufunuo wa fumbo.

Hii ni hisia geni kwa watu wengi, hata kwa Wakristo wengi, kwa sababu ndoa ni tendo la kilimwengu na pia ya Kikristo. Utaipata katika tamaduni zote, sio tu katika jamii za Wakristo. Basi kila mara hatufikirii juu ya ndoa ambazo si ya Wakristo ambazo tunazijua kama alama ya fumbo ya uhusiano wa Kristo na tunazijua kama alama ya fumbo ya uhusiano wa Kristo na Kanisa. Lakini ni hivyo na kuishi kwetu kama mwanamke na mwanamume katika ndoa kunalilia Kristo kupata kujijulisha kwa uhusiano wake na Kanisa. Ukristo unakamilisha ufahamu wetu kuhusu agano la ndoa.

Wacha nikuchoree taswira hapa na niupatie mwelekeo ambao hukuwa umeutarajia. Kristo arudi tena ulimwenguni. Ingawa ulivyomwona akienda, atarudi tena, malaika walisema. Hebu tafakari juu ya siku hiyo pamoja nami. Mbingu zafunguliwa na mlio wa baragumu na Mwana wa adamu anatoka mawinguni kwa nguvu na utukufu mkuu pamoja na malaika maelfu kumi wanaong’aa kama jua. Anawatuma kukusanya wateuliwa wake kutoka kwa pande nne na anafufua kwa wafu wale walioaga katika Kristo. Anawapa miili mpya na yenye utukufu kama wake, na kutubadilisha tuliozali kwa kufumba na kufumbua macho kufikikia kiwango cha utukufu.

Matayarisho ya kutoka jadi ya bibi harusi ya Kristo (kanisa!) hatimaye imekamilika na anauchukua mkono wake, vile ilivyo, na kumwelekeza kwa meza. Chakula cha ndoa cha Mwana wa kondoo kimefika. Anasimama kando ya meza na kimya kuu huja juu ya mamilioni ya watakatifu. Na anasema, “Huyu, mpendwa wangu, ndiye aliyekuwa maana ya ndoa. Ndiyo ilikusudia. Ndio maana niliwaumba mume na mke na kudhibitisha agano la ndoa. Kwanzia sasa hakutakuwa na kuoa ama kuoleka, kwa sababu uhakika wa mwisho umetimia na kivuli yaweza pita.” (Tazama Mariko 12:25: Luka 20:34-36).

Sasa kumbuka yale tunayafanya: tunajaribu kuona ukweli wa tatu, Mungu alituumba kwa mfano wake kama mwanamume na mwanamke; laonyesha Ukristo kama ukamilifu wake. Na nilisema inafanya hivyo kwa njia mbili. Njia ya kwanza ni kwa fumbo la ndoa. Kuumbwa kwa wanadamu kama mwanamume na mwanamke kunaleta muundo ufaayo katika uumbaji kwa uthibiti wa ndoa. Hungekuwa na ndoa bila mume na mke. Na maana ya ndoa haujulikani kwa kiini ama ukamilifu mpaka tuuone kama mfano wa uhusiano kati ya Kristo na Kanisa.

Basi uumbaji kama mume na mke unaelekeza katika ndoa, na ndoa unaelekeza kwa Kristo na Kanisa. Na hivyo basi imani kwamba Mungu alituumba katika mfano wake kama mwanamume na mwanamke haijakamilika bila Ukristo—bila Kristo na kazi yake ya kuokoa kwa Kanisa.

Ubaya wa kihistoria katika uhusiano kati ya mke na mume

Basi nilisema kuwa kulikuwa na njia nyingine vile uumbaji wa mume na mke kwa mfano wa Mungu unaonyesha Ukristo kama ukamilifu unaohitajika, kusema, kupitia kuharibika kwake katika ubaya wa kihistoria uliotokana na uhusiano kati ya mume na mke. Wacha nijaribu kufafanua.

Dhambi ilipoingia duniani, athari za uhusiano wetu kama mume na mke ilikuwa ya kutamausha. Mungu anamjia Adamu baada ya kula tunda lililokataliwa na anamuuliza kile kilichotendeka. Adamu anasema katika Mwanzo 3:12, “Huyu mwanamke uliyenipa awe pamoja nami, ndiye aliyenipa sehemu ya tunda kutoka kwenye huo mti nami nikala.” Kwa maneno mengine ni kosa lake (ama lako kwa kunipa yeye!), basi kama ni lazima mtu afe kwa sababu ya kula tunda, inafaa iwe yeye!

Hapo upo na mwanzo wa vita vyote vya nyumbani, kudhulumu wanawake, ubakaji, matamshi mabaya ya ngono, na njia zote za kudunisha mwanamke ambaye Mungu aliumba kwa mfano wake.

Mwanzo 3:16 inatangaza laana juu ya mume na mke walioanguka hivi: Kwa mwanamke nasema, “Nitakuzidisha sana uchungu wakati wa kuzaa kwako, kwa uchungu utazaa watoto, tamaa yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.” Kwa maneno mengine chanzo cha dhambi na laana kwa wakati wetu ni utata kati ya mwanamke na mwanamume. Mstari huu si maelezo ya vile vitu vinafaa viwe. Hili ni elezo ya vile kwa laana vitu vitakuwa kama dhambi itazidi kutawala. Waume wanyanyasi na wake watukutu. Hii si maana ya mwanaume na mwanamke katika mfano wa Mungu. Ni ubaya wa dhambi.

Ubaya huu unaonyeshaje Ukristo? Unaegemea Ukristo kwa sababu unahitaji uponyo ambao Ukristo unaleta katika uhusiano kati ya mume na mke. Kama Mungu alituumba kwa mfano wake KAMA MWANAMUME NA MWANAMKE, hiyo inaashiria usawa katika umbile, hadhi, heshima, umoja, kuhitajiana, hatima ya pamoja. Lakini hii iko wapi katika historia ya ulimwengu? Upo katika uponyo uletwao na Yesu.

Mitazamo miwili kuhusu uponyo uletwayo na Yesu

Kuna mengi ya kusema hapa. Lakini wacha nitaje mambo mawili tu.

3.1. Hatima ya kuumbwa mwanamke na mwanamume

Kwanza, Petro anasema katika 1 Petro 3:7, Kuwa bibi na bwana Wakristo ni “warithi pamoja katika kipawa cha thamani cha uzima.” Hili lamaanisha nini? Inamaanisha kwamba katika Kristo waume na wake wanapata tena kile kilichokusudiwa kwa kuumbwa mwanamume na mwanamke kwa mfano wa Mungu. Inamaanisha kuwa pamoja kama mwanamume na mwanamke wanafaa kuonyesha utukufu wa Mungu na pamoja kama warithi inafaa warithi utukufu wa Mungu.

Uumbaji kama mwanamume na mwanamke katika mfano wa Mungu (unapoiona sambamba na dhambi) unahitaji ukamilifu wa uponyo unaokuja pamoja na kazi ya kufanywa upya ya Kristo na urithi aliyoununua kwa ajili ya wenye dhambi. Kristo anarudisha kutoka kwa dhambi uhakika kuwa mwanamume na mwanamke ni warithi wa pamoja katika kipawa cha thamani cha uzima.

3.2. Maana ya ukapera kama Mwanamume na Mwanamke

Kitu kingine ya kutajwa juu ya vile Kristo anageuza vitu na kushinda ubaya wa vita vyetu na kutimiza hatima ya kuumbwa mwanamume na mwanamke katika mfano wa Mungu kinapatikana katika 1 Wakorintho 7. Hapo Paulo anasema kitu ambacho karibu kinatatanisha kwa siku hiyo. “Kwa wale wasio na kwa wajane, ingekuwa vizuri wabaki kama mimi nilivyo . . . mwanaume ambaye hajaoa amejishughulisha na mambo ya Bwana, yaani, jinsi ya kumpendeza Bwana . . . mwanamke asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili awe mtakatifu kimwili na kiroho . . . nasema hii . . ..sio ili kuwawekea kizuizi chochote lakini ili . . . kuvutwa pengine katika kujitoa kwenu kwa Bwana.” (1 Wakorintho7: 8, 32-35)

Unaona kile hiki kinachomaanisha? Kinamaanisha kuwa uponyo ambao Yesu huleta kwa mwanamke na mwanamume walioumbwa katika mfano wa Mungu hautegemei ndoa. Yamkini matukio ya Paulo kama asiyeoa (na muundo wa Yesu kama mume asiyeoa) ilimfundisha kuwa kuna aina ya hisia ya kipekee ya kujishughulisha na Bwana inyowezekana kwa mwanamke na mwanamume asiyeoa ambayo si sehemu ya watakatifu waliooa.

Njia nyingine ya kusema hii: ndoa ni tendo la muda kwa nyakati huu hadi wakati wa ufufuo wa wafu. Lengo la maana na kusudio lake ni kuwakilisha uhusiano wa Krtisto na Kanisa. Wakati ukweli unapokuja, uwakilishi vile tujuavyo utawekwa kando. Na hakutakuwa na kuoa wala kuolewa wakati ujao. Na wale ambao wamekaa bila kuoa na kujishughulisha na Bwana wataketi katika chakula cha ndoa cha Mwana Kondoo kama warithi wa pamoja ya neema ya uhai. Na kulingana na kujishughulisha kwao kwa Bwana na dhabibu zao watazawadiwa kwa upendo na uhusiano na furaha juu ya fahamu zetu.

Kwa Ufupi

Basi wacha tuweke kwa ufupi yale tumeyaona.

1. Mungu aliumba wanadamu. Na vile Agano la Kale latamatika, neno hili la ajabu lahitaji hadithi yote iliyozalia, Ukristo, ili ifahamike kile Mungu alichokusudia. Malengo yake katika uumbaji hayajakamilika bila kazi ya Kristo.

2. Mungu alituumba KWA MFANO WAKE. Lakini tumeharibu mfano huu vibaya sana kwa kiasi kwamba ni nadra utambulike. Hivyo basi ukweli huu wahitaji ukamilifu wa Ukristo kwa sababu kile Yesu anafanya ni kumiliki tena kile ambacho kimepotea. Inaitwa “uumbaji mpya katika Kristo.” Mfano warejeshwa katika haki na utukufu.

3. Muungu alituumba kwa mfano wake KAMA MWANAMUME NA MWANAMKE. Na hii pia inahitaji ukamilifu katika ukweli wa Ukristo. Hakuna mtu ambaye anaweza kufahamu kabisa kile kinamaanisha kuwa mwanamume na mwanamke katika ndoa mpaka waone kuwa ndoa inakusudiwa kuonyesha Kristo na Kanisa. Na hakuna anayeweza kujua hatima ya kweli ya kuumbwa mwanamume na mwanamke kwa mfano wa Mungu mpaka wajue kuwa mwanamume na mwanamke ni warithi wa pamoja katika neema ya uhai. Na mwisho hakuna anayeweza kufahamu kwa yote maana ya kutooa ama kuolewa kama mwanamume na mwanamke katika mfano wa Mungu mpaka wajue kutoka kwa Kristo kuwa wakati ujao hakutakuwa na ndoa, na hivyo basi hatima tukufu ya kuwa mwanamume na mwanamke katika mfano haitegemei ndoa, lakini kujishughulisha kwa Bwana.

Basi dumu katika ukweli huu: Mungu alikuumba kwa mfano wake; alikuumba kama mwanamke mwanamume ndipo ujishughulishe kwa Bwana kwa yote na umuhimu wote na kwa kipekee.