Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa ili atuponye kutokana na ugonjwa wa dhambi na ule wa kawaida

Kutoka Gospel Translations Swahili

(Tofauti baina ya masahihisho)
Pcain (Majadiliano | michango)
(Created page with '{{info|Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Heal Us from Moral and Physical Sickness}}<br> <blockquote> ''“Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, gali alimtoa kwa ajili<br> yetu ...')
Badilisho lijalo →

Sahihisho kutoka 15:45, 11 Agosti 2011

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Heal Us from Moral and Physical Sickness

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 18 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Ikiwa Mungu hakumhurumia Mwanawe, gali alimtoa kwa ajili
yetu sote, atakosage basi kutupatia vitu vyote kwa ukarimu
pamoja Naye?” (Warumi 8:32).

Katika mstari huu, tunaambiwa kwamba mahitaji yetu yote yanapeanwa katika Kristo Yesu. Kile Biblia inasema ni: Mungu ametupatia zawadi kuu ambayo ni Mwanawe. Je, atawezaje kukosa kutupatia mambo mengine ambayo ni ya manufaa kwetu? Ikiwa ametupatia kile ambacho ni cha muhimu sana, basi hawezi kukosa kutupatia mambo ambayo ni madogo.

Kile mstari huu unafunza ni kwamba Mungu hatatunyima chochote ambacho anajua kwamba ni kizuri kwetu. Ikiwa anajua kwamba kuna kitu ambacho kitakuwa cha manufaa kwa maisha yako ya kiroho, basi atapeana kitu hicho.

Swali ambalo tunafaa kujiuliza ni, “Je, Biblia inamaanisha nini wakati inasema kila kitu?” Biblia haimaanishi kwamba Mungu atatupatia maisha yenye starehe hapa ulimwenguni. Pia haimaanishi kwamba hatutakuwa na maadui. Tunajua hivi kwa sababu katika kifungu hicho hicho Paulo anasema, “Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, tunahesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa” (Warumi 8:36). Kuna wakristo wengi katika ulimwengu leo ambao wanapitia mambo magumu sana ambayo yanasababishwa na maadui wa Mungu. Lakini wanafaa kuhimizwa kutokana maneno haya, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga?” (Warumi 8:35). Biblia inazungumza kuhusu mambo haya yote katika mstari huu kwa sababu Mungu anajua kwamba mambo haya yatawafikia wakristo wote. Tunakumbana na majaribu haya, “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, naam na zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda” (Warumi 8:37).

Je, Biblia inamaanisha nini wakati inasema kwamba kwa sababu ya kifo cha Bwana Yesu Kristo, Mungu atatupatia kila kitu? Inamaanisha kwamba Mungu atatupatia kila kitu ambacho ni kizuri kwetu. Inamaanisha kwamba atatupatia kila kitu ambacho kitatusaidia kukamilika katika mfano wa Kristo Yesu (Warumi 8:29). Inamaanisha kwamba atatupatia kile ambacho kitatuwezesha kuingia mbinguni.

Biblia inatufunza jambo hili wazi wakati inasema, “Naye Mungu wangu atawajaza ninyi kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri Wake katika utukufu ndani ya Kristo Yesu” (Wafilipi 4:19). Katika kifungu hicho hicho tunasoma, “Ninajua kupungukiwa, pia ninajua kuwa vingi. Nimejifunza siri ya kuridhika katika kila hali, wakati wa kushiba na wakati wa kuona njaa, wakati wakuwa na vingi na wakati kupungukiwa. Naweza kuyafanya mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:12-13).

Paulo katika kifungu hiki anasema kwamba anaweza kufanya kila kitu katika Kristo. Kuwa mwangalifu sana kwa sababu katika maneno haya anazungumza kuhusu kuvumilia katika kila hali, kama hali ya njaa au wakati ako na hitaji lolote. Kwa maneno haya anamaanisha Mungu atatosheleza kila hali kwa mapenzi yake. Hiyo haimaanishi kwamba atatupatia chakula, mavazi, afya njema, na utajiri kila wakati. Bali inamaanisha kwamba atatuwezesha kuvumilia wakati wa njaa, umaskini na wakati tuko na hitaji lolote ambalo tunaweza kuwa nalo. Kupitia kwa mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo, Mungu atatupatia kila kitu ambacho kitamletea utukufu.