Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Destroy the Hostility Between Races

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Destroy the Hostility Between Races

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 44 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Kwa maana Yeye mwenyewe ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi
tuliokuwa wawili, yaani, Wayahudi na watu wa Mataifa tuwe
wamoja kwa kuvunja kizuizi na kubomoa ule ukuta wa uadui
uliokuwa kati yetu. Kwa kuibatilisha ile sheria pamoja na amri
zake na maagizo yake alipoutoa mwili wake, ili apate kufanya
ndani yake mtu mmoja mpya badala ya hao wawili, hivyo,
akifanya amani” (Waefeso 2:14-16).

Katika Agano Jipya tunasoma kuwahusu Wayahudi na watu wa Mataifa. Ni wazi kwamba kulikuwepo uadui kati ya watu hawa. Mfano wa haya ni katika kitabu cha Wagalatia 2:11-12, “Lakini Petro alipofika Antiokia, mimi nilimpiga ana kwa ana kwa sababu alikuwa amekosa kwa wazi. Kabla baadhi ya watu waliotoka kwa Yakobo hawajafika, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa. Lakini hao watu walipofika alianza kujiondoa na kujitenga na watu Mataifa kwa sababu aliwaogopa wale wa kundi la tohara.”

Kefa (yaani Petro) alikuwa akiishi katika uhuru wa Kristo hata kama alikuwa Myahudi. Alikuwa akila na watu wa mataifa kwa sababu kwake hakukuwa na uadui kati yake na watu wa mataifa ambao walikuwa wameokoka. Lakini wakati Wayahudi ambao walishikilia desturi sana walikuja Antiokia, Kefa aliwaogopa sana. Kwa hivyo aliacha kula na watu wa mataifa na akawa sasa anakula tu na Wayahudi pekee. Aliogopa kwamba wale Wayahudi ambao walikuwa wamekuja Antiokia wangemkemea sana.

Wakati Paulo aliona yale ambayo yalikuwa yametendeka, alikasirika kwa sababu ya tabia ya Kefa. Siyo jambo jema machoni pa Mungu mkristo kukataa kushiriki na mkristo mwingine kwa sababu ya kabila. Wakati Paulo aliona ni nini inatendeka, aliongea na Kefa uso kwa uso kumrekebisha kuhusu mambo haya (Wagalatia 2:14). Wale wote ambao wako na ukabila wanakataa ujumbe wa injili. Wakati Kefa alikataa kushiriki na wakristo wa mataifa alikuwa anakataa ujumbe wa injili. Kristo alikufa kwa ajili ya watu wake wote na kwa hivyo hatufai kuwa na ukabila miongoni mwetu.

Kwa hivyo wakati Paulo aliona kile ambacho kilikuwa kikifanywa na Kefa, alizungumza mbele ya watu kwamba, “Wewe ni Myahudi, nawe unaishi kama mtu wa Mataifa na wala si kama Myahudi. Imekuwaje basi, mnawalazimisha watu Mataifa kufuata desturi za Kiyahudi?” (Wagalatia 2:14). Wakati Kefa alikataa ushirika na watu wa mataifa alikuwa akisema, lazima muwe Wayahudi ndipo niweze kushiriki nanyi. Ni kama mtu leo aseme, lazima uwe mtu wa kabila yangu ndipo uwe mshirika wa kanisa langu. Lakini Bwana Yesu Kristo aliondoa mambo haya yote wakati alipokufa msalabani.

Kristo alikufa ili makabila ya ulimwengu yapatanishwa kwake. Anawaleta pamoja watu wake wote, haijalishi wanatoka katika kabila gani au rangi gani au nchi gani, wote ni wake.

Utenganisho ambao uko katika ulimwengu kote ni kati ya wale ambao wameokoka na wale ambao hawajaokoka. Wale wote ambao wameokoka ni wa Mungu na ni watoto wake wapendwa. Wale wote ambao hawajaokoka ni wa shetani. Watu hawa hawako katika ufalme wa Mungu na hawataingia mbinguni wakati watakapokufa. Kristo Yesu ndiye njia ya pekee mtu yeyote anaweza kuingia ufalme wa Mungu.