Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?/Kristo alikufa amfurahishe Mungu Baba

Kutoka Gospel Translations Swahili

Related resources
More By John Piper
Author Index
More About The Death of Christ
Topic Index
About this resource
English: Fifty Reasons Why Jesus Came to Die/To Please His Heavenly Father

© Desiring God

Share this
Our Mission
This resource is published by Gospel Translations, an online ministry that exists to make gospel-centered books and articles available for free in every nation and language.

Learn more (English).
How You Can Help
If you speak English well, you can volunteer with us as a translator.

Learn more (English).

By John Piper About The Death of Christ
Chapter 2 of the book Je, Kwa Nini Kristo Alikufa Msalabani?

Translation by Desiring God


“Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana kumchubua na
kumsababisha ateseke” (Isaya 53:10).

“Mkiishi maisha ya upendo, kama vile Kristo alivyotupenda sisi
akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na
dhabihu kwa Mungu” (Waefeso 5:2).

Watu mara mingi hufikiria kwamba nia ya Mungu Baba ni kuwahukumu watu jahanum, Wanafikiria kwamba Mungu Baba hana huruma kamwe na kwamba kama kila kitu kingeachiwa Yeye, basi wanadamu wote wangeangamia jahanum. Na wanaendelea kufikiria kwamba Mungu Baba anataka kuwaadhibu watu wote, lakini Yesu Kristo aliingilia kati na akatuokoa. Kwa mfano, mtoto akikosa na babake atake kumpiga kwa sababu ya makosa ambayo amefanya, mamake mtoto anaingilia kati na kushauriana na baba mtoto ili mtoto asije akapigwa. Baada ya kushauriana na mama mtoto, baba anamua kwamba hatamwaadhibu mtoto. Hivi ndivyo watu wengi wanafikiria kuhusu Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.

Lakini ni lazima tujue Biblia haisemi kitu kama hicho. Biblia haisemi kwamba nia ya Mungu ni kupeleka watu jahanum. Biblia inafundisha kwamba ni mpango wa Mungu Baba kwamba Bwana Yesu Kristo aje duniani na kufa kwa ajili ya dhambi zetu. Biblia inatuambia kwamba kabla ya kuumbwa kwa mbingu na aridhi Mungu Baba alipanga wokovu wetu na vile atamtuma Mwanawe duniani kuhakikisha kwamba tunaokolewa. Biblia inasema hivi kuhusu Mungu, “Alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele” (1 Timotheo 1:9).

Tunaposoma Agano la Kale, tunasoma kuhusu mpango huu wa Mungu Baba wa kumtuma Mwanawe duniani afe kwa ajili ya dhambi za watu wake. Nabii Isaya alitabiri mateso na kifo cha Bwana Yesu Kristo. Isaya alisema Kristo, “Hakika alichukua udhaifu wetu na akajitwika huzuni zetu, hata hivyo tulifikiri amepigwa na Mungu, amepigwa sana naye na kuteswa. Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu...Sisi sote, kama kondoo, tumepotea, kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe, naye Bwana aliweka juu yake maovu yetu sisi sote” (Isaya 53:4-6).

Kifo cha Yesu msalabani Kalivari ulikuwa mpango wa Mungu Baba. Hii ndiyo sababu Agano la Kale linasema, “Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana kumchubua na kumsababisha ateseke” (Isaya 53:10).

Hii ndiyo sababu katika Agano Jipya tunasoma kwamba kifo cha Yesu kilimpendeza Mungu Baba. Wakati Kristo alikuwa msalabani, alisema, “Eloi, Eloi, Lama sabakthani? Maana yake, ‘Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha’” (Mathayo 27:46). Maneno haya yanamaanisha kwamba Mungu alimwacha Yesu Kristo wakati alikuwa msalabani kwa sababu alimwekelwa dhambi zetu juu yake. Pia Agano Jipya linasema, “Kristo alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu” (Waefeso 5:2).

Mungu aliimwaga ghadhabu yake juu ya mwanawe na akamwaadhibu kwa sababu ya dhambi zetu. Wakati Yesu alikufa, Mungu Baba alipendezwa na kifo chake, kwa sababu tangu mwanzo alikuwa amepanga hivyo.